12th Africa Games, Morocco 2019: #TeamKenya Official Thread.

12th Africa Games, Morocco 2019: #TeamKenya Official Thread.

Leo ndio siku ya pili ya mchuano huo, na tayari kina dada wa Kenya wanaipeperusha bendera yetu juu kwa juu. Ni katika mchezo wa beach volleyball, timu ya Kenya ilifika kwenye fainali, bila kushindwa kwenye mechi zote za hapo awali! Fainali tulicheza dhidi ya Misri. Misri waliibuka washindi, 2-0 na wakanyakua medali ya dhahabu. Kenya tukajinyakulia medali ya fedha. Jamani majirani mpooo tunawamisi sana kule Rabat.
Tupooo. Bado tunabangua korosho na kuvuna mbaazi, tutajiunga nanyi hivi karibuni.Hongereni sana majirani.
 
Mitanzania mtachoka lini wanamichezo wenyu kwenda kote duniani na kurudi bila chochote kila wakati? Mtachoka lini kulipia wanamichezo kwenda tu utalii kupoteza "pesa zenu za ndani"???
 
Jamani majirani mpooo tunawamisi sana kule Rabat.
Obsession!
Badala ya kuhangaika tuwape mahindi unatumiss kwenye soccer beach!
Hongereni tupo bize kuwakusanyia mahinde majirani msije kufa njaa
 
Obsession!
Badala ya kuhangaika tuwape mahindi unatumiss kwenye soccer beach!
Hongereni tupo bize kuwakusanyia mahinde majirani msije kufa njaa
Africa Games zinajumuisha michezo tofauti, zaidi ya 30! Kenya tumewakilishwa na wanamichezo 290, kwenye michezo 22, sio beach volleyball tu. Tz mmewakilishwa na wanamichezo 6! 😀 Ni utani tu lakini, usiwe serious sana kwenye masuala kama spoti, utakufa mapema.
 
https://www.standardmedia.co.ke/article/2001339303/kenya-team-bags-two-medals-in-taekwondo-show
Kenya-Taekwondo.jpg
#TeamKenya[emoji1139][emoji1139] wanaendelea kung'aa kule Morocco. Riadha zinaanza tarehe 26 na kwenye mpira wa wavu, mechi ya kwanza ya Malkia Strikers itakuwa leo hii, dhidi ya kina dada wa Cameroun. Meanwhile..... wakenya wamejishindia medali zingine mbili, kwenye mchezo wa Taekwondo, ndani ya Prince Moulay Abdellah Sports Complex, Rabat. Faith Wanjiru Ogalo na Everlyn Alouch wamejinyakulia medali za fedha na shaba, mtawalia. Faith Wanjiru alimenyana na mshindi Yassine Hezami wa Morocco kwenye fainali za kitengo cha 73kgs. Huku Everlyn Alouch akimenyana na mmisri Maisoun Tolba kwenye mchuano wa kuwania medali ya fedha ya kitengo cha 67-73kgs.
IdXotn7QCoisRJDyFc2wowwayW5n__WhALsH2be73dOAqFiJHMW4IT3IYMCJksW-XTtYJF6AqKZlOZL9nnAXyXSYAZUNug=s750
 
Najivunia kuwa Mkenya.Tuendelee kuchapa kazi safi.
Kenya volleyball queens Malkia
Strikers just did it again.
MALKIA-STRIKERS-AFRICA-GAME-600x400.jpg
Seen here having fun after the match while celebrating their victory against Cameroon. They just beat their tough archrivals 3-1. Hongera kwa Malkia Strikers! [emoji1139]
 
Hongera, Ila warudi home wapambane na bei ya unga!!
Wapo kazini sio kwenye ziara za kukenua kenua kama wanamichezo wenu 6, ambao wamesindikizwa na wanachama 20. Riadha zinaanza kesho na TeamKenya ina wanamichezo 290 ambao wanashiriki kwenye michezo 22 tofauti. Msururu wa medali ndio unaanza na wameahidiwa mapochopocho ya ziada wakirudi nyumbani na medali za kueleweka. Wanamichezo wa Kenya hawana njaa kama hao wauza sura wenu. [emoji1139][emoji1139][emoji1139] Hii bendera ipe heshima inayostahili.
 
Hongereni Manyang'au, sisi huko ni Kilio hatujui tufanye Nini vile Ndege yetu ya ATCL imewekwa rehani kule kwa ndugu zetu tulikomboa miaka ya wakoloni.
 
Back
Top Bottom