YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Ni kweliNasikia kwamba wamewarejesha nyumbani wale vijana wa JKT kufuatia malalamiko ya wananchi na pia ukweli kwamba hao vijana ndio wamekufa wengi baada ya kuwekwa mstari wa mbele wa mapigano.
Iko hivi Russia kuna uhaba mkubwa wa ajira
Hivyo nafasi nyingi za kazi zilikuwa jeshi la Russia
Kilichofanyika watoto wengi wa vigogo ambao wazazi wao ni vigogo serikalini,bungeni na Jeshini na wanasiasa wakubwa,na ndugu zao ndio walipata hizo ajira.Watoto wa wanyonge wakakosa wakaishia tu kujitolea JKT
Ok wakajaza mitoto yao kuku wa mdondo jeshini waliokulia maisha ya raha wasio jua shida kuwa wanajeshi
Vita na Ukraine ilipolipuka kila mzazi kigogo wa Russia hataki mwanawe aende vitani na mitoto wenyewe haitaki inaogopa vita!!! Ajira jeshini yanataka ila kupigana vita hayataki !! ndipo Putin na vigogo wenzie wakasukumiza hao wa JKT ndio wakapigane ili mitoto yao ibaki salama !!! Wananchi wa kawaida ndipo wakaanza kupiga yowe baada ya kuona watoto wao wanauawa mno Ukraine. Wakaandamana kumpinga Putin kuwa rudisheni watoto wetu hao wa JKT pelekeni hao wenu wanenu mliowaajiri kiupendeleo kama professional soldiers ndio wakapigane huko Ukraine !!