Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
"Sasa tuje kwenye mgomo wenyewe wa 1960.
Vipi waliweza kugoma kwa siku 82 hawana mshahara?
Kabla ya ule mgomo TRAU ilipata msaada wa fedha kutoka Ujerumani ya Mashariki na Chama Cha Wafanyakazi wa Reli wa Uingereza na sehemu nyingine.
TRAU ikachagua maduka maalum ya vyakula na wakatoa kadi kwa wanachama wao wote ambayo kadi hii iliwawezesha kupata mahitaji yao ya kila siku kuanzia mchele, unga, maharage, mafuta ya kupikia mafuta ya taa hadi viberiti.
Treni zilisimama, meli na mabasi yote ya Railway.
Nyumbani kwa babu yangu ikawa ndiyo Command Post wafanyakazi waliokuwa katika mgomo wanakutana hapo kupashana taarifa."
Railway African Association ilianzishwa 1945 na tarehe 10 Septemba 1947 wanachama wao 2000 walijunga na mgomo uliokuwa unaendelea Dar es Salaam (sio Tabora). Mgomo huo uliungwa mkono na wafanyakazi wegine wa reli waliokuwa Morogoro, Kilosa, Dodoma na Tabora. Kilichoongezwa na wafanyakazi wa Tabora ni kudai walipwe mshahara sawa na wahindi.
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi lilianzishwa mwaka 1955 baada ya Tom Mboya kutoka Kenya alipotembelea Tanganyika. Tom Mboya alikuwa karibu sana na shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa dunia, International Confederation of Free Trade Unions ambacho kwa AFL-CIO ya Marekani ilikuwa na nguvu sana. AFL-CIO ilitumia ICFTU kupambana na ushawishi wa ukomunisti duniani. Mashirika mengine yaliokuwa yakitoa msaada na ushauri kwa TFL ni the Fabian Colonial Bureau, the British Trade Union Congress (TUC) na the International Transport Workers Federation (ITWF). Kutokana na kuwepo kwa vita baridi hamna namna mashirika haya yangeweza kushirikiana GDR ( Ujerumani Mashirika). Sidhani kama the National Union of Railmen ya UK iliwahi kuhusika moja kwa moja maana wao walikuwa wanaangalia maslahi ya wanachama wake wakati TUC ilikuwa na ajenda ya kusaidia vyama vingine vya wafanyakazi popote vilipo.
Tarehe 20 Januari 1956, TFL iliitisha mgomo ambao ulikuwa uanze tarehe 11 Februari wakitaka uongozi uwarudishe wafanyakazi 5000 walioachishwa kazi. Wawakilishi kutoka T.U.C na I.C.F.T.U walikuja Dar kusuluhisha mgogoro. Mgogoro ulisitishwa baada ya A.F.L-C.I.O ( bila shaka kupitia I.C.F.T.U) kuwapa TFL fedha za kuwalipa wafanyakazi walioachishwa kazi.
Mwaka 1957, Katibu Mkuu wa TFL, Rashidi Kawawa alihutubia mkutano wa I.C.F.T.U ambapo aliwaomba msaada wa mali na ushauri.
Mwaka 1958 I.C.F.T.U walianzisha chuo kwa ajili ya wafanyakazi katika vyama vya wafanyakazi. Chuo hicho kilikuwa Kampala Uganda.
Kati ya mwaka 1951 mpaka 1955 palikuwa na wastani wa migomo 60 kwa mwaka iliyohusu wafanyakazi 7805. Kati ya mwaka 1956 mpaka 1960, migomo iliongezeka hadi 146 kwa mwaka na ilihusisha wafanyakazi 59,457.
TRAU ilikuwa siku zote ikifanya mazungumzo na EARH kwa nia ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwa haswa mishahara na hali ya wafanyakazi. Lakini uongozi wa EARH ulikuwa ukipinga nyongeza yeyote ya mishahara kwa madai kuwa hawana uwezo wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi wake wote wa Afrika Mashariki ( Mishahara ilikuwa inakula £8,990,000 katika bajeti yao ya £19,500,000.).
