MTENDAJI wa Kijiji cha Mpwayungu Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Selemani Kibakaya, amesema wazazi wawili waliowaoza binti zao wenye umri wa miaka 14, wamekubali kurejesha fedha na mifugo waliyopokea kama mahari na kurudi na watoto wao nyumbani baada kugundua kuwa watoto wamekuwa wakiteseka...