1884 Africa was divided without a presence of any African

1884 Africa was divided without a presence of any African

Walitafuta wakalimani waliposaini mikataba na wakina Chifu Mangongo. Wangekua na nia njema wangepandisha Machifu na wakalimani kwenye meli.
Sasa huyo Chief Mangungo alikijuwa anachokisaini ambacho kiliandikwa kwa kijerumani?

Hata wangepelekwa hayo mamikataba wangeambulia nini humo? Kumbuka enzi zile hakukuwa na mwanasheria msomi Mtanganyika, kwa hivyo wangeishia kuweka thumbprint kuainisha kukubali basi.
 
This is where they sat in 1884(Berlin) and divided Akebulan (Africa) among themselves without inviting a single African. They destroyed our heritage and made us become beggars of foreign aid.​

The one time United Africa was destroyed and it becomes a shadow of herself. They loots away our riches and build their country with, they made us vulnerable, brought in the system of divide and rule so we will keep on fighting against each other while the continue looting our resources, they decided our leaders who will serve their interest not the interest of Africa.

African youths the time is now, if we don't rewrite our history, no one will do that for us.
Kaka nakubali sentensi yako ya mwisho!
Ila yale yanayotangulia kuna kasoro.
1. Kwenye mkutano wa Berlin wa 1884/85 hawakufanya maazimio kuhusu ugawaji wa Afrika kati yao. Ugawaji huo uliwahi kuanza kidogo kabla na hasa kufuata baada ya mkutano. Uliweka kanuni kadhaa zilizolenga kupunguza hatari ya ugomvi kati nchi za Ulaya wakati zikikutana kwenye bara la Afrika. Kwa njia hiyo mkutano uliandaa ugawaji wa Afrika.

2. Kuhusu habari za kimsingi soma hapa: Mkutano wa Berlin wa 1885 - Wikipedia, kamusi elezo huru, hasa kifungu kuhusu "Maazimio". Maazimio ya mkutano ka Kiingereza utapata hapa kama pdf: https://loveman.sdsu.edu/docs/1885GeneralActBerlinConference.pdf, pia hapa ikifupishwa kidogo: (1885) General Act of the Conference of Berlin •.

3. "United Africa was destroyed"?? Hii ni ndoto, haikuwepo kamwe bali ni kazi ya siku zetu. Shabaha moja iliyokubaliwa pale Berlin 1885 ilikuwa kukomesha kwa biashara ya watumwa. Wakati ule biashara hiyo iliendelea kwa nguvu NDANI ya Afrika ya Magharibi, kwa kiwango fulani pia NDANI YA Afrika ya Mashariki. Sokoto, Bornu, Dahomey, Benin - falme hizo zote zilistawi kwenye msingi wa vita zilizopganiwa kwa kusudi la kukamata watumwa waliokuwa msingi wa uchumi wao. Wayao walipeleka watumwa kutoka Malawi hadi Kilwa, Mirambo alikuwa na jeshi la watoto watumwa.
Wangeunganaje katika mazingira ambako njia kutoka Bagamoyo hadi Ziwa Tanganyika ilikuwa safari ya miezi kadhaa (kama umefika bila kuuawa na majambazi au chifu fulani aliyeona unafaa kuuzwa kuwa mtumwa).
Umoja wa Afrika ni kazi ya leo.
 
Ninafahamu kuwa Uingereza ilitunga sheria ya kusitisha biashara ya utumwa nchini mwake na katika makoloni yake yote 1838. Inamaana ilichukua miaka karibu 20 nchi nyingine za Ulaya kusitisha biashara ya utumwa?
 
Mkutano wa Vienna wa 1815 uliamua kusitisha biashara ya watumwa kutoka Afrika. Uingereza ulitumia miaka iliyofuata kudhibiti biashara hiyo (angalia hapa). Mnamo 1850 hivi, idadi ya watumwa waliopelekwa kama magendo hadi Amerika kutoka Afrika ya Magharibi ilikuwa imepungua sana. Milki za Afrika ya Magharibi zilizowahi kuuza watumwa kwa Wazungu zilibadilisha uchumi wao. Badala ya kuuza watumwa (walijaribu kuendelea, hata hivyo) walianza kuwatumia kwenye kilimo chao. Katika nchi kama Dahomey na Benin, pia khilafa za Kiislamu kama Sokoto zilendesha uchumi wao kwa kazi ya watumwa. Kutoka Afrika ya Mashariki biashara ya watumwa iliendelea kuelekea Uarabuni na kwenye visiwa vya Bahari Hindi, lakini pia kwa mahitaja ya mashamba makubwa ya Waarabu kwenye pwani na kule Zanzibar.
Changamoto kubwa ya kukomesha biashara ya watumwa ilikuwa mwanzoni biashara kuelekea visiwa vya Karibi, Brazil na Marekani.
Baadaye zilikuwa taarifa za Livingstone zilileta habari za uwindaji wa watumwa katika Afrika ya kusini-kati mbele ya macho ya mataifa ya Ulaya;
harakati ya kisiasa ilihamasihsa wanasiasa kuchukua hatua dhidi ya biashara hiyo lakini mkono mwingine wa siasa ilichukua nafasi ya kuanzisha vituo vyao Afrika - vilivyoendelea kuwa koloni.
 
Back
Top Bottom