tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. SAYVILLE

    Ni kituo gani cha Television kilipigwa faini na TCRA wakati wa uchaguzi?

    Kuna taarifa naifanyia kazi sasa nahitaji baadhi ya information muhimu. Ningependa kujua, wakati wa kampeni kuna kituo cha television kilirusha matangazo ya BBC yaliyojumuisha taarifa fulani nadhani kuhusu Tundu Lissu. Kile kituo kilipigwa faini nadhani ya milioni 20. Ningependa kujua kituo...
  2. Kelela

    Naomba Ufafanuzi Online Content Regulations za TCRA

    Habari wa taalamu, Regulation iliyotolewa na TCRA kuhusu uhitaji wa leseni ya maudhui mtandaoni imesema ni kwa wale wanaotoa Predominant Content, ambayo si chini ya 85% kwa wiki. Hii ina maana gani? Naomba ufafanuzi zaidi kutoka kwa Wanasheria. Nimeambatanisha na sehemu inayotaja hiyo...
  3. D

    Vipindi vya Mashamsham, Mgahawa na SportsArena vimesheheni Waropokaji; TCRA ni waungwana sana vinginevyo wangeshavifutilia mbali

    Tunapozungumzia uthubutu; Tusisahau kuthubutu bila kuzingatia kanuni (Ethic's) katika kazi husika! Wamiliki wa Wasafi wamethubutu na wanania njema ya kuleta mabadiliko kwenye media lakini malengo yao yataendelea kuwa butu kutokana na aina ya baadhi watangazaji wanaowaajili kushindana kuropoka...
  4. W

    Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?

    Habari, Kuna clip moja nimeiona kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha mtu mmoja ambaye bila shaka alikuwa ni kiongozi wa tour ya jana ya WCB ya tumewasha na tigo waliofanya jijini Dododma akiomba radhi ya jambo linaloonesha sio la kiungwana na lisilokuwa na stahala lililofanya na "Msanii"...
  5. Elius W Ndabila

    TCRA, nawaombea msamaha Wasafi TV

    TCRA NINAUNGANA KUWAOMBEA RADHI WASAFI TV. Na Elius Ndabila 0768239284 Leo TCRA wametoa mvua ya miezi sita kwa Wasafi TV kwa kile kinachosemekana ni kurusha maudhui kinyume cha sheria. Niwapongeze TCRA kwa kusimamia sheria hizi kwa uangalifu na nidhamu kubwa. Tunajua kuwa sheria ni msumeno...
  6. Replica

    RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

    TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha kurusha matangazo kwa miezi sita kuanzia leo kutokana kwa kukiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui ya utupu. Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money akicheza...
  7. mgt software

    Nikusaidie Waziri Faustin Ndugulile kudhibiti TCRA, TRA na TBS juu ya vifaa vya telecom feki

    Jf oyee Kwako Dkt. Ndugulile, vyombo hivyo Hapo juu vimekuwa vikilalamikiwa kwa kutokuwa makini, kweli vyombo hivi vinatumia gharama Kubwa kuwepo huku ufanisi Wa kazi upo chini sana. Nikianza na TRA, hawa wanaruhusu kuingia kwa vifaa ambavyo havina certificate of compliance. Hi yo kuruhusu...
  8. Miss Zomboko

    TCRA yapewa miezi mitatu kumaliza changamoto za bando na vifurushi zinazotolewa na kampuni za simu za mkononi kwa wananchi

    Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile ametembelea TCRA na kuipa miezi mitatu kumaliza changamoto za bando na vifurushi zinazotolewa na kampuni za simu za mkononi kwa wananchi kwani hawana imani na vifurushi vya intaneti. Pia, Waziri Ndugulile ameiagiza TCRA...
  9. robinson crusoe

    TCRA achieni Twitter yetu! Tunaojitambua tunaihitaji kwa elimu yetu

    Tuko mikoani tukilamba x-mas yetu lakini tunataka kuwa connected na dunia. Tangu iliposikika kwamba kuna video ya ngono ya wanasiasa wawili, twitter haiko hewani. Tunahangaika kupitia njia za panya ili kuwasiliana na kusoma mambo ya muhimu. Hii kufunga funga itaendelea hadi lini wakati kuna...
  10. Z

    Mtandao wa Smile ni kweli na nyie mmeanza wizi?

