Ukweli utaupata kwenye Quran kama Yesu alivyokuambia;
John 16:7
Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.
John 15:26
Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
Huyo msaidizi ni Mtume Muhammed(Rehma na amani zimfikie). Katika Biblia ya Hebrew ametajwa kwa Jina la Ahmed ambayo kwa kiarabu ni maana sawa na Mohammed. Sasa kama Yesu amekuambia umfuate Muhammed ndiyo mtume aliyekuja baada yake vipi wewe unasitasita? Inamaana haufuati maagizo ya Yesu. Utafute ukweli upate kujikomboa kiimani.