tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Pre GE2025 TCRA yataka Vyombo vya Habari kuripotiwa uchaguzi bila upendeleo

    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevitaka vyombo vya habari nchini katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu kuvipatia vyama vya siasa nafasi sawa katika kuripotiwa habari bila upendeleo ili kuondoa malalamiko. Meneja wa Kitengo cha Utangazaji TCRA...
  2. Ally Kamwe: Habari za kufungiwa sio za kweli TCRA washughulikie taarifa kama hii

    "Na mimi nitumie nafasi hii kuwaomba watu wanashughulikia mitandao ya kijamii (TCRA) washughulikie taarifa kama hii, kwasababu Unapotoa taarifa kama ile huenda una vyanzo, lakini madhara ya taarifa kubwa kama ile ni makubwa kweli kweli, ule usiku wa taarifa imetoka nilienda kukesha hospitali na...
  3. TCRA HESHIMUNI HAKI ZA WAALIKWA MLIWAALIKA MKUTANO MKUU WA DODOMA

    Mamlaka ya Mwasiliano acheni ubabaishaji fanyeni malipo ya washiriki waliofika dodoma kwenye mkutano mkuu wa vyombo vya habari mliufanya Dodoma kitendo cha kutowalipa washiriki mpaka sasa toka siku ya tukio kumalizika ni jambo ajabu sana sio heshima wapo watu walitoka mbali wakatumia gharama zao...
  4. Hivi TCRA imewashindwa kabisa hawa watu wanaotuma SMS za kitapeli au kuna nini kinachoendelea?

    eti wakuu Kunani hapa? Mbona bado hizi meseji za ajabuajabu zinaendelea kutumwa licha ya mabiti yanayopigwa kila mara na hawa jamaa wa TCRA? Kwanini hawafungiwi hawa watu?
  5. TCRA tunaomba mtusaidie Wananchi wenu, kuna mitandao ya simu kila ukiweka salio la fedha unatafutwa na namba ngeni

    Serikali ya Tanzania kupitia TCRA tunaomba mtusaidie Wananchi wenu, kuna mitandao ya simu (..) kila ukiweka salio la fedha unatafutwa na namba ngeni Kuna mitandao fulani ya simu kila ukiweka salio la fedha katika account yako au ukitumiwa pesa unatafutwa na namba mpya yenye viashiria vya...
  6. P

    TCRA mnahamasisha jamii kuchangamkia fursa za uchumi wa kidigiti wakati mnaongoza kukandamiza raia mtandaoni!

    Wakuu, Feb 6 Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Jabir Bakari alisema dhima ya serikali ni kuhakikisha jamii inanufaika kwenye uchumi wa kidigiti, uchumi ambao shughuli zote zinategemea TEHAMA, na kwamba ili tuweze kunufaika ni lazima tutengeneza jamii yenye fursa ya kutambua fursa zinazopatikana kwenye...
  7. TCRA matapeli wa tuma kwa namba hii dawa yao ni moja tu Ban NIDA iliyosajili hizo namba, pamoja na ku Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA

    TCRA matapeli wa tuma kwa namba hii dawa yao ni moja Ban NIDA iliyosajili hizo namba, pamoja na ku Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA TCRA chukueni ushauri wangu mtateketeza matapeli wote ndani ya miezi mitatu Swala la utapeli wa meseji za tuma kwenye namba hii ni kama limewazidi akili...
  8. S

    kwani TCRA hawawezi kuangalia namna ya kuzuia namba mpya kutuma ujumbe kwenye namba ambayo haijawahi kuwasiliana nayo??

    Kumekuwa na hili swala la kupokea sms mfululizo kutoka kwa namba zisizojulikana, yaani ukikaa kidogo utaona mara "iyo hela tuma kwa namba hii" mara "mzee nani nani anatibu mvuto, pete ya nini sijui" hujakaa sawa mara "jiunge na chama chetu" mara " mimi mwenye nyumba wako" na nyingine nyingi...
  9. TCRA wafungie ama wasifungie Simu Feki? Kariakoo na Makumbusho imejaa Simu za "kimarekani" na "Korea" feki!

    Wauza simu wa Kariakoo mtaa wa Aggrey , Makumbusho na Mwenge wanaongoza kwa kuuza "copy" ya simu halisi! Hawa wauzaji wanachanganya na simu original na feki kuhadaa wanunuzi ambo wengi wanatoka mikoani na kuamini ni original. Simu yeyote ukikuta ina ki-dude kama maskini tape na haipo kwenye...
  10. K

    TCRA pigeni faini Mpesa na Airtel kwa kushindwa kutoa huduma kwa wateja tangua juzi. Wananchi wanashindwa kuburudika na sikukuu

