09/11/2022: Simba Queen inaenda kuirudisha heshima ya Taifa tena baada ya Yanga SC kujaribu kuipoteza

09/11/2022: Simba Queen inaenda kuirudisha heshima ya Taifa tena baada ya Yanga SC kujaribu kuipoteza

Wametolewa Geita Gold na Azam mapema kabisa, wasiipoteze hiyo heshima! Imetolewa timu ya U17, U23!! Hawa wote wasiipoteze hiyo heshima!

Ila Yanga ikitolewa hiyo kesho, ndiyo ipoteze heshima ya Taifa!! Taifa lipi hilo kwanza!! Hili hili la kichwa cha mwenda wazimu!!

Nyinyi mbona mlitolewa misimu michache iliyopita na UD Songo na wale Galaxy? Hamkupoteza hiyo heshima ya Taifa? Isipokuwa tu Yanga!!!

Hakika aliyewaita mbumbumbu hakukosea hata kidogo.

By the way, hiyo timu yenu haina uwezo wa kuitoa Mamelodi Sundowns. Hivyo acheni porojo zenu za kucheza mpira nje ya uwanja.
Kesho Taifa litaingia kwenye aibu nyingine kuuuubwa sana
 
giphy.gif
JamiiForums685660863.gif
 
Ungeweza kuwapongeza au kuwatia moyo hawa wakina dada wa simba bila kuisema vibaya yanga, kwa timu ambazo yanga imecheza nazo hatua ya mtoano wala hakuna aibu yoyote maana ni timu nzuri ingekua aibu yanga angetolewa na wale zalan.. kwenye hatua ya mtoano sometimes kuna bahati ya kupangwa na timu dhaifu au timu imara kama yanga ingepangwa na big bullets au agosto ingepita bila ubishi ila simba kwa ubora wao wa sasa sina uhakika kama wangeweza kuwatoa al hilal au club african

Mkuu inakuakuaje hiii bahati mbaya iwe kwa Yanga kila msimu?! Hamuoni kama imefika mda sasa hii michuano msiwe mnapeleka timu, mana mnakua hamna tofauti na timu za Somalia au Sudan Kusini.
 
Kuna team ilikua inapigwa gwara kila wiki wala Taifa halikuhusika na hio aibu , kila mtu abebe mzigo wake
Wahenga wana msemo wao..
" Siku zote anayecheka mwisho ndio anacheka sana"
Huo msimu unaousema, nani alicheka mwisho?

Shida yenu Uto, si mwanzoni wala mwishoni hamcheki.. Ni majonzi mda wote.
 
Mkuu inakuakuaje hiii bahati mbaya iwe kwa Yanga kila msimu?! Hamuoni kama imefika mda sasa hii michuano msiwe mnapeleka timu, mana mnakua hamna tofauti na timu za Somalia au Sudan Kusini.
Yanga bado hajawa na dna na hii michuano anahitaji kushiriki mara kwa mara akiwa na focus kwa sasa ni msimu wa pili tu wa gsm pale yanga huwezi kulinganisha na simba ambae alianza kujipanga miaka takribani 5 nyuma
 
Sawa Mkuu.. Kila la heri mnapoendelea kujitafuta katika michuano hii. Ila mkumbuke siku gari lenu likichanganya, Simba SC atakua hakamatiki CAF.
 
Sawa Mkuu.. Kila la heri mnapoendelea kujitafuta katika michuano hii. Ila mkumbuke siku gari lenu likichanganya, Simba SC atakua hakamatiki CAF.
Inawezekana pia yanga akakaa sawa na akaja kufanya vizuri zaidi ya simba ambae mafanikio yake ya juu zaidi ni robo fainali yote yanawezekana mkuu
 
Back
Top Bottom