09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

1575901313459.png


Waziri mkuu za zamani, Edward Lowassa amesema Rais Magufuli akiongoza nchi kwa miaka 10 itapiga hatua kubwa katika maendeleo.

Lowassa ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mjini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.

"Amani ndio msingi anaoutumia mheshimiwa Magufuli leo kuongoza nchi yetu, kuleta mshikamano na umoja, nampongeza amefanya kazi nzuri sana…kama akiachiwa akapiga miaka yake kumi…kumi mheshimiwa nchi hii itabadilika,” – Amesema Lowassa

Lowassa alikihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015 na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako alipitishwa kugombea urais mwaka 2015 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu, lakini baadaye Machi Mosi, 2019, alirejea CCM.
 
Makomandoo wale wako kwajili ya Watu fulani na sio vinginevyo. Ila kwa upande mwingine ni ujumbe tosha kwake kuwa inakuaje watu maarufu wanatekwa na sisi tupo ila hutaki kutupa kazi ya kuonyesha umahiri wetu.
 
wajuvi tupieni hiyo clip ya sungusungu...waganga
 
Huwezi kuonyeshwa kila kitu Mkuu

Ila ukitaka kupata uhalisia jitie kichaa usogee jukwaa kuu wanapokaa wakubwa bila taarfa utajifunza kitu
Ule ni ujumbe kwa jiwe kuwa rasimali watu zipo kwanini asizitumie kwenye Matukio ya ajabu kama hayo
 
Hili ni swali au maoni yako mkuu maana kichwa kimeakaa kiainatu.
 
Huwezi kuonyeshwa kila kitu Mkuu

Ila ukitaka kupata uhalisia jitie kichaa usogee jukwaa kuu wanapokaa wakubwa bila taarfa utajifunza kitu

Acha kuongea vitisho vya kitoto, umeambiwa Mo alikuwa mtu maarufu na akatekwa, hayo maigizo hapo uwanjani mbona hayakugeuzwa kuwa kweli? Hilo zoezi kila mwaka linafanyika mpaka linachosa maana uhalisia ni tofauti na huo usanii hapo uwanjani. Labda ilikuwa ni kuwakoga wasukuma wasiojua lolote.
 
Back
Top Bottom