John 16: 7 - 13
7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.
8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;
11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
12 Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote;
Ukisoma hapo juu ni wazi kuwa huyo msaidizi ni mtu atakayeletwa na Mungu. Ni vigumu kwa wewe kuweza kuthibitisha haya maneno yangu kwa sababu ya uhaba wa material resources. Bible zote unazozisoma ni tafsiri. Huwezi kujua Original Scriptures ya Bible huyo Msaidizi ametajwa kwa jina gani. Manake MSAIDIZI sio jina bali ni Sifa. Kwanini watafsiri JINA??? Hapo kuna jambo walitaka kuficha. Sikiliza hiyo U-Tube video ya Debate kati ya Muslim and Christian Scholars regarding the same. Unaweza pata picha kamili hapo.
Pia Katika Original Hebrew Songs of Solomon 5:16 Muhammed ametajwa kwa jina. Lakini Kwenye Old Tastement vile vile wametraslate jina la Muhammed kwa neno 'lovely'. Ni kwanini jina litafsiriwe??? Kwanini liasiandikwe kama lilivyo??