Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.
TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).
Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.
Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
Bwana nape hii imekaaje kuna hizi tasisi za kukopesha mitandaoni zinaomba namba ya watu wa karibu wawili au watatu ajabu sasa mwisho wa siku wanatuma meseji kwa namba zako za sm zote ulizonazo kwenye sm yako na ambazo ukuwapa hapa mchawi nani.
Kampuni ya sm au TCRA maana tumeshahisi hakuna...
MAMALAKA ya mawasiliano nchini(TCRA)imetangaza kuwa kuanzia sasa masafa ya radio yatashindaniwa kwa kutangazwa zabuni huku wadau wakitaka kuwepo na uwazi ili kuwa na uwanja sawa.
Kwenye kikao cha wamiliki na maneja wa vituo vya radio pamoja na waandishi wa habari kilichokaa hivi karibuni...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama ifuatavyo:-
Amemteua Dkt. Jones A. Killimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano...
bodi
bodi ya wakurugenzi
makamu
makamu mwenyekiti
mamlaka
mamlaka ya mawasiliano
mawasiliano
mwenyekiti
mwenyekiti wa bodi
rais
rais samia
samia
tanzania
tcra
wakurugenzi
Nasikia Rais kavunja Bodi ya TCRA. Naona hawa hapa ndio walikua Wajumbe wake
MAWASILIANO: BODI YA TCRA YAVUNJWA
Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangu amteue Mwenyekiti wa Bodi hiyo
Kwa mujibu taarifa ya Kurugenzi...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kuvunja bodi kama ifuatavyo:
1. Amemteua Balozi James Gilawa Bwana kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika kusini. Balozi Bwana anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Gaudence...
Kuna mitandao nchini kama Jambo tv ambayo inashabikia kutoa taarifa zinazowachanganya na kuwagawa wananchi. Serikali inasubiri hadi wapi ili kuifuta?
Kule Marekani kulikuwa na mtandao wa you tube the Dive wa kijana anaeitwa Jackson Hinkle ambao ulikuwa ukiripoti habari za vita ya Ukraine...
Ninaandika andiko hili kutoa malalamiko yangu kuhusu huduma za wateja zinazotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania. Nilipojaribu kupata msaada kuhusu masuala yanayohusu mawasiliano, nilikumbana na changamoto kubwa.
Inaonekana kwamba wafanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel hawana ujuzi wala...
Aboubakar Ally alienda kamati ya malalamiko ya TCRA kulalamikia suala la kupokea sms kutoka Umojabet bila ridhaa yake. Suala hilo alilalamika Voda lakini hawakuchukua hatua.
Walipofika kamati ya malalamiko Vodacom walikubali kuwa mteja wao alikuwa anapokea sms hizo lakini wao hawahusiki na...
Ikiwa umepata huduma mbovu ya kimawasiliano, iwe kwenye kisimbuzi au mtandao wa simu ambao wote wanaratibiwa na TCRA. Ziko hatua kadhaa za kufuata ili uweze Kamati ya Malalamiko ikusikilize.
1. Kwanza ni kuwaambia kampuni yako (i.e tigo, voda au azam) ili muelezane vizuri
2. Mkishindwana hapo...
Bahati Mekene alipeleka malalamiko katika kamati ya malalamiko ya TCRA kuhusu Vodacom kufanya swap ya laini yake ambapo ilimletea shida hata kwenye mahusiano yake kwani aliashindwa kuendelea na mpenzi wake baada ya mwenza wake huyo kupiga simu na kupokelewa na mwanaume.
Tukio hili lilitokea...
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kwa Mkuu wake wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Rolf Kibaja imesema taarifa kwa Umma iliyotolewa juzi October 13,2023 haijakataza matumizi ya VPN kama baadhi ya Watu wanayopotosha kupitia mitandao ya kijamii.
Kibaja ameiambia Ayo TV...
Swali kwa TCRA: Mnajua sababu ya matumizi ya VPN kuwa makubwa nchini?
Uhalisia ulivyo: Kwenye teknolojia ukiwabinya sana wananchi pale, wao wanatokea kule kwa sababu ya kukua kwa teknolojia kila siku, kila kitu kina option B.
Katika mambo ambayo serikali ilikuwa haijawahi kuwaza basi ni...
Zuio la TCRA Matumizi ya VPN linakandamiza uhuru wa habari Nchini.
Chama cha ACT Wazalendo kupitia Wizara Kivuli ya Habari na Mawasiliano tunapinga vikali taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA ya kukataza matumizi ya Mtandao binafsi maarufu kama VPN (Virtual Private Network)...
Leo nimepiga simu airtel huduma kwa wateja kupitia namba 100 kama wenyewe wanavyoelekeza. Ajabu hadi dakika 10 zinakwisha, sijaunganishwa na mtoa huduma, napewa tu maelekezo, bonyeza 1, mara bonyeza 6.
Baada ya maelekezo hayo, napata sms kuwa nimetumia dakika 10, na kweli dakika 10 hizo...
Naomba kufahamu kwa wajuvi wa sheria hapa JF.
TCRA ni taasisi inayosimamia mawasiliano hapa TZ.
Je hawa watu wanahusika na kutunga sheria?
Mfano ni kuhusu hili suala la VPN
Nimeona katazo la Tcra kuzuia matumizi ya Vpn nakusema kuwa kuna faini ya mil 5. Sasa kwa sababu karibu kila Mtanzania mwenye smart foni amedownload VPN na anaitumia kuangalia mambo yake binafsi ya kifaragha .
Je, TCRA itawag'amua vipi watu wakiwa na simu zao mkononi.
Msaada wa kitalaamu
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imewataka wananchi na makampuni kiujumla ambazo kwa asili ya kazi zao hawawezi kuepuka matumizi ya VPN kutoa taarifa juu ya VPN wanazotumia na taarifa muhimu kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.
Aidha mamlaka hiyo imesema iwapo itabainika umetumia VPN kinyume na kanuni...
TCRA mimi ni mtumiaji wa takwimu zenu, ila angalieni ripoti zenu nyingi mnakosea jina lenu, badala ya kuwa "Authority" mnajiita "Authory" hii inanipa mashaka kama data mnazotoa ziko sahihi ikiwa jina lenu tu mnakosea.
Ripoti ya June 2023, mmejiita "Authory"
June 2022, mmejiita "Authory"...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.