tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. ACT Wazalendo

    Macheyeki: BASATA iifungulie Mara Moja Wimbo wa Ney wa Mitego

    JUZI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) ilivitaka vyombo vya Habari vya kielektronic hususan redio Tv na mitandao ya kijamii kutoutumia wimbo wa msanii wa Kizazi Kipya Emanuel Elibariki(Ney wa Mitego) walioutaja kwa jina la Tozo, wakieleza kuwa wamepokea taarifa kutoka baraza la Sanaa la...
  2. BARD AI

    TCRA yapiga marufuku wimbo wa Nay wa Mitego uitwao "Tozo"

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetoa agizo hilo kwa vyombo vyote vya Utangazaji nchini baada ya kupokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa BASATA. Kwa mujibu wa barua ya TCRA imesema baada ya BASATA kuhakiki wimbo huo imebaini kuwa maudhui yake hayafai kutumika katika jamii na...
  3. BARD AI

    TCRA: 80% ya tamthilia zinazorushwa kwenye TV ni za nje

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevihimiza vyombo vya habari kuangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa tamthiliya, muziki na michezo zenye maudhui ya ndani ili kulinda utamaduni na nembo ya Taifa. Akizungumza kwenye mkutano wa wadau mbalimbali wa vyombo vya habari, sanaa na michezo...
  4. Suley2019

    Maxence Melo: TCRA sikilizeni pande zote kabla ya maamuzi. Sheria na Sera za Nchi zilenge kuchochea Uchumi wa Kidigitali

    Baadhi ya masuala aliyoongelea Mkurugenzi mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, katika warsha ya kukuza maudhui ya ndani yaliyofanyika TCRA. Kukosoana si kubaya Ukosoaji uwe wa pande mbili, kama kamati inavyokosoa watengeneza maudhui na wao pia wakubali kukosolewa, lakini kukosolewa huku kuwe...
  5. The Sheriff

    TCRA ina 'task force' ya kuwashughulikia wenye televisheni za online ambazo hazijasajiliwa

    Engineer Kisaka ameyasema hayo leo Septemba 16, 2022 wakati wa Warsha ya Kuhamasisha Uandaaji, na Uzalishaji wa Maudhui ya Ndani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo Waziri wa Habari na Mawasiliano. "…lazima tumsikilize kila mmoja anasemaje. Muafaka uliofikiwa ni kuwa...
  6. BARD AI

    TCRA yaipiga faini ya Tsh. Milioni 2 Zama Mpya TV (Dar Mpya), Maudhui ya Afande Sele kuhusu Tozo yatajwa

    Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)imeiamuru ZamaMpya TV Online kulipa faini Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) ndani ya siku 21 kufuatia kuchapisha hisiyo na midhania ya habari. Taarifa hiyo ilihusu maudhui ya Selemani Msindi (Afande Sele) ambayo yanatuhumiwa kuwa ya...
  7. J

    TCRA imeendesha kikao Kazi na Wadau wa sekta ya Mawasiliano Kanda ya Kati

    TCRA imeendesha kikao Kazi na Wadau wa sekta ya Mawasiliano Kanda ya Kati Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari, ameongoza kikao kazi baina ya TCRA na Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Kati, kilichofanyika Mkoani Tabora, katika ukumbi wa Isike...
  8. BARD AI

    Maxence Melo: Bei za vifurushi vya internet ni ghali, na huduma ni mbovu. TCRA watetea kupanda kwa bei

    Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo amesema kupanda kwa Bei ya Data hakukuwa na utaratibu mzuri na pia huduma imekuwa mbovu kwa gharama kubwa zaidi, jambo ambalo linaua ndoto za wabunifu wengi wanaotumia Mtandao. Melo amesema hayo wakati akijibu utetezi wa Bei Mpya za Vifurushi...
  9. Jidu La Mabambasi

    Ujumbe kwa TCRA: DStv wanarusha vipindi vya kuhamasisha ushoga kwa watoto?

    TCRA Please take note. Kuna ujumbe wa malalamiko kuwa kuna vipindi wanavyovipenda watoto vya NICKELODEON, vinavyorushwa na DsTV, vimeleta taharuki kwa wazazi. TCRA kama mhusika tafadhali chukua hatua. Ujumbe: Dear Parents/Guardians. This is to bring to your notice that the cartoon channel...
  10. sky soldier

    MB 1 iliuzwa senti 65, sasa tunakamuliwa shilingi 1 na senti 77, elfu 2 ilitupa GB 3 lakini sasa ni gb 1. Kenya na Zambia wametupindua

    Ndani ya muda mfupi kabisa gharama za internet zimepanda mara 2.7 yani tatu kasoro. Ni mwaka jana tu hapo kabla ya mabadiliko machunu ya vifurushi tulikuwa tunaweza kununua mb moja kwa senti 65 (shilingi 0.65) lakini sasa ni takribani shilingi 1.8. Hii elfu 2 tunayotumia kwa sasa kununua gb 1...
  11. mgt software

