1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Fundi...
Nimependa sana hii kuwa mimi siyo ''authority,'' historia ya uhuru wa Tanganyika bali ni ''authority,'' wa akina Sykes.

Umenikosha sana hapa.

Ulikuwa unajua mchango wa akina Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika kabla mimi sijawaandika?

Historia ya TANU ya Kivukoni ilikuwepo toka 1981 na iliwafuta akina Sykes na wapigania uhuru wengi mbona hukusema kitu ulikuwa kimya?

Unajua kuwa umuhimu wa akina Sykes katika historia ya uhuru wa Tanganyika ni kuwa ni wao katika wale waasisi wa African Association ndiyo walioandika historia ya AA na kuacha nyaraka ambazo ndizo hizi nimezitumia kuandika historia yao na historia ya kuamka kwa Waafrika kudai haki zao katika nchi yao.

Huyu ni baba yao Kleist Sykes mwaka wa 1929.

Sasa njoo kwa watoto Abdul na Ally hawa wanaanza harakati 1942 wakiwa Burma.

Nimetumia nyaraka za Sykes kuandika historia ya TANU na historia ya Julius Nyerere.

Kuna yeyote mwenye ushahidi wa picha na nyaraka wa historia ya Nyerere katika TAA kuanzia alipokutana na Abdul Sykes 1952 na kutiwa katika uongozi wa juu 1953?

Umepata kuona au kusoma popote pale historia ya Nyerere kama nilivyoieleza katika kitabu cha Abdul Sykes?

Sikujua kama kurudisha historia ya zaidi ya miaka 50 iliyofutwa ni udini.

Vipi wale walioifuta historia hii na kuweka ya kwao nini kiliwasukuma kufanya hivyo?

Haikuwa uoga wa kuona kuwa Waislam watakuwa kila mahali katika historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika?

Kaa kitako jitulize na fikiri iweje Nyerere afikie mahali asahau hata kama alimkuta Abdul Sykes Secretary na Act. President wa TAA pale alipompokea Dar es Salaam 1952?

Asahau pia aligombea na yeye nafasi ya urais wa TAA.

Inawezekana vipi Nyerere atoe medali 3, 979 wakati anaacha uongozi na Abdul na Dossa hawamo katika orodha ile?

Unajua nini alisema alipoulizwa na watu wake wa karibu kuhusu hili?

Mimi nimewarejesha katika historia Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Sulemaiman Takadir, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Halima Selengia, Tatu bint Mzee. Mama bint Maalim, Amina Kinabo, Nyange bint Chande, Zarula bint Abdulrahman kwa kukutajia wachache katika wanawake waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Si akina Sykes peke yao.

Naijua historia kubwa ya Tanganyika kutoka kila pembe.

Sikuwapiga Mama Mkello na Mohamed Mkwawa picha sebuleni kwangu.

Picha hizo nimezipiga majumbani kwao Tanga nikiwa na Ann Lee.

Mimi haya mambo kaka nayajua na si kwa kuwa mimi nina akili kuwapita watu wengine.

Hii historia imekuwapo nyumbani kwetu mimi mdogo wala sikuwa najua nashuhudia jambo kubwa katika historia ya Tanganyika na Zanzibar.

Hivi hujajiuliza kwa nini akina Sykes walinifungulia mimi ile hazina ya nyaraka zao na si mtu yeyote yule.

Hivi unajua baada ya historia ya kweli kuwa hadhir kila mtafiti akienda kuwahoji akina Sykes na kutaka kuona nyaraka zao jibu lao ni, ''Mohamed Said keshaandika someni kitabu chake.''

Unajua kwa nini wanasema maneno haya?

Leo tunaisoma upya historia ya Nyerere na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hivi hujajiuliza kwa nini Dr. Ghassany alinichukua mimi kama msaidizi wake katika utafiti wa kitabu chake na si mtu mwingine yeyote yule?

Jiuilize maswali haya yote na jaribu kupata majibu.

Hivi unajua kuwa ni Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo waliompeleka Nyerere Zanzibar kumjulisha kwa Karume?

Baba yangu alikuwa rafiki mkubwa wa Abdulaziz Twala na Jaha Ubwa wote hawa ASP na wanamapinduzi na waliuliwa baada ya mapinduzi.

