tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. R

    DG Mpya wa TCRA, hili la exorbitant prices za vifurushi litakuondoa kama hukulitatua kwa umakini

    Sasa DG mpya usipoyatafutia ufumbuzi utatumbuliwa within no time haya matatizo hapa chini, nawe utatumbuliwa. Ujue kuwa huyu ameondoka kwa matatizo haya chini! 1. Kwa muda mrefu wateja wa simu wamelalamikia wizi wa makampuni ya simu kwa wateja, mara zote James Kilaba umetia pamba kwenye...
  2. R

    Nina courage ya kuwapigia: Naomba namba ya Ndungulile na DG wa TCRA

    Naomba namba ya Dk Ndungulile na DG wa TCRA niwapigie. Naongea nao kwa wema tu na kumpa hoja yangu kuhusu makampuni yaliyogoma kutekeleza amri ya TCRA
  3. Mukulu wa Bakulu

    Mfanano wa TCRA na EWURA

    Ewura mafyta yakishuka leo kwenye soko la Dunia Tanzania inaweza kuchumua wiki 2 kushusha ama kutoshusha kabisa, utaambiwa bado kuna shehena ya zamani lakini mafuta yakipanda leo jioni tu unawaona wanapandisha bei, unajiuliza kwani shehena ya zamani yenyewe imeisha ghafla? TCRA wakiambiwa...
  4. Idugunde

    Vifurushi vya Data: TCRA yasema mfumo wa zamani unaweza kurudi ndani ya siku nne

    Mkurugenzi mtendaji wa TCRA amesema kuwa sababu kiufundi zitasababisha ichukue siku nne kurejesha mfumo wa vifurushi wa awali
  5. M

    Makampuni ya simu yadharau agizo la Serikali (TCRA)

    Mpaka sasa hivi makampuni ya simu yanaendelea kuuza vifurushi kwa bei ileile onevu ambayo ililalamikiwa na wananchi hapo jana. Licha ya Serikali kupitia TCRA kuagiza usitishwaji wa viwango hivyo, bado makampuni hayo yamekaidi na yanaendelea 'kuwaibia' wananchi kwa kuuza bando kwa bei ambazo...
  6. M

    TCRA na Waziri Ndugulile, wanyonge mliotuumiza jana tunahitaji tu kupata majibu ya haya maswali yetu

    1. Baada ya Kuamuru jana kuwa Vifurushi vya zamani virejeshwe na viendelee je, ni Saa ngapi hilo litafanyika kwani mpaka sasa bado havijabadilika? 2. Je, wale ambao Jana walinunua Vifurushi vyenu vya Ukatili na Kutukomoa mtawasaidiaje na kuwafidia kutokana na Upuuzi wenu? 3. Ni saa ngapi...
  7. B

    TCRA; Rais anatumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na wananchi. Kuendelea kuzuia mitandao ni kimhujumu yeye na sisi wananchi

    Mhe. Rais anatumia akaunti zake za mitandao ikiwemo Twitter kuweka video na maelekezo mbalimbali kwa ajili ya wananchi hasa wale ambao hawakupata muda kumsilikiza live. Ili tupate taarifa hizi lazima mitandao iwe inafanya kazi la sivyo Kama mitandao itaendelea kuzimwa Mhe. Rais hatoweza kutimuza...
  8. Ndebile

    TCRA imulike hujuma inayofanywa na Star TV (Kisimbuzi cha Continental)

    Wamefunga channel za bure kama TBC1, nk. kwa muda sasa, mwanzoni walikuwa wanazifunga kwa siku za mwisho wa juma na kuzifungua Jumanne ila sasa naona kwasababu ya ukimya wenu wamezifunga kabisa na hivyo kuwanyima Watanzania habari ambayo ni haki yao. Tunaiomba TCRA hawa watu wafuate masharti ya...
  9. C

    TCRA na Airtel Mtusaidie

    Katika hali isio ya kawaida mmefunga laini za mawakala zenye kutumia majina ya wakala wakuu kama NITAK LTD, bila ya kutoa taarifa. Mmezifunga laini zenye pesa zetu, tunaomba mtufungulie japo kwa siku moja ili tuzihamishe
  10. Idugunde

