kisutu

  1. Erythrocyte

    Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA aliyekamatwa Zanzibar, Hashimu Issa Juma apelekwa Kisutu

    Hii ndio Taarifa mpya kutoka Chadema kwa sasa, ambapo watu wasiofahamika wakiwa na bunduki wamemchukua Mzee Hashimu Issa nyumbani kwake Unguja na kuondoka naye, tena bila kusema wanampeleka wapi. Taarifa zaidi zitaendelea kuwajia kwa kadri zitakavyotufikia. ==== UPDATES Jeshi la Polisi Kanda...
  2. Hashpower7113

    DPP awafutia Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kesi ya Uchochezi

    Criminal Case No.208/2016 iliyokuwa ikimkabili Tundu Lissu na wenzake watatu katika Mahakama ya Kisutu, imefutwa na DPP kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo ya Makosa ya Jinai. Watuhumiwa wote wako huru. Mbali na Lissu washtakiwa wengine walikuwa ni Mhariri wa Gazeti la...
  3. B

    Kilio cha akina Mama Kisutu kitaondoka na nafsi ya kiongozi mkubwa nchini

    Tunaoamini Kwenye imani ya dini tunajua namna kilio Cha wanawake pale wanapodai haki kinavyoleta laana Kwenye familia. Haiwekani wale wakina Mama wakatoa machozi Yakapita bila kuleta madhara. Ni maoni yangu tuombe toba hasa viongozi ambao machozi yalielekezwa kwako la sivyo tunakwenda...
  4. J

    Hamza Mohamed Hassan azikwa makaburi ya Kisutu, Dar. Mazishi yachelewa kutoa risasi zilizokwama mwilini

    Hamza Mohamed Hassan aliyefanya mauaji pale Selender bridge azikwa. Jamii, rafiki na ndugu zake Wamzika ==== Dar es Salaam. Mwili wa Hamza Mohammed aliyefariki dunia katika tukio la majibizano ya risasi kati yake na jeshi la Polisi amezikwa leo Jumapili Agosti 29, 2021 saa 2:30 usiku katika...
  5. figganigga

    Kisutu-Dar: Lusubilo Mwakabibi na Edward Haule wafikishwa Mahakani

    Salaam Wakuu, Aliyekuwa Mkurugenzi wa Temeke Lusubilo Mwakabibi na Edward Haule, Wamefikishwa Mahakamani Kisutu asubuhi hii. Hatua hii imekuja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa siku nne kwa TAKUKURU kumfika Mwakabibi Mahakamani ajibu Mashitaka yanayomkabiri. Katika ziara yake ya...
  6. Erythrocyte

    Kisutu: Maafisa wa EU, UN na Mabalozi wa Marekani, Sweden na Ujerumani wahudhuria Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe

    Hivyo ndivyo ilivyokuwa leo Mahakamani, ambapo Wadau wa Maendeleo wa Tanzania kutoka kwenye Taasisi za Kimataifa wameshiriki kesi hiyo ya Ugaidi kwa lengo la kujua kinachoendelea, Maofisa hao wengi wao wamefika ili kujiridhisha na mwenendo wa kesi hiyo. Ugaidi katika nchi ni jambo baya...
  7. chiembe

    Fatma Karume na Maria Sarungi sijawaona katika maandamano Mahakama ya Kisutu, wanachochea halafu wamejificha nyuma ya kabati

    Hawa wadada wakiwa twitter wanaonekana kama tembo au simba, linapokuja suala LA kwenda saiti kutekeleza uchochezi wao, wao hawafiki! Yaani wanataka rule rungu, tufe,wao wabaki wakila bata. Maria Sarungi mama yake ni mzungu, ana pakwenda endapo njama zake za kuvuruga amani zikifanikiwa, sisi...
  8. chiembe

    Kiusalama kesi ya Mbowe iendeshwe kwa njia ya mtandao akiwa gerezani ili kuepusha mkusanyiko

    Teknolojia iko mbele sana na tunaipongeza mahakama kwa kuendesha kesi kimtandao. Kwa kuwa ugaidi ni jambo zito sana linalohatarisha usalama wa nchi, na hatuna uhakika kama magaidi wote wamekamatwa, ni vyema kesi ya mtuhumiwa wa ugaidi, Mbowe iendeshwe kwa njia ya mtandao akiwa gerezani. Naona...
  9. M

    Yaliyojiri Kisutu, Dar: Kesi ya Freeman Mbowe, yaahirishwa hadi 13 Agosti, 2021, Mashtaka yasomwa upya

