09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

Stori ni mbowe aomba POO..dadeki...
 
Huwezi kuonyeshwa kila kitu Mkuu

Ila ukitaka kupata uhalisia jitie kichaa usogee jukwaa kuu wanapokaa wakubwa bila taarfa utajifunza kitu
Hata ukisogea jukwaa kuu watakuua bila kujua ulikuwa unataka nini au umetumwa na nani, uhalisia wa kitu unatakiwa uanzie kwenye maonyesho kama yale na kwenye field , sio mnajidai wajuaji likitokea tukio mnategemea wananchi ndio wawe msaada. yani wananchi ndo wakuyahurumia majeshi yetu klweli au wao ndio wa kutuhurumia?
 
Hili ni swali au maoni yako mkuu maana kichwa kimeakaa kiainatu.
mchanganyiko mkuu swali pamoja na maoni kuwa mwakani sio mbaya na akina wema sepetu wakahusika maana kama ishu ni maigizo tu hata wao wanaweza kufanya maigizo na kufikisha ujumbe
 
Huwezi kuonyeshwa kila kitu Mkuu

Ila ukitaka kupata uhalisia jitie kichaa usogee jukwaa kuu wanapokaa wakubwa bila taarfa utajifunza kitu
Na wewe kila mada umo, kazi unafanya saa ngapi? au hii ndo kazi uliyoajiliwa nayo?
 
kusema za ukweli wasukuma wamefurahi saaaaana. na magufuli si anawajua ndugu zake lazima awakoleze, watu saa 12 asubuhi wameshajaa uwanjani ha ha ha ha wakati wengine ndio wanaamka wao sijui wamekesha kwa kusubiri kuona maigizo fake ya makomandoo, ila makomandoo kama mpo humu mniwe radhi nadhani mnaelewa fika kuwa ujumbe wenu wote tumeuelewa kasoro wazee wa elf 7
 
CCM imelitia aibu Taifa huli kwa miongo mingi sasa karata waliiokuja nayo ni kura za Wasukuma
Kuongea kikabila katika dhifa hii ni kuligawa taifa hili
 
Aliye kwambia hayo mambo hayana uhalisia ni nani?
Sasa we jichanganye ndo ujue kuna uhalisia au ni maigizo
 
Sijui mleta mada ulikuwa na umri gani wakati ndege ya kijeshi ilipoanguka pale pembeni ya uwanja wa taifa mwaka 1979.

Tulikuwa tumetoka vitani Uganda, pakawa na onyesho la ndege kama zile zilizokatiza leo pale Kirumba.

Vita ni sawa na ugomvi wa mtu na rafiki yake, haijulikani ni lini marafiki watagombana na sababu itakuwa ni ipi, ndivyo yalivyo mataifa, na hapo ndipo ulipo umuhimu wa maandalizi ya kijeshi ya namna yoyote ile.
 


Heri ya Kuzaliwa Baba na Mama Tanganyika!
 
Viongozi wote makini na wazalendo wa nchi leo walikuwa pamoja na Watanzania Kirumba Mwanza kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru.

Ukiacha wale waliotoa udhuru kama JK, Bilal na wengineo sherehe zilipambwa na Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, JPM, Mbowe, Sumaye, Lowassa, Malecela Pinda, Lipumba, Shibuda, Shein, Majaliwa, Mama Samia n.k.

Sasa angalia wasaliti sasa walikokuwa:

1. Zitto Kabwe taarifa za kuaminika ni kwamba leo alionekana akiingia hoteli fulani akiwa na binti fulani hivi na kila alipokuwa akipumua kdg alikuwa ama akitumia akaunti yake ya twitter au ya Kigogo kubeza uhuru na kumbeza Mbowe binafsi!

2. Tundu Lissu: Huyu kaitumia siku hii kama kawaida yake akikutana na Wazungu akieleza uongo kuhusu nchi yake hadi wazungu wanajisemea moyoni "Hili boya la mwaka."

Membe: Alijifungia mahali akitokwa udenda akiangalia JPM akikagua gwaride.
 
Na Mwamba wa Kaskazini

Rais John Pombe Magufuli leo amefanya mambo kadhaa ya kihistoria akiwa katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa nchi yetu huko Jijini Mwanza.

