Kwa jinsi Iran inavyosigana na mataifa makubwa kama Marekani, inaweza kuleta picha kuwa ni nchi hatari kuishi. Lakini ukifuatilia taarifa za hapa Tanzania, ni wazi kuwa nchi ya Tanzania na Iran hazijawahi kuhasimiana. Hata kipindi fulani, Iran iliipatia Tanzania msaada wa matrekta madogo 100...