tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. GENTAMYCINE

    TCRA mmebariki huu Upuuzi wa Viongozi wa Timu za Ndondo Cup Kusifia kufanya Ushirikina Mubashara Redioni Clouds FM?

    "Hela tuliyopata tumeenda kununua Mayai Viza, Kuku Mweusi na Udi na kumpelekea Mganga wetu wa Kienyeji na kwa jinsi tunavyoenda Kuwaroga Watatukoma" Shabiki wa Timu Moja inayoshiriki Michuano iliyosifiwa na inayosapotiwa na Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya Ndondo Cup' kwa Mikoa...
  2. S

    TCRA kuufungia wimbo "Amkeni" wa Ney wa Mitego na kuacha nyimbo za matusi ni uchawa, kujipendekeza na unafiki

    TCRA acheni kutumika vibaya. Mmeufungia wimbo wa Ney Wamitego "Amkeni" kwasababu tu umemparura aliyewateua lkn mmeacha nyimbo kibao za matusi zkiendelee kwenda hewani. .....sijui kutongoza.... .....ikiiingia inateleza.. ....paka mate niteleze.. .....nampatia sukari ananambia ongeza.. n.k, n.k...
  3. Hismastersvoice

    TCRA, hivi kwanini hamtulindi wananchi dhidi ya dhuluma? Badala yake mpo kwa kutukandamiza!

    Nilinunua kifurushi cha wiki cha Airtel nikiwa safarini Marangu Moshi, nilipofika nikakuta Airtel haipatikani hivyo kifurushi kikaisha kwa muda niliokuwepo hapo! TCRA wao wanajionea sawa tu. Nilitika Marangu nikaenda Moshi mjini eneo la KCMC ah! Nako ni shida tu mpaka mwenyeji akuelekeze...
  4. NostradamusEstrademe

    TCRA naomba mchunguze namba hii inanisumbua

    Kuanzia jana napata message kutoka namba 0738264152 inaniambia naomba unitumie hiyo hela kwenye namba hii ya Airtel 0695662564 jina AGNES ALKADO nakusubilia kwa wakala. Naomba fuatilieni tukomeshe usumbufu huu
  5. lufungulo k

    TCRA itoke hadharani kukiri kuwa muziki wa matapeli wa mtandaoni umewashinda

    Sasa imekuwa KERO, KERO KERO jumbe za kitapeli mtandaoni zimekuwa nyinginyingi mno! Hapa nadhani TCRA umefikia wakati watoke hadharani na kukubali kuwa muziki wa matapeli umewashinda. Kama kupata line za simu lazima uwe na namba ya NIDA, iweje tabia hii ya kitapeli izidi kushika kasi? TCRA...
  6. BARD AI

    Ripoti TCRA: Dar yaongoza kwa idadi kubwa ya Watumiaji wa huduma za Simu Tanzania

    Katika kipindi cha miaka 5 kumekuwa na ongezeko la Watumiaji 16,327,131 wa Huduma za Simu Nchini kutoka 47,685,232 mwaka 2019, sawa na 88% ya Idadi ya Watu hadi 64,088,651, sawa na 101.5% ya Idadi Watu Mikoa yenye Idadi kubwa ya Watumiaji wa Huduma za Simu Tanzania Bara ni Dar es Salaam...
  7. J

    AIRTEL Mnatukosea sana Mbeya, poor Quality of service by TCRA Q3 Report

    Airtel mna call drops kubwa sana , ndio maana hata ukipiga simu Mbeya kwa watumiaji wa Airtel hatusikiani . Hii Report ipo kwenye site za TCRA na iko wazi msiseme tunawasagia kunguni. Mmezidiwa hadi na TTCL kweli...
  8. Analogia Malenga

    Mabadiliko ya muonekano wa tovuti ya TCRA yameathiri upatikana wa ripoti za mawasiliano nchini

    TCRA tunaomba mfanye jambo maana leo kuna takwimu nimezifuata lakini kiunga kuelekea kwenye communications statistics hakifikiki Japo muonekano ni mzuri lakini tatizo hili ni kubwa kwa sisi watumiaji wa takwimu kutoka kwenu, Hili nalo mkaliangalie Uzi tayari
  9. Analogia Malenga

    Nimeshtushwa na TCRA kukosea jina lao kwenye ripoti yao

    Nimeshtusha na ripot ya mwezi wa March 2023, ya TCRA ambayo jina lako limekuwa ni Authory badala ya Authority. Yaani hii ni sawa na mtu kujikosea jina lako mwenyewe. Ni aibu
  10. Analogia Malenga

    Kuna shida ya takwimu za TCRA kuhusu matumizi ya GB kwa mitandao ya kijamii

    Nimeangalia matumizi ya GBs kwa robo mbalimbali nchini nimegundua kuna shida kwenye takwimu wanazotoa TCRA. Kwa robo ya mwisho ya mwaka 2022 walionesha kuwa tulitumia jumla ya GB Trilioni 90.1 Kwa robo ya kwanza ya mwaka 2023, data zimebadilika hadi kufikia GB milioni 48 Mimi niombe...
  11. ngungwangungwa

