Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, amesema nchi yake itasitisha mapigano kuanzia saa nne asubuhi ya leo kwa majira ya Moscow na kufunguwa njia salama kuwahamisha raia kutoka miji ya Kiev, Cher-nigov, Sumy na Mariupol. Kwa mujibu wa Nebenzia, pendekezo hilo halina masharti...