    Ukatikaji wa mawasiliano katika mtandao wa smile kwa sasa limeanza kuwa jambo la kawaida sana. Kila wakati mtandao wao unapotea hewani na hawatoagi feedback yoyote unaporudi kwa wateja wao. Ila pia kinachokwaza ni wizi unaoendelea kwa hivi sasa. Kwa mara kadhaa umeshawahi kupotea na bundle za...
  11. KAGAMEE

    Uozo Vodacom na TCRA

    Morning wakuu!Naomba niende kwenye mada yangu moja kwa moja. Siku ya jumatatu tarehe 30/11/2020 niliishiwa muda wa maongezi na nikaamua kujiunga kifurushi cha TSH 2,500/ ambapo nilipewa dk50 kwenda mitandao mwingne na dk180 voda kwenye voda tu. Maana yake nilikuwa na jumla ya dk230,cha...
  12. Kelela

    Msaada: Leseni ya Maudhui ya Mtandaoni TCRA

    Wataalamu naomba kujua, Kama una YouTube Channel na Blog ambayo maudhui yake yanafanana na Channel. Je unatakiwa kusajili leseni mbili tofauti? au Ni leseni moja tu inajitosheleza? Maana leseni kwa mwaka ni Tsh 500,000 - 1,000,000
  13. Miss Zomboko

    Watu 2 wahukumiwa kwa hatia ya kusambaza Huduma ya Internet bila kibali na kuisababishia hasara TCRA

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu Mhandisi Baraka Mtunga (43) na Rajabu Katunda (42) kulipa faina ya Sh. Milioni 1.5 kwa kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza Huduma ya Internet bila kibali na kuisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zaidi ya Sh...
  14. mgt software

    Kushindwa kwa TCRA kudhibiti Simu feki ni ushahidi kuwa TRA na TBS zimesinzia Kabisa

    Wana JF, Vyombo muhimu vya serikali vyote kwa pamoja vimeshindwa kudhibiti Simu feki hivyo kuongezeka kwa uharifu pamoja nakuikosesha serikali mapato. Kazi ya kudhibiti bidhaa feki ni ya TBS kazi ya kukagua uingiaji bidhaa halali kutoka viwanda vinavyotambulika na kutoza kodi ni TRA. Tra...
  15. Roving Journalist

    Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) yatembelea Ofisi za Jamii Forums

    Kamati ya Maudhui ya TCRA ikiongozwa na Makamu Menyekiti wake, Ndugu Joseph Mapunda, imetembelea ofisi za Jamii Forums ikiwa na lengo la kujifunza mambo kadha wa kadha kuhusu Taasisi na kujionea namna huduma inavyotolewa kwa wananchi. Kamati hiyo ilipokelewa na watendaji wa Jamii Forums...
  16. Jidu La Mabambasi

    TCRA, mmeshakuwa irrelevant

    Katika dunia hii ya teknolojia, alternatives to communication zinajitokeza kila uchao. Kwa sababu za kisiasa tu TCRA imeamua kuminya upatikanaji na upashanaji wa habari kwa waTanzania. Hili ni kosa la kimsingi, kwa sababu yoyote ile. Teknolojia hailali, watu wamekwisha anza kutumia njia...
  17. Suley2019

    LHRC yawataka TCRA na Makampuni ya Mawasiliano kutoa ufafanuzi kuhusu hali ya kukatika kwa mtandao nchini

    Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Makampuni ya Mawasiliano ikiwamo TTCL, Vodacom, Tigo, Airtel kutoa taarifa rasmi kwa wateja kufafanua kuhusu changamoto inayowakabili watumiaji wa mitandao.
  18. M

    Uchaguzi 2020 TCRA, hamuwaoni TBC wanavyopiga kampeni wazi siku ya Uchaguzi?

    Kwa wote mnaoangalia TBC, wana “Mchambuzi wa Masuala ya Siasa” anamwaga sifa kemu kemu kwa Dkt. Magufuli ambaye ni mgombea Urais kupitia CCM. Mchambuzi wao huyu anaonekana wazi kuwa amekuja kuhamasisha watu kumpigia kura Ndg. Magufuli na mbaya zaidi anamkandia Mzee Mwinyi na kueleza mazuri ya...
  19. Kirchhoff

    TCRA mnaniharibia Kazi kuzima mitandao ya Kijamii. Mitambo ya Kiwanda inakufa

    Hakika Kitendo chenu Cha kuzima WhatsApp kimeniuzi na kuniumiza sana. Nimepata hitilafu kwa mitambo ya kiwanda. Nikiwa napokea maelekezo ya Nini cha kufanya kupitia Whatsapp ghafla mmeifungia. Mmenipa hasara kubwa sana. Ninyi mngeacha WhatsApp. Mtu akivunja sheria mumuadhibu.
  20. Komeo Lachuma

    TCRA huu wizi wa Makampuni ya simu mbona mmeufumbia macho? Angalieni Airtel

    Wananchi tumekuwa tukilalamika sana kuhusiana na wizi unaofanywa na mitandano ya simu. Mmeziba masikio yenu kwa Vigondo. Hamsikii.Na macho yenu mmeyavalisha miwani ya Mbao. Hamuoni. Airtel kwanza wana utaratibu ambao mimi nmeshindwa uelewa.napotaka kuangalia data bundle iliyobaki sipewi majibu...
Back
Top Bottom