Naona kuna propaganda mnaeneza mitandaoni kuwa mlisaidia CCM kupata ushindi 2015 na baada ya uchaguzi mkuu hayati JPM alipokamata madaraka aliwatenga na kuwaona hamfai wakati mlimuweka madarakani.
Acheni kupindisha maneno. Kila mtu anajua mlishazoea masuala ya kihuni ya kupora mali za umma...
Ufisida ni janga la taifa letu na ni viongozi wachache ambao hujitoa kupinga ufisadi kwa moyo wa dhati.
Lyatonga Mrema alipinga ufisadi kwa maisha yake yote akiwa mtumishi wa umma mpaka sasa akiwa mzee.
Nakumbuka kupewa stori na wazee wa Wanaomfahamu Mrema kupambana na walanguzi na maadui wa...
Balozi Dk Wilbroad Slaa anatarajiwa kuongoza kongamano la tafakuri tunduizi ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli.
Kongamano hilo litakalofanyika Ijumaa Machi 25, mwaka huu katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza pia linalenga kufanya...
Wanasiasa usiwaamini
Sisi tukishangilia hotuba za JPM zilizoutukuza umasikini wetu, na kwa kweli watanzania wengi tuliona fahari kubwa sana kuwa masikini na kuwa wanyonge. Mtu yeyote aliyejifanya kutafuta utajiri tulifanya hima kimchongea Kila mahala, na kama ana shamba, basi tulilivamia, na...
Leo ni Maadhimisho ya Mwaka mmoja tangu Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli atukote. Maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Geita katika wilaya ya Chato.
Maadhimisho hayo yatahudhuriwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia suluhu, Makamu wa Rais Dkt. Isdori Mpango...
Mambo 10 kuelekea mwaka mmoja bila jpm/ bulldozer.
JASIRI
Hayati Magufuli alikuwa ni kiongozi jasiri ambaye aliamini kwenye kuamua hata kama mawazo yake hayaungwi mkono na walio wengi. Ujasiri wake ndio ulisaidia kutekeleza miradi Mingi na mikubwa ambayo haikuwahi kufikiriwa kuwa ingetekelezwa...
Meli za kutoka Dubai kuja DSM huchukua siku 14, Mzigo ukifika Dar Es Salaam bandarini utakaa siku hata 20-28 ukisubiri kupakuliwa.
Meli ikitoka UK au China itatumia siku 28-30 kufika Dar, Mzigo ukifika hapo Bandarini unachukua siku 20-28 zingine kupakuliwa.
Gharama za Usafiri imebidi...
Hayati JPM alikuwa mtu wa vitendo na mtu wa kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa manufaa ya umma.
Kwa manufaa ya umma na watu wa chini na wanyonge lazima angekomaa na bwawa la JNHP kukamilika ili watanzania wapate umeme wa bei rahisi na wa uhakika.
Watanzania tusitarajie huu mradi...
Watanzania wengi hawakujua kwa nini waliomchukia hayati Magufuli walikuwa wakimkebehi kupitia mitandao ya hasa Twita.
Baadhi yao wakaanza kupost picha za magari ya kijeshi yakifanya mazoezi ya parade ya kuaga mwili wa mkuu wa nchi.
Wengine wakapost Brassband ya jeshi ikifanya mazoezi ya nyimbo...
Wakati wa JK mfumo uliona Rushwa ilivyokithiri ukaona namna Mali za umma zinavyoliwa na watu wachache . Walimwona JK alivyo mwanasiasa mahiri lakini ambaye siyo mwepesi wa kusoMa sana na kwake yeye wasaidizi wake wanaweza wakafanya Kila kitu. Watu walimwona alivyokuwa busy kuzunguka Duniani...
Video ya Vladmir Putin akihojiwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya magharibi inatembea mitandaoni. Putin anajitahidi sana kujenga hoja za kujibu maswali lakini kama kawaida yake anarudia makosa yale yale ya miaka yote. Putin aidha hana team nzuri ya Diplomasia au anaogopwa na...
Hayati JKN siwezi kumlaumu sana maana wakati akitawala enzi hizo nchi nyingi zilikuwa bado hazijajitambua na mkono wa mataifa ya nje ulididimiza mataifa ya kiafrika.
Chukulia tu kwa awamu tatu zilizopita kila moja ingethubuti kutekeleza miradi mikakati mikubwa ya maana ya kimaendeleo leo...
Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, leo Alhamisi amesema atatoa leseni za kuanza kuchapishwa kwa magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima, Mseto na Mawio “Kifungo kimetosha. Kikubwa kazi iendelee,” amesema Nape.
"Agizo la Rais ni Sheria,leo nitatoa leseni kwa...
Sasa naona Katibu mkuu wa UVCCM Kenani Kihongosi ameamua kuingia mstari wa Mbele kuongoza mapambano dhidi ya wamachinga. Bavicha tunalaani vitendo hivyo na tutaongoza mapambano ya kudai #KatibaMpya itakayotoa Uhuru wa vijana kufanya biashara bila bugdha.
Asante mama kila unachoshika kinazaa matunda bila ubabe Wala mbwembwe za eti kishindo Cha jpm tofauti mtangulizi wako ambaye kitu kidogo tu kelele nyingi.
Tumeona watalii wanavyomwagika nchini na bila shaka watanzania vinana maskini wameanza kuona umuhimu wako baada ya kilazimishwa kuwa...
Furaha Dominic ambaye ni mpwa wa hayati Magufuli aliyegombea ubunge jimbo la Kawe na kushika nafasi ya kwanza huku Pascal Mayalla akiwa wa 162 amesema siku atakayokutana na Rais Samia atampa orodha ya Wafitini wote waliomzunguka.
Furaha anadai CCM kumejaa siasa chafu za kupakana matope...
Ndugu zangu
kwanza niwape pole waathirika wote na wafiwa wa ugonjwa wa corona ndo mapito tuwe na imani corona itaondoka, ila itaondoka pale tu sisi binadamu tutakapokuwa wanyenyekevu mbele ya Mungu.
Hii corona ni pigo kutoka kwa Mungu kwa sababu sisi wanadamu ni washenzi tumezidi maasi na...
Kumbe ukitaka uchukiwe na wanaCcm basi we ziba mianya yao ya kuiba mali ya umma.
Hayati JPM alichukiwa na wanaCcm japokuwa walicheka nae na kumzunguka hio hii ni sababu aliwabana sana juu ya rushwa na ufisadi.
Sasa wanatoa michongo namna ya kupiga madili.
Naona tangu amefariki wanachekelea...
Katika Nchi ambayo Viongozi wanajipimia kama hii Tanzania ya Sasa tunahitaji vitu vitatu :-
1. Katiba Mpya ,tunahitaji katiba inayong'ata ili viongozi na wananchi waheshimu madaraka.
2. Chama kimoja (ingawa linaendana na katiba),Tanzania bado ni nchi changa kuwa na mfumo wa vyama vingi hivyo...
Tunatoa sana ushauri humu JF na wakati mwingine tunaonekana kama wavurugaji waliotumwa na wapinzani au watu tusiokuwa na uzalendo na taifa letu, mwisho wa siku ushauri inapuuzwa na kumsikia mama analalamika kua wapo watu ndani ya serikali hawako naye na wengine hawaelewi.
Tulishauri kwamba Mama...