1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

"Sasa tuje kwenye mgomo wenyewe wa 1960.
Vipi waliweza kugoma kwa siku 82 hawana mshahara?

Kabla ya ule mgomo TRAU ilipata msaada wa fedha kutoka Ujerumani ya Mashariki na Chama Cha Wafanyakazi wa Reli wa Uingereza na sehemu nyingine.

TRAU ikachagua maduka maalum ya vyakula na wakatoa kadi kwa wanachama wao wote ambayo kadi hii iliwawezesha kupata mahitaji yao ya kila siku kuanzia mchele, unga, maharage, mafuta ya kupikia mafuta ya taa hadi viberiti.

Treni zilisimama, meli na mabasi yote ya Railway.

Nyumbani kwa babu yangu ikawa ndiyo Command Post wafanyakazi waliokuwa katika mgomo wanakutana hapo kupashana taarifa."

Railway African Association ilianzishwa 1945 na tarehe 10 Septemba 1947 wanachama wao 2000 walijunga na mgomo uliokuwa unaendelea Dar es Salaam (sio Tabora). Mgomo huo uliungwa mkono na wafanyakazi wegine wa reli waliokuwa Morogoro, Kilosa, Dodoma na Tabora. Kilichoongezwa na wafanyakazi wa Tabora ni kudai walipwe mshahara sawa na wahindi.

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi lilianzishwa mwaka 1955 baada ya Tom Mboya kutoka Kenya alipotembelea Tanganyika. Tom Mboya alikuwa karibu sana na shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa dunia, International Confederation of Free Trade Unions ambacho kwa AFL-CIO ya Marekani ilikuwa na nguvu sana. AFL-CIO ilitumia ICFTU kupambana na ushawishi wa ukomunisti duniani. Mashirika mengine yaliokuwa yakitoa msaada na ushauri kwa TFL ni the Fabian Colonial Bureau, the British Trade Union Congress (TUC) na the International Transport Workers Federation (ITWF). Kutokana na kuwepo kwa vita baridi hamna namna mashirika haya yangeweza kushirikiana GDR ( Ujerumani Mashirika). Sidhani kama the National Union of Railmen ya UK iliwahi kuhusika moja kwa moja maana wao walikuwa wanaangalia maslahi ya wanachama wake wakati TUC ilikuwa na ajenda ya kusaidia vyama vingine vya wafanyakazi popote vilipo.

Tarehe 20 Januari 1956, TFL iliitisha mgomo ambao ulikuwa uanze tarehe 11 Februari wakitaka uongozi uwarudishe wafanyakazi 5000 walioachishwa kazi. Wawakilishi kutoka T.U.C na I.C.F.T.U walikuja Dar kusuluhisha mgogoro. Mgogoro ulisitishwa baada ya A.F.L-C.I.O ( bila shaka kupitia I.C.F.T.U) kuwapa TFL fedha za kuwalipa wafanyakazi walioachishwa kazi.

Mwaka 1957, Katibu Mkuu wa TFL, Rashidi Kawawa alihutubia mkutano wa I.C.F.T.U ambapo aliwaomba msaada wa mali na ushauri.

Mwaka 1958 I.C.F.T.U walianzisha chuo kwa ajili ya wafanyakazi katika vyama vya wafanyakazi. Chuo hicho kilikuwa Kampala Uganda.

Kati ya mwaka 1951 mpaka 1955 palikuwa na wastani wa migomo 60 kwa mwaka iliyohusu wafanyakazi 7805. Kati ya mwaka 1956 mpaka 1960, migomo iliongezeka hadi 146 kwa mwaka na ilihusisha wafanyakazi 59,457.

TRAU ilikuwa siku zote ikifanya mazungumzo na EARH kwa nia ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwa haswa mishahara na hali ya wafanyakazi. Lakini uongozi wa EARH ulikuwa ukipinga nyongeza yeyote ya mishahara kwa madai kuwa hawana uwezo wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi wake wote wa Afrika Mashariki ( Mishahara ilikuwa inakula £8,990,000 katika bajeti yao ya £19,500,000.).

Mwezi Mei 1959 uongozi wa EARH uliwaachisha kazi wafanyakazi waafrika waliokuwa senior. TRAU wakausihi uongozi wa EAHRC wawarudishe lakini wakakataa. Ilipofika Julai 1959, Katibu Mkuu wa TRAU, Christopher Kasanga Tumbo akatangaza kujitoa katika chombo cha usuluhishi kati yao na EARH. Mwezi Agosti 1959, mkutano mkuu wa TRAU uliamua kuwa sasa mgomo haukwepeki. Mgomo ukapangwa kuanza tarehe 18 Desemba 1959 lakini ukasogezwa baada ya wafanyakazi wa Posta nao kuanza kugoma tarehe 24 Desemba wakidai kima cha chini cha mshahara cha shilingi 150 kwa mwezi, mshahara ambao TRAU waliona unakubalika. Wafanyakazi 1200 wa Posta waligoma.

Hata hivyo mwezi Oktoba palitokea mgomo katika karakana za EARH ambapo wafanyakazi walidai kubadilishwa madaraja yao ya kazi. TRAU iliweza kuwarudisha kazini baada tu ya kuwahidi kuwa mazungumzo na utawala yataanza mara tu watakapoacha kugoma. Lakini haikuwa hivyo.

Baada ya uongozi kuendelea kuwazingua mgomo ulitangazwa tarehe 9 Februari 1960 na tarehe 10 Februari wafanyakazi 12000 wa reli walianza kugoma. Ilipofika tarehe 15 Februari wafanyakazi wa posta walikubali kima cha chini cha shilingi 107 kwa mwezi.
Mwezi Machi, ITWF na I.C.F.T.U walimtuma Jack Purvis kusaidia kuleta suluhisho. TRAU walikubali kupunguza madai yao kutoka kima cha chini cha mshahara cha shilingi 7 na senti 75 kwa saa hadi nyongeza ya shilingi 10 kwa mwezi kwa wafanyakazi wote wa daraja la C ambalo ingawa lilikuwa la chini kabisa lilikuwa na madaraja tofauti. Jack Purvis hakuweza kuwa convince uongozi wa EARH kukubali ofa hii.

Tarehe 22 Machi TFL walikutana na kutoa tamko kuwa hawataitisha mgomo mkuu ili kuwaunga mkono TRAU. Badala yake walimtaka Gavana Sir Reginald Turnbull kuingilia na kuleta suluhisho. Wasiwasi wa TFL ulikuwa kuwa mgomo huo ungeweza kuvuruga maandalizi ya uhuru uliopangwa kutokea mwaka unaofuata.

I.C.F.T.U baada ya kuona Christopher Kasanga Tumbo bado analeta ubishi walimualika kwenda Brussels kwa mazungumzo kati ya tarehe 29 Machi na 4 Aprili. Matokeo ya mazungumzo hayo ni I.C.F.T.U kumtuma Charles Millard na I.T.W.F kumtuma Pieter De Vries kusimamia majadiliano badala ya Christopher Kasanga. Uongozi wa EARH ulikuwa tayari na mgomo kwa sababu waliishapata mafanikio katika kupunguza makali ya mgomo kwa kuwatumia wafanyakazi wa kihindi na kizungu. Ila serikali iliwalazimisha wafikie muafaka kwa kuhofia kuwa ungeweza kuathiri shughuli za uhuru mwakani. Tarehe 30 Aprili ukakubali kuongeza kima cha chini cha mshahara cha C.6 kwa sh. 10 kwa mwezi ambao ulipungua hadi Sh. 4 kwa mwezi kwa wale wa daraja lla juu la C.1-3. Kiwango hiki kilikuwa pungufu sana ya kiwango walichotegemea lakini watu walikuwa wamechoka. Ila kwa kiasi kikubwa mgomo huu ulimjenga sana Christopher Kasanga Tumbo kwa wafanyakazi wa chini wa reli.

