1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Nazungumzia Chattel Slavery ambapo mtu na uzao wake ulihesabiwa kuwa bidhaa na ulimilikiwa na binadamu mwenzake. Afrika bado upo Mauritania na Sudan. Labda uniambie Tanzania ni wapi watu wanawamiliki wenzao na uzao wao na wanawauza kama bidhaa nyingine.

Amandla...
Ndio huohuo, vyovyote utakavyoupamba, hakuna "chief" bara ambae alikuwa hana watumwa, na ma chief ndio walikuwa ma don wakuuza watumwa.

Tazama watumwa waliopo Amerika, wote walitokea Zanzibar? Usitake kujaza watu ujinga uliojazwa nao. Unajuwa kuwa Meli maarufu iliyopeleka watumwa Amerika ikiitwa Jesus? Unajuwa kuwa jela ya watumwa na pahala walipoteswa pako ndani, chini ya kanisa la wazungu?
 
Ndio huohuo, vyovyote utakavyoupamba, hakuna "chief" bara ambae alikuwa hana watumwa, na ma chief ndio walikuwa ma don wakuuza watumwa.
Hakuna mtu anayepinga ushiriki wa baadhi ya machifu kwenye biashara ya utumwa. Ushiriki wao hakubadilishi ukweli kuwa waarabu walichukua waafrika ( kwa kununua kutoka kwa machifu au kuteka ) na kuwageuza kuwa bidhaa ambayo waliiuza katika masoko yao.
Tazama watumwa waliopo Amerika, wote walitokea Zanzibar? Usitake kujaza watu ujinga uliojazwa nao. Unajuwa kuwa Meli maarufu iliyopeleka watumwa Amerika ikiitwa Jesus? Unajuwa kuwa jela ya watumwa na pahala walipoteswa pako ndani, chini ya kanisa la wazungu?
Nani amesema watumwa walioukuwa( sasa hivi hamna chattel slavery ) Amerika wote walitokea Zanzibar. Kwa upande ule wengi walitokea Afrika Magharibi na Angola. Je unajua kuwa Jesus ni jina la kawaida kwa waspanish? Ni kweli kuna meli iliitwa Jesus wa Lubeck na Malkia Elizabeth aliikabidhi kwa John Hawkins mwaka 1564 ambae aliitumia kwa safari ya kwanza rasmi ya uingereza kwenye biashara ya watumwa. Meli ya kwanza iliyopeleka watumwa Marekani iliitwa White Lion na iliwasili Point Comfort Agosti 20 1619. Je unajua biashara ya utumwa ilipigwa marufuku 1873 na sultan baada ya shinikizo kutoka kwa waingereza? Je unajua kuwa kanisa la kianglikana la Christ Church lilijengwa mwaka 1879 mahali palipokuwa soko la watumwa kama uthibitisho wa ushindi wa mwanga dhidi ya giza? Je unajua sehemu palipokuwa pana mlingoti wa kuwapiga mijeledi watumwa ndipo palipojengwa altare? Je unajua kwenye nyumba yake ya wageni kuna mahandaki yaliyobakizwa kama ukumbusho wa sehemu ambako waarabu walitumia kama ghala ya watumwa? Je unajua kuwa nje ya kanisa kuna sanamu za watumwa ambazo zimefungwa minyororo halisi iliyotumiwa kufungia watumwa?

Je unajua kuwa mji wa Raqqa ulikombolewa mwaka 2017? Je unajua kuwa wazungu walimuua Abu Bakr al Baghdadi mwaka 2020? Na mapema mwezi huu wamemuua Abu Ibrahim al-Hashmi al-Qurayshi? Sidhani kama hizi taarifa zinapatikana makambini huko Syria.

Amandla....
 
Ndio maana nimesema waafrika wanaojiita washirazi. Waliochanganya damu ya kiafrika na kishirazi walijiita washirazi sio Afro Shirazi. Hata hao wanaojiita waarabu wengi wao ni waafrika waliochanganya damu ya uarabu na hawajiiti Afro Arabs. Hoja za kubuni kama hiyo ya Afro Shirazi ndio inayonifanya nikuone mpumbavu. Mpumbavu hana tiba. Ni kipaji.

Afro Shirazi Party kiliundwa tarehe 5 Februari mwaka 1957 baada ya vyama vya African Association kuungana na cha Shirazi Association. Thabit Kombo Jecha Al Shiraz alikuwa mwanachama wa Shirazi Association na mwaka 1956 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wake. Siku zote alitambulika kama mshirazi na sio mafro shirazi. Chama cha Afro Shirazi hakina uhusiano na watu kuchanganya damu.

Ushahidi upi wa kuokoteza? Mimi nahoji kwa sababu huo unaouita ushahidi hauna mashiko. Ndio maana tukiwahoji mnakimbilia kudai tunawachukia.
Ujinga wangu utaondoka mkinielimisha lakini kwa vile mpaka sasa hivi hamjafanikiwa nitabaki kuwa mjinga.

