tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Analogia Malenga

    TCRA yatoa onyo kwa waagizaji na wasambazaji wa vifaa vya mawasiliano ya simu ambavyo havijaidhinishwa

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya 2003, na kupewa jukumu Ia kusimamia Sekta ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta nchini Tanzania. TCRA imebaini kuwa yapo baadhi ya Makampuni au wafanyabiashara...
  2. BARD AI

    TCRA yadai Clubhouse ilipotea kwasababu ya Kiufundi, sasa ipo hewani

    Siku moja tangu utokee mkwamo wa upatikanaji wa mtandao wa Clubhouse nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haikuufungia bali kulikuwa na changamoto za kiufundi, lakini umesharejea. Mtandao huo ambao watu huutumia kuwasiliana kwa sauti, kufanya mikutano na mijadala mbalimbali...
  3. BARD AI

    Mchina aingilia Miundombinu ya TCRA na kusababisha hasara Tsh. Milioni 221

    Raia wa China Li Naiyong amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka sita likiwemo kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh221 milioni. Naiyong amesomewa mashtaka yake leo, Februari 15, 2023 na...
  4. BARD AI

    TCRA yafungia Laini za Simu 900,000 zisizo na Usajili wa Alama za Vidole

    Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hadi kufikia Jumanne, Februari 14, 2023, Jumla ya laini za simu 900,000 ambazo hazikuwa na Usajili Rasmi wa Alama za Vidole na Kitambulisho cha Taifa, zilikuwa zimefungiwa mawasiliano.
  5. Msanii

    TCRA fahamuni kuwa Watanzania ni waelewa kuliko mnavyodhani

    Jana jioni nilikuwa namsikiliza kipindi cha JAHAZI cha Clouds Radio. Studioni alialikwa mkurugenzi wa TCRA ambaye alitoa fafanuzi mbalimbali kuhusu kuhakiki namba za simu na alielezea mwishoni kuhusu kupanda kwa gharama za mitandao. Bahati mbaya sana vipindi vingi vya redioni ambavyo...
  6. M

    Mfanyabiashara wa mihogo Kawe, Bwana Charahani akamatwa akiwa kwa mganga Bagamoyo

    Ni yule ambaye aliripotiwa hapa JamiiForums na Member mmoja nimemsahau jina kuwa alimjeruhi aliyemhusi mwizi wa mkewe (mama Zai ambaye sasa ni mjamzito) kwa kumkata kiukatili sikio na kidole kisha kupita navyo sokoni Kawe akiwa anatamba na kuvionyesha kwa watu huku akisema hakuna wa kumtisha...
  7. chizcom

    Baba Levo una 'bullying' za waziwazi, TCRA wanakuangalia tu pamoja na uongozi wako

    kiukweli huyu jamaa Baba Levo hapa tu kupewa rungu Wasafi na Media kapitiliza kwenye kuongea. wanakipindi chao cha kutafuta vipaji, una katabia cha ajabu kukosoa wanadamu na kuwakejeli. Hata kama unatafuta sifa kufika kama Salama Jabir ila huwezi. Salama ana hayo mambo na uwezi kuona ujinga...
  8. McCollum

    Naomba kujuzwa kuhusu aina za channel za YouTube zinazotakiwa kusajiliwa TCRA

    Natoa salam kwa wana jamvi wa Jf kwa ujumla, specifically nazitoa salam kwa wana jukwaa wa Tech. Tukiachana na salam, naomba niende moja kwa moja kwenye mada tajwa. Naomba kuuliza je, ni aina gani za channel za YouTube zinahitajika kusajiliwa na TCRA?. Je, ni kila aina ya channel inahitaji...
  9. Cannabis

    TCRA yatoa onyo kali kwa makampuni na watu binafsi wanaosambaza visimbuzi vya CANAL PLUS

    TCRA imetoa onyo kali kwa Makampuni na Watu binafsi wanaoingiza nchini vifaa vya mawasiliano vikiwemo visimbuzi vya CANAL PLUS na kufanya biashara ya kutoa huduma za Televisheni kupitia satelaiti bila kuwa na leseni, imesema visimbuzi hivyo havijaidhinishwa.
  10. Hismastersvoice

    TCRA acheni kushiriki kwenye wizi wa vifurushi unaofanywa na AZAM TV

    Azam Tv imekua na tabia ya kutuibia wateja wa vifurushi vya Azam Tv, mteja ananunua kifurushi cha bei kadhaa na chaneli kadhaa kwenye kifurushi husika lakini kabla haujamaliza muda wa kifurushi husika Azam Tv wananyofoa baadhi ya chaneli ulizolipia, huu ni wizi na ni sawa na mwenye basi...
  11. JanguKamaJangu