Mimi nadhani msaada wa kifedha ulitoka kwa I.C.F.T.U, ITWF na TUC na Tumbo alipoenda Brussels walimtishia kusitisha misaada yao kama angeng'ang'ania kusimamia mazungumzo ya usuluhisho. Inawezekana kabisa msaada huo ulitumiwa kama ilivyosimuliwa hapo juu kuwasaidia wagomaji kumudu maisha.Lakini kilicho wazi ni kuwa mgomo haukuongozwa na Mzee Salum Abdallah. Kiongozi alikuwa Christopher Kasanga Tumbo. Nadhani wakina mzee Salum Abdallah walikuwa wanampiga taf, kitu ambacho hakikuwa kidogo na wanastahili heshima kwa hilo.

Amandla...

Bwana Mdogo Fundi Mchundo

Cc. Nguruvi3
 
Fundi Mchundo sasa anapumzika. Ila ruksa kwa mtu yeyote kuchambua, kukosoa na kurekebisha pale wanapoona Fundi Mchundo amekosea. Ila kwa facts, sio picha.

Ahsante sana Fundi kwa mchango wako katika mjadala, umesaidia jamii sana

Nafunga pazia na kumwachia Mohamed ukumbi wa kusomesha.

Naenda kusoma sisubiri kusomeshwa!

Mohamed kule Sandrigham House wakisema ' the floor is yours''

Masalam!
 
Mnaojua mmQUOTE="Nguruvi3, post: 41263900, member: 24272"]
Fundi Mchundo
Katika hili la kuweka Historia katika muktadha wake hatupo wenyewe

Prof Issa Shivji na Prof Saida Othman Haroub walikwenda kwa Mohamed na tuliona Picha kama kawaida. Soma huzuni aliyo nayo Mohamed Said kwa kutosikilizwa

Kuna neno hapa, kwanza, hawa si watu wa kanisani . Pili, hawa wasomi wametafuta ukweli na katika hilo walibaini ima kujichanganya, au kutokuwa na ushahidi au kuzusha au kukosa mtiririko na hivyo kuweka pembeni maandiko ya Mohamed na kitabu chake cha Abdulwahid Sykes.

Maprofesa wameshindwa kuona 'connection' ya matukio mfano wa yale ya trade union
Kwamba Mzee Salum Abdallah , Babuye Mohamed alikuwa Rais wa TRAU na katibu mkuu C.K.Tumbo mwaka 1955.

Umetuonyesha chimbuko la trade union' kufikia mwaka 1959 C. Tumbo akiwa katibu mkuu

Hoja ya lini picha za Salum Abdallah na C.K. Tumbo zimechukuliwa haijibiwi, haina jibu.

Hoja ya vipi Abdul Sykes alieneza harakati za Uhuru Tanganyika kupitia mikutano inapojibiwa kwamba alifanya mikutano na Kenyatta na Kapenguria team

Habari kama hii unawezaje kuiweka katika chapisho la University?
Profesa waliandika Historia ya Mwalimu hawakuwa na interest nani alikuwa na Benz mjini

Mohamed hataki kukosolewa ''Anasomesha ' tu wale waliokubali kusomeshwa.
Wengine tunasoma! tumekataa kusomeshwa ! mwana 2022 bado mtu asomewe kitabu!
[/QUOTE]

Walimu mliovaa barkoa jitokezeni tuwajue mnajificha nini Kama nyinyi Mnajua ?
 
Fundi Mchundo sasa anapumzika. Ila ruksa kwa mtu yeyote kuchambua, kukosoa na kurekebisha pale wanapoona Fundi Mchundo amekosea. Ila kwa facts, sio picha.

Amandla...

Cc. Nguruvi3

Vuweni hizo mask mnaogopa nini ,
Mzee Mohammed yupo wazi , jitokezeni tuwaone wazi mkipambana naye

Mnamwogopa nani?
 
"Sasa tuje kwenye mgomo wenyewe wa 1960.
Vipi waliweza kugoma kwa siku 82 hawana mshahara?

Kabla ya ule mgomo TRAU ilipata msaada wa fedha kutoka Ujerumani ya Mashariki na Chama Cha Wafanyakazi wa Reli wa Uingereza na sehemu nyingine.

TRAU ikachagua maduka maalum ya vyakula na wakatoa kadi kwa wanachama wao wote ambayo kadi hii iliwawezesha kupata mahitaji yao ya kila siku kuanzia mchele, unga, maharage, mafuta ya kupikia mafuta ya taa hadi viberiti.

Treni zilisimama, meli na mabasi yote ya Railway.

Nyumbani kwa babu yangu ikawa ndiyo Command Post wafanyakazi waliokuwa katika mgomo wanakutana hapo kupashana taarifa."

Railway African Association ilianzishwa 1945 na tarehe 10 Septemba 1947 wanachama wao 2000 walijunga na mgomo uliokuwa unaendelea Dar es Salaam (sio Tabora). Mgomo huo uliungwa mkono na wafanyakazi wegine wa reli waliokuwa Morogoro, Kilosa, Dodoma na Tabora. Kilichoongezwa na wafanyakazi wa Tabora ni kudai walipwe mshahara sawa na wahindi.

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi lilianzishwa mwaka 1955 baada ya Tom Mboya kutoka Kenya alipotembelea Tanganyika. Tom Mboya alikuwa karibu sana na shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa dunia, International Confederation of Free Trade Unions ambacho kwa AFL-CIO ya Marekani ilikuwa na nguvu sana. AFL-CIO ilitumia ICFTU kupambana na ushawishi wa ukomunisti duniani. Mashirika mengine yaliokuwa yakitoa msaada na ushauri kwa TFL ni the Fabian Colonial Bureau, the British Trade Union Congress (TUC) na the International Transport Workers Federation (ITWF). Kutokana na kuwepo kwa vita baridi hamna namna mashirika haya yangeweza kushirikiana GDR ( Ujerumani Mashirika). Sidhani kama the National Union of Railmen ya UK iliwahi kuhusika moja kwa moja maana wao walikuwa wanaangalia maslahi ya wanachama wake wakati TUC ilikuwa na ajenda ya kusaidia vyama vingine vya wafanyakazi popote vilipo.

Tarehe 20 Januari 1956, TFL iliitisha mgomo ambao ulikuwa uanze tarehe 11 Februari wakitaka uongozi uwarudishe wafanyakazi 5000 walioachishwa kazi. Wawakilishi kutoka T.U.C na I.C.F.T.U walikuja Dar kusuluhisha mgogoro. Mgogoro ulisitishwa baada ya A.F.L-C.I.O ( bila shaka kupitia I.C.F.T.U) kuwapa TFL fedha za kuwalipa wafanyakazi walioachishwa kazi.

Mwaka 1957, Katibu Mkuu wa TFL, Rashidi Kawawa alihutubia mkutano wa I.C.F.T.U ambapo aliwaomba msaada wa mali na ushauri.

Mwaka 1958 I.C.F.T.U walianzisha chuo kwa ajili ya wafanyakazi katika vyama vya wafanyakazi. Chuo hicho kilikuwa Kampala Uganda.

Kati ya mwaka 1951 mpaka 1955 palikuwa na wastani wa migomo 60 kwa mwaka iliyohusu wafanyakazi 7805. Kati ya mwaka 1956 mpaka 1960, migomo iliongezeka hadi 146 kwa mwaka na ilihusisha wafanyakazi 59,457.