Amandla...
Unawaita wewe Waarabu na hata Washirazi unawaita wewe.

Mzanzibari, iwe ana asili yoyote ile yupo so proud kujiita Mzanzibari. si leo si jana. Tatizo ni wewe usieweza kujiita Mtanganyika.

Hata Karume ni Mnyasa lakini hajawahi kujiita Mnyasa, kashika mila na desturi za Wazanzibari alizozikuta, anajulikana kama Mzanzibari tu. Mwinyi halikadhalika, hajitambulishi hata siku moja kama ni Mzaramo au Mndengereko or whatever, anajitambulisha kama Mzanzibari tu.

Na wewe kwa Mzaanzibari yeyote yule utabaki kuwa chogo tu. Unafahamu kwanini?
 
Unawaita wewe Waarabu na hata Washirazi unawaita wewe.

Mzanzibari, iwe ana asili yoyote ile yupo so proud kujiita Mzanzibari. si leo si jana. Tatizo ni wewe usieweza kujiita Mtanganyika.

Hata Karume ni Mnyasa lakini hajawahi kujiita Mnyasa, kashika mila na desturi za Wazanzibari alizozikuta, anajulikana kama Mzanzibari tu. Mwinyi halikadhalika, hajitambulishi hata siku moja kama ni Mzaramo au Mndengereko or whatever, anajitambulisha kama Mzanzibari tu.
Wazanzibari ndio wanaoitana muarabu au mshirazi au mngazija au mpemba. Hilo la uzanzibari ni pale wanapotaka kujitofautisha na machogo. Watanzania ( isipokuwa wazanzibari) tukiwa nje ya mipaka yetu tunajitambulisha kama watanzania ila tukiwa wenyewe ndio utasikia mnyasa au mdengereko. Hayo ya uzanzibari ni mambo ya siku hizi. Kabla ya hapo kila mtu alijitambulisha kwa asili yake ndio maana walikuwa na vyama vya siasa vya waafrika, waarabu na washirazi.
Mimi siwezi kujiita mtanganyika kwa sababu jina hilo halitumiki kwa sasa. Natumia na nina jivunia jina la sasa la Tanzania. Hauwezi kumkuta mzimbabwe akijiita mrhodesia. Au mburkinabe mupper volta. Mtu wa California akiwa kwao anajulikana kama mcalifornia lakini nje ya mipaka ni Mmarekani. M'scot hakubali kuitwa m'english lakini nje ya mipaka ni m'british.

Amandla...
 
Hakuna mtu anayepinga ushiriki wa baadhi ya machifu kwenye biashara ya utumwa. Ushiriki wao hakubadilishi ukweli kuwa waarabu walichukua waafrika ( kwa kununua kutoka kwa machifu au kuteka ) na kuwageuza kuwa bidhaa ambayo waliiuza katika masoko yao.

Nani amesema watumwa walioukuwa( sasa hivi hamna chattel slavery ) Amerika wote walitokea Zanzibar. Kwa upande ule wengi walitokea Afrika Magharibi na Angola. Je unajua kuwa Jesus ni jina la kawaida kwa waspanish? Ni kweli kuna meli iliitwa Jesus wa Lubeck na Malkia Elizabeth aliikabidhi kwa John Hawkins mwaka 1564 ambae aliitumia kwa safari ya kwanza rasmi ya uingereza kwenye biashara ya watumwa. Meli ya kwanza iliyopeleka watumwa Marekani iliitwa White Lion na iliwasili Point Comfort Agosti 20 1619. Je unajua biashara ya utumwa ilipigwa marufuku 1873 na sultan baada ya shinikizo kutoka kwa waingereza? Je unajua kuwa kanisa la kianglikana la Christ Church lilijengwa mwaka 1879 mahali palipokuwa soko la watumwa kama uthibitisho wa ushindi wa mwanga dhidi ya giza? Je unajua sehemu palipokuwa pana mlingoti wa kuwapiga mijeledi watumwa ndipo palipojengwa altare? Je unajua kwenye nyumba yake ya wageni kuna mahandaki yaliyobakizwa kama ukumbusho wa sehemu ambako waarabu walitumia kama ghala ya watumwa? Je unajua kuwa nje ya kanisa kuna sanamu za watumwa ambazo zimefungwa minyororo halisi iliyotumiwa kufungia watumwa?

Je unajua kuwa mji wa Raqqa ulikombolewa mwaka 2017? Je unajua kuwa wazungu walimuua Abu Bakr al Baghdadi mwaka 2020? Na mapema mwezi huu wamemuua Abu Ibrahim al-Hashmi al-Qurayshi? Sidhani kama hizi taarifa zinapatikana makambini huko Syria.

