BORA NIKAOE TANGA
Bora nikaoe Tanga, tena binti wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongea kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.
Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa...