tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. mgt software

    TBS, TCRA na TRA washindwa kuisaidia Serikali kuondoa spea feki za Simu. Mafundi simu waishia lockup wasijue lakufanya

    Wana Jf Serilikali kupitia ajent zake za kitaifa kwa pamoja wanaungana kuikosesha mapata serikali na kuleta mtafaruku mkubwa kati ya mafundi simu na wateja wao. TBS, TCRA na TRA zilivyoshindwa Nazi zao kila moja nitaelezea makosa yao TBS wameshindwa kuajiri vijana wenye weledi kutambua vitu...
  2. Kurzweil

    TCRA: Yatoa neno kwa Vyombo vya Habari vinavyowatumia watangazaji wasio na Taaluma ya Habari

    MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) YATOA ONYO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUAJIRI WATANGAZAJI WASIO NA TAALUMA. Mamlaka ya Mawasiliano nchini imetoa onyo kwa vyombo vya habari hususani redio na televisheni kwa kile inachodai kuwa vyombo hivyo vimekua na tabia ya kuajiri watangazaji wasio...
  3. MamaSamia2025

    TCRA, TRA na Mamlaka zingine za Serikali hazipaswi kulaumiwa

    Natumaini mko salama. Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kuhusu mamlaka za kiserikali hasa zinazolaumiwa zaidi. Kwa muda mrefu Mamlaka hasa TCRA na TRA zimekuwa zikitupiwa lawama wanapofanya kazi zao kwa mujibu wa sheria. Binafsi naona hawastahili kulaumiwa endapo hakuna...
  4. J

    TCRA yawafungia Wasafi FM kwa kutumia lugha za matusi

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha utoaji huduma za utangazaji kwa Wasafi FM kwa muda wa siku saba kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 18 mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatua hiyo ni kutokana na...
  5. J

    Clouds wamaliza adhabu ya TCRA warudi hewani kwa mbwembwe!

    Hatimaye Clouds Media Group wamemaliza kutumikia adhabu ya kifungo cha siku 7 waliyopewa na TCRA na wamerudi hewani rasmi. Kinachoendelea sasa luningani ni sherehe ya wafanyakazi baada ya kutoka kifungoni, ni full shangwe. CCM hoyeeee! Maendeleo hayana vyama!
  6. FRANCIS DA DON

    Napendekeza TCRA wapige marufuku matangazo ya BBC nchini Tanzania. Wameitukana kumbukumbu ya Mwl. Nyerere

    Eti wameonyesha kipindi cha historia ya ukombozi wa Afrika, ambapo wametaja wapambania uhuru kama akina Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba na Nelson Mandela, Jomo Kenyatta miongoni mwa wengi. Lakini cha ajabu walipofika kwenye ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika wameishia kumtaja Mandela tu na...
  7. Miss Zomboko

    TCRA yaipiga faini ya Tsh. bilioni 11.89 Kampuni ya Intaneti ya Raha Limited kwa kuendesha shughuli zake bila kuwa na kibali

    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipiga Faini ya Sh.bilioni 11.89 Kampuni ya Raha Limited watoa huduma ya Internet kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutumia masafa ya mawasiliano ya Radio katika wigo 1452-1482 MHZ bila kuwa na leseni halali kutoka TCRA tangu 24 Machi 2020. Akizungumza na...
  8. Return Of Undertaker

    TCRA, inakuwaje magazeti ya Uhuru na Jamvi la Habari hayajafungiwa kwa kuripoti habari sawa na Clouds Media?

    Hapa kuna tofauti gani au nayo ni sehemu ya kuendeleza udhalimu na kutishia vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu kutotangaza habari za upinzani.
  9. Roving Journalist

    Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia vituo vya habari vya Clouds TV na Radio kwa siku saba kuanzia kesho Agosti 28 na adhabu ya kuomba radhi siku nzima ya leo kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za Uchaguzi. TCRA imesema kosa walilolifanya ni...
  10. K

    TCRA wana Mamlaka makubwa kuliko Mhimili wa Mahakama?

