Nashika tena kalamu, kwa Jina lake Karimu,
Naishika kitalaamu, nashika kiufahamu,
Napanga tungo adhimu, kama gwiji na mwalimu,
Kuaga kwa mwenye njaa, huaga na haondoki!!
Yametokea nyumbani, siku si nyingi jamani,
Hapa kwetu kijijini, nilipokea mgeni,
Mida yenyewe jioni, Mama Chanja yu...