tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Mau

    Hivi TCRA wanaitambua hii biashara ya Vodacom?

    Kuna kabiashara ka mkopo kameanzishwa na kampuni ya Vodacom, wanacharge riba pamoja na processing fee. Swali nililojiuliza ni mbona sipati message za mgawanyo wa hayo mapato kwa serikali kama vile wanavyotutumia ukinunua voucher? You have received an overdraft of TZS.10,107.00 You will be...
  2. beth

    Naibu Waziri Nditiye aagiza TCRA kukagua mabasi yote yanayosafirisha vifurushi bila kuwa na leseni

    Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhakikisha wanasimamia na kukagua mabasi yote yanayosafirisha vipeto, bahasha na vifurushi bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka hiyo na kuwataka wanaofanya hivyo kuacha...
  3. Analogia Malenga

    TCRA yafichua utapeli mpya wa fedha mitandaoni

    Angalizo hilo limetolewa baada ya kuibuka kwa kundi la watu waliobuni mbinu mpya kwa kutumia fursa hiyo kufanya utapeli jijini Mwanza kwa kuwashawishi kuwa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa unaendana na uhakiki wa akaunti ya benki ya mhusika...
  4. Nancyjoa13

    TCRA, NIDA waanika siri kukwama usajili laini

    BENJAMIN MASESE - MWANZA MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) zimeeleza sababu zilizochangia wengi kushindwa kusajili laini za simu zao kwa wakati. Zimesema hadi kufikia Desemba 31, mwaka jana, laini za simu zilizokuwa zimesajiliwa kwa njia ya...
  5. Miss Zomboko

    TCRA yazipiga faini kampuni za simu kwa kushindwa kutekeleza masharti ya huduma bora

    Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezipiga faini kampuni saba za simu baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya leseni na kukidhi viwango vya ubora wa huduma kwa mujibu wa Kanuni za Ubora wa Huduma za mwaka 2018. Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria wa...
  6. Kilele9

    TRA, NIDA na TCRA zishirikiane

    Viongozi na wataalamu wa TRA, TCRA na NIDA shirikianeni msiwe kama mpo nchi tofauti. Inavyoonekana hamuishauri serikali ipasavyo kwa kutokushirikiana kwenu. Serikali inapata kiasi kikubwa cha fedha kama kodi kupitia miamala inayofanyika kupitia mitandao ya simu. Kufungwa kwa laini za simu hata...
  7. MakinikiA

    TCRA mtakapofunga Simcard za watu mjiandae kulipa madeni ya kwenye simu

    Ebwana eee kwa yule anayeweza kukopa kwenye simu muda ndio huu kopa kopa kopa kwa bidii mlipaji yupo kwa maana fedha zipo pale TCRA za kulipa hayo madeni ,hakuna kampuni itakayokubali hasara kirahisi, Mpawa tu wana kama bilions of money hazijarejeshwa, ebwana wekeni mikakati kupata vitambulisho...
  8. Richard

    TCRA kufunga simu zisizosajiliwa ni mpango wa serikali kuwabana wale wanaotumia simu kusambaza habari za uzushi au fake news

    Habari za uzushi za kutekwa kwa mdhibiti mkuu wa fedha za serikali wa zamani Profesa Assad zimezusha taharuki kubwa. Na mpaka ilipoibuka video mitandaoni ambapo Profesa Assad anaonekana yupo salama na mwenye afya njema, watu wengi waliingiwa na hofu kubwa. Ifikapo tarehe 31 Desemba mwaka huu...
  9. Suley2019

    TCRA: Laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba za NIDA zitafungwa kufikia Desemba 31, 2019

    Mamlaka hiyo imesema kwamba hakuna laini ya simu itakayofungwa kabla ya tarehe hiyo. Aidha, imesema wananchi wanatakiwa kwenda kusajili laini zao kwa kutumia vitambulisho vya uraia, na kuthibitisha usajili huo kabla ya muda uliowekwa kwa kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya kuzifunga. Akizungumza...
  10. S

    Hivi TCRA wanaweza kutupa sababu za msingi kwa nini bei ya internet Tanzania ni zaidi ya mara kumi ya bei ya internet Rwanda?

    Bei za internet ya wastani kwa Tanzania na baadhi ya nchi zinazotuzunguka ni kama ifuatavyo: Source: Worldwide mobile data pricing: The cost of 1GB of mobile data in 230 countries Reference: Worldwide Mobile Data Pricing League | Cost of 1GB in 230 countries - Cable.co.uk Hivi TCRA wanaweza...
  11. beth

    Serikali yazindua kituo cha Tehama Chato

    Serikali imesogeza huduma za mawasiliano kwa wananchi wa Chato kwa kuzindua kituo cha Tehama, Telesenta Chato mkoani Geita baada ya kukamilisha usimikaji miundombinu ya mawasiliano kituoni. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe jana alizindua kituo hicho cha Tehama ambacho...
  12. Return Of Undertaker

    Nape: Hoja ya Bunge live ilitoka nje ya Bunge na ilikuwa dhaifu. Bunge kwa sasa halina mvuto na wananchi wamelisusa

    "Sio mimi niliyezuia bunge Live, haukua uamuzi wangu. Bunge lenyewe liliunda kanuni za kuendesha matangazo yake. Lakini ukweli ni kuwa hatukutenda haki na watu wanalalamika sana. Kuhusu watu kutizama TV na kushindwa kufanya kazi hiyo hoja niliitoa mimi lakini ni kwa sababu za kisiasa tu. Ilikua...
Back
Top Bottom