Amandla....
Wewe jitetee ujiteteavyo lakini juu hapo umekiri mwenyewe, hata meli ya Watumwa ilikuwa Jesus.

Mpaka leo mnauzana na kujiuza. Pita Ohio au Corner Bar Sinza ukaone dada zako wanavyojiuza. Kama si utumwa ule nini?
 
Pichani ni Julai 16, 1963, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Julius Nyerere akiweka katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa U Thant pini yenye alama ya mwenge wa taifa.

Kulia kabisa ni mwakilishi wa kudumu wa Tanganyika kwenye Umoja wa Mataifa wakati huo Chifu Erasto A.M Mang'enya na kushoto kabisa ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Tanganyika Oscar Kambona.

Mwenge wa taifa ulipandishwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro pindi Tanganyika ilipopata uhuru wake, mnamo tarehe 9, Desemba, mwaka 1961.

View attachment 2050781

📸: UN Photo

Mmewatambulisha Nyerere, Kambona na Chief Mang'enya mbona huyo mwingine hamkumtambulisha? Chale akiwa ofisi ya uwakilishi New York!
 
Wazanzibari ndio wanaoitana muarabu au mshirazi au mngazija au mpemba. Hilo la uzanzibari ni pale wanapotaka kujitofautisha na machogo. Watanzania ( isipokuwa wazanzibari) tukiwa nje ya mipaka yetu tunajitambulisha kama watanzania ila tukiwa wenyewe ndio utasikia mnyasa au mdengereko. Hayo ya uzanzibari ni mambo ya siku hizi. Kabla ya hapo kila mtu alijitambulisha kwa asili yake ndio maana walikuwa na vyama vya siasa vya waafrika, waarabu na washirazi.
Mimi siwezi kujiita mtanganyika kwa sababu jina hilo halitumiki kwa sasa. Natumia na nina jivunia jina la sasa la Tanzania. Hauwezi kumkuta mzimbabwe akijiita mrhodesia. Au mburkinabe mupper volta. Mtu wa California akiwa kwao anajulikana kama mcalifornia lakini nje ya mipaka ni Mmarekani. M'scot hakubali kuitwa m'english lakini nje ya mipaka ni m'british.

Amandla...
Huwajui Wazanzibari wewe, kaa utulie. Huna jipya. Hata Mwarabu humjui ni yupi.
 
Wewe jitetee ujiteteavyo lakini juu hapo umekiri mwenyewe, hata meli ya Watumwa ilikuwa Jesus.

Mpaka leo mnauzana na kujiuza. Pita Ohio au Corner Bar Sinza ukaone dada zako wanavyojiuza. Kama si utumwa ule nini?
Mbona hatusemi Mohammed Atta alifanya aliyofanya kwa sababu aliitwa Mohammed? Jesus ni jina tu kama Faiza wala lisikusumbue.
Zanzibar hawajiuzi? Waislamu hawajiuzi? Waarabu hawajiuzi? Pemba malaya wako nje nje. Hapo corner bar wakina Faiza kibao! Na wengine wamevaa mpaka ushungi.
Tangu lini kujiuza kumekuwa utumwa? Wanamtumikia nani kwa kujiuza? Na ulinganishaji mtu anaejiuza na chattel slave aliyenunuliwa na waarabu halafu akahasiwa ili asitamani wake zake?
Mimi ukiniambia kuwa wazungu walituanyia maovu mengi sitakubishia maana ushahidi upo. Hata wao wenyewe hawatabisha.
Ila mtu kama wewe hawezi kukubali kuwa waarabu walitufanyia maovu mengi kwa sababu una waabudu na unachanganya dini na matendo ya wafuasi wake.

Amandla...
 
Huwajui Wazanzibari wewe, kaa utulie. Huna jipya. Hata Mwarabu humjui ni yupi.
Wewe ndio una Ph.D ya uzanzibari na waarabu? Kwa vile tu wewe ni muislamu mwenzao?

Au ulikuwa Syria ndio ukawajua vizuri?

Amandla...
 
Wewe ndio una Ph.D ya uzanzibari na waarabu? Kwa vile tu wewe ni muislamu mwenzao?

Au ulikuwa Syria ndio ukawajua vizuri?

Amandla...
Si Wazanzibari wote au Waarabu wote ni Waislam? Si unaona ulivyo poyoooooooooyo.
 
Tuseme nchi ingeenda alivyotaka mwalimu Nyerere ni nini kingetokea ?

Hakuwa na tamaa ie mzee Kenyatta aliyejigawiya karibia ardhi ya nchi nzima.

Madini huku akijua kabisa chini kuna madini ila akasema ngojeni

Nidhamu ya kazi ilikuwepo.

All things changed sasa
Nyerere alikuwa kiongozi bora Africa kuliko wengine wote wa kipindi chake.
 