TRAU ilikuwa siku zote ikifanya mazungumzo na EARH kwa nia ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwa haswa mishahara na hali ya wafanyakazi. Lakini uongozi wa EARH ulikuwa ukipinga nyongeza yeyote ya mishahara kwa madai kuwa hawana uwezo wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi wake wote wa Afrika Mashariki ( Mishahara ilikuwa inakula £8,990,000 katika bajeti yao ya £19,500,000.).

Mwezi Mei 1959 uongozi wa EARH uliwaachisha kazi wafanyakazi waafrika waliokuwa senior. TRAU wakausihi uongozi wa EAHRC wawarudishe lakini wakakataa. Ilipofika Julai 1959, Katibu Mkuu wa TRAU, Christopher Kasanga Tumbo akatangaza kujitoa katika chombo cha usuluhishi kati yao na EARH. Mwezi Agosti 1959, mkutano mkuu wa TRAU uliamua kuwa sasa mgomo haukwepeki. Mgomo ukapangwa kuanza tarehe 18 Desemba 1959 lakini ukasogezwa baada ya wafanyakazi wa Posta nao kuanza kugoma tarehe 24 Desemba wakidai kima cha chini cha mshahara cha shilingi 150 kwa mwezi, mshahara ambao TRAU waliona unakubalika. Wafanyakazi 1200 wa Posta waligoma.

Hata hivyo mwezi Oktoba palitokea mgomo katika karakana za EARH ambapo wafanyakazi walidai kubadilishwa madaraja yao ya kazi. TRAU iliweza kuwarudisha kazini baada tu ya kuwahidi kuwa mazungumzo na utawala yataanza mara tu watakapoacha kugoma. Lakini haikuwa hivyo.

Baada ya uongozi kuendelea kuwazingua mgomo ulitangazwa tarehe 9 Februari 1960 na tarehe 10 Februari wafanyakazi 12000 wa reli walianza kugoma. Ilipofika tarehe 15 Februari wafanyakazi wa posta walikubali kima cha chini cha shilingi 107 kwa mwezi.
Mwezi Machi, ITWF na I.C.F.T.U walimtuma Jack Purvis kusaidia kuleta suluhisho. TRAU walikubali kupunguza madai yao kutoka kima cha chini cha mshahara cha shilingi 7 na senti 75 kwa saa hadi nyongeza ya shilingi 10 kwa mwezi kwa wafanyakazi wote wa daraja la C ambalo ingawa lilikuwa la chini kabisa lilikuwa na madaraja tofauti. Jack Purvis hakuweza kuwa convince uongozi wa EARH kukubali ofa hii.

Tarehe 22 Machi TFL walikutana na kutoa tamko kuwa hawataitisha mgomo mkuu ili kuwaunga mkono TRAU. Badala yake walimtaka Gavana Sir Reginald Turnbull kuingilia na kuleta suluhisho. Wasiwasi wa TFL ulikuwa kuwa mgomo huo ungeweza kuvuruga maandalizi ya uhuru uliopangwa kutokea mwaka unaofuata.

I.C.F.T.U baada ya kuona Christopher Kasanga Tumbo bado analeta ubishi walimualika kwenda Brussels kwa mazungumzo kati ya tarehe 29 Machi na 4 Aprili. Matokeo ya mazungumzo hayo ni I.C.F.T.U kumtuma Charles Millard na I.T.W.F kumtuma Pieter De Vries kusimamia majadiliano badala ya Christopher Kasanga. Uongozi wa EARH ulikuwa tayari na mgomo kwa sababu waliishapata mafanikio katika kupunguza makali ya mgomo kwa kuwatumia wafanyakazi wa kihindi na kizungu. Ila serikali iliwalazimisha wafikie muafaka kwa kuhofia kuwa ungeweza kuathiri shughuli za uhuru mwakani. Tarehe 30 Aprili ukakubali kuongeza kima cha chini cha mshahara cha C.6 kwa sh. 10 kwa mwezi ambao ulipungua hadi Sh. 4 kwa mwezi kwa wale wa daraja lla juu la C.1-3. Kiwango hiki kilikuwa pungufu sana ya kiwango walichotegemea lakini watu walikuwa wamechoka. Ila kwa kiasi kikubwa mgomo huu ulimjenga sana Christopher Kasanga Tumbo kwa wafanyakazi wa chini wa reli.

Mimi nadhani msaada wa kifedha ulitoka kwa I.C.F.T.U, ITWF na TUC na Tumbo alipoenda Brussels walimtishia kusitisha misaada yao kama angeng'ang'ania kusimamia mazungumzo ya usuluhisho. Inawezekana kabisa msaada huo ulitumiwa kama ilivyosimuliwa hapo juu kuwasaidia wagomaji kumudu maisha.Lakini kilicho wazi ni kuwa mgomo haukuongozwa na Mzee Salum Abdallah. Kiongozi alikuwa Christopher Kasanga Tumbo. Nadhani wakina mzee Salum Abdallah walikuwa wanampiga taf, kitu ambacho hakikuwa kidogo na wanastahili heshima kwa hilo.

Amandla...

Bwana Mdogo Fundi Mchundo

Cc. Nguruvi3
Umejitahidi kurudufu kazi za Moh na kuziwekea dhana zako ambazo wewe umeona zina mantiki kichwani mwako na wa upande wako japo nafsi yako imebainikiwa haki, Kukithirisha neno "nadhani" kumedhoofisha sehemu kubwa ya hoja zako
Ni mjinga pekee ndie asieweza kutambua nafasi ya Moh, wewe nilipokuwekea utambuzi wa jamii forums kwa Moh ukajipiga kifua kwamba nawe ni expert member (kwakweli inasikitisha).
Mohamed Said amekuwa akikipa Toleo Kitabu chake na yote ni kutazama mapungufu na kuboresha kwakuwa kazi ya utafiti haina mwisho huwa endelevu sasa ni toleo la 5, moh kawavuta watafiti wengi wa historia ndani na nje baada ya kueleza kwa ustadi historia iliyokuwa imewekwa kando kwa makusudi, hata huyo Kasanga Tumbo na Dr kyaruzi ambao wewe umechagua kwa sababu zako unazozijua (fallacy), Mohamed ndie aliewaeleza vyema kuliko muandishi yoyote labda kama iko mahala utuwekee, hivyo hebu uwe na Adabu unapotaka kumgonganisha Moh na khiyana kwa hao wazee wetu

Kadhalika kama ni shule mmeipata ya kutosha ima mtakubaliana na hilo au laa, kwakuwa haliondoi ukweli na jukwaa limekushuhudia mara zote ukinukuu kazi iliyotukuka ya Mohamed Said ambae akiwa kijana alitenga muda wake kutafiti na kuandika ukweli wa historia iliyowekwa kando kwakweli lazima apewe kongole, hata ulipojaribu kukileta Kitabu cha mdau mwingine kilipwaya hakikuwa na details, facts na taarifa muhimu kukaribia hata kwa mbali Kitabu cha Moh, ndio tukawaomba mjadala wa wazi badala yake mkaleta hadaa.
Kwa kuhitimisha, niendelee kuwapa moyo kujifunza historia, pia kuwanasihi kutokuwa wakaidi wa kweli kwasababu hamtoweza kuzizuia ndio Ilikwisha andikwa na wenyewe (wapigania uhuru), Ahsanteni na karibuni
 
Makala...
Ahsante sana.

Kuna tofauti kubwa kati ya mwandishi anaeleta maandishi ya mwandishi mwingine aliyemsoma na mwandishi ambae anaweka kauli yake mwenyewe aliyoandika.

Ukiandika kwa staili ya kunakili yale uliyosoma kwenye kitabu kujibu yale aliyeandika mwandishi kutoka ayajuayo kutokana na utafiti panakuwa na tofauti kubwa sana.