    Sijui kama tumebaini TCRA wanachukua jukumu la mahakama na kujitwisha wao. Wamejitungia kanuni za wao kutuhumu, kusikiliza na kuhukumu kitu ambacho siyo haki. Uwezi nituhumu then ukajakusema nimekushinda kwa hoja lazima utaonesha nimeshindwa Hiki wanachofanya cha kutafsiri hadi Sheria zisizo...
  11. GENTAMYCINE

    Hadi Kesho nisipoona Clouds Media Group, MCT, TCRA na Serikali ( Wizara ) husika vimemchukulia hatua Kali Mtangazaji Adam Mchomvu nitawadharau mno

    Hatuwezi kumuacha Mpuuzi Mmoja kwasababu tu ya Mibange yake na Malezi yake ya hovyo hovyo atuchafulie Tasnia yetu nzima nchini Tanzania.
  12. dubu

    TCRA wanafanya kazi kwa upendeleo, wakati wakipiga mikwara wanaojiunga mubashara na vituo mbalimbali, wale wa CCM wanaachwa

    Wakuu Salaam, Nchi yetu Utawala wa Sheria wa Sheria Umeshrink Nchini Tanzania, Tunafuata Matanko ya Wanasiasa ndiyo yamegeuka kuwa Sheria. Hivi karibuni MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilivitaka vituo vya redio, televisheni na wanaotoa huduma za maudhui mtandaoni kuomba kibali/ ruhusa...
  13. Miss Zomboko

    Rungu la TCRA lawashukia Wasafi Tv, Clouds FM, Carry Mastory, Radio one na RFA kwa kurusha maudhui yaliyo kinyume na Sheria

    TCRA imetoa onyo kali na kuziweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu Radio Free Africa na Radio One Stereo kwa kukiuka kanuni za utangazaji viliporusha kipindi cha Amka na BBC ambapo Tundu Lissu aliituhumu serikali kuwazuia viongozi wa Chadema kumuaga Hayati Rais Benjamin Mkapa. Wasafi Media...
  14. Miss Zomboko

    Fahamu sababu zinazolazimisha vituo vya habari kuomba kibali TCRA kuweza kurusha matangazo kutoka vituo vya nje

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeeleza sababu tatu za kutaka vituo vya utangazaji nchini vinavyojiunga na vituo vingine vya kanda, nje ya nchi na raia wa kigeni kuwatembelea kupata kibali kabla ya kufanya hivyo. Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye gazeti hili jana, na Mkurugenzi...
  15. Erythrocyte

    Sheria mpya za TCRA : Vipindi vya mapenzi kama Ala za Roho na Chombeza Time kuanza saa 6 usiku

    Kumbe sasa vinatakiwa kuanza saa 6 usiku badala ya saa 4 usiku , labda uchumi wa kati umesababisha watoto kuchelewa kulala .
  16. Jidu La Mabambasi

    TCRA an instrument of repression? Chombo cha kukanyaga haki za uhuru wa habari?

    Mimi si mwanasiasa. Mimi si mpenzi wau mfuasi wa Lissu(actually nimekuwa nikipinga mambo mengi ya Lissu na maneno yake) Mimi ni mtanzania huru chini ya katiba ya nchi ya Tanzania. Kinachonishangaza ni juhudi za watu fulani ndani ya serikali kukiuka uhuru wa Mtanzania wa kawaida kupata habari na...
  17. Erythrocyte

    Uchaguzi 2020 Lissu ailipua TCRA na Idara ya Habari Maelezo kwa kunyanyasa Vyombo vya Habari vinavyoripoti habari zake, aahidi kuifutilia mbali

    Akizungumza kutoka Singida Mgombea huyo wa Urais wa CHADEMA, Mhe. Lissu amefichua njama za kishamba za TCRA na idara ya habari maelezo za kushughulikia vyombo vya habari vinavyoripoti habari zake. Tayari BBC wamepigwa faini ya Tsh. mil. 15 kwa kurusha mahojiano na Tundu Lissu huku RFA ikiambiwa...
  18. Return Of Undertaker

    Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

    Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo amevitaka Vituo vya Utangazaji (Radio, Televisheni, Blogs na Online Tv) kuzingatia Kanuni mpya za Maudhui Mtandaoni 2020 na Kanuni Mpya za Redio na Televisheni 2020. Mihayo ameyasema hayo wakati wa kikao kati...
  19. E

    Nashauri TAKUKURU waichunguze TCRA Tanzania

    Wana jf, nimatumaini yangu jukwaa letu pendwa la jf haliwezi kukoswa watu wa takukuru ambao siku hizi ndio kimbilio na mkombozi kwa watanzania wanyonge. Takukuru nawaomba muwachunguze TCRA na makampuni ya simu yote. Hii ni kwasababu kumekuwa na wizi mkubwa kwa wateja wanaotumia mitandao ya...
Back
Top Bottom