tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. S

    TCRA, acheni kujitetea kuhusu mikopo ya mtandaoni; je, hamna uwezo wa kuagiza makampuni ya simu kutosajili lipa namba wanazotumia kupokea marejesho?

    Watanzania, tufike mahali tujiulize swali hli dogo tu: Mikopo ya mitandaoni hutolewa kwa wateja kutumiwa hela kwenye simu zao na zaidi marejesho hutumwa kwa haya makampuni kwa kutumia lipa namba za mitandao ya simu. Sasa kama mpaka wanakuwa wamesajili lipa namba kwenye menu ya mitandao ya simu...
  2. Mkalukungone mwamba

    TAMWA na TCRA waandaa Tuzo za Umahiri za Waandishi wa Habari 'Samia Kalamu Awards 2024'

    Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wameandaa tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari Watanzania zinazojulikana kwa jina la “Samia Kalamu Awards 2024.” Zoezi la kutoa tuzo hizo linatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu 2024...
  3. P

    TCRA toeni adhabu kali kwa baadhi ya redio na TV

    Kumekuwa na wimbi kubwa sana la uanzishaji wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini jambo ambalo ni zuri sana. Ila kutokana na jinsi vyombo hivi vingi vya habari haswa redio na TV zinavyofanya kazi zake nyingi hazina tija katika jamii. Redio na TV nyingi zimekuwa ni wakala wa kuharibu jamii...
  4. P

    TCRA toeni adhabu kali kwa baadhi ya redio na televisheni

    Kumekuwa na wimbi kubwa sana la uanzishaji wa vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini jambo ambalo ni zuri sana. Ila kutokana na jinsi vyombo hivi vingi vya habari haswa redio na TV zinavyofanya kazi zake nyingi hazina tija katika jamii. Redio na TV nyingi zimekuwa ni wakala wa kuharibu...
  5. Chachu Ombara

    ACT Wazalendo: Kufungiwa kwa Gazeti la Mwananchi Mtandaoni ni kuminya Uhuru wa Habari

    KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANANCHI MTANDAONI NI KUMINYA UHURU WA HABARI ACT Wazalendo tunapinga vikali kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi Mtandaoni na kuitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio hilo ili gazeti liendelee kutoa huduma ya habari kwa umma...
  6. D

    TCRA Polisi wako wapi watu wanaibiwa kupitia hii mikopo mtandaoni? Jerry Silaa msaidie Rais

    Kuna wimbi kubwa sana la matapeli likitumia majina ya watu maarufu km Mohamed Dewji(MO), Tulia Ackson, Jokate Mwegelo n.k. Hawa watu ni matapeli na wana mtandao mkubwa, unakuta kwenye comments wanashukuru kuwa wamepata mikopo kumbe ulaghai ili uiingie mkenge. Namna ya kukuingiza mkenge...
  7. lufungulo k

    TCRA nahitaji Mrejesho

    Nimekuwa mara nyingi nikitumiwa ujumbe wa WIZI na ULAGHAI kupitia simu yangu ya mkononi. Kutokana na kero hii TCRA wameweka utaratibu wa kureport kadhia hii kupitia no 1540 na wanajibu kwa sms muda huo huo. Wanakiri kupokea taarifa yako na kuahidi KUISHUGHULIKIA . Ombi langu kwako warudishe...
  8. Mr Chromium

    Kulalamika kwa SGR kuhusu kuhujumiwa ni management failure!

    Hii habari nimeiona wasafi. Takukuru wameibua hujuma za wateja wanaokata ticket za masafa mafupi kisha wanasafiri masafa marefu!! Kwanza ncheke😂😂😂😂 Ni kweli tumefikia huku yaani kaishu kadogo hivo hadi takukuru igundue Uongozi wa Treni haujajua? Na kwwnini iwe ishu wakati ni vitu ambavyo huwa...
  9. A

    Tumechoka wananchi wa Karagwe na mamlaka za TANESCO pamoja na TCRA

    Kutoka Rwambaizi Karagwe Kagera wananchi tumekuwa tukiteseka Sana kwanza kuna swala vocha wenye maduka wamekuwa wakijapangia Bei za vocha ya sh 500 wanaiuza kuanzia 600 hadi 700 tunaomba Jamiiforums mtupazie sauti watanzania kwa mamlaka husika. Pili swala la umeme wamekuwa wakikata umeme...
  10. guojr

    Ushauri Kwa TCRA na Jeshi la Polisi

    Habari za muda huu wana jukwaa. Leo nimekuja na ushauri kwa TCRA na jeshi la Polisi kutokana na uhalifu wa mtandaoni. Uhalifu wenyewe ni huu unaohusu kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno wa kitapeli. Katika utafiti wangu mdogo, nimegundua mambo kadhaa. Mosi, namba zinazotumika kufanya utapeli ni...
  11. S

    Mikopo ya online: Rais Samia wachunguze Mkurugenzi Mkuu TCRA, Gavan BOT na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