Katika hali kama hii msomaji anakuwa kawekewa kabrasha.
Na kabrasha ni kabrasha.

Kabrasha haliwezi kuchukua nafasi ya kitabu au paper.

Kabrasha siku zote itabakia kuwa kabrasha.

Msomaji akibahatika kusoma kitabu Historia ya TANU cha Chuo Cha Kivukoni mara moja atatambua kuwa mikononi kwake hana kitabu ila ana kabrasha.

Mpaka hapa nimeandika maneno 90 na nimetumia neno ‘’kabrasha,’’ mara 6.

Kuanzia mwaka wa 1998 kilipochapwa kitabu cha Abdul Sykes hadi kufikia kuchapwa kitabu cha Julius Nyerere imepita miaka 20.

Kama nilivyoeleza ni kuwa kitabu cha Mwalimu kisingetoka ila kwa Prof. Haroub Othman kumwendea Mwalimu na kumfahamisha athari iliyoletwa na kitabu cha Abdul Sykes.

Katika duru zetu watu wengi walimlaumu Prof. Haroub Othman kwa kitendo kile wakisema, ‘’Ina muhusu nini?’’

Lakini nilijibu kuwa Prof. Haroub Othman yeye kwa bahati mbaya sana hakuwa anaijua historia ya TANU historia aliyokuwa anaijua ni ile ya Kimambo na Temu.

Ghafla msomi huyu anakutana na historia tofauti sana tena sana na historia ya Kimambo na Temu historia iliyoandikwa na walimu wenzake wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Mshtuko alioupata ulikuwa mkubwa na mwandishi aliyeandika ni mwanafunzi wake.

Mimi sikuwa na shida na hili na nilipokutananae Prof. Haroub alinieleza mazungumzo yake na Mwalimu na akaniambia kuwa Mwalimu kakubali maisha yake yaandikwe na amempa yeye kazi ya kuandika kitabu chake.

Mwalimu alimuomba aunde kamati ya watu watano na yeye atashirikiana na kamati hii kueleza historia ya maisha yake kwani yeye hakuwa katika hali ya kuweza kukaa kitako kuandika.

Kipindi kile ndiyo maradhi yanamuanza.
Bahati mbaya kazi hii haikufanyika kwa kuwa Mwalimu alikuwa mgonjwa na hatimae akafariki.

Lakini nilibahatika kuzungumza na Prof. Ahmed Mohidin mmoja waliokusudiwa kuwa katika kamati ile ya uandishi wa kitabu cha Julius Nyerere na tulizungumza mengi kuhusu Mwalimu.

Jamaa wengi wangependa mimi nifanye patio la kitabu cha Julius Nyerere lakini nimewakatalia.

Nimewakatalia kwa kuwa kuhofia nisije kupewa tafsiri nyingine na sababu ya kusema haya ni kuwa yapo ambayo nimesoma mle yanapisha na ninayoyajua mimi na walioandika hayo ni watu wakubwa katika duru za kisomi mimi siwezi hata kuwabebea viatu vyao.

Isitoshe ni walimu wangu.

Lakini kama kawaida yangu mimi huchukulia vitu kama hivi ni kwa mtu kukosa kujua na kama hajui kama hajui kile anachoona anakijua ndicho atakachoandika kwa kuamini kuwa huo ndiyo ukweli.

Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng'wazi Kamata hakuna hata mmojawao aliyewajua wazee wangu hawa ninaoeleza historia zao hapa.

Kitabu cha Julius Nyerere ndani yake ukikisoma utaona bado kina hofu ile ile waliyokuwanayo waandishi wa Chuo Cha CCM Kivukoni – kukwepa historia ya Abdul Sykes na uhusiano wake na AA, TAA, Nyerere, TANU na uhuru wa Tanganyika na hofu hii ni kubwa sana.

Kitabu kinasema kuwa Mwalimu aliishi nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata baada ya kuacha kazi na kinamnukuu Abbas Sykes.

Huu ni mtihani mkubwa kwanza kwa taarifa yenyewe na pili kwa Abbas Sykes mwenyewe mtoa taarifa.

Lakini mimi nimewaeleza waandishi wa kitabu cha Julius Nyerere kwa urefu uhusiano uliokuwapo baina ya Abdul Sykes na Nyerere toka siku ya kwanza Joseph Kassela Bantu alipompeleka Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes.

Naamini sikubakisha kitu.
Kwenye kitabu imeandikwa Nyerere aliishi nyumbani kwa Ally Sykes.

Ally Sykes hakupata kuniambia kama aliishi na Nyerere nyumbani kwake Mtaa wa Kipata.

Ikiwa wasomaji wataamini kuwa Nyerere aliishi kwa Ally na si kwa Abdul maana yake ni kuwa yote yale ambayo nimeeleza yaliyopitikana nyumbani kwa Abdul hayakupata kutokea wala kuwepo.

Hapo ndipo iliposemwa kuwa maprofesa wameshindwa kuanisha maneno yangu na ukweli na hii ndiyo sababu ya wao kupuuza yale niliyowaeleza.

Siku zote husema si lazima mimi mtu kuniamini lakini nitaeleza kile nikijuacho.
Nahitimisha kwa maneno ya Daisy Sykes hapo chini:

‘’Nakumbuka katika akili yangu ya kitoto kumuona Mwalimu Nyerere akiishi nyumbani kwetu kwa muda katika nyumba yetu ya Mtaa wa Stanley baada ya kuacha kazi wakati marafiki zake wa karibu baba na Dossa Aziz walikuwa wanamtafutia nyumba ya kuishi.

Nyumba yetu ya Stanley kwa kuwa ilikuwa kwenye makutano ya barabara mbili ilikuwa na mjengo wa kipekee kwa nyakati zile.

Nyumba kubwa na yenye vyumba kadhaa ilikuwa upande wa Mtaa wa Stanely na upande wa Mtaa wa Sikukuu ilikuwa nyumba nyingine inayojitegemea ikiwa na sebule na chumba cha kulala hapo hapo.

Ingawa upande huu wa nyumba ilikuwa na nafasi ya kutosha ilikuwa vigumu kwa wanaume wawili wakubwa kuishi pamoja.

Naamini baba yangu mdogo Abbas ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba ile ikabidi ahame aende kweye nyumba yetu nyingine Mtaa wa Kipata au ajibane nyumba kubwa ili Mwalimu Nyerere apate utulivu na faragha katika nyumba ile.’’

Nina makala, ‘’Simulizi ya Balozi Abbas Sykes na Jeneza la Julius Nyerere.''
Makala itaongeza mengi katika historia hii.

Naweka hapo chini kipande kifupi kutoka makala hiyo:

‘’Ilikuwa tabu sana kwangu kukwepa kulitazama sanduku lile lenye mwili wa Nyerere.

Kila mara fikra zinakwenda mbele na kurudi nyuma zinakwenda mbele zinarudi nyuma namkumbuka Nyerere kijana na Bwana Abdul kijana wote vijana wako pale nyumbani kipindi kile ameacha kazi na siku za mwanzo za TANU.

Endapo mtu angelinambia kwa wakati ule kuwa Nyerere atakuja kuwa kiongozi mkubwa barani Afrika ingekuwa tabu kwangu kuamini kuwa mambo yale waliyokuwa wanayanzungumza wakipanga na kuoangua yatakuja kuwa makubwa kwa kiasi kile kilichofikia.’’

Nakuwekea picha yangu ya ujana wakati naanza utafiti huu kwa kuwa umeligusia hili.
Marehemu mama yangu akinigombesha,''Umeshikilia kucheza mpira tu unaacha kujituliza nyumbani ukasoma.''

