ng'ombe

Ng'ombe
Ng'ombe ni wanyama wakubwa wanaokula nyasi. Ni wanyama wanaofugwa kwa wingi sana kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi au pia kwa kuvuta plau au gari la kukokotwa.

Kwa asili kuna aina mbili za ng'ombe-kaya: ng'ombe wa Ulaya na ng'ombe wa Uhindi ambazo ni nususpishi za B. primigenius (B. p. taurus na B. p. indicus mtawalia, ingawa mara nyingi nususpishi hizo zinaainishwa kama spishi za B. taurus na B. indicus). Zinatoka kwa nususpishi za zamani B. p. primigenius na B. p. namadicus.

Ng'ombe hula nyasi na hutembea kwa kwato. Ng'ombe waliofugwa na binadamu walitokana na ng'ombe-mwitu ili kujipatia nyama na maziwa. Katika nchi nyingi hutumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
  1. Second Lieutenant

    Biashara ya Kuuza Nyama (Butcher's Shop): Mambo Mbalimbali ya Kujifunza

    Habari za Mchana wana JF, Ndugu yenu hapa naomba info kuhusu biashara ya Nyama (Burchery), Bei wanazonunua Machinjioni inakuwa kiasi gani? wangapi wamefanikiwa through this business. WADAU WENGINE NAOHITAJI MUONGOZO WA BIASHARA HII MICHANGO NA MIONGOZO
  2. Tony254

    Aisee sio kwa vichwa vya ng'ombe hivi

    Baada ya Watanzania kutudanganya kwa miaka nyingi kwamba wao wamenunua bullet train kama zile Shikansen za Japan, sisi Wakenya tulinyamaza tu kwa sababu tulijua kwamba hamna pesa wala uwezo wa kununua treni yenye kichwa mchongo. Sasa tulieni msibiri vichwa vya ngombe vyenu viwasili 👇 👇 👇
  3. Geza Ulole

    Baada ya ng'ombe toka Kenya sasa Wakenya wanaleta ng'amia

    MY TAKE Hawa wapumbavu wakiachwa watasababisha migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji imagine ngamia 89 wanaswagwa kwa njia za vichochoro! Hii si mgogoro unatafutwa kwa mazao ya wakulima? Ni vizuri uhamiaji wameingilia kati, wacha mahakama iamue hili!
  4. Erythrocyte

    Freeman Mbowe akabidhiwa zawadi ya Ng'ombe na Wazee wa Mwanza kama Shukrani ya Kutambua mchango wake kwa mapambano ya Demokrasia ya Tanzania

    Zawadi hii yenye maana nzito sana amekabidhiwa Mwamba Mbowe na Wazee wa Kata ya Igombe wakati wa Kikao cha ndani cha Operesheni Haki kwa majimbo ya Nyamagana na Ilemela. Kwa niaba yangu na familia yangu nachukua nafasi hii kuwashukuru Wazee wa Mwanza kwa zawadi hii kwa Mwamba Mbowe ikiwa ni...
  5. The only

    Ewe Mama Ng'ombe za Nyakanazi za mnada hewa zilizo chato zirudishiwe wenyewe

    Mkuu! Nakusihi ewe Tumaini letu uchunguze hili kupitia vyombo vyako urudishe tabasamu la wafugaji wa ngombe za nyakanazi. Mkuu zilikamatwa ngombe nyingi ambazo ziliingia eneo la maliasili (Japo wao wanakataa) Maafisa wakazikamata inasemekana kwa maagizo toka juu zikapigwa faini kubwa sana...
  6. BARA BARA YA 5

    Fursa ya ufugaji wa ng'ombe wa asili kwa ajili ya nyama na maziwa kwa maeneo yaliyokaribu na soko

    Wajasilimali wenzangu msije mkasema sijawaambia,iko hivi kama una shamba karibu na Dar,maana ya Mkuranga, Bagamoyo nk fikiria mradi huu unalipa.Nimeiba idea hii kwa jirani yangu kupitia meneja wake nikaone ni FURSA muhimu. Iko hivi kwa mfano: Kama una eneo lako hata kama ni ekari moja tu ya...
  7. beth

    Spika Ndugai: Sheria ya kutaifisha ng'ombe wanaoingia hifadhini ni dhuluma. Ilipita tukiwa tumelala?

    Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Sheria ya Serikali kutaifisha Ng'ombe wanaoingia maeneo ya Hifadhi ni tatizo, akiita kuwa Sheria yenye dhuluma. Amesema, "Hii Sheria sijui ilipita wapi, tulikuwa tumelala au ilikuaje. Ile kwamba Ng'ombe wakiingia kwenye Hifadhi wanataifishwa wote, hapana! Kama...
  8. Nigrastratatract nerve

    Polisi wakamata gari lililokuwa na mizoga ya ng'ombe machinjio ya Tegeta

    Polisi jijini Dar es Salaam wamelikamata gari lililokuwa na mizoga ya ng'ombe katika machinjio ya Tegeta. Kilichopelekea Polisi kufanya msako katika machinjio hayo ni taarifa waliyopewa na wasamaria wema walioshtushwa na harufu kali ya uozo kutoka eneo hilo Habari za awali zilizopatikana katika...
  9. daktarii

    Ng'ombe wangu hawashiki mimba

    Habari ! Ngombe wangu wana tatizo. Kwanza walikua wanamimba wote wawili, then zlivyofika miezi minne - mitano zikatoka wote. Baada ya hapo wamekua wakiingia joto lakini kila nikiwapandisha hawashiki mimba wote na ndama wao wameshakua wakubwa wanakaribia mwaka, still ng'ombe bado wanakamuliwa...
  10. D

    Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)

    Ndg wana jf hope sote tu wa afya njema baada ya hekaheka za wiki nzima. Naomba mwenye EXPERIENCE ya kutosha na hii biashara ya Mifugo hasahasa Ng'ombe kuwaleta Dar kutoka Mikoani kama inalipa coz nimewahi enda pale PUGU Mnadani wakati wa Christmas angalau nijitafutie Mbuzi wa kumtafuna na...
Back
Top Bottom