CHAGOSI GERALD
Senior Member
- Jan 25, 2020
- 162
- 286
Haya ndiyo maneno ambayo vijana wengi wanashindwa kuyameza kwa sababu yana ladha kali kuliko ukoko wa ugali wa Mpangala.
Ukisusa JKT, mfumo unacheka.
Kicheko cha mfumo hakisikiki masikioni, lakini kinatetemesha mustakabali wako.
Akikuona huendi, anasema: “Huyu ndio rahisi kutumia baadae. Hana nidhamu, hana malezi, hana network, hana uelewa.”
Unadhani unaukwepa utumwa, kumbe unaingia kifua wazi kwenye utumwa wenye sumu zaidi: utumwa wa kutojua nguvu yako.
JKT sio tatizo.
Tatizo ni JKT iliyoporwa na mfumo, ikaachwa kuwa kivuli cha taasisi inayotakiwa kujenga taifa.
Wewe ukikaa pembeni, unaikomoa? La hasha.
UNAJIKOMOA na kizazi chako masikini.
Wewe ndio bidhaa. Wewe ndio nguvu kazi. Wewe ndio ungetengeneza mabadiliko.
Lakini umeamua kuhama kiwanja na kuwa shabiki wa pembeni, wakati mchezo unaoamua maisha ya vizazi vyako unaendelea bila wewe.
“HAMNA CHAMA CHA SIASA KINACHOKUPENDA.”
Ukiamini chama kinachopigania maslahi ya mwananchi, basi wewe ni aina maalum ya kiumbe ambaye hata malaika akikusimamia, bado utahonga shetani kwa ridhaa.
Vyama si wahisani.
Vyama ni madalali wa nguvu yako.
CCM inadalali. CHADEMA inataka kudalali.
Zote zina njaa ya mamlaka - si njaa ya kukutengenezea maisha bora.
Kila chama kinataka umfuate, halafu kikutumie kama ushahidi: “tuna wananchi wetu.”
Lakini hakuna chama kinachokuambia:
“Haki yako inalindwa na umoja wa wananchi, sio sisi.”
Hicho ndicho kipande cha ukweli vijana wengi wanaogopa kusoma:
Hakuna chama kilichowahi kuzuia umasikini wa kijana.
Hakuna chama kilichowahi kujenga mustakabali wa kijana.
Vyama vinatengeneza vyeo.
Wananchi wanatengeneza taifa.
“MAJESHI YOTE SI YA WANANCHI TENA.”
Wanasiasa wameshafika huko kabla yako.
Wameweka watu wao, wameweka mizizi yao, wameweka masikio yao.
Na sasa unadhani ukisusa, umewafundisha adabu?
Hapana.
Umejitenga na mahali ambapo ungeweza kupenyeza sauti yako, ujasiri wako, nguvu yako, intelijensia yako - na kuanzisha kizazi kipya cha maafisa wa kijeshi wanaotambua kuwa taifa si chama, taifa si chama, taifa SI chama...
Kwa kuikimbia JKT, umeacha uwanja wazi kwa wale ambao wanaenda ili kupata ulaji, si ili kujenga.
Kwa hiyo mfumo unaendelea kuzaa askari wanaomtii mwenye pesa, sio mwenye haki.
“SULUHISHO NI KUIPIGANIA JKT, SI KUIKIMBIA.”
JKT unayoiona leo ni kivuli cha ile JKT iliyoanzishwa miaka ya mwalimu - yenye viwanda, mashamba, uzalishaji, ujenzi wa utaifa, na nidhamu ya kuunda viongozi, si wafuata maagizo.
Leo imebaki kuwa sehemu ya kupitisha kijana alipige pushup, alime majaruba, na ajifunze kukaa kimya mbele ya amri hata kama amri ni upuuzi.
Lakini kijana mwenye akili anajua…
Huwezi kurekebisha nyumba kwa kukaa nje.
Lazima uingie ndani, uone ufa ulipo, uanze na tofali moja.
Uanze kuibadilisha ndani, si kwa mabango ya twitter.
Tengeneza kizazi kinachoingia ndani kikiwa na ufahamu, sio hofu.
Wenyewe wanasema “Tunaitekeleza kwa amri.”
Sisi tunapaswa kusema: “Tunairejesha kwa haki.”
Na ndio maana nakuambia:
Elimu niliyokupa si ya kupendeza - ni ya kuamsha.
Ukishindwa kuitumia, basi utakuwa unajichoma moto halafu unasema moto ni baridi.
Kushindwa kutumia elimu ni aina mpya ya upumbavu ambao hata Socrates asingependa kuufundisha.
Mimi nishamaliza kazi yangu.
Nyinyi wote mtakufa -
lakini maneno yangu hayatakufa.
Yatatembea mtaani yakivaa miili ya vizazi vipya.
Watayaita “mitazamo ya Gen Alpha.”
Wataamini ninakuja tena kila kizazi kuwakumbusha kwamba mabadiliko hayaji kwa kelele za nje, bali kwa ujasiri wa kuingia ndani ya moto bila kucheka wala kulia.