tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. GENTAMYCINE

    Je, hili Tangazo la Tigo linalotuhimiza kupata cha 'Asubuhi cha Tigo' TCRA na Serikali wamelibariki na kuona limekaa Kimaadili?

    Tuendeleeni tu Kuruhusu 'Upuuzi' na 'Uhuni' huu wa maneno yanayoashiria 'Ufirauni' kutumika na Makampuni ya Simu huku Serikali mkipokea Kodi yenu Kubwa na Maadili kwa Jamii na Kizazi kuzidi 'Kudidimia' tu. Kuna Kampuni nyingine nayo nimedokezwa inataka kuja na 'Promo' yake isemayo ' Ukitaka...
  2. K

    Namba tuliyoambiwa na TCRA kuitumia kuhakiki vitambulisho haisaidii chochote

    TCRA na "106# wanafaidika na nini? Maana ni kama usanii. Hiyo ni namba tuliyoambiwa kuitumia kuhakiki iwapo vitambulisho vyetu vimesajili namba ambazo hatuzitambui. Kwa bahati mbaya kila nikijaribu wala sipati majibu. Sasa nauliza, iwapo TCRA wanatumia nguvu nyingi kuitangaza kupitia clouds...
  3. Rufiji dam

    MCT na TCRA chunguzeni kipindi cha Clouds 360

    Hiki kipindi kimekuwa kinaleta ukakasi sana katika afya ya habari nchini. Mara nyingi kimetumika kama dekio la kusafisha watuhumiwa hasa watendaji wa serikali. Kipindi kimekuwa kinaendeshwa kwa waandaji kujipendekeza rejea zama za utawala wa JPM. MCT na TCRA chukue hatua juu ya kipindi hiki...
  4. ommytk

    TCRA, matapeli wa kupiga simu na kutuma meseji wataisha lini?

    TCRA hivi awa matapeli kutumia simu mbona bado wapo wengí na sasa wanazidi kuongezeka si line tunasajiri na alama za vidole iweje waendelee kuwepo. Leo naona tuanze kuolozesha humu namba za matapeli wanautuma msg zile za waganga na mtoto wako kaumia tupo hospital na wale wanajifanya huduma kwa...
  5. Lububi

    Nawatetea Serikali, TCRA, Polisi na mitandao ya simu kuhusu utapeli wa "Tafadhali tuma kwa namba hii"

    Nitangulize samahani kwa wadau watakaodhani natetea uhalifu (ubaya) wa namna yoyote. Lakini wema na ubaya havijawai kuachana kama mwanga na giza. Ifikie hatua waibiwaji tujitathmini. Ubaya ukikwaza wengi mtu timamu huangalia wapi tatizo linaanzia. Hili la wizi wa mtandaon kama "tafadhari...
  6. K

    TCRA CCC Yatoa Ushauri kwa Watumiaji wa Huduma za mawasiliano

    Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano latoa ushauri kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ikiwemo kutumia fursa zilizopo kwa manufaa ya kujiletea maendeleo
  7. The Palm Tree

    Kuhusu TCRA na huduma za internet bundle mitandao mbalimbali: Mbona haiko kama tulivyoambiwa?

    Kwenu TCRA na waziri wa mawasiliano na uchukuzi, mbona mambo hayako kama ambavyo mlitaka tuamini kuwa yatakuwa? 1. Gharama ya bundle bado zinatofautiana kutoka mtandao mmoja na mwingine japo mlisema mnaweka uniformity (Sera ya Ujamaa na Kujitegemea) 2. Hakuna kushea bando kama ambavyo...
  8. S

    Kwa TANESCO sawa, kwanini sio kwa BASATA na TCRA?

    Hongera Mh. Kalemani kwa kuwawajibisha watumishi ambao aidha wamehisika kusababisha usumbufu au vyovyote vile. Pia Mh. Kalemani amekua muungwana kwa kuwaomba radhi Watanzania kwa usumbufu uliojitokeza. Wakati huohuo waziri mkuu ameenda mbali zaidi kwa kutoa maagizo kwamba wakae pembeni wapishe...
  9. Miss Zomboko

    TCRA yakaribisha maoni juu ya maboresho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018, ili ziwe rafiki

    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewakaribisha Watanzania, kutoa maoni yao juu ya maboresho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018, ili ziwe rafiki kwa matumizi. Wito huo umetolewa leo Jumanne tarehe 11 Mei 2021, Mkoani Morgoro na Mkuu wa Sheria wa TCRA, Dk. Phillip Filikunjombe...
  10. Kelela

    Vipi hatma ya wito wa kutumia kikoa cha .com Tanzania?

