NAMPENDA PRISKA
Nampenda Priska, shairi namtungia,
Mwili umetakasika, hakika anavutia,
Sauti akitamuka, hoi mie nabakia,
Nampenda Priska, shairi namtungia.
Macho yake ya gololi, Mungu mempendelea,
Kimtazama kwa mbali, anarembua rembua,
Kama anapenda wali, mie tamnunulia,
Nampenda Priska...