Mwezi Mei 1959 uongozi wa EARH uliwaachisha kazi wafanyakazi waafrika waliokuwa senior. TRAU wakausihi uongozi wa EAHRC wawarudishe lakini wakakataa. Ilipofika Julai 1959, Katibu Mkuu wa TRAU, Christopher Kasanga Tumbo akatangaza kujitoa katika chombo cha usuluhishi kati yao na EARH. Mwezi Agosti 1959, mkutano mkuu wa TRAU uliamua kuwa sasa mgomo haukwepeki. Mgomo ukapangwa kuanza tarehe 18 Desemba 1959 lakini ukasogezwa baada ya wafanyakazi wa Posta nao kuanza kugoma tarehe 24 Desemba wakidai kima cha chini cha mshahara cha shilingi 150 kwa mwezi, mshahara ambao TRAU waliona unakubalika. Wafanyakazi 1200 wa Posta waligoma.
Hata hivyo mwezi Oktoba palitokea mgomo katika karakana za EARH ambapo wafanyakazi walidai kubadilishwa madaraja yao ya kazi. TRAU iliweza kuwarudisha kazini baada tu ya kuwahidi kuwa mazungumzo na utawala yataanza mara tu watakapoacha kugoma. Lakini haikuwa hivyo.
Baada ya uongozi kuendelea kuwazingua mgomo ulitangazwa tarehe 9 Februari 1960 na tarehe 10 Februari wafanyakazi 12000 wa reli walianza kugoma. Ilipofika tarehe 15 Februari wafanyakazi wa posta walikubali kima cha chini cha shilingi 107 kwa mwezi.
Mwezi Machi, ITWF na I.C.F.T.U walimtuma Jack Purvis kusaidia kuleta suluhisho. TRAU walikubali kupunguza madai yao kutoka kima cha chini cha mshahara cha shilingi 7 na senti 75 kwa saa hadi nyongeza ya shilingi 10 kwa mwezi kwa wafanyakazi wote wa daraja la C ambalo ingawa lilikuwa la chini kabisa lilikuwa na madaraja tofauti. Jack Purvis hakuweza kuwa convince uongozi wa EARH kukubali ofa hii.
Tarehe 22 Machi TFL walikutana na kutoa tamko kuwa hawataitisha mgomo mkuu ili kuwaunga mkono TRAU. Badala yake walimtaka Gavana Sir Reginald Turnbull kuingilia na kuleta suluhisho. Wasiwasi wa TFL ulikuwa kuwa mgomo huo ungeweza kuvuruga maandalizi ya uhuru uliopangwa kutokea mwaka unaofuata.
I.C.F.T.U baada ya kuona Christopher Kasanga Tumbo bado analeta ubishi walimualika kwenda Brussels kwa mazungumzo kati ya tarehe 29 Machi na 4 Aprili. Matokeo ya mazungumzo hayo ni I.C.F.T.U kumtuma Charles Millard na I.T.W.F kumtuma Pieter De Vries kusimamia majadiliano badala ya Christopher Kasanga. Uongozi wa EARH ulikuwa tayari na mgomo kwa sababu waliishapata mafanikio katika kupunguza makali ya mgomo kwa kuwatumia wafanyakazi wa kihindi na kizungu. Ila serikali iliwalazimisha wafikie muafaka kwa kuhofia kuwa ungeweza kuathiri shughuli za uhuru mwakani. Tarehe 30 Aprili ukakubali kuongeza kima cha chini cha mshahara cha C.6 kwa sh. 10 kwa mwezi ambao ulipungua hadi Sh. 4 kwa mwezi kwa wale wa daraja lla juu la C.1-3. Kiwango hiki kilikuwa pungufu sana ya kiwango walichotegemea lakini watu walikuwa wamechoka. Ila kwa kiasi kikubwa mgomo huu ulimjenga sana Christopher Kasanga Tumbo kwa wafanyakazi wa chini wa reli.
Mimi nadhani msaada wa kifedha ulitoka kwa I.C.F.T.U, ITWF na TUC na Tumbo alipoenda Brussels walimtishia kusitisha misaada yao kama angeng'ang'ania kusimamia mazungumzo ya usuluhisho. Inawezekana kabisa msaada huo ulitumiwa kama ilivyosimuliwa hapo juu kuwasaidia wagomaji kumudu maisha.Lakini kilicho wazi ni kuwa mgomo haukuongozwa na Mzee Salum Abdallah. Kiongozi alikuwa Christopher Kasanga Tumbo. Nadhani wakina mzee Salum Abdallah walikuwa wanampiga taf, kitu ambacho hakikuwa kidogo na wanastahili heshima kwa hilo.
Amandla...
Bwana Mdogo Fundi Mchundo
Cc. Nguruvi3