tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Travis 1

    WhatsApp, Facebook na Instagram zatoweka hewani Oktaba 4, 2021

    Au tatizo hili ninalo mimi tu? ---Update---
  2. Mtini

    Watendaji wa TCRA na makampuni ya simu yanashirikiana na matapeli kutuibia wananchi?

    TCRA walituambia baada ya usajiri wa alama za vidole utapeli wa tuma fedha kwenye namba hii utaisha kwani watu hao itakuwa rahisi kuwatambua. Kitu za kushangaza hili suala bado linaendelea, TCRA na makampuni ya simu yanashindwa nini kuzifunga hizi line ikiwa ni pamoja na kuwakamata hawa jamaa...
  3. N'yadikwa

    TCRA yatoa onyo kali kwa Kampuni za Mabasi kuhusu usafirishaji vipeto. Wapewa muda kujisajili

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa Kampuni za Mabasi ambazo zimekuwa zikisafirisha vipeto bila kuwa na Leseni. Wamepewa muda hadi Oktoba wawe wamejisajili la sivyo kitanuka.
  4. Red Giant

    Mpesa inakataa kutuma pesa tigo pesa, TCRA waangalieni hawa voda.

    Siku nyingi. Nikijaribu kutuma pesa kutoka Mpesa kwenda Tigopesa inakataa. Inarudiarudia kusema niweke namba ya siri hata mara kumi. Nahisi Voda wanafanya hili makusudi, labda wana bifu na Tigo. Maana hata kununua airtime tigo kwa kutumia Mpesa haiwezekani. Kama wana bifu, basi linatukwamisha...
  5. J

    Dkt. Ndugulile: Kuanzia sasa ni namba 100 pekee itatumika kwa mawasiliano kati ya Kampuni ya simu na Mteja wake

    Waziri wa Tehama Dkt. Ndugulile amesema kuanzia sasa ni namba 100 pekee itatumika kwa mawasiliano ya kampuni ya simu na mteja wake. Hii ni katika lengo la kuondoa utapeli na wizi na kwa maana hiyo namby za kawaida haziruhusiwi kutumika.
  6. B

    Website za ngono zimefungiwa Tanzania?

    Nasikia website za ngono zimefungiwa Tanzania, kama ni kweli basi na support Kwa asilimia 100 uamuzi huu wa serikali maana siku hizi watoto wanajua kuchezea simu sana. Licha ya hiyo, itasaidia vijana wengi kupunguza addiction ya picha hizi maana wameathirika wengi kisaikolojia. Nashauri...
  7. mshale21

    Idris Sultan, wenzake wafutiwa mashtaka na mahakama

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi na kumwachia huru msanii wa vichekesho, Idris Sultani na wenzake wawili baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) akielezea mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo. Sultan na wenzake walikuwa wanakabiliwa na shtaka moja...
  8. Hismastersvoice

    TCRA imewashindwa matapeli wa mitandao imewageukia raia wema!

    Tarehe 06/11/2019 nilisajiri laini yangu ya AIRTEL na kupewa namba ya usajiri, tarehe 19/07/2021 laini yangu ya AIRTEL ikafungwa kwa madai ya kutosajiriwa! Nikalazimika kwenda kwenye ofisi za AIRTEL na nilichoambiwa huko ni maluweluwe eti siku mbili zilizopita nilisajiri laini kwa alama za...
  9. J

    TCRA yazindua mfumo ulioboreshwa wa utoaji wa leseni mtandaoni

    TCRA YAZINDUA MFUMO ULIOBORESHWA WA UTOAJI WA LESENI MTANDAONI. Leo 31 Julai,2021. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefanya uzinduzi wa Mfumo ulioboreshwa wa Utoaji wa Leseni kwa njia ya Mtandao. Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt...
  10. PureView zeiss

    TCRA mnajua usanii unaofanywa na DStv?

    Usanii huu wa DStv utaendelea mpaka lini? Leo wameondoa channel namba 228 (super sport variety) Kwa vile Tu mashindano ya Olympic yataanza kesho kutwa!! Huu sio uungwana na ni wizi wa mchana tena ni usanii mtupu, haiwezekani tumelipia kifurushi ambacho hiyo channel inakuwepo halafu ghafla...
  11. V

    SoC01 Ushauri: TCRA wafanye nini kumaliza tatizo la wizi wa simu

    Kuna vitu ni vigumu kuvisahau kwenye maisha yangu, vipo vyenye kufurahisha na vile vyenye kuleta maumivu moyoni mwetu. Jambo la kushukuru ni namna Mungu ameweka kitu kusahau ili maisha yaendelee, Mungu wetu ana nguvu sana. Mwaka 2019 ninaweza nikasahau matukio yote yaliyojiri mwaka huo lakini...
  12. Informer

    Tozo za Miamala: Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA - CCC) linataka maoni yako

    Wadau, tutiririke hapa au mnaonaje? Unaweza kusoma maoni ya wengine kupitia hii TAG on JF: tozo za miamala
  13. SankaraBoukaka

    TCRA na Wizara ya Afya, mnamsikia huyu daktari anayejitangaza kupitia Kiss FM 98.9?

