tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Clark boots

    Kurasimisha namba na TCRA

    Wakuu, habari za mda huu. Nimekuwa nikipokea messages kibao kupitia simu yangu kuwa nirasimishe namba zangu zote za simu nilizosajiri kupitia kitambulisho changu. But kwa mujibu wa maelezo yao wanasema nipige *106# then nifuate maelezo Ila nimejaribu kufanya hvyo bado naona messages hazikauki...
  2. K

    TCRA hivi mmeshindwa kufuatilia YouTube channels contents zilizosajiliwa?

    Kwa kweli ni kichefuchefu, watu wanafanya promo kama hawana wazazi au ndugu, mbaya zaidi wana promote Sodoma na Gomora na vitoto sijui walikuja kufanya kazi za ndani wakaasi? Manake ni zaidi ya huyo anayewasimamia (mkuu wa mashetani) Hebu fuatilieni hii channel ya Ophoro Tube. Kwa kweli ni...
  3. kokudo

    Vodacom wanavyonitesa na kuonekana tapeli

    Ndugu Wasalam, Nimekua mteja wa kununua bidhaa mtandaoni mara kwa mara na mzigo wangu wa mwisho nimelipa kwa Mpesa MasterCard. Lakini Vodacom wameng'ang'ania hela yangu niliyoweka Mpesa MasterCard kumbe Card ime expire ila wao wakakubili pesa iingie nilipojaribu kuitoa IMEGOMA. Kinachoniuma...
  4. Influenza

    Uchaguzi 2020 Katibu wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Dkt. Philip Filikunjombe achukua fomu ya Ubunge Ludewa kupitia CCM

    Mwanasheria Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzaniania (TCRA) ambaye ni Katibu wa Kamati ya Maudhui inayofungia Vyombo vya Habari kwa kukiuka Kanuni za Maudhui mitandaoni, Dkt. Philip Filikunjombe amechukua fomu kuomba kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Ludewa
  5. Jidu La Mabambasi

    TCRA kazi ya kudhibiti muingiliano wa masafa imewashinda?

    Kazi moja kubwa ya TCRA toka wakiwa kitengo cha kudhibiti masafa ya kurusha mawimbi ya redio wakiwa Posta na Simu(TP &TC), ilikuwa kuangalia ni nani anarusha mawimbi yake katika masafa yepi. Sasa hivi tuna TCRA ambao siyo siri wana mitambo mikubwa na makini zaidi lakini wasomi hapo na mainjinia...
  6. gluckkcom

    TCRA tunaomba msaada tafadhali

    Sisi hatukufanya makosa kuitikia wito wa kusajili lain zetu kwa alama za vidole Ila makosa yanafanywa na mawakala ambao mmewaamini na kuwapa dhamana ya kutupatia huduma hiyo wananchi Wana dumplicate data za mteja wa awali na kuzitumia data hizo kuwasajilia wateja wengine sim card huku...
  7. Chachu Ombara

    Kwanza Online TV yafungiwa miezi 11, kwa kuchapisha taarifa ya Marekani

    Ni kwa kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta 2018 kwa kuchapisha taarifa ya Ubalozi wa Marekani TCRA imesema taarifa hiyo ilijaa upotoshaji na Kwanza TV waliichapisha bila kuzingatia mizania
  8. E

    Ushauri kwa makampuni ya simu nchini na TCRA jambo hili

    Baada ya sheria ya mitandao nchini kuanza kazi, na makampuni ya simu kuweka no 106 kama njia ya kuhakiki namba uliyosajiri kwa mfumo wa finger print. Basi nashauri hivi: ingekuwa vyema makampuni pamoja na TCRA wangeweka option ya mtu kuikataa namba ambayo anataka iondolewe ili kukidhi takwa la...
  9. Miss Zomboko

    Vituo vya habari vyapigwa rungu na TCRA kwa kurusha maudhui katika muda ambao watoto hawapaswi kuangalia ama kusikiliza

    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitoza faini ya Sh milioni 30 vyombo vya habari sita, kwa kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji ikiwamo redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa katika muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto. Mbali ya Clouds FM...
  10. JoJiPoJi