1641200220280.png

Vuweni hizo mask mnaogopa nini ,
Mzee Mohammed yupo wazi , jitokezeni tuwaone wazi mkipambana naye

Mnamwogopa nani?
Jagina,
Kuandika ukiwa umejificha kunatia ujasiri mkubwa.
Unakejeli, unatukana, unakebehi bila uoga wowote kwa kuwa hujulikani.

Kujificha kunatoa nafasi ya kufanya kila aina ya vituko na vichekesho.

Ukimvua hili gunia usoni mtu aliyejificha anakuwa siye yeye nguvu ile aliyokuwa kaingianayo katika mjadala inakuwa umeiondosha anakuwa uchi hana cha kujistiri.

Huyu anakuwa sawa na Dracula nguvu yake iko usiku kwenye giza.
Kukicha na jua likatoka akibakia penye mwanga wa jua anakufa.

Angalia video:

Njoo kwenye mjadala wa wazi ,usijipe majina ya wajerumani , Kama nyinyi ni wasema kweli Na mnaijua historia ya uhuru wa Tanganyika

Kunitukana hakutomfanya Nyerere kuwa Saint 😝😝😝😝
S
Umejitahidi kurudufu kazi za Moh na kuziwekea dhana zako ambazo wewe umeona zina mantiki kichwani mwako na wa upande wako japo nafsi yako imebainikiwa haki, Kukithirisha neno "nadhani" kumedhoofisha sehemu kubwa ya hoja zako
Ni mjinga pekee ndie asieweza kutambua nafasi ya Moh, wewe nilipokuwekea utambuzi wa jamii forums kwa Moh ukajipiga kifua kwamba nawe ni expert member (kwakweli inasikitisha).
Mohamed Said amekuwa akikipa Toleo Kitabu chake na yote ni kutazama mapungufu na kuboresha kwakuwa kazi ya utafiti haina mwisho huwa endelevu sasa ni toleo la 5, moh kawavuta watafiti wengi wa historia ndani na nje baada ya kueleza kwa ustadi historia iliyokuwa imewekwa kando kwa makusudi, hata huyo Kasanga Tumbo na Dr kyaruzi ambao wewe umechagua kwa sababu zako unazozijua (fallacy), Mohamed ndie aliewaeleza vyema kuliko muandishi yoyote labda kama iko mahala utuwekee, hivyo hebu uwe na Adabu unapotaka kumgonganisha Moh na khiyana kwa hao wazee wetu

Kadhalika kama ni shule mmeipata ya kutosha ima mtakubaliana na hilo au laa, kwakuwa haliondoi ukweli na jukwaa limekushuhudia mara zote ukinukuu kazi iliyotukuka ya Mohamed Said ambae akiwa kijana alitenga muda wake kutafiti na kuandika ukweli wa historia iliyowekwa kando kwakweli lazima apewe kongole, hata ulipojaribu kukileta Kitabu cha mdau mwingine kilipwaya hakikuwa na details, facts na taarifa muhimu kukaribia hata kwa mbali Kitabu cha Moh, ndio tukawaomba mjadala wa wazi badala yake mkaleta hadaa.
Kwa kuhitimisha, niendelee kuwapa moyo kujifunza historia, pia kuwanasihi kutokuwa wakaidi wa kweli kwasababu hamtoweza kuzizuia ndio Ilikwisha andikwa na wenyewe (wapigania uhuru), Ahsanteni na karibuni
Wewe umejitwika urefa ukiwa kama nani? Huna sifa hiyo kabisa. Wewe ni mchangiaji tu sambamba na Sakina. MS kaulizwa maswali hadi sasa ameshindwa kutoa majawabu, na nyie sidekicks wake pia mmeshindwa kumsaidia na badala yake mnaleta kioja eti ufanyike mjadala wa wazi. Mbona wewe mwenyewe hujajitambulisha kwa jina lako halisi? Mngeanza nyie mnaodai ufanyike mjadala wa wazi kujitambulisha kwa majina yenu halisi na picha zenu ili tuwajue ni watu wa aina gani. Halafu huo mjadala wa wazi utasaidia nini cha ziada ambacho maandishi tayari yameweka wazi?
 
Azarel hayo maswali aliyoulizwa Mzee Mohammed yajibu wewe kama yeye yamemshinda au waambie Hao waulizaji wavue mask kwanza baadaye wanaweza kujibu wao
 
Ndugu zanguni,
Si kama najipigia zumari langu mwenyewe lakini naamimi wasomaji wangu wanaweza kuona tofauti ya uandishi wangu na wa wenzangu.

Kwa nini wanaandika wameghadhibika na kutukana?

Kalamu yangu haiwezi kuandika tusi wala kejeli, kebehi nk.

Jibu langu kwa haya ni kuwa kimya.

Mtu akiniandikia kwa nia ya kunidhalilisha hubakia kimya kwa sababu kumjibu ni mimi kujidhalilisha.

Nimesoma mara kadhaa hapa kuwa nimekimbia mjadala, nimeshindwa kujibu swali la babu yangu na Kassanga Tumbo nk. nk.

Kwanza nataka nieleze jambo.

Nyumba ya Kassanga Tumbo Isevya, Tabora Mtaa wa Kanoni zilikuwa zikiangaliana kwa hiyo walikuwa majirani na nyumba nyingine jirani ilikuwa ya Yunge Mwanansali mchezaji mpira maarufu sana wakati ule wa Kombe la Gossage.

Mwanae mmoja marehemu Gossage alikuwa umri wangu.

Babu yangu alikuwa na nyumba mbili mtaani hapo mwanzo na mwisho wa mtaa.

Hii ya mwisho ya mtaa ndiyo ilikuwa moja ya nyuma nzuri kabisa mtaani na ilifanana na nyumba ya Kassanga Tumbo.

Wote hawa watatu watu maarufu na wote wanafanyakazi Railway.

Naeleza haya ili wenzangu wafahamu wanapomkejeli Salum Abdallah watambue nafasi yake katika jamii.

Kuna picha mbili za babu yangu Salum Abdallah na Kassanga Tumbo.

Moja ni ‘’group photo’’viongozi wengi wa TRAU wako kwa pamoja na nyingine siku babu yangu alipovishwa mgolole kama ishara ya TRAU kuingia katika mapambano na nikasema kuwa huenda hii picha ni wakati wa mgomo wa 1960.

Kwanza hebu tuanze na historia yenyewe ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.

Hii historia haikuwapo kwa hiyo si Abdul Sykes, si Kassanga Tumbo si Salum Abdallah waliokuwapo.

Sasa tatizo nini?

Lakini historia ya Kimambo na Temu ilikuwapo.

Mbona hatuwalaumu kwa kutokuwa makini katika uandishi wa historia ya Tanganyika?

Lakini kila pakiandikwa babu yangu na mimi tutakejeliwa.

Kwa kuwa siwezi kujibu kejeli nabakia kimya.

Na si kama ukimya wangu ulikuwa bila sababu.

Kuna nilichokuwa nakitafuta.

Saikolojia ya binadamu ina namna yake ya kufanya kazi ya utambuzi.

Ubongo ukishajua kuwa fulani ni mtu wa kejeli, kebehi na matusi basi hiyo ndiyo inakuwa ‘’identity’’ yake na hii ndiyo inakuwa ‘’label’’ yake.

Watu wa matusi na kejeli wote wanafahamika na staili yao ya uandishi.
Nilieleza hapa pia mtu mwenye hasad mwepesi kumfahamu.

Atakichukia kile ambacho yeye anakiona wewe unacho yeye Allah kamnyima.

Ule moto ambao Iblis anaukoleza ndani ya moyo wake unamzuia yeye kuona neema aliyopewa yeye ambayo mwingine hakupewa.

Hasad ni katika maradhi mabaya sana ya nafsi.