    Laini zisizohakikiwa kuzimwa Januari 31, 2023

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema ikifika Januari 31, 2023 namba za simu ambazo hazitakuwa zimehakikiwa zitazuiliwa kupokea na kutoa huduma za Mawasiliano. Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA imesisitiza kuwa kila mtumiaji wa huduma za Mawasiliano anapaswa kutekeleza na kukamilisha...
  12. kavulata

    TCRA lindeni walaji wa habari

    Vyombo vya habari redio na tv havipaswi kuwa na ratiba za vipindi vyao zinazoonyesha muda na siku? Kama zipo ratiba ni nani anapaswa kuhakikisha kuwa ratiba hizi zinafuatwa na vyombo vya habari ili kuwalinda wasikilizaji na watazamaji wa vipindi vyao? Mfano, Redio inasema watakuwa na taarifa ya...
  13. T

    Wale mliofungiwa NIDA zenu (Blacklist) na TCRA kusajili line mpya njooni hapa mtoe shuhuda zenu na jinsi mlivyopata solution

    Mimi ni kiongozi wa timu za usajili wa line mpya. Hivi karibuni kumetokea wimbi la wateja wengi wanaotaka kusajili line mpya na vitambulisho havijajaa lakini wanaambiwa (nin blacklisted). Je wewe ni mmoja wao? Na je ulitumia njia gani kuondoa tatizo hilo? Karibu utuelezee ili na wengine wenye...
  14. BARD AI

    TCRA: Usikubali kuingiza Alama za Vidole mara mbili wakati wa kusajili Line

    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeeleza wahalifu wa mitandao ya simu maarufu kama 'Tuma kwa namba hii' wanavyosajili laini kinyemela kwa kutumia vitambulisho na alama za vidole vya watu, bila wahusika kugundua. Imesema uhalifu huo hufanywa na mawakala wanaosajili laini za simu mteja...
  15. Joseph_Mungure

    Ni kwanini TCRA haisimamii na ku-regulate bei za huduma za mitandao?

    Habari ya asubuhi wana JF. Nimeleta hoja hii mbele yenu, kupata maoni kutoka kwenu. Hii ni kutokana na kubadilika kwa bei za vifurushi mara kwa mara bila kutolewa sababu za kubadilika kwa gharama za huduma hizo. Kwanini hakuna chombo kama EWURA!? Kinachofanyika kwenye mafuta kifanywe na huku...
  16. Njowepo

    TCRA saidieni kwenye hili la vifurushi, hali tete

    Hii mitandao ya simu kila leo wanapunguza package zao ila kwa bei ile ile. Mfano Vodacom kwa mwezi wa Nov na Oct kwa malipo ya Tshs 50,000 nimekuta wamepunguza 3GB na dk 200. wamepunguzakama ifuatavyo; ~ 50,000 Nov Package unapata :1200minutes 500sms 20GB. ~ 50,000 Oct Package nilipata...
  17. NetMaster

    Serikali ndio ya kulalamikiwa, Mitandao ya simu inafidia gharama zinazoongezwa na Serikali kwa kupandisha bei vifurushi

    Nimekuwa nikiona sehemu nyingi watu wanalalamikia mitandao ya simu kuongeza bei za vifurushi, hii sio sawa, tunalalamikia 2 badala ya kulalamimikia chanzo cha 1+1. Ni kama vile gharama za mafuta zikipanda basi nauli nazo zinapanda, si haki kuwalaumu wafanya biashara wenye mabasi. Ndivyo ilivyo...
  18. Bujibuji Simba Nyamaume

    Mfalme Zumaridi kama umeshindwa kuongoza kanisa, pisha mchungaji mwingine

    Duh.... Hapana Mfalme Zumaridi aache visingizio sasa. Kama ameshindwa kuongoza kanisa si aseme tu. Anashindwaje kuwakaripia wapiga vyombo kwa kuongeza sauti hadi inakuwa kero kwa waumini? Sisi ndio tunatoa sadaka, lakini hatuoni sadaka zetu zinafanya kazi gani. Yeye kila siku yuko kwenye...
  19. BARD AI

    Thamani ya miamala ya Simu yapungua nchini

    Wakati idadi ya watumiaji wa huduma za fedha kwa simu za mkononi ikizidi kuongezeka, thamani ya miamala wanayoifanya inapungua kila uchao. Ripoti ya robo mwaka inayoishia Septemba 2022 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha idadi ya miamala imeongezeka kutoka zaidi ya milioni...
  20. N

    Haki Itendeke; Hili la Mbowe TCRA wafungieni gazeti la Mwananchi kama mlivyofanya kwa Kwanza TV

    Kwanza tv ya maria sarungi iliandika Gwajima apata ajali, ikala rungu la TCRA , soma sababu zake na uniambie kwa nini mwananchi wasile rungu kwa jinsi walivyoandika habari ya mbowe kushinda huko ccm HAKI ITENDEKE, ACHENI DOUBLE STANDARD kilichofanya kwanza tv ikala rungu hiki hapa, bwana Joseph...
Back
Top Bottom