tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. AbuuMaryam

    Betting ni biashara inayolipa, mpaka radio zimeamua kuachana na malengo ya msingi zimehamia huku. TCRA mpo kimya tu

    Radios na TVs ila Radios sana sana, yaani ukifungua tu unakutana na tangazo la kamari. Kama zamani ilikuwa matangazo ya waganga wa kienyeji. Sasa hivi Radio zimeamua zichezeshe zenyewe michezo hii. Hii biashara inaonekana kulipa sana. Sijui tunatengeneza kizazi cha aina gani? Ukifungua hapa ni...
  2. I am Groot

    TCRA ni kati ya vyombo vya kiserikali vyenye kujiendesha kienyeji sana.

    Ni aibu kuona chombo kikubwa kama hiki ndani ya serikali kikiendeshwa bila weledi na sembuse kisichopenda kuwajibika litokeapo kosa kati ya matawi inayoyasimamia. Mfano hai ni hiki kinachoendelea sasa kwenye mgogoro kati ya watoa huduma na wateja juu ya upandishaji holela wa bei za data...
  3. JanguKamaJangu

    TCRA, BASATA zafungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft Zuchu - "Watasubiri Sana"

    Mamlaka ya wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeufungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz na Zuchu unaoitwa "Watasubiri Sana' baada ya kupata taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwa wimbo na video hiyo inaleta ukakasi kwa waumini wa dini na dhehebu fulani. Wimbo huo unafungiwa...
  4. Mwande na Mndewa

    Tanesco na tenda kwa kampuni binafsi; TTCL na kampuni binafsi za simu kuanzishwa TCRA

    TANESCO NA TENDA KWA KAMPUNI BINAFSI;TTCL NA KAMPUNI BINAFSI ZA SIMU KUANZISHWA TCRA. Leo 12:15pm 03/05/2022 Tanesco wameazimia kuongeza ufanisi na kasi katika kuunganisha umeme kwa wateja,Tanesco itaanza kutoa tenda kwa kampuni binafsi kufanya kazi hiyo huku wao wakijikita kwenye uzalishaji...
  5. JanguKamaJangu

    TCRA inachunguza mabadiliko ya mabando ya simu yaliyofanyika kimyakimya

    Baada ya malalamiko mitandaoni kuwa kampuni za mawasiliano ya simu Nchini Tanzania zimefanya mabadiliko ya kushusha vifurushi vya huduma za intaneti (mb's) pasipo kutoa taarifa kwa wateja wao, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema inafuatilia. TCRA imesema: “Tumeona malalamiko kutoka...
  6. D

    Serikali (NEMC na TCRA) kuna pesa za bure hapa wala msijiulize mara mbili

    Kila idara ya serikali siku hizi ina vyanzo vya mapato! Ndungu zangu NEMC naona bado wamelala usingizi wa pono wakati kuna pesa kibao za kuokota! 1. Sheria na kanuni za mazingira ziko wazi kabisa! Hivyo basi! Nashauri NEMC ianze kutoza kodi ya spika na miziki mikubwa katika kumbi na taasisi...
  7. JanguKamaJangu

    TCRA: Tumia simu vizuri, ukimdhalilisha mwanamke mtandaoni jela inakuhusu

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaonya watu wanaofanya vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake mitandaoni, ikisema kufanya hivyo ni kosa la kihalifu kwa mujibu wa sheria za nchi na kunaweza kumpelekea mtu kutozwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja. Wito huo umetolewa hivi...
  8. N

    TCRA /COSOTA au Mamlaka zinazohusika hamuoni tamthilia ya BONDITA Azam two unavyoharibu watoto kwa kuhamasishwa ndoa za utotoni.?

    -Hao waigizaji wakuu Bondita na mumewe mbona wanatofautiana sana umri. -Watoto wanajifunza nini wakiona mtoto mwenzao analiita baba zima ''mumewangu'' -watoto wadogo wanawaza kuolewa kuliko hata homework -Na Mamlaka zinazohusika mpo tu,, sasa mna msaada gani kama tatizo kama hili hamulioni? -Ee...
  9. Mwanga Lutila

    TCRA, Vodacom wanatukata 200 kila tuongezapo salio za nini?