Ndiyo kila akizunguka atarejea kwenye Mercedes ya Abdul Sykes na kumwaga kejeli.

Ile ‘’context’’niiyoandikia haioni yeye anaona ile gari tu na kama si chochote.
Mercedes mwaka wa 1959 uhuru bado iwe si chochote kweli?

Atarejea kwenye picha zangu.
Yeye hana.

Tujaalie atakuwa na picha.
Yuko Trafalgar Square London?

Nimetajiwa hapa ''Buckingham.''

Mbona hapo palikuwa meeting place yangu London?

Ndiyo nikaweka picha niko Buckingham Palace.

Nafanya hivi makusudi ili tulewane na tuheshimiane.

Sijataka kujibu mimi kuhusu Abdul Sykes kuhutubia mkutano.

Kwanza kwa sababu niliamini kabisa mtu aliyesoma historia ya urafiki na udugu wa Abdul Sykes na Nyerere katika kitabu changu atajua nini hisani iliyokuwapo baina yao.

Lakini nikaandika kueleza mkutano wa siri wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta Nairobi mwaka wa 1950 Abdul akiwa ijana wa miaka 26.

Niliamini atatambua kuwa hili ni jambo kubwa kuliko Abdul Sykes kupanda kwenye jukwaa la TANU Mnazi Mmoja kuhutubia mwaka wa 1954.

Lakini nikaenda mbali zaidi nikaeleza kuwa Abdul Sykes hata kama ukimpandisha jukwaani wala hatajua aseme nini kuwaambia wananchi kwani yeye hakuwa mtu wa majukwaa na kwa kueleza hili vizuri nikasema kuwa Nyerere ungemfuata ukamwambia lete fedha kwa ajili ya jambo kadha wa kadha asingeweza kutoa kwani hakuwa na fedha.

Allahu Akbar.

Nimeambiwa nimemdhalilisha Mwalimu kuwa alikuwa masikini na mwandishi anasema kahamaki sana kwa maneno yangu.

Imekuwa kwangu mimi ‘’Catch 22.’’

Mipango ya mikutano yote ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na ratiba ikipangwa pale na Nyerere yupo na hakuna atakaemwambia Abdul kuwa, ‘’Abdul kesho utapanda jukwaani kuhutubia.’’

Hatoambiwa hayo kwa kuwa wanajua hiyo si idara yake hiyo ni kazi ya TANU President Julius Kambarage Nyerere.

Lakini baada ya mkutano walikuwa na kawaida ya kukutana Princes Hotel kwa ajili ya kujipongeza na kuangalia mkutano ulikwendaje nk. nk.

Huu mgahawa ulikuwa unamilikiwa na Goa moja jina lake Ommy.

Bili ya vinywaji na vyakula ikija hapelekewi Nyerere bili itakwenda kwa Abdul na Dossa na hivi ndiyo walivyokuja kupewa lakabu zao yaani ‘’nickname,’’ Abdul akiitwa ‘’The Sweet,’ na Dossa ‘’The Bank.’’

Abdul kapewa jina hilo kwa wema na ukarimu wake na Dossa kwa fedha nyingi alizokuwanazo.

Baadae Bi. Titi akaja kumpa Nyerere jina la ‘’Mwalimu,’’ na likamkaa hadi kaingia nalo kaburini.

Huwa nakaa kimya si kwa kuwa sina majibu nakaa kimya kuepusha shari.

1641233713188.png

Dossa Aziz na Bi. Titi Mohamed katika utu uzima.
 
Jagina,
Kuandika ukiwa umejificha kunatia ujasiri mkubwa.
Unakejeli, unatukana, unakebehi bila uoga wowote kwa kuwa hujulikani.

Kujificha kunatoa nafasi ya kufanya kila aina ya vituko na vichekesho.

Ukimvua hili gunia usoni mtu aliyejificha anakuwa siye yeye nguvu ile aliyokuwa kaingianayo katika mjadala inakuwa umeiondosha anakuwa uchi hana cha kujistiri.

Huyu anakuwa sawa na Dracula nguvu yake iko usiku kwenye giza.
Kukicha na jua likatoka akibakia penye mwanga wa jua anakufa.

Angalia video:

1641240037801.png

Picha ya Mtaa wa Jaribu magomeni Mapipa ambayo inadhaniwa ni Mtaa wa Congo 1920 hapa ni nyumbani kwa Ali Msham aliyefungua tawi la TANU nyumbani kwake 1954/55.
 
Si unasema mliandika wote hicho kitabu? Kwa nini haukumsahihisha wakati mnakiandika? Yote haya unayaleta baada ya kukuambia kuwa tofauti na ulivyotaka kutuaminisha, Mwakikagile alikuita mdini.

Sasa turudi kwenye hiyo taarifa ya Tanganyika Welfare Association unayoikosoa. Chama hiki kilianzishwa na Mwalimu, Andrew Tibaindebage na Hamza Mwapachu wakiwa wanafunzi Makerere ili kutetea maslahi ya wanafunzi waliokuwa wanasoma huko. Baadae walikigeuza kuwa tawi la TAA Makerere, Nyerere akiwa Rais wa tawi hilo. Shida yako unadhani Nyerere aliijua TAA kutokana na wakina Sykes na kwa sababu wakina Sykes hawakwenda Makerere basi hamna jinsi Nyerere angeweza kujiunga na TAA.

Huu ni ushahidi kuwa haujui historia kamili ya uhuru wa Tanganyika kwa sababu kwako wewe historia yote ilianzia na kuishia Gerezani.

Amandla...

Kijana Fundi Mchundo

cc. Nguruvi3

Mwalimu Nyerere mwenyewe, katika mahojiano na Ikaweba Bunting, New Internationalist December 1998, alisema ni yeye aliyeanzisha the Tanganyika Welfare Association mwaka 1943 alipokuwa Makerere:

Ikaweba Bunting: When did you first encounter the idea of liberation from colonialism?

Nyerere: I cannot say I encountered the idea of liberation in a totality like a flash of light. I did not have an experience like Paul on the road to Damascus. For me it was a process – something that grew inside of me. Our elders fought and were defeated by the Germans and the British. We were born under colonialism. Some of us never questioned it. Those who got educated began to think about it. What many of us went through was simply a desire to be accepted by the white man. At first this is what it was – a kind of inert dissatisfaction that we were not accepted as equals.

World War Two and what it was fought for – democracy and freedom – started the process for many people, especially those who were in the Army. For me the transformation came later. At Makerere in 1943 I started something called the Tanganyika African Welfare Association. Its main purpose was not political or anti-colonial. We wanted to improve the lives of Africans. But inside us something was happening.

I wrote an essay in 1944 called The Freedom of Women. I must be honest and say I was influenced by John Stuart Mill, who had written about the subjugation of women. My father had 22 wives and I knew how hard they had to work and what they went through as women. Here in this essay I was moving towards the idea of freedom theoretically. But I was still in the mindset of improving the lives and welfare of Africans: I went to Tabora to start teaching.
 
Mwalimu Nyerere mwenyewe, katika mahojiano na Ikaweba Bunting, New Internationalist December 1998, alisema ni yeye aliyeanzizha the Tanganyika Welfare Association mwaka 1943 alipokuwa Makerere:

Shwari,
Hii kaui ya Mwalimu Nyerere haina tatizo lolote.

Lakini hebu angalia picha hiyo hapo chini na maelezo yake yanavyopishana na ukweli.
Hili ni gazeti la Daily News (bahati mbaya sikuandika tarehe) linasema kuwa nyumba hii ya Mwalimu ina utajiri mkubwa wa historia ya uhuru.

Ukweli ni kuwa nyumba hii imejengwa mwaka wa 1958 na Mwalimu alihamia hapa baada ya kuhama hiyo nyumba nyingine iliyo chini mkono wa kulia ambayo ilikuwa sehemu hapo hapo Magomeni panaitwa Maduka Sita.

