WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya CPC Jimbo la Shanxi, Komredi Tang Dengjie. Katika kikao hicho kilichofanyika Juni 21, 2024...