    Wadau mitandao ya Airtel na Voda ina sumbua wateja sababu haiwezi kupokea pesa kutika Bank nk au kutuma pesa Matokeo yake wananchi wanakula sikukuu kwa shida. TCRA piga fain au fungueni Hawa jamaa kwa siku tatu Hadi waingeze ubora na umakini. Vitendo wanavyofanya wanmzarau Rais Samia?.Mbona...
  11. Kamanda Muliro asisitiza Ulomi amekufa kwa ajali, asema ndugu sio TCRA

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesisitiza kuwa kifo cha mfanyabiashara Daisle Ulomi aliyetoweka katika mazingira yenye utata Desemba 11, 2024 akiwa kazini kwake Sinza Kijiweni, kimesababishwa na ajali na si vinginevyo. “Ukiniambia simu ilisoma wao ni watu...
  12. TCRA: Matapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" tumewapunguza

    Vitendo vilivyoripotiwa vya ulaghai kwenye mitandao ya simu vimepungua kwa asilimia 28 kati ya Juni na Septemba mwaka huu, kutokana na hatua kali za serikali na kampeni za kuongeza uelewa wa watumiaji. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt Jabiri Bakari, alifichua...
  13. Apigwa faini ya milioni 5 kwa kutumia laini ya simu iliyosajiliwa na jina lisilo lake

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Ernest Lwila (30) kulipa faini ya TSh5 milioni au kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani, baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine. Pia, mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa huyo...
  14. 0

    Ipi sababu ya TCRA kuomba maoni ya wanachi kwa ujio wa Starlink? Hii haiwezi ikawa njia ya kuikataa?

    Nimeona huko TCRA wanaomba maoni ya wanachi kwenye kupitisha kibali cha Starlink kufanya kazi Tanzania Ipi sababu ya kufanya hivi na Je, hii haiwezi ikawa njia ya kuja kuikataa Starlink na kusingizia wananchi ndio wameikataa. Hatujawahi ona TCRA ikiomba maoni ya wanachi kwa makampuni kama...
  15. M

    TCRA ishirikiane na Shirika la Mawasiliano la Kenya kuwasaka matapeli hawa wa mitandaoni

    Ni wito kwa TCRA ishirikiane na Shirika la Mawasiliano la Kenya kuwasaka matapeli hawa wa mitandaoni. Huu utapeli wa mtandaoni umevuka mpaka kutoka kuwa wa Kitaifa sasa ni utapeli kimataifa. Namba za simu zifuatavyo ni baadhi ya zinazotumiwa na matapeli, +254794812691 (Alex Kairi), +254102269805...
  16. M

    TCRA simamieni namba za simu zilizosajiliwa zisipate usajili mpya

    Salam kwenu. Naona sasa imekuwa kero sana kwa makampuni ya simu kuamua kuzifanyia usajili upya namba simu kwa kigezo hazijatumika kati ya miezi 3 hadi 6. Leo nimemtafuta mtu kwa namba ta tigo ambayo tulikuwa tukiwasiliana kwa muda mrefu isipokuwa siku za karibuni. Naastaajabu anapokea mtu...
  17. H

    Jumbe za matangazo na taarifa za serikali zimekuwakero kwetu wateja TCRA jitafakarini

    Habarini, Kwakweli sasa imekuwa kero kwa jumbe za matangazo,promotion,taarifa,nk kutoka serikalini, makampuni, taasisi, wafanyabiashara,nk yaani kwa siku mmiliki wa simu/line anapokea zaidi ya jumbe 20. Kulingana na sheria ya mitandao huu ni usumbufu na kuingilia uhuru wa mteja kwani makampuni...
  18. TCRA: Utapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" umepungua sana nchini

    Akizungumza kupitia Power Breakfasta leo Oktoba 30, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma amesema "Kwenye utapeli kabla na baada ya zoezi la usajili wa laini za simu tofauti ipo kubwa sana. Ukiangalia ripoti ya Robo mwaka ya performance ya mawasiliano kwenye takwimu za mawasiliano...
  19. Kwa hiyo TCRA kazi yenu ni kuuza masafa tu?

    Huwa nawatazama kwenye tv mmenawiri mnapendeza kweli. Mnaongelea masafa/frequency kila leo. Kuna ishu ya hawa wapigaji wa mitandao. Wapo wengi ila leo nitaongelea hawa wa mesejo za "ile hela tuma kwenye namba hii". Ni kero kero sana. Wapo pia wale wanaopiga kujifanya wafanyakazi wa mitandao...
  20. Polisi yakiri changamoto za Mikopo Mtandaoni, TCRA yajiweka kando yasema "haituhusu"

    UCHUNGUZI wa Nipashe umebaini baadhi ya namba za simu zinazotumika kudhalilisha wakopaji hazina utambulisho wa Tanzania, yaani ZIP CODE +255. Katika ufuatiliaji wake, mwandishi alibaini kuwa kwa siku mtu mmoja anaweza kupigiwa simu na watu 10 tofauti wakizungumza jambo tofauti juu ya mkopo...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…