Nimeona katika kuelewa mambo yatakayokumbukwa katika siku hii nitafakari nawe mambo haya 10:

1. Ameweka historia kwa mara ya kwanza sherehe za Uhuru wetu kufanyika nje ya Dar na Dodoma. Atakumbukwa;

2. Sherehe za Mwanza zimeleta umoja kati ya Bara na Zanzibar ambapo viongozi waandamizi wa pande zote wameshiriki akiwemo Rais Shein wa Zanzibar;

3 Rais ameweka rekodi ambapo katika siku mbili za kuelekea sherehe tu yeye Makamu, Waziri Mkuu na viongozi wengine wamezindua miradi ya marndeleo inayofikia Trilioni moja jijini Mwanza. Zote zikiwa fedha za walipakodi. Haijapata kutokea;

4. Wakati baadhi ya wanasiasa wakiishia kupiga soga twitter kuwa eti wananchi hawana furaha katika miaka 59 ya uhuru kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi, Uwanja wa Kirumba leo ulifulika pomoni wananchi wa Mwanza waliojawa na furaha kubwa hadi kulazimika wengine kuhamishiwa na kuwekewa screen kwenye Viwanja vya Furahisha. Tena wananchi hawa hawakusombwa na malori wala mabasi, wamekuja wenyewe kwa usafiri wa umma, binafsi, bodaboda, bajaji na hata kwa miguu;

5. Viongozi wastaafu kibao wameshiriki wakiongozwa na Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, Mzee Malecela na Mzee Pinda hii ni kuonesha umoja wa kupigiwa mfano na mshikamano baina ya viongozi wastaafu na walioko sasa madarakani;

6. Viongozi wa vyama vya upinzani nao waweka tofauti zao kando na kusimama na MagufuliTena. Ukiona sehemu yupo mtu kama Mbowe, Lipumba na wengineo ujue hapo, sio lazima mtu aseme kaunga mkono juhudi, bali ni wazi pana upako wa umoja wa kisiasa.

7. Rais katambua mchango wa watangulizi wake wote wanne na amewashukuru kwa mchango wao mkubwa. Hii ni muhimu sana katika ujenzi wa Taifa. Ukiona mwanasiasa anabeza tu, anabeza nchi, anabeza mpaka watangulizi wa nchi basi ujue pana shida na upo uwezekano mkubwa wa njaa kuwa imehama kutoka tumboni hadi kichwani, Rais Magufuli kawatukuza, kawaenzi, kawashirikisha, wasijione wanyonge;

8. Rais kawatukuza viongozi wenzake wa kisiasa wakiwemo wapinzani na wanasiasa wastaafu kwa kuwapa nafasi ya kusalimia na kusema machache kuhusu uhuru mbele ya wananchi. Safi kabisa.

9. Rais kaeleza kwa ufasaha safari yetu ya miaka 58 mafanikio na changamoto zake. Kasema bayana tulipewa uhuru tukiwa tumechoka katika nyanja zote, ilibidi kupiga kazi na leo miaka 58 walau tunaiona nchi yetu iko mahali fulani katika sekta anuai;

10. Rais Magufuli sijabahatika kukutana naye walau kupeana naye mkono lakini ukweli unabaki huyu Mzee ni mnyenyekevu na mwenye huruma sana....Mungu amjaalie zaidi maana kuachia wafungwa 5533 haijapata kutokea idadi kubwa kama hiyo. Ni historia lakini inatokana na unyenyekevu wa ndani katika yakini ya moyo wake.

Alamsiki.

Ni mimi Mwamba (sema mara tatu) wa Kaskazini.
 
Leo hawa kuvunja matofali kwa kutumia vichwa?!

Huwa najiuliza vita ya matofali itaaanza lini au imewahi kupiganwa wapi?!
 
hivi yale maonyesho ya magwaride huwa yanasaidia nini?? miaka nenda rudi mambo ni yaleyale hawana ubunifu wowote!
 
hivi yale maonyesho ya magwaride huwa yanasaidia nini?? miaka nenda rudi mambo ni yaleyale hawana ubunifu wowote!
Daaah nami pia hili swali nimejiuliza mnooo, mfano lile la kimya kimya sijuii
Hivi lengo ni ninii??
Maaana naona watu wazima wenye familia wanacheza cheza tuu
Malengo haswaaa ni niniiiii???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…