MUDA ni sehemu muhimu sana katika mpangilio wa mambo mengi duniani, na hii ni tangu kwa kuumbwa kwake, kutokana na maandiko ya vitabu vya dini, vimeandikwa kwamba hata Mungu aliutumia muda katika kuumba ulimwengu, na kuongeza kuwa Dunia iliumbwa kwa siku sita na ya saba ikawa ni mapumziko yake...