MAGOMENI KWA ZITO USIKU
Miaka ya 1970 kulikuwa na mgahawa Magomeni Mapipa si mbali na hoteli ya Butiama ukiitwa Michuzi Mikali.
Mwenye mgahawa huu jina lake lilikuwa Shomvi na alikuwa shabiki mkubwa sana wa Yanga.
Yeye alikuwa anafungua mgahawa wake mchana kwa ajili ya chakula cha mchana...