    Jana Alhamisi muda wa saa 5 usiku hivi nikiwa natafuta Station za Radio nikaangukia Kiss FM 98.9, niliposikia neno "PID" ikabidi nisikilize kidogo kinachoongelewa maana nami nipo kwenye uwanja huo huo wa mambo ya Afya.. Nilipigwa na bonge la mshangao kwa yale niliyokuwa nikisikia,, maana...
  14. Nelson Kileo

    TCRA ingilieni hili tatizo la mitandao ya simu kuchelewa kurudisha miamala waliyoikata kimakosa

    Imekua ni kawaida na mazoea sasa endapo mtandao wa simu utakata kimakosa fedha kwnye akaount yako utaona kabisa wanakuoa mda wa masaa 74 hadi 96 na pengine hata week nzima kwa wao kurudisha pesa yako. Kumbuka hapa mtumiaji yaani mteja alikua na matuzi immediatlly ya pesa hizo lakini wao bila...
  15. Vanlizerfx__

    Huu wizi TCRA hawajawahi kuusikia au kuna ujanja unafanyika?

    Kama uliwahi kuweka vocha kwenye simu yako alafu ukakuta ile hela uliyoweka haipo na wala hujaitumia, ulishawahi jiuliza inaenda wapi nini kifanyike ili kuzuia wizi wa namna, nini kinafanyika kuzuia wizi wa aina hiyo. “Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wanapoteza pesa kujiunga...
  16. Dive

    Hivi TTCL na TCRA wanashindwa kuzuia matapeli kwa njia ya simu?

    Kiukweli inasikitisha sana Kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ilielekeza lines zote za simu zisajiliwe Kwa kutumia vitambulisho vya NIDA ilu ktambua watumiaji na kuepusha uhalufu lakini leo hii lines za simu hasa hasa za TTCL zinatumika sana kutapeli watu. Kumekuwa na ongezeko la...
  17. K

    TCRA mmeridhika na wizi wa vifurushi unaofanywa na Vodacom? Kifurushi Cha 1.2GB kinaisha less than 24hrs for normal chatting?

    Makampuni ya simu Uhuru na mamlaka mnazojitwalia za kuwaibia wananchi kwa kutukomoa au kurejesha fedha za hasara mlizopata kipindi Cha nyuma si sahihi. Nimejiunga kifurushi cha wiki 1.2GB cha Vodacom jana saa sita kasoro usiku. Then nikazima data hadi saa nne asubuhi. Nimewasha data since saa...
  18. Kasomi

    TCRA: Ripoti utapeli kwenye namba 15040

    Mamlaka Ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaomba wanachi kuripoti utapeli wowote unao fanywa kwa njia ya mitandao kwa kutuma aina ya message na namba iliyo tumika kufanya utapeli kwenye namba 15040. Utapeli huo ni wa Aina yeyote hata ule unao andika "...Ile pesa itume kwenye namba..." Au...
  19. masopakyindi

    TCRA Taasisi ya umma inayowakandamiza wadau wake kwa makusudi

    Kwanza nianze kwa kuliweka wazi, namfahamu jamaa yangu wa karibu aliyewekeza kwenye FM Radio. Ni bora Mama Samia naye kalizungumzia tatizo la FEES a TCRA , tozo ambazo ni za juu mno bila sababu yoyote. FEES za mwaka ni Dola $3,070 (na zaidi ya hapo kwa leseni ya kanda au Taifa) na ukichelewa...
  20. GENTAMYCINE

    TCRA mebariki Tangazo linalorushwa Clouds FM lenye Sauti iliyoigizwa ya Dkt. Kikwete ikisema "Tukutane kwa Mpalange Kumenoga?"

    Baada ya nyie Kuwakataza wasiendelee kutumia Kauli fulani ya Rais Samia kama 'Kibwagizo' chao sasa wameamua kuja na Sauti ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Kikwete (iliyoigizwa) ikihamasisha Wasikilizaji tukutane kwa Mpalange na kwamba huko ndiko 'Kumenoga' kwa sasa. Hapa GENTAMYCINE nimejikuta...
Back
Top Bottom