Nje ya nyumba hiyo huyo anaeingia ndani nia Mwalimu Nyerere.

Ukweli ni kuwa Mwalimu hakuishi sana nyumba hiyo aliyojenga mwaka wa 1958 akahama akahamia nyumba ya serikali Tanganyika inaelekea kupata Madaraka.

Hakuna mikutano yoyote ya siri iliyokuwa kifanyika si hapo wala katika nyumba ya zamani Majumba Sita.

Nyumba ya kushoto ni nyumba ya Abdul Sykes ambayo ndipo Nyerere aliishi kwa muda mwaka wa 1955 baada ya kuacha kazi ya ualimu.

Hii ndiyo nyumba mipango yote ya harakati na mikutano ya siri ikifanyika hapo toka enzi za TAA.

Ni katika nyumba hii ndipo Nyerere alipojuana na Abdul Sykes mwaka wa1952.
Iweje hadi leo miaka 60 ya uhuru historia ya uhuru wa Tanganyika haijakaa sawa?

1641243249687.png
 
Mr Mwakikagile wrote that TAWA ( Tanganyika African Welfare Association or Tanganyika Student Welfare Association or the Tanganyika Students Association) was a students' organisation formed at Makerere for the Tanganyikan students studying there. TAWA was founded by Julius Nyerere, Andrew Tibandebage and Hamza Bakari Mwapachu ( who was Nyerere's best friend at Makerere and shared a dormitory with him) in 1943. This was confirmed by Mr Tibandebage who wrote in his memoirs that after forming TAWA, Nyerere was elected its Secretary and its Chairman. Mwalimu Nyerere, in the above interview further confirms the veracity of what Mr Mwakikagile wrote.

TAWA was transformed in 1946 into a branch of the Tanganyika African Association whose official title was "the African Association, Makerere Branch, Kampala, Uganda". Some members of the Makerere African Association were David Makwaia, Andrew Tibandebage, Abdullah Fundikira, Hamza Mwapachu and Vedastus Kyaruzi).

Him-who-shall-not-be-mentioned had written that Mwakikagile was not to be trusted because of his claim that Nyerere had found the National Tanganyika African Welfare Association and later replaced it with the Tanganyika African Association. This was not what Mwakikagile had written ( as I have shown above) and was only meant to impugn Mwakikagile for the temerity of implying that he-won't-be-mentioned was a religious bigot ( my words). What was being done in this insinuation was character association of the highest order. This, unfortunately, is something that we are used to.

Nyerere's TAWA should not be confused with the Tanganyika African Welfare and Commercial Association formed in 1936 by Erica Fiah who had in 1934 founded the African Commercial Association ( he was its secretary and treasurer). Fiah was disappointed by the non-political nature of the African Association that he had joined in 1934. Fiah was influenced by Marcus Garvey and the TAWCA was definitely Graveyite and much more political than TAA. The radical nature of TAWCA is evident from its promise to bury any " African whether Christian, Mohammedan or Pagan who dies in a hospital or outside....who has no relative in Dar es Salaam". TAWCA was a rival to TAA which Fiah " regarded as worse than useless because it was not only afraid of 'politics' as almost all its members were government employees who did nothing to help the bulk of the African population". Fiah's efforts to turn the TAA ( he was elected its secretary in 1938) were rebuffed and he decided to focus more on his journal, Kwetu, which he had established in November as a mouthpiece for TAWCA. While we hear lamenting about the sidelining of one group that was active in TAA and TAWCA, how many out there are aware of the contributions and sacrifices that this man, born in Uganda in the struggle for the independence of Tanganyika?

I have only responded to you because you have raised pertinent questions and this is the first time that I have heard from you.

Having said that, I will continue with my break, contemplating on how come I never got to stay at Buckingham Palace.

Samahani kwa kuandika kwa lugha nisiyoimudu vizuri. Nilifanya hivyo baada ya kudhani ni lugha uliyotumia kutokana na "quote " ndefu uliyoiweka.

Umeuliza mahusiano ya Nyerere na TAWA na umejibiwa kwa kuwekewa picha ya nyumba yake Magomeni na unakumbushwa kuwa aliwahi kuishi kwa Abdul Sykes! Na kuthubitisha hilo unawekewa picha ya nyumba ya Sykes. Halafu tunaambiwa tumejaa matusi tukiuliza hizo picha zina husiana vipi na TAWA. Go figure.

Amandla...

Cc. Nguruvi3
 
Shwari,
Hii kaui ya Mwalimu Nyerere haina tatizo lolote.

Lakini hebu angalia picha hiyo hapo chini na maelezo yake yanavyopishana na ukweli.
Hili ni gazeti la Daily News (bahati mbaya sikuandika tarehe) linasema kuwa nyumba hii ya Mwalimu ina utajiri mkubwa wa historia ya uhuru.

Ukweli ni kuwa nyumba hii imejengwa mwaka wa 1958 na Mwalimu alihamia hapa baada ya kuhama hiyo nyumba nyingine iliyo chini mkono wa kulia ambayo ilikuwa sehemu hapo hapo Magomeni panaitwa Maduka Sita.

Nje ya nyumba hiyo huyo anaeingia ndani nia Mwalimu Nyerere.

Ukweli ni kuwa Mwalimu hakuishi sana nyumba hiyo aliyojenga mwaka wa 1958 akahama akahamia nyumba ya serikali Tanganyika inaelekea kupata Madaraka.

Hakuna mikutano yoyote ya siri iliyokuwa kifanyika si hapo wala katika nyumba ya zamani Majumba Sita.

Nyumba ya kushoto ni nyumba ya Abdul Sykes ambayo ndipo Nyerere aliishi kwa muda mwaka wa 1955 baada ya kuacha kazi ya ualimu.

Hii ndiyo nyumba mipango yote ya harakati na mikutano ya siri ikifanyika hapo toka enzi za TAA.

Ni katika nyumba hii ndipo Nyerere alipojuana na Abdul Sykes mwaka wa1952.
Iweje hadi leo miaka 60 ya uhuru historia ya uhuru wa Tanganyika haijakaa sawa?

View attachment 2067614
Shwari na ndugu zangu wengine,

Kwanza napenda nikufahamisheni kuwa kuhusu historia ya Mwalimu Nyerere na maneno ambayo yeye mwenyewe kasema au kaandika hakuna tatizo ila katika historia yake mwenyewe katika uhuru wa Tanganyika ambapo Mwalimu hakusema mengi.

Hii ndiyo sababu ya makosa kama hayo katika Daily News.

Hapa ambapo Mwalimu hakusema mengi ndipo yako mengi ambayo yanahitaji mchango wa watafiti huru kufahamika.

Mimi nimesoma kila kitabu kinachomuhusu Mwalimu na nimesoma vitabu vyake vyote alivyoandika kwa hiyo naweza kusema kwa kiasi fulani ninamfahamu.

Nimemsoma pia katika nyaraka nyingine binafsi za watu waliokuwa wanamfahamu.

Nimemsoma Mwalimu katika ''notes'' za Dr. Wilbard Mwanjisi, barua za Mangi Mkuu Thomas Marealle na katika Nyaraka za Sykes na nyaraka zote hizi zimehifadhiwa na ukoo wa Sykes.

Picha hiyo hapo chini nilisahau kuweka pale nilipoweka ''cutting,'' ya gazeti la Daily News lililo na taarifa ambazo si sahihi kuwa nyumba ya Mwalimu Magomeni ina historia kubwa ya uhuru wa Tanganyika.