    Mwaka jana (2020) mwezi wa kwanza TCRA ilitoa wito ya watu wote kutumia .co.tz na ukitumia .com ni kosa ambalo unaweza kulipishwa faili au kifungo. Swali langu ni je, mpaka sasa sheria hiyo ipo? na kama bado ipo kwa nini baadhi ya watu wanaendelea kutumia .com? naomba ufafanuzi kwa wanaofahamu...
  11. Analogia Malenga

    Zimbabwe yashutumiwa kukiuka haki za binadamu

    Vikundi vya haki za binadamu nchini Zimbabwe vinasema serikali imekuwa ikikiuka haki za kimsingi za watu tangu kuanza kwa ugonjwa wa COVID-19. Vikundi hivyo viliwasilisha uchunguzi wao katika mkutano wa njia ya mtandao na maafisa katika mji mkuu Alhamisi. Katika mkutano huo, vikundi vya haki...
  12. MPUNGA MMOJA

    TCRA: Sasa vifurushi vimerudi kama awali

    “Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuwajulisha kwamba sasa vifurushi vya mawasiliano ya simu vimerudi kama awali, endapo kuna Mwananchi bado anapata changamoto ya huduma hii tuandikie TCRA ==== Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaarifu kuwa vifushi vya mawasiliano...
  13. GENTAMYCINE

    Serikali na TCRA kuurudisha rasmi Mtandao wa Twitter bila kutumia VPN 'Kimya Kimya' bila kutuomba Radhi ni 'Kutudharau' Watanzania

    Hivi ni kwanini wenye Mamlaka wengi nchini Tanzania neno Samahani ( Naomba Radhi ) Kwenu huwa ni Gumu sana huku mkidhani mkisema itakuwa mnajidhalilisha au kuonekana dhaifu? Yaani kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka Jana ( 2020 ) hadi hii Leo Huduma ya Mtandao wa Twitter ilikuwa haipatikani mpaka...
  14. MPUNGA MMOJA

    TCRA: Mawakala wa mitaani ruksa kusajili line za simu

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeondoa zuio la kampuni za simu nchini kuwatumia mawakala kusajili laini za simu mitaani. Akizungumza Jumatano Aprili 14, 2021 mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Dk Jabir Bakari amesema mamlaka hiyo imeondoa zuio hilo na sasa kampuni za simu zitaendelea...
  15. M

    Tafadhali mliowaelewa TCRA na sababu zao walizotoa kuhusu bei za 'Vifurushi' katika Ukurasa wa 3 Gazeti la The Citizen la leo mtueleweshe na wengine

    Kila kukicha tu 'Maajabu' mengi yanagundulika nchini Tanzania na huenda nchi yetu ikawa imebarikiwa Kimaajabu hadi Raia wake ni wa ajabu. Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Makampuni ya Simu yanaweza Kupandisha bei za 'Vifurushi' haraka, ila katika Kuvishusha wanachelewa. TCRA hongereni...
  16. S

    TCRA itupieni macho kampuni ya Vodacom kwa kukata fedha za wateja kwa madai mteja kajiunga na huduma fulani wakati si kweli

    TCRA, nawaomba muichunguze kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom kwa kukata fedha unaponunua muda wa maongezi kwa hoja kuwa mteja uliomba/ulijiunga na huduma fulani ambayo hutakiwa kulipia kwa kukatwa fedha mara tu unaponunua muda wa maongezi. Mimi binafai ni mhanga wa hili jambo kwani...
  17. Full charge

    Maoni na maswali yangu kwa TCRA

    Poleni na majukumu ndugu zangu wana jamvi. (a)Kwanini kusiwe na namba ya huduma ya TCRA? [emoji117] Yaani mteja wa mtandao husika anaponunua kifurushi kikaisha kabla ya muda wake apige simu TCRA ili wahoji au kuchunguza uhalali wa matumizi. Hapa ikibainika mtandao umefanya wizi umrudishie mteja...
  18. R

    Mitandao ya simu bado wamegoma kurudisha vifurushi vya zamani, DG TCRA nadhani nawe hapo hapakutoshi, ukimzingua atakuzingua

    Lilitoka Tangazo TCRA kuwa warudishe vifurushi vya zamani wakati wanapitia upya new rates. Wamegoma kwa viburi na DG hajafanya lolote. Jana Rais kampa angalizo juu ya "uchafu" uliopo TCRA. Naona bado DG amelala, haamini kama kuna uchafu katika makampuni ya simu! Wana viburi.
  19. Maleven

    Sijasikia viongozi, wabunge na watu maarufu wakitetea wananchi kuhusu vifurushi vipya

    Au ndo haifai kuongea wakati wa kula? Au ndo wenzetu wanayumia wifi za office hawajapata taarifa? Nani wa kupaza sauti kueleza hali hii? Kwanini mitandao mingi imekaidi?
  20. Mtini

    Kuhusu vifurushi: TCRA, Ndugulile na Serikali mmetufanya Watanzania kama watoto wadogo

    Wanabodi mnakumbuka mwezi wa pili walipandisha bei za vifurushi, tukalalamika zipunguzwe wakatuahidi mwezi wa 4. Mwezi wa 4 vimepanda zaidi tumepiga kelele wameturudisha kwenye bei zilezile za mwezi wa pili tulizokuwa tunazipigia kelele, nasi bila kujua tunashangilia. Kifupi Serikali...
Back
Top Bottom