    Wizi wa Airtel kwenye vifurushi na huduma mbovu za TCRA

    Wakuu, Nilijiunga kifurushi cha Airtel cha Uniofa ambacho unapata dakika 40, sms 10 na mb 350 kwa muda wa siku 7. Kilichonishangaza leo asbh nilipoangalia salio, ikaonyesha kifurushi changu zile dakika 40 na sms zinaisha tar 04 June. Lkn zile mb zinaisha leo tarehe 31 May saa 2 asbh...
  12. Mr Why

    Ushauri kwa TCRA kitengo cha Tovuti

    TCRA napenda kuwashauri kuhusiana na tovuti hasa zinazo onesha maudhui yasiyo faa. Napenda kuwashauri kuwa hakuna haja ya kufungia tovuti za ngono kwasababu tovuti hizo haziwafuati watumiaji na wala hazilazimishi watumiaji kuzifuata bali ni watumiaji ndio wanaozifuata. Kitendo cha TCRA...
  13. olimpio

    Tigo yaongoza kwa simu za kitapeli Report ya Quarter ya 3 TCRA

    Report ya Quarter ya 3 ya mwaka 2022/2023 yaonesha Tigo kinara simu za kitapeli yaonesha pia TTCL kushuka sana kimapato na internate penetration
  14. GENTAMYCINE

    Ile harufu Kali ya Kinyesi iliyoko usawa wa Hostels za Magufuli za UDSM na TCRA kwanini haitafutiwi Ufumbuzi?

    Kwa Wapanda DalaDala ( Bayankata ) Wenzangu najua hapa watakuwa Wananielewa sana tu. Ni harufu ya Kinyesi ( na inaonyesha kuna Shimo Taka ) ama la Magufuli Hostels au za TCRA limejaa hivyo linatema na kuwa Kero katika Pua zetu. Tafadhali Mamlaka ifanyie Kazi hili.
  15. ChawaWaMama

    Je TCRA au Mamlaka ya Tanzania wanaweza kusoma meseji za Whatsapp? Au zile za kawaida kwenye iPhone?

    Great Thinkers, Naomba kufahamu, je mamlaka yetu nchini inaweza kusoma jumbe za whatsapp? Na je zinaweza pia soma texts za sms za kawaida kwenye simu za iPhone? Asanteni.
  16. RoadLofa

    Hii ni sawa TiGO wanachofanya na TCRA wanafanya nini?

    IVI TIGO WANACHOFANYA ni sawa kweli kumuunganisha mteja na huduma bila idhini yake Kisha kumpa kazi ya kujiondoa, nashangaa sana sijui wizara ya tech na habari na mawasililiano na TCRA,WANAFANYA kazi Gani, au ndo wanakazi ya kutetea telecom companies Screen shot iyo hapo chini ya sms waliyonitumia
  17. BARD AI

    TCRA kuanza ukaguzi wa Vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki kwenye Nchi vinakoagizwa

    Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), John Daffa amesema kuwa ukaguzi utaanza Mei 23, 2023 kwa lengo la kuepusha na kudhibiti uingizaji wa Vifaa vilivyokwisha muda wa matumizi Nchini. TCRA imesema Hatua hiyo ni katika kutekeleza Kanuni zilizoazimiwa katika Mkutano wa Taasisi...
  18. The Assassin

    Clouds TV imeanza kuwa kituo cha kutetea wauza madawa ya kulevya

    Clouds TV jana iliita muuza madawa ya kulevya anaeitwa Jack Cliff kuja kujitetea jinsi alivyokamatwa na madawa ya kulevya. Taarifa za uhakika zinaonyesha kua mamlaka nchini China/Macau zilimkamata Jack akiwa na madawa ya kuelvya aina ya Heroine kilo 1.1 mwilini mwake na kupelekea kufungwa...
  19. Heparin

    Unazungumziaje hali ya Utapeli unaofanyika kwa njia ya Simu baada ya kuzimwa kwa laini zisizohakikiwa?

    Kwa mujibu wa ripoti ya TCRA ya robo ya nne ya mwaka, hadi Desemba 2022 mitandao ya simu nchini ilikuwa imesajili jumla ya laini milioni 60.277. Laini hizo ni sawa na ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na zile milioni 58.1 waliokuwapo mwisho war obo ya tatu ya mwaka 2022 yaani Septemba...
  20. commonmwananchi

    Usajili wa line na vibao vya makazi havina tija kwa Wananchi

    Wezi wa mitandao wameishinda serikali! Vibao vya makazi vimeimarisha nini tangu kuwekwa kwa gharama ya zaidi ya B360? Tunashuhudia kila mwaka nchini, Serikali kupitia TCRA, tukielekezwa na kulazimishwa kusajili line za simu kwa watumiaji wapya, lakini pia kuhakiki kwa wale ambao walikwisha...
Back
Top Bottom