    TCRA yatolea ufafanuzi sheria ya umiliki wa laini moja iliyoanza kutumika leo

    Sheria ya umiliki wa laini moja ya simu kwa kila mtandao imeanza kutumika leo Julai Mosi 2020 ambapo ndio siku ya kwanza ya mwaka wa fedha wa serikali. Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja...
  11. Mwamuzi wa Tanzania

    TCRA inawaendesha wamiliki wa mitandao ya simu kadri watakavyo

    Walianza na kusajili line kwa alama za vidole, wamiliki wa mitandao wakaishiwa nguvu wakijua kuwa sasa mavuno yatapungua kwakuwa watumiaji (walaji) watapungua. Ashukuriwe Mungu watu wakawasajilia watu wao wa karibu maisha yakaanza kutengamaa. Sasa TCRA inapofosi mtu awe na line moja tu kwa...
  12. E

    Ukishangaa ya msanii wa vichekesho Idris Sultani utayaona ya baadhi ya makampuni ya simu. Eng Kamwelwe na TCRA tusaidieni

    Msanii idris sultan na mwezake walifikishwa mahakama ya kisutu kwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao, moja ya makosa waliyokuwa nayo ni pamoja na yeye Idris kutumia namba isiyo yake, na mwenzake alishtakiwa kwa kuruhusu line yake itumiwe na mtu mwingine. Nakumbuka mahakama ya Kisutu iliwapa...
  13. E

    TCRA Tanzania kwa haya yanayofanywa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa wateja wanaotumia simu janja yako sawa?

    TCRA tanzania, naomba mnisaidie kujua kama mambo yanayofanywa na kampuni ya simu ya vodacom tanzania nisahii! Nakama nisahii mtupe ufafanuzi, kama siyo sahihi mkomeshe jambo hili na muwaagize warudishe gharama tulizotumia katika huduma ambayo kimsingi ni haki kwa mteja kuipata bila gharama...
  14. Mzukulu

    TCRA kama bado mna Meno yenu Makali natumaini hiki nilichokisikia leo kutoka Wasafi FM mtawaadhibu upesi

    Nina uhakika kuanzia Sheria za nchi na hata za Utangazaji hadi zenu nyie TCRA haziruhusu Kituo chochote kile cha Redio kupiga Wimbo ambao / Nyimbo ambazo ndani yake kuna Matusi makubwa makubwa yanatajwa hata kama hayatajwi kwa Lugha ya Kiswahili na yanatajwa kwa Lugha ya Kiingereza ambayo bahati...
  15. mgt software

    TBS na TCRA mmeruhusu wizi, watu wamepata hasara

    Wana JF, Katika serikali makini TBS na TCRA wametuangusha sana kwa kuruhusu wizi wa kichina. Anavyokuwa: watu ambao hawana fani yeyote ya ufundi, wamevamia mitaa na kulaghai watumiaji wa smart phone kuwa wanatengeneza kioo cha simu kwa kuweka liquid ambayo inakifanya kiwe imara, kwamba...
  16. J

    Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

    Akizungumza katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari mwandishi nguli Pascal Mayalla amewataka TCRA kuwafuatilia wale wanaoandika uchafu kwenye mtandao wa Twitter na kama wameshindwa basi waufungie mtandao huo hapa nchini. Na kama hayo yote hayawezekani basi Watanzania wazalendo wajulishwe...
  17. I

    TCRA imulikeni Airtel

    Huu mtandao wa Airtel ni muda wa zaidi ya wiki sasa mawasiliano yake yamekuwa mabovu sana. Unapiga huwezi kusikilizana kabisa kwani simu aidha ikatike au ikorome kama redio iliyokosa mawimbi . Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua kwani ni sawa na kuibiwa pesa zetu za vocha huku tukikosa...
  18. M

    TCRA na TRA, mchezo wa Vodacom mnada poa si sahihi kwa uchumi wa nchi

    Kuna mnada umeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa wateja wake ambapo ili kushiriki inabidi utoe kiasi cha Tshs. 500 kama kiingilio. Kisha wanaweka dau la kupata rice cooker kwa kima cha chini lakini ukijumlisha hizo 500/- wanazotoa ni hela nyingi sana . Hii ni kama bahati nasibu lakini voda...
  19. Vodacom Tanzania

    Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

    Ndugu mteja, Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu? Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi. Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya: - Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika...
Back
Top Bottom