Ameunguruma Simba, Nchi imetetemeka
Manyang'au yamevimba, Aibu imewashika
Yalijiona miamba, Ile isiyovunjika
Hongera sana Mbowe, Wewe ni mtu makini
Hawa watu waonevu, Ni watu waso na soni
Matendo yao uovu, Na ghiliba za shetani
Mipango yao mibovu, Kaivunja Freemani
Hongera sana Mbowe, Wewe ni...