Sikuwahi kufikiria nitawahi kupata upenyo wa kuongea yaliyositirika kwa muda sana ila hatimae nimefikiwa. Nakumbuka mama aliwahi kuniambia "Mwanangu, siku zote tembea duniani ukivaa viatu vya watu." Kauli ile ilinichanganya ila kadri siku zilivyosonga nilielewa kuwa si kila kiatu ninaweza kuvaa...