1 Zambian Kwacha equals 142.40 Tanzanian Shilling

1 Zambian Kwacha equals 142.40 Tanzanian Shilling

Una maanisha nini ukisema wana maisha kuliko sisi?
Hii kitu ndio uwa inawachanganya hata wakenya wakijinasibu pesa yao ina thamani kubwa kuizidi ya so wana maisha kuliko sisi,huku wakiwa hawajui pesa yao ina thamani kuliko yen,iwapo thamani ya pesa ingekua inaenda life la huku ground wako wangekua na good time kuliko wajapenga
 
Uchumi kuwa juu ina maana gani? Unamaanisha nini unaposema uchumi upo juu au upo chini?
Sidhani kama unanitendea haki kunibambika swali wakati huo ktk maelezo yangu kuna maswali yakujibu.
Ila kwa ufahamu wangu na kwa baadhi ya rejea uchumi juu maana yake vipo vigezo vingi.Haswa GDP matters!
 
Pesa ya Kenya ipo juu kuishinda pesa ya China na Japani!! lakini tukija kwenye uchumi ni kinyume chake Kenya ipo chimoni

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Hapo kuhusu Ksh kuwa juu zaidi ya pesa ya china (Yuan) si kweli.

Pesa ya China ipo juu sana ukibadilisha na pesa ya Kenya

1 Chinene Yuan = 17.59 Ksh
 
Hawa Zambia waliamua ku-demote sifuri kadhaa katika thamani za pesa zao. Hivyo thamani halisi si ile uionayo machoni. Ni kama vile sarafu 500 za Mozambique kwa Tanzania ni 18000 kitu ambacho si kweli.
Mara nyingi hii huchangizwa pale pesa ikosapo thamani(yaani purchasing power) kwa sababu mbalimbali kuu ikiwa ni inflation.
Katika hali hiyo Serikali huamua kufanya hivyo.
Njia hii inaweza kufanya kazi au ikafeli vilevile. Mfano Zambia wamefanikiwa kuwashawishi wananchi wao lakini Zimbabwe hawakuweza kufanya hivyo. Mengine fanya Utafiti. Ahsante.
 
Ni kweli mkuu japo cc tunaobadili huwa tunapewa kwa 140
,ila imeshuka thamani maana kuna kipindi ilikuwa 1kwacha ni sasa na 200tzsh
 
Zambia sukari 1kg 20k = 2840sh

Zambia mafuta ya kupikia 2ltr 100k = 14200sh

Zambia mche wa Sabuni 28k = 3976sh

Zambia petrol 1ltr 27k = 3834

Zambia diesel 1ltr 29k = 4118sh

Haya tuambie huko kwenu hizo bidhaa mnanunua Kwa bei gani.
Hapo kwenye sukarii umedanganya,tunduma tunategemea sukari ya zambia ambayo ni bei nafuu kuliko ya tz,sijui wanajumlishaje ila rejareja tunauziwa 1kg kwa 2500
 
Zambia waliondo sifuri tatu kwenye kwacha. Kwacha 1000 sasa hivi ni sawa na kwacha 1. Mfano na sisi tuamue kupunguza sifuri tatu na buku tukaita tsh 1. Mwekundu tukamuita tsh 10.
Hapana,10k ndio sawa na buku kwao,na 100k ndio sawa na elfu10
 
Hapo kwenye sukarii umedanganya,tunduma tunategemea sukari ya zambia ambayo ni bei nafuu kuliko ya tz,sijui wanajumlishaje ila rejareja tunauziwa 1kg kwa 2500
Hiyo sukari unayonunua 2500 ni ya Malawi sio ya Zambia, Sukari ya Zambia bei ya jumla kwa katoni 390k haya piga hesabu 390x144= 56160

Kwa hiyo ajumue 56160 auze 2500 apate 50,000.......ya Malawi katoni 44000sh ndio hiyo unayouziwa 2500 (ilovo) soma

Tunduma 90% ya sukari unayoiona mtaani ni ya Malawi.
 
ASALI KUTOKA TABORA.

Nauza Asali Ya Jumla Na Rejareja
Ipo Ya Nyuki Wadogo Na Nyuki Wakubwa.

Tunafunga Kwa Vipimo Tofauti Tofautii

Bei Ya Rejareja
Lita1 - 10,000 (Nyuki Wa Kubwa)
Lita1 - 25,000 (Nyuko Wa Dogo)

Bei Ya Jumla
Tuwasiliane Maana Kuna Ofa Zaidi

[emoji3513]0658 357537
Call/ WhatsApp/Sms
Tabora

[emoji625] [emoji593] Tunafanya Delivery Nchi Nzima.
 
Back
Top Bottom