Matatizo yalianza baada ya athari za sera ya Ujamaa.
Ni nchi gani haikuwa na Socialism features katika kipindi kimoja au kingine - From United Kingdom na nchi nyinginezo; Na je unaweza kusema hata US ya leo Inayojipambanua na kujitahidi kwamba iwe a Social Democracy unasemaje hapo ? Kwa leo hii naweza kusema hata US au UK wana welfare systems kushinda hata sisi huku; Ingawa Ujamaa wa US ni mambo yakienda vizuri sisi ni Mabepari (yakienda pearshaped mfano mabenki kufirisika wanakuwa wajamaa kwa walipa kodi kulipia uzembe wa hayo makampuni)

Tunachokosea haya yote ni Mawazo / Ideas ambazo practically huwezi ukawa na 100 percent upande mmoja au mwingine (100 percent socialist au capitalist) they are all mixed economies - na ni socialist which has given capitalism a human face....;

Ukiongelea matatizo yalianza unaongelea individuals na sio majority; Matatizo ya sasa yameondoa middle income na kuipeleka kwenye have nots na kutengeneza wachache sana wanaomiliki kila kitu...; Hadi kufika hapo ni kweli sacrifices were made (maybe for a better good kwa sisi leo kuwa na Umoja wa Kitaifa ambao sasa tunauchezea na kutaka kuupote which in the end we will truly remain with nothing)

Watu walihamishwa pasi kuwa na maandalizi ya kutosha. Vijiji vingi havikuwa na maji, umeme wala barabara za kueleweka. Pia dhana ya kufanya kazi kwa pamoja ilizalisha goigoi wengi.
Kwahio huo ni utendaji na utekelezaji na sio concept...; vijiji vya ujamaa vya zamani ndio hizi modern cities..., huwezi kupeleka maji umeme na huduma zozote kwa watu waliotapakaa kila mahali, ukitaka kupata huduma za kijamii lazima uwe na jamii unless otherwise unaweza kuishi off-grid kwa kujitegemea kama unaweza ukawa sustainable; ila sio kuishi kwenye estate peke yako alafu utegemee watwana wakufanyie kila kitu (it was inevitable soon or later mambo yangebaki vile gap ya have and have nots ingeongezeka mapema na hata ambao leo wameweza kutoka kwenye poverty cycle wasingetoka - hata wengine wasingesoma zaidi ya wale ambao kwa njia moja au nyingine wakati wa ukoloni walikuwa na advantage (be it color au position / but not for the lack of hard work)
Uchumi uliharibika sana baada ya vita ya Kagera. Hata mwenyewe alitangaza miezi 18 ya kufunga mikanda.
Uchumi uliharibika ni kweli as well as kuweka sera za kufanya kazi pamoja wakati uzalishaji na vitendea kazi ni sifuri the whole lot was bound to fail - heri angekuwa na uwezo uliopo sasa ukusanyaji wa mapato kwa kutumia computer; transparency ya kujua nini kinapatikana wapi na saa ngapi na nani anafanya nini wapi.., as well as mashine za kulima; combined harvesters na mitambo inayopanda na kuvuna masaa 24 - we would have been talking a different story.....

Lakini efficiency ikiwa sifuri when the going gets tough na wale unaotegemea wakusaidie mna itikadi tofauti it was just a matter of time before the whole thing went pear-shaped...;

Kila kitu kina wakati wake; Just kama Political systems zilizopo sasa hazitakuwepo miaka 50 ijayo (time have / will change)
 
Chief Erasto Mang'enya ni Marehemu. Huyu alikuwa Mbunge wa Muheza kabla ya Luka Kitandula
Mang'enya aliwahi kuwa Spika wa Bunge la JMT

JokaKuu Mag3
Chief Erasto Andrew Mbwana Mang'enya alikuwa Mbondei msomi, aliwahi kuwa Mwalimu mkuu wa Old Moshi Middle/Technical school miaka hiyooo hata Tanzania haijakaribia kuzaliwa

Pia alikuwa Waziri wa wizara tofauti na hapo pichani alikuwa waziri wa mambo ya nje

Aliishi New York City sio Uingereza
 
Matatizo yalianza baada ya athari za sera ya Ujamaa. Watu walihamishwa pasi kuwa na maandalizi ya kutosha. Vijiji vingi havikuwa na maji, umeme wala barabara za kueleweka. Pia dhana ya kufanya kazi kwa pamoja ilizalisha goigoi wengi.

Uchumi uliharibika sana baada ya vita ya Kagera. Hata mwenyewe alitangaza miezi 18 ya kufunga mikanda.
Uchumi uliharibika sana baada ya vita ya Kagera lakini bado inasemwa Nchi aliikabidhi ikiwa na neema kila kona akaiharibu Ally
 
Back
Top Bottom