    Rais Samia, kwanza nashukuru umemuondoa Nape Nnauye kwasababu TCRA na Tume ya Ulinzi wa Taaifa Binfsi(PDPC), ni taasisi zilikuwa chini yake na mpaka anaondoka, hatuijaona hizi taasisi zikiwa serious katika kuchukua hatua(sijaona wala kusika waliokamatwa kwa kudhalilisha watanzania). Naomba...
  12. De Professor

    Madudu ya APP za mikopo online.Wizara husika Mnakazi gani ofisini??? #Wizara ya Fedha #Wizara ya Mawasiliano (TCRA)

    Kwa Niaba ya Wadau wananchi wa kawaida kabisa nadhani ni wakati sahihi wa kupazia sauti kadha hii ambayo imefumbiwa macho kwa muda mrefu na vyombo vyetu husika. Week chache zilizopita niliamua kuvalia njunga swala moja la mtu ambae alikua akidaiwa na App moja ya Mtandaoni ikiitwa *SUNN LOAN...
  13. Kanye2016

    Fursa Kwa Madada WA Kitanzania ambao hawajaolewa.

    Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza. Kwenye pita pita zangu huko mtandaoni nikakutana na Habari ya kijana Mmoja WA ki Jerumani anataka msichana WA Kitanzania Kwa lengo la ndoa. Nimeweka screenshot hapo chini inajieleza kabisa. Mkitaka maelezo zaidi mnaweza kwenda kwenye account yake ipo...
  14. Stuxnet

    TCRA Walimpongeza Nape Baada Ya Kutumbuliwa na Rais: Hii ni Dharau Kwa Mamlaka

    Labda wawe wamefuta kwa vile wao ndiyo custodians wa mitandao nchini. Ila Bodi na Menejimenti ya TCRA ilimpongeza Waziri wao wa Zamani Nape Nauye baada ya kutumbuliwa juzi sambamba na TTCL, UCSAF na Posta. Pongezi kwa kazi nzuri kwa waliotenguliwa ni kama kashfa kwa Mamlaka ya Uteuzi...
  15. Kaka yake shetani

    Kwanini TCRA ilijiondoa mtandao X na wahanga wengi wapo mtandao huu?

    Kwa sasa naamini ili wasionekane hawausiki na yanayotokea TCRA waliondoa account yao. Ukweli mtandao X kuna viongozi wanaogopa kuwa na account au kama wanazo basi sio zao. Na lingine kama TCRA inaonekana kuwa vikwazo sana kwenye mambo mengi inawezekana na google nayo ikajiondoa tz
  16. Kamanda Asiyechoka

    Aliyekamatwa kwa kuchoma picha ya Rais Samia ahukumiwa faini Tsh. Milioni 5 au miaka miwili jela

    Kijana Shadrack Chaula (24) mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amehukumiwa faini ya Sh5 milioni au kifungo cha miaka miwili jela akishindwa kuilipa faini hiyo kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo mtandaoni. Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Julai 4...
  17. N

    FCC, TCRA, Pitieni jina la Crown Fm linashabihiyana na Clouds Fm!

    Jana (Julai 01' 2024) ndio siku rasmi Crown Fm wameanza kutangaza baada ya kumaliza majaribio, na leo ( Julai 02' 2024) wamerusha kipindi cha michezo. Kwa mtazamo wangu naona jina la Crown Fm na Clouds Fm kama hautakuwa makini katika usikilizaji unaweza sikIa kama wametamka Clouds Fm, na hiyo...
  18. Roving Journalist

    Nape: Tumewaagiza TCRA wachunguze wale wanaodhalilisha watu waliowakopesha Mtandaoni

    Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye amesema Serikali imetoa maeleko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwafuatilia na kuchunguza Watu wanaotumia taarifa za waliowakopesha Mtandaoni kwa lengo la kudhalilisha wakopaji. Amesema maelekezo hayo pia...
  19. Cute Wife

    Akaunti ya TCRA imeondolewa X (Twitter), kuna nini?

    Wakuu salam, Kama utakuwa mtembeleaji wa mtandao wa X utakuwa umeona hili. Accout ya TCRA imeondolewa X, na pia TCRA imeondoa X kwenye list ya matandao ambayo wanapatika! Je, nini kimetokea? Anko Elon atakuwa amewatimua baada ya sekeseke la kutaka kutufungia X? Au sababu wamegoma kuruhusu...
  20. The Supreme Conqueror

    TCRA yafuta akaunti yake ndani ya X/Twitter. Je, ni maandalizi ya kuifungia mtandao huo wa kijamii?

    Japo hatua hiyo inaweza kuwa imetokana na sababu nyingine, ukweli kwamba imetokea katika kipindi hiki cha vuguvugu kubwa kuishinikiza serikali iifungie X/Twitter unweza kuyumkinisha kuwa hizi ni dalili za awali za mtandao huo wa kijamii kufungiwa. Hata hivyo, wakati viongozi mbalimbali wakuu wa...
Back
Top Bottom