Inawezekana kweli mimi si ''authority,'' lakini wengi wakitaka kujua mambo wanakuja kwangu hata jopo la Prof. Shivji walioandika Biography of Julius Nyerere walikuja kunihoji na nikawapa picha na baadhi ya Nyaraka za Sykes.

Hii ndiyo nafasi yangu katika historia ya Tanganyika na Zanzibar.

View attachment 2058609
Kulia Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng'wazi Kamatha wakinihoji nyumbani kwangu kuhusu Julius Nyerere wakati wanatafiti maisha yake kwa ajili ya kitabu chake.
Unathibitisha tena kuwa wewe ni authority wa historia ya wakina Sykes. Na kuhusu wakina Sykes, nilijua kuhusu mchango wao kabla ya wewe kuandika. Tofauti na wewe unavyotaka kutuaminisha mapambano ya uhuru hayakuwa ya watu wa Gerezani peke yao. Hao wakina Sykes na wengine uliowataja wasingekubalika kwa wanyakyusa bila wakina Mwakangale, Kanda ya ziwa bila wakina Bomani, Kilimanjaro bila wakina Mbowe, mission quarter bila wakina Phombeah na sehemu nyingine ni watu kama wakina Kasanga Tumbi, Rupia wazee wako wasingeona ndani. Bila wakina Robert Makange na gazeti lake kazi ingekuwa ngumu. Mimi sikatai mchango wa wakina Sykes, Mwapachu na wengine. Ninachopinga ni wewe kuwavisha joho la udini wakati wengi wao walikuwa Nationalists kuliko wadini ndio maana waliwakubali watu kama Dr. Kyaruzi, Julius Nyerere, Oscar Kambona na wagalatia wengine tu katika mpambano wa kudai uhuru. Hao wakina Sykes walikuwa wapiga muziki, watu wa Klabu, leo unataka kuwageuza wapigania ukombozi wa waislamu na sio watanzania wote?
Kupiga picha na kuhojiwa na watu kama Issa Shivji hakukufanyi authority wa historia ya Tanganyika, bali authority wa sehemu ya historia ya Tanganyika. Badala ya kutuwekea mapicha ukinywa chai nao weka mahali walipo ku cite kama source ya maandiko yao! Wewe unatoa anecdotal evidence ambazo unajipa authority ambayo sio yako. Kitabu kuwa Library of Congress sio ushahidi kuwa wewe ni authority maana ile ni maktaba na inakusanya maandiko karibu yote yanayofanyika Marekani.

Unasema uliwaona wakina Sykes katika party zao wakati Ally Sykes alikuwa active katika muziki katika miaka ya mwisho ya 1940s ( ulikuwa haujazaliwa). Ally Sykes na Peter Bernard walitoa nyimbo zao 1947, Ally Sykes na bendi yake the Merry Blackbirds nao walitamba katika miziki ya dansi ya early 1950s wakati ulikuwa haujazaliwa maana ulienda middle school 1960s. Wewe tambia nyimbo za wakina Salum Abdallah Yazide, sio za Ally Sykes.
Unasema Dennis Phombeah alikuja baadae lakini unakiri kuwa kadi ya 5 ya chama cha TANU alipewa yeye. Ni yale yale ya kutaka kuwazima wagalatia.

Wewe unaona tu kuwa Nyerere aliwanyima medali ndugu zako waislamu, niambie kama aliwapa medali wakina Kyaruzi, Phombeah, Kirilo n.k. na wagalatia wengi tu waliopigania uhuru wa nchi ya Tanganyika. Unajifanya hauoni yaliyompata Oscar Kambona na wakina Kassanga Tumbo.

Mimi shida yangu na wewe ni pale unapotaka kutuaminisha kuwa ni ndugu zako wa kiislamu peke yao ndio waliopigania uhuru. Unafanya kosa lile lile ambalo wapambe wa Nyerere walitaka kutuaminisha kuwa ni yeye peke yake ndie aliyepambana na mkoloni. Ninachojua mimi ni kuwa wakina Sykes walipigania uhuru wetu kwa kushirikiana kikamilifu na wengine bila kujali dini, kabila au rangi zao. Watu kama nyinyi ndio mnataka ku distort mchango wao kwa kuingiza udini.

Amandla....
 
Katika utafiti huu ndipo nilipojua historia ya kweli ya mapinduzi nani kahusika nani katoa fedha, mchango wa askari mamluki kutoka kambi ya Kipumbwi Tanga, mchango wa Algeria, Wayahudi, Waingereza, serikali ya