    Mwigulu Nchemba: Tunawafuatilia wanaopotosha na kuzushia viongozi vifo

    Waziri wa Katiba na Sheria amesema wanawafuatilia wote wanaozushia watu vifo. Na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Mpaka sasa kuna baadhi wameanza kushughulikiwa. Mh waziri hata watoto wa vigogo utawachukulia hatua?
  11. J

    TCRA wakomesha wizi wa kwenye mitandao tuma ujumbe kwenda namba 15040

    Endapo umetapeliwa au umetumiwa ujumbe wa utapeli, tuma ujumbe husika na namba ya aliyekutapeli au kukutumia ujumbe wa utapeli kwenda 15040. Huduma hii ni bure. Tushirikiane kutokomeza utapeli kupitia simu za mikononi. Sambaza ujumbe huu cc @TCRA_Tz @ConsumerCcc
  12. beth

    TCRA kudhibiti utoaji huduma za vifurushi kwa kampuni za simu

    Katika kukabiliana na malalamiko juu ya huduma ya vifurushi zinazotolewa na kampuni mbalimbali za simu nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetengeneza kanuni ndogo zitakazoratibu utoaji wa huduma hizo. Kuandaliwa kwa kanuni hizo kumekuja kufuatia maoni 3278 yaliyotolewa na...
  13. Cpp

    TCRA rungu lao lingekuwa linafika Kenya, wangeifungia Citizen maisha

    Hawa ndugu zetu Wakenya naona wameamua kuishika Serikali yetu sharubu kwa kutuita “Hamnazo”
  14. Sa 7 mchana

    TCRA: Laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri, Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama

    Ndugu Mteja, laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri ambalo Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama. I smell a fish juu ya laini hizi. Nitahakikisha sipotezi laini ilikuepuka kurenew laini nakuingia huku. -- MAMLAKA ya Mawasiliano...
  15. Analogia Malenga

    TCRA: Utoaji wa Leseni za Maudhui Mtandaoni umesitishwa hadi Juni 30, 2021

    Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo akizungumza kwenye Usiku wa Waandishi wa Habari na Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza. Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) imetangaza kusitisha utoaji wa leseni za Maudhui Mtandaoni kwa muda kuanzia...
  16. Replica

    TCRA wajifunze kwa Waingereza, kampuni ya simu yalambwa bilioni 33 kwa kuwaongezea gharama wateja

    Pamoja na agizo la waziri mwenye dhamana ya mawasiliano kuitaka mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano nchini(TCRA) kudhibiti gharama za mawasiliano bado wameonekana kugonga mwamba huku kampuni za simu zikiweka pamba masikioni. Uingereza sehemu kubwa ya gharama ya mawasiliano ni kwa bili na moja ya...
  17. Granite

    Vodacom Kulikoni? TCRA hebu tuokoeni na hizi gharama za Data

    Nilizoea kujiunga Vifurushi vya aina mbili vya wiki 2Gb kwa Tsh.3,000/= au 4Gb kwa Tsh.5,000/= Leo nimekutana na hali tofauti, 1Gb kwa 3,000/= na 2GB kwa 5,000/= kwa kweli nimechanganyikiwa kidogo hasa ukiangalia hali tunayoipitia mtaani. Mbona hii mitandao imekuwa na upandishaji wa gharama...
  18. Elius W Ndabila

    Hawa wanaofanya uhalifu mitandaoni wako juu ya TCRA?

    HAWA WATU WAKO JUU YA TCRA? NITUMIE KWENYE NAMBA HII 0657523389 Na Elius Ndabila 0768239284 Itakumbukwa kuwa tuliambiwa kuwa watu wamekuwa wanatumia simu kufanya uhalifu kwa kuwa hakukuwa na namna nzuri ya usajili wa laini zetu. Kwa kutambua hilo serikali iliweka mkazo kwa kila Mtanzania...
  19. B

    Naibu Waziri wa TEHAMA, Kundo Andrea ashauri TCRA kuanzisha mitandao yetu ya kijamii tuachane na Twitter, FB, YouTube n.k

    Kuelekea uchumi wa kidigitali Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeitaka mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kufikiri namna ya kutoa fursa kwa waTanzania wenye uwezo wa kuanzisha mitandao ya kijamii ya ndani ya nchi ili kukuza uchumi na usalama wa nchi. Naibu...
Back
Top Bottom