    Kupanda kwa bando kuathiri kilimo na ufugaji. Video call zilipunguza sana udanganyifu. TCRA msilichukulie poa

    Wana Jf. Wakati serikali ikijitahidi sana kuingiza fedha nyingi kwenye kilimo, makampuni ya simu yapo mstari wa mbele kuumiza matumiaji wa Internet kwa kuongeza gharama lukuki kila mwezi. Uwezi kumaliza mwezi kabla ya vodacom na airtel hazijapunguza vifurushi vya bando. Hii ni kudidimiza juhudi...
  12. chiembe

    Makampuni ya simu na TCRA +BOT wanashindwa kuzuia malipo yanayoenda kwa akaunti za Mange Kimambi? Zinafadhili uhalifu

    Hizi Hela zinatoka katika akaunti za mpesa/tigo/halotel/Airtel. Watu hulipia Application ya Mange kutokea makampuni hayo, kwa wingi. Watanzania wengi hawana ujanja wa kutumia Mastercard and the like, ni ku-highlight destination ya Hela inakotumwa na kuingiza mfumo wa ku-block transaction...
  13. sky soldier

    TCRA GB 1 Yafikia shilingi 1,861 ambayo itapanda, Ni jitihada za kuiminya internet kwa lengo lipi ?

    TCRA kuna nini huko, Nachojua hizi internet TCRA ndio kama anaewajumulia mitandao ya simu waje kutuuzia kwa reja reja, Hatuwezi kuilaumu mitandao ya simu bali TCRA, Wao wakipandisha bei basi na mitandao inapandisha. Kuna nini hasa ? Hizi ni danadana za haba na haba hujaza kibaba sitakja...
  14. BigTall

    Utahitaji Kibali cha TCRA Kuweza Kuishitaki TCRA Mahakamani

    Utahitaji kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ili kuishitaki TCRA mahakamani kwa mujibu wa kifungu namba 68, kifungu kidogo namba mbili, cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010. Sheria hii ni moja kati ya sheria zinazolalamikiwa sana kwa kuminya uhuru...
  15. M

    TCRA Wafungie API za malipo ya Selcom kwenye app ya Mange Kimambi

    Tunawapongeza TCRA kwa kuifungia app ya Mange Kimambi, kwa TZ mpaka uwe na VPN ndo unaipata. Lakini Hilo halitoshi kwani Bado anaendelea kuwachangisha Watanzania kupitia Selcom. Yaan watu wanalipia upumbavu na ikiukwaji wa maadili kwenye app yake. TCRA tunajua mna uwezo wa kumwambia Selcom...
  16. May Day

    TCRA wekeni utaratibu hawa 'Majambazi wastaafu' wawe wanahojiwa na Watu wenye weledi

    Kama ilivyo kawaida yangu leo nilikuwa nafuatilia moja ya vipindi ninavyopenda kusikiliza kupitia Redio Free Africa...Kipindi kinaitwa "sintosahau". Si mara ya kwanza nimeona kuna mapungufu mahali na sijui kama Mamlaka huwa zinafuatilia, au labda kwao sio tatizo...mara kadhaa nimeshasikia...
  17. Suley2019

    TCRA, biashara ya ngono inashamiri mitandaoni hamuoni au mmeuchuna tu?

    Salaam wakuu, natumai nyote mpo salama Ndugu zangu kijana wenu nimekuwa mtumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Telegram, Instagram, Twitter na mingineyo. Kama utakukubaliana na Mimi ukipita kwenye mitandao hii Kuna kiwango kikubwa Cha biashara ya ngono (umalaya) inayohusisha watu...
  18. Getrude Mollel

    Nape issues a stern warning to TCRA and Telecoms

    The Minister of Information, Communication and Information Technology, Hon Nape Nnauye, has unleashed a stern warning against TCRA and Telecoms in Tanzania to stop sending texts to people without their prior consent. Hon Nape made those remarks in Dodoma, calling TCRA and telecoms in Tanzania...
  19. J

    Waziri Nape aitaka TCRA kushughulikia malalamiko ya wananchi kuunganishwa huduma ambazo hawajaomba

    WAZIRI NAPE ATOA MAELEKEZO KWA TCRA, MAKAMPUNI YA SIMU Na Mwandishi wetu, DODOMA Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ametoa maelekezo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na makampuni ya simu kutatua kero na malalamiko ya wananchi kuhusu huduma za...
  20. The Sheriff

    KERO TCRA, hawa matapeli wa “TUMA KWA NAMBA HII” tutaishi nao milele?

    Ni kipindi kirefu sasa kumekuwepo aina hii ya utapeli tulioubatiza jina la “TUMA KWA NAMBA HII”. Wapo waliofanikiwa kukwepa na wapo waliolizwa, na bado kuna wahanga watarajiwa. Haya yanatokea hata baada ya zoezi la usajili wa laini za simu ambao uliaminisha wengi ungekuwa suluhu ya jambo hili...
Back
Top Bottom