Shirikisho la Riadha Tanzania (AT) leo tarehe 08/10/2023 limekabidhi vifaa mbalimbali kwa timu mbili za riadha zinazoenda kushiriki mashindano ya Kimataifa Japan na Switzerland.
Timu mojawapo iliyokabidhiwa vifaa ni timu ya riadha ya JWTZ inayokwenda kushiriki mashindano ya Majeshi (CISM)...
Mapokezi Makubwa ya Mwanariadha wa Kimataifa wa Tanzania, Magdalena Chrispin Shauri (alie vaa bendera ya 🇹🇿) Jijini Arusha, katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na Kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela , Charles Maguzu kutoka BMT na Kiongozi wake Jeshini (JWTZ) Arusha.
mara...
Wakuu nimeona nianzishe huu uzi uwe kama kijiwe chetu cha kujadili na kushauriana mambo mbalimbali kama familia ya riadha. Mwenye maoni, kero, dukuduku na jambo lolote la riadha tutatumia huu uzi. Nina uhakika riadha ndo mchezo pekee hapa nchini uliowahi kuweka alama zisizofutika duniani...
Mwanariadha wa kimataifa Gabriel Gerald Geay ashindwa kumaliza baada ya kupata changamoto ya kiafya kuanzia kilomita 30 na alipofika kilomita 35 akashindwa kuendelea na kapumzika.
Walichoandika World Athletics (WA);
After a half way split of 1:03:56, they passed 30km together in 1:30:58 but...
Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania Gabriel Gerald Geay atua jijini Sydney Australia kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa ya Sydney Marathon tarehe 17 septemba 2023 jumapili.
Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha wanariadha zaidi ya elfu arobaini (40,000) wanaotoka katika nchi 66...
RAIS NA KATIBU MKUU WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA WAMEONGOZA TOC TANGU 1/1/2002, HIYO NI ZAIDI YA MIAKA 21.
Katibu Mkuu huyo na familia yake wanamiliki Shule iliyopo Mkuza Kibaha iliyopewa jina la FILBERT BAYI INTERNATIONAL SCHOOLS, anapanga shughuli zote za TOC zinazofadhiliwa na...
Jezi atakayoivaa Alphonce Felix Simbu siku ya Mashindano.
Mwanariadha wa Kimataifa wa Riadha Tanzania na Mwakilishi Pekee , Alphonce Felix Simbu anatarajia kutuwakilisha kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia yanayofanyika huko Budabest, Hungary ; kuanzia 19 -27 Agosti 2023.
Simbu anatarajia...
Somalia imemsimamisha kazi afisa wa ngazi ya juu wa riadha baada ya mmoja wa wanariadha wake kuweka rekodi mpya ya mbio za mita 100 - ambayo ni ya polepole zaidi kuwahi kutokea katika mashindano ya kimataifa.
Mwanariadha huyo Nasra Ali Abukar, alikimbia na alivuka mstari wa kumaliza kwa sekunde...
Mwanariadha wetu, wa kimataifa wa riadha tanzania , Gabriel Gerald Geay anatarajia kushiriki mashhindano ya Sydney - Marathon , inayotarajiwa kufanyika tarehe 17 Septemba, 2023.
Anaenda kushiriki na wanariadha wengine wenye muda bora.
Geay, ni mwanariadha wa 9 bora duniani kwa muda wake wa saa...
Mwanariadha wa kimataifa, Gabriel Gerald Geay anogesha mashindano ya majaribio ya Uwanjani leo 8/7/2023 kwa kutoa zawadi ya pesa kwa baadhi ya wanariadha washindi na wenye muda mzuri kwa baadhi ya michezo hiyo.
Mashindano hayo yamefanyika kwa mara ya pili mfululizo na kushirikisha wanariadha...
Mwanariadha wa Kimataifa wa Tanzania Gabriel Gerald Geay amezidiwa sekunde chache na Mkenya na kuwa kwenye nafasi ya pili, kilomita 10 kwa muda wa dakika 27:43 ambapo ni muda bora kuliko wa siku chache zilizopita alizokimbia Boston B.A.A 10K na kutumia muda wa dakika 27:49.
Mashindando hayo...
Wanariadha Faraja Lazaro Damas na Magdalena Shauri ambao ni Mume na mke na ni waajiriwa wa (JWTZ) wameshinda mbio za JKT Half Marathon 2023, Zilizofanyika tarehe 25 Juni 2023, jijini Dodoma.
Faraja na Magdalena walishinda mbio hizo za kilomita 21.1 (21K) kwa muda wa (1:03:45) na (1:11:22 ) na...
Mwanariadha wa Kimataifa Gabriel Gerald Geay ashinda mbio za Boston 10K (B.A.A 10K) na kuweka muda wake bora wa 27:49 huko Boston, nchini Marekani Jumapili, tarehe 25 Juni 2023.
The B.A.A. 10K 2023 Results:
Men’s 10k results:
Gabriel Geay (Tanzania) – 00:27:49
Edwin Kurgat (Kenya) – 00:28:01...
Mashindano ya Mbio za barabarani za nusu marathoni za JKT ( JKT Half Marathon 2023) Kufanyika Jumapili tarehe 25 Juni 2023 Jijini Dodoma.
Mbio hizo ni za Kilomita 21 (21.1K), kilomita 10 (10K) na Kilomita tano (5K, Fun Run).
Zawadi za Washindi zimeshatangazwa, 21K anachukua milioni moja na...
Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi anaelekea Ujerumani kuhudhuria kwenye Ufunguzi wa mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu ~ Special Olympics World Games yatakayofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 25 Juni , 2023.
Mwanariadha wa Kenya , Faith Kipyegon ameahidi kumnunulia baba yake mzazi Gari ya ndoto yake; baada ya kuzawadiwa zaidi ya milioni 85 ya Kitanzania na Rais Ruto Ikulu Jijini Nairobi.
Faith, amezawadiwa pesa hizo baada ya kuvunja rekodi mbili za dunia katika mbio za mita 1500 na mita 5000 huko...
Na John Walter-Mbulu
Hospitali ya Kilutheri Haydom Dayosisi ya Mbulu imeandaa mbio za nyika (HAYDOM MARATHON 2023) kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wasioweza kugharamia matibabu hospitalini hapo na kuboresha huduma zaidi.
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dr.Pascal Mdoe akizungumza na waandishi wa...
Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) inatarajiwa kufanya uchaguzi Novemba 27 mwaka huu jijini Dodoma, nafasi zinazowaniwa ni Makamu wa Rais na Mjumbe wa Kamati Tendaji Kanda ya Pwani, ambazo waliokuwa wakizishikilia, John Bayo na Robert Kalyahe, walijiuzulu kutokana na sababu mbalimbali.
Zoezi la...
Shirikisho la Riadha Tanzania (AT) linatarajiwa kuziba nafasi za uongozi zilizo wazi Novemba 27 jijini Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa AT Wakili Jackson Ndaweka alisema, kikao cha kamati tendaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba mosi...
Binafsi nimekuwa nikimfahamu Mzee Bayi toka nikiwa mdogo ila sikuweza kujua kiundani kwamba kwanini hadi leo dunia inamheshimu mno kwenye riadha wakati wapo wanariadha wengi wa enzi zake waliofanya vizuri na hatuwakumbuki.
Serikali yetu inabidi ibadilishe mitaala ili historia za mashujaa wetu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.