Kwa ajili ya kujifungua salama, andaa vifaa vifuatavyo: -
Sabuni na maji kwa ajili ya kunawa mikono mara kwa mara, kumsafisha mama, na kusafisha vifaa tiba. Vilevile andaa beseni au bakuli kwa ajili ya kunawia na kupokea kondo la nyuma.
Viwembe vipya au mkasi wenye makali kwa ajili ya kukata...