    Ijumaa Imefika kukiwa na Baridi asubuhi hii katika jiji la DSM. Freeman Mbowe aliyebambikwa kesi ya Ugaidi na dola kutokana na vuguvugu la kudai Katiba impya inaendelea Leo baada ya kuahirishwa Jana kutokana na tatizo la kimtandao. Itakumbukwa mwanzoni mwa wiki hii Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP...
  10. Erythrocyte

    Wakili Msomi Peter Kibatala amhakikishia kumpigania Mwanachadema aliyekamatwa Kisutu, aahidi kumtoa selo

    Kumbe kwa Mujibu wa Sheria za Tanzania, kuonyesha bango si kosa na wala halijawahi kuwa kosa, Polisi wengi wanaowakamata walioshika mabango yenye ujumbe usio na matusi ama udhalilishaji wanafanya hivyo ili kuwafurahisha waliowatuma ili wapandishwe vyeo ama waongezwe Marupurupu tu. Msikilize...
  11. Kijogoodi

    Kama hii ndiyo idadi ya CHADEMA kutoka mikoa kuja kwenye kesi ya Mbowe, basi chama kimepoteza mvuto kabisa

    Kwa wiki moja sasa Chadema walikuwa wakihamasishana kuhudhuria kwa wingi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wao Mbowe. Kuanzia katibu mkuu wa chama John Mnyika alitokwa povu sana akiwaambia polisi liwalo na liwe maelfu ya wananchi watafurika mahakamani Kisutu siku ya tarehe 5, akaja...
  12. M

    Kisutu: Kesi ya Freeman Mbowe yaahirishwa hadi Kesho 06/08/2021, Mtandao umesumbua

    Ni Asubuhi tulivu ya siku ya Alhamisi. Kiongozi mkuu wa Upinzani Freeman Mbowe anatarajiwa kuletwa mahakamani Kisutu Leo katika Kesi ya Ugaidi. Kesi hii inavuta kila mpenda haki na mwanademokrasia kutokana na ukweli Mbowe amebambikizwa kesi hii ili kumnyamazisha kutokana na Kampeni aliyoasisi...
  13. VUTA-NKUVUTE

    Kesi ya Mbowe kesho: Kisutu hapatatosha, maandalizi yanaogofya

    Kesho tarehe 5/8/2021, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itatajwa kesi ya jinai inayomjumuisha Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA Ndugu Freeman Aikaeli Mbowe. Mbowe pamoja na wenzake watatu wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali ya kijinai. Kwake binafsi, Mbowe anashtakiwa kwa mashtaka ya kula...
  14. M

    Mikoa 20 yathibitisha kuhudhuria kesi ya Mbowe Kisutu Agosti 5, 2021

    Kesi ya kubambikizwa Ugaidi Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe inatarajiwa kutajwa Alhamisi August 5 Kisutu jijini DSM. Akizungumza na wanahabari jana Jumamosi Katibu Mkuu John Mnyika aliwataka wana Chadema na wananchi kufurika Kisutu siku ya Alhamisi August 5 ili kufuatilia kwa ukaribu kesi...
  15. mugah di matheo

    Dar: Mahakama ya Kisutu yamfutia kesi na kumwachia huru dereva aliyetuhumia kumteka Mo Dewji

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemfutia kesi na kumwachia huru dereva taksi Mousa Twaleb aliyekuwa akituhumiwa kuhusika na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji almaarufu ‘Mo Dewji’. Twaleb alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 28, 2019...
  16. Stroke

    Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

    Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kusomewa mashtaka mawili likiwemo la Ugaidi. Mbowe amefikishwa katika Mahakama hiyo leo July 26, 2021 na kusomewa mashataka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu...
  17. Replica

    Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

    Habari wakuu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akiwa Soko Kuu la Kariakoo, amesema serikali imeunda tume ya watu kumi kuchunguza na kupata ukweli wa chanzo cha moto na athari zilizopatikana ikiwemo mali zilizoteketea, pia amesema Waziri mkuu yuko njiani kuja kukagua na kuongea na...
  18. Erythrocyte

    Naomba kufahamishwa wasifu wa Mhe. Thomas Simba, Hakimu wa Mahakama ya Kisutu

    Si vibaya na wala haijawahi kuwa kosa kisheria kufahamu wasifu wa Mtumishi wa Umma, hasa yule anayegusa maslahi ya watu wengi kwa kuhakikisha haki zao zinapatikana. Binafsi namfahamu kidogo tu kama Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu, ameshiriki kwenye kuamua kesi kadhaa za wanasiasa...
  19. Roving Journalist

    Kisutu: DPP Biswalo, awaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo Alhamisi imewaachia huru, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso Tabura. Hatua hiyo imefikiwa Baada ya aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga kutokuonesha nia ya kuendelea na kesi dhidi...
Back
Top Bottom