Serikali imezindua mkakati wa taifa wa awamu ya pili wa miaka 10, wa kuendeleza zao la mpunga nchini ili kuhakikisha wanafikia hekta milioni moja ifikapo mwaka 2025.
Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ambapo alisema lengo ni kuona wanaongeza uzalishaji wa zao la mpunga...