Maadhimisho ya Uhuru na Jamhuri pia Muungano wa Tanzania tokea tupate Uhuru yamekuwa yakitumika kutoa msamaha ya wafungwa kwa masharti yaliyopo kikanuni.
Tokea Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa hadi Kikwete wamekuwa wakifanya tendo hilo la kiutu kimya kimya. Kwa maana tunatangaziwa idadi na aina ya walio nufaika.
Maajabu ya awamu hii ni kila jambo wafanyalo kulitumia kisiasa, hata msamaha wa wafungwa?
Leo mikoa mingi Wakuu wa mikoa wamekuwepo kwenye kuachiwa na huku baadhi ya wafungwa wakiwa tayari wamepewa maelekezo ya nini waongee kwa waandishi walio ongozana nao kuhusu sifa kwa Rais.
Kweli kizuri chajiuza kibaya chajitembeza, wasipofanya hivyo watapotea mazima.
Nguvu ya kujionyesha ni wema ni kubwa mno kwa vile ni wabaya.