    Hii sasa kwangu ni mara ya tatu, Sijawahi kopa Ila nashangaa kila nikiweka salio. Sina huduma yoyote ambayo nimejiunga. Huu ni wizi.
  10. Analogia Malenga

    TCRA: Kasi ya internet inasababisha kifurushi kuisha haraka

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja vitu vitatu vinavyosababisha kuisha kwa bando haraka ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kasi ya internet, uwezo wa simu janja na kuwa na application nyingi kwenye simu. Pia imesema gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini...
  11. Ego is the Enemy

    TCRA hivi mpo kwa ajili yetu ama? Waziri wa Mawasiliwano tusaidie hili

    Habari zenu wanajukwaa. Ninaomba hili suala limfikie mwenye dhamana na haya Mambo yanaboa Sana. Unanunua kifurushi wanakupangia muda wa kutumia. Mfano hapa nimeshajiunga sms za shs1500 kwa Airtel sms 9000. Shida mpaka napangiwa sms za kutuma kwa siku hivi kweli hii ni uungwana ama wao...
  12. BUMIJA

    Naomba Msaada wa kutoa taarifa ya utapeli

    Hii namba kapiga huyu jamaa akijifanya ni Airtel Customer Care na kuniambia amekosea kutuma hela laki moja. Huku akaunti yangu haina hiyo hela. Naomba mnisaidie kumripoti TCRA mnaojua, kanitukana sana nlipomgundua.Namba za Tapeli ni 0683595613
  13. John Haramba

    Picha aliyoposti Makonda siku moja baada ya Mahakama kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani

    Siku moja tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na kuubandika wito huo katika Makazi yake ya Dar na Kijijini kwao Koromije, Makonda amepost picha kwenye ukurasa wake ikimuonyesha akiwa...
  14. B

    Waziri Nape, kuhusu vifurushi vya simu tatizo lipo TCRA

    NDUGU NAPE, KUHUSU VIFURUSHI VYA SIMU Bashir Yakub, WAKILI. +255714047241. Ndugu yangu Nape tatizo liko hapo TCRA. Haya makampuni ya simu yanafanya biashara na hivyo yanaweza fanya lolote yasipopata usimamizi. Tunahitaji Kanuni za vifurushi kama vifurushi kutoka hapo TCRA ili zitusaidie...
  15. beth

    TCRA yasimamisha kipindi cha EFATHA cha Nabii Josephat Elias Mwingira kwa miezi mitatu, Star TV yapewa onyo

    Kamati ya Maadili ya TCRA imesema Kituo cha Star Tv kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries ambacho hurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja, kwa kuruhusu maudhui yenye ukakasi ambayo ni kinyume na Kanuni za Mawasiliano TCRA ikimnukuu Askofu Josephat Mwingira...
  16. GENTAMYCINE

    Nape acha 'Kukurupuka' hili la 'TCRA' laweza 'Kukuharibia'. 'Boss' wako 99% anategemea hizo 'Tozo' ili nchi iende

    Umeanza kwa Pupa sana Kamarada ( Comrade ) sijui bado 'appointment hangover' inakusumbua pamoja na Ujana ulionao? Jeuri ya Boss wako ( Mama ) ipo katika hizi Tozo mbalimbali sasa leo hii unavyotaka TCRA ipunguze kwa kutafuta Kwako Sifa kwa Watanzania huku ukimkosesha Mama Mapato ya Kuongezea...
  17. Chachu Ombara

    Waziri Nape Nnauye aitaka TCRA kuyaagiza Makampuni ya Mawasiliano kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi

    Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye ameiagiza TCRA kuyaagiza makampuni ya simu kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi mpaka hapo watakapokaa na Serikali kuzungumza kuhusu jambo hilo. Chanzo: DarMpya Pia soma - Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya...
  18. NostradamusEstrademe

    TCRA Naomba fuatilieni hii kitu hawa watu wanatapeli watu sana

    Leo nimetumiwa message kutoka kwenye namba +255733326905 kuwa nimeshinda Biko ya milioni 5 waliniona mimi ni zuzu wa kuona milioni tano nitahaha. Wakanipa maelekezo nipige kwenye namba hii 0719254427 Nawaomba cyber polisi na TCRA fuatelieni nyendo za hizi namba mishowe mtamkamata huyu mtu. +
  19. MR.NOMA

    Matapeli wa Simu wanazidi, licha ya simu kusajiliwa! Nani alaumiwe, Makampuni ya simu, TCRA, Polisi au Raia?

    Wakuu hizi sms Mzee flani ni mganga maarufu, atakupa utajiri wa freemason, mara utajiri wa ndagu nk. sasa zimetawala sana, na hizi zingine za umeshinda milioni 700000000, piga Simu 0000 ili upate zawadi zako. Au unapigiwa simu na litapeli likisema Kuna Hela imetumwa kwako kimakosa. Simu zote...
  20. Inside10

    TCRA waipa onyo wasafi Tv kwa kukashifu dini ya kikristo.

    Kamati ya Maudhui ya TCRA, leo Jumatano imeipa onyo Wasafi Televisheni, pamoja na kuitaka iombe radhi mara tatu kwa siku, kuanzia kesho Alhamisi hadi Jumamosi, huku ikiiamuru ilipe faini ya Sh. 2 Mil., baada ya kukutwa na hatia katika kosa la kurusha maudhui yenye kukashifu dini ya Kikristo...
Back
Top Bottom