Niliweka picha ya nyumba ya Abdul Sykes tunaweza kusema Baba wa Taifa alikuja kufahamiana na wenyeji wake waliompokea Dar es Salaam ya 1950.

Pili ni nyumba ambayo mikutano ya siri ilipokuwa ikifanyika wakati wa TAA na TANU na Baba wa Taifa aliishi hapo baada ya kuacha kazi kama nilivyokwisha eleza.

Nyumba ile sasa haipo imevunjwa na badala yake akina Sykes wamejenga nyumba hiyo hapo chini.

Watafiti wengi wanaokuja Tanzania kwa ajili ya utafiti huniomba kuona nyumba hii ambayo Baba wa Taifa aliishi na ndipo mikakati ya kupambana na Mwingereza ilipokuwa ikifanywa.

Watafiti hawa huwa tayari wameshafika kwenye Kumbukumbu ya nyumba ya Mwalimu, Mtaa wa Ifunda Magomeni.

Watafiti hawa hushangaa kwa nini hakuna kibao cha maelezo ya umuhimu wa mahali pale yalipokuwa makazi ya Abdul Sykes na huniuliza kwa nini nyumba inayobeba historia ya Baba wa Taifa ilivunjwa.

Sehemu ya pili huniomba nikawaonyeshe Soko la Kariakoo ilipokuwa ofisi ya Abdul Sykes ambako umuhimu wake ni kuwa ni moja ya vituo vya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ndugu zanguni nakuwekeeni picha hizi na kukuelezeni historia hii kwa kuwa naamini wengi wetu hatukuwa tunaijua kwa hiyo sasa tuko katika kuisoma upya historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

1641265753824.png
 
View attachment 2067703
Shwari na ndugu zangu wengine,
Niruhusini nikupeni historia ya wazalendo watatu katika siasa za vyama vya wafanyakazi mwishoni miaka ya 1940s kuelekea 1950s mjini Dar es Salaam.

Wazalendo hawa ni Erika Fiah, Kleist Sykes na mwanae Abdulwahid Kleist Sykes.

Nafanya hivi kwa kuwa Erika Fiah katajwa mara kadhaa hapa jamvini ningependa nikuhadithieni historia yake ili mpate kumfahamu vizuri.

Kwa kuwa ni historia ndefu nitatanguliza link ambayo ni kisa kizima na baadae In Shaa Allah nitaiweka historia hii kwa ufupi:

''...tunakutana na Abdulwahid Sykes na African Association na hii ikiwa mwaka wa 1947 miaka miwili imepita baada ya yeye na mdogo wake Ally kurudi kutoka Burma walipokwenda kupigana katika Vita Kuu ya Pili.

Dhiki ilitawala mji mzima hasa kwa kuwa ndiyo kwanza Tanganyika ilikuwa inatoka katika kishindo na mkiki mkiki wa vita.

Hali hii ndiyo iliyomsukuma Abdul Sykes katika siasa na ikamfanya aelewe maana ya harakati za wananchi dhidi ya utawala wa kigeni akiwa bado kijana mdogo sana.

Kidogo kidogo baba yake alianza kumkabidhi Abdul kazi za African Association na mara akawa msaidizi wa baba yake katika siasa za Dar es Salaam.

Ilikuwa katika kutimiza haya ndipo Abdulwahid akajikuta anahusika na ule mgogoro wa makuli ulioibuka bandarini Dar es Salaam ambao ulikuwa ukichemka pole pole chini kwa chini kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili.

Hatimaye, Abdul Sykes alihusika na harakati za siri za wafanyakazi bandarini ambao, wakiwa wamechoshwa na sheria za kazi za ukandamizaji na wakiwa wamechoka kunyonywa na makampuni ya meli, walikuwa wanapanga kuitisha mgomo.

Kleist mwenyewe alikuwa hakuwa mbali na siasa za wafanyakazi yeye akiwa mwajiriwa wa Tanganyika Railways alijaribu kuwakusanya wafanyakazi wa Railway kuasisi chama chao.

Kamati ndogo ya siri iliundwa na Abdulwahid akatiwa ndani ya kamati hiyo ili kuongoza mgomo uliokusudiwa.

Kazi ya kamati hiyo ilikuwa kupanga na kuratibu mikakati ya kuitisha mgomo ambao ungelisaidia katika kuondoa ile dhulma iliyokuwepo. Makuli waliitisha mkutano pembeni kidogo mwa mji, mahali palipokuwa pakijulikana kama ‘’Shamba kwa Mohamed Abeid,’’ katika bonde la Msimbazi.

Mohamed Abeid mwenye shamba hili alikuwa Muarabu mwenye asili ya Yemen na shamba lake lilianzia Msimbazi kuelekea Mchikichini.

Sehemu hii ilichaguliwa makhususi mbali na macho ya watu ili ipatikane faragha waweze kufanya shughuli yao waliyokusudia kwa utulivu.

Makuli walikula kiapo na kusoma Ahlal Badr ilii kujikinga na unafiki, usaliti pamoja na shari ya vizabizabina wangeokataa kugoma.

Siri ya mgomo huu ilihifadhika hakuna nje yao aliyejua nini kitatokea.

Mapema asubuhi moja kile kilichoanza kama mipango ya siri dhidi ya makampuni ya Wazungu bandarini, kililipuka na kuwa mapambano ya dhahiri.

Watu katika mitaa jirani ya Mtaa wa Aggrey, alipoishi Abdul na baba yake walikuwa hawajatoka vitandani mwao alifajiri moja wakasikia vishindo na makelele vimetanda mtaani.

Makuli, baadhi yao wakiwa vidari wazi, walikuwa wameizingira nyumba ya Kleist, wakipiga makelele wakimtaka Abdulwahid atoke nje.

Makuli wale walipiga kwata njia nzima kutoka bandarini huku wakitoa maneno ya kupinga ukoloni na wakiimba kupandisha morali zao.

Tukio hili halikuwa na kifani. Ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Tanganyika kwa wananchi kushuhudia katika mitaa ya Dar es Salaam uasi wa dhahiri kama huo dhidi ya serikali ya kikoloni.

Abdul Sykes wakati ule kijana mdogo kabisa wa umri wa miaka 23, akichungulia kupitia dirisha la chumba chake alichokuwa amelala, alishangazwa kuona umati mkubwa wa watu nje ya nyumba yao.

Aliweza kuwatambua baadhi ya wenzake katika kamati ile ya siri iliyokuwa inapanga mipango ya mgomo.

Alipotoka nje kuonana nao makuli wenye hasira walimfahamisha kuwa mgomo ulikuwa umeanza na wasingerudi kazini hadi madai yao yote yamekubaliwa.

Mgomo huu ulienea kama moto wa makumbi ulikumba nchi nzima kwa kasi ya ajabu.

Ilikuwa kama vile wafanyakazi wa nchi nzima wametaarifiana.

Wafanyakazi wa Tanganyika Railways huko Tabora wakiongozwa na babu yangu Salum Abdallah waliingia kwenye mgomo tarehe 11 Septemba, siku tano baada ya mgomo wa makuli kuanza Dar es Salam.

Mgomo ule ulisababisha serikali ya kikoloni kupitisha sheria ambayo iliruhusu kuundwa na hatimae kusajiliwa kwa Dar es Salaam Dockworkers’ Union.

1641294214503.png

Abdul Sykes katika unifom ya KAR
Burma Infantry

Itaendelea...
 
Mohamed darsa limekwama! teh teh teh . Umeamini sasa ha ha ha!

Wasomaji wanatunasoma si wewe. Tumekuacha na vijana darsa limekufa

Tuna mada nyingine muhimu, tukutakie heri wewe na 'wanaosomeshwa'

Masalam

Na uso umevaa kikoi unarusha madongo 😄😄😄😄
 
Back
Top Bottom