mwenge wa uhuru

Mwenge wa Uhuru
Mwenge wa Uhuru una muundo wa tochi ya mafuta ya taa ambayo inaashiria uhuru na mwanga. Mwenge wa uhuru ulinyanyuliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo Desemba 9, 1961 na shujaa Brigedia Alexander Nyirenda ikiashiria kuangaza nchi na kuvuka mipaka kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo palipo uadui na heshima palipo chuki.

Sababu ya huyu brigedia kunyanyua mwenge huu ni kuonesha fahari ya nchi na pia kuleta matumaini kwa Watanzania wote kwa kutokata tamaa, kupendana, kuheshimiana na kutogombana ikimaanisha kuwa na ushirikiano.

Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyika kila mwaka kuanzia maeneo mbalimbali nchini.
  1. and 300

    Mwenge wa Uhuru: Alama ya Uzalendo

    Leo tarehe 02 April 2022 Mwenge wa Uhuru unawasha Mjini Njombe. Makamu wa Rais Dr Philip Mpango (PhD) na Waziri mwenye dhamana Prof Ndalichako (PhD) wanatoa hotuba zilizojaa Elimu, Hekima na Maelekezo sahihi. Kidumu Chama Cha Mapinduzi
  2. Q

    Kulikuwa na sababu yeyote leo kuweka Mashada kwenye kaburi la Magufuli?

    Ni takribani miezi 6 tu imepita viongozi walikuwa Chato kuweka mashada kwenye kaburi la Magufuli mashada mengine yangalipo na hayajakauka, ni sababu zipi zimefanya tena leo kuweka mashada kwenye kaburi lile lile, kama lengo lilikuwa kuzima mwenge kwa nini wasingeitumia siku ya leo kwa shughuli...
  3. Baraka Mina

    Rais Samia Suluhu ashiriki katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Mwalimu Nyerere

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan akishiriki katika kilele cha mbio maalum za mwenge wa uhuru na kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere katika uwanja wa Magufuli - Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Oktoba 2021.
  4. M

    Mbio za 29 za mwenge wa Uhuru kumaliza siku 150 na wilaya 150 kesho Wilayani Chato | Mhe Rais Samia Suluhu Hassan mgeni rasmi

    Mwenge wanusa harufu ya rushwa na ufisadi kwenye miradi 49 kati ya miradi 1,097 yenye thamani ya 1.2trilioni iliyozinduliwa | TZS 65b zahofiwa kutafunwa na mchwa, " Chato tunasema Asante " Mtakumbuka Mwenge wetu wa Uhuru uliwashwa rasmi tarehe 17|05|2021 Makunduchi Zanzibar na leo tarehe...
  5. Linguistic

    Rais Samia kuwa Mgeni Rasmi Kilele cha Uzimaji wa Mwenge Kitaifa Chato 14/10/2021

    Wakuu, Chifu Hangaya anatarajia Kuwa Mgeni Rasmi kwenye Kilele Cha Uzimaji Mwenge Wa Uhuru Octoba 14 Huko Chato Mkoani Geita. Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 Ulianzia Kukimbizwa Mei 17 Huko Kusini Unguja na utakamilika Oktoba 14 mwaka huu Huko Chato. Wazee Wa Chato Wanatarajia siku Hiyo Chifu...
  6. T

    Karibu Mwenge wa Uhuru mkoani Mbeya

    KARIBU MWENGE WA UHURU MKOANI MBEYA. Mwenge wa Uhuru baada ya kumulika maeneo mbalimbali nchini sasa ni zamu ya mkoa wa Mbeya. Ni Jumamosi hii ya Septemba 11, 2021 Mwenge wa Uhuru utapokelewa wilayani Mbarali katika eneo la Igawa tayari kwa kuanza kukagua miradi na shughuli mbalimbali mkoani...
  7. J

    Mwenge wa Uhuru utazimwa Chato mkoani Geita ukiambatana na Misa takatifu ya kuwaombea mahayati Magufuli, Mkapa na Nyerere katika Kanisa Katoliki

    Waziri Jenister Mhagama amesema Mwenge wa Uhuru utakamilishia mbio zake katika wilaya ya Chato mkoani Geita ikiwa ni kumbukumbu ya kumuenzi hayati Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 wa JMT Katika hitimisho hilo la mbio za mwenge itafanyika misa takatifu ya kitaifa katika Kanisa Katoliki...
  8. Peter Madukwa

    NACHINGWEA: Mwenge wa uhuru wazindua, kutembelea na kuzindua miradi sita (6) wilayani Nachingwea

    Tarehe 25.8.2021 Mwenge wa Uhuru umetembelea, kuzindua na kuweka jiwe la msingi jumla ya miradi sita katika wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi. Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa maji katika kijiji cha Namikango, mradi wa wodi ya wazazi ya kisasa katika hospitali ya wilaya na mradi wa...
  9. K

    #COVID19 Ifike muda Mwenge wa Uhuru uhifadhiwe Makumbusho ili kupambana na COVID-19

    Leo ulikuwa maeneo ya Chalinze. Tumesimama tangu asubuhi hadi muda huu gari haziendi kisa Mwenge! Wanafunzi wamekatishwa masomo yao wapo wamejipanga mistari hapo kushuhudia Mwenge! Tunaanzaje kupona na hii Corona? Wagonjwa wangapi wameathirika kutokana na kucheleweshwa na misafara ya Mwenge...
  10. kavulata

    #COVID19 Kwanini tukimbize mbio za Mwenge kipindi hiki cha COVID-19?

    Juzi nilikutana na mbio za Mwenge pale Mkata, watu wamekusanyika balaa na msafara umezuia magari yasiende. Jamani mbona hatuko serious na afya za watu wenyewe? Dunia itatuelewaje sisi jamani? Kwani kwenye Mwenge kuna nini kiasi hiki?
  11. C

    Halmashauri ziache kuwalazimisha Watumishi kuchangia Mwenge

    Hii tabia ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwataka watumishi wa umma ndani ya Halmashauri imetoka wapi? Yaani mkuu wa wilaya anaagiza wakuu wa idara kusimamia zoezi na kuomba majina ya wachangiaji, sasa hatujui wasiochangia wafanywaje. Pia wakuu wa idara wamekuwa wakionywa endapo atashindwa...
  12. Pascal Mayalla

    Mapokezi ya Mwenge Dodoma: Wilaya ya Bahi yafanya Kufuru

    Wanabodi, kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, huzungukia maeneo mbalimbali ya nchi yetu kushuhudia haya na yale. Leo nimepata fursa kushuhudia shamra shamra za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Dodoma. Jana Mwenge ulilala Kijiji cha Mwitikira Wilaya ya Bahi. Mambo niliyoyaona usiku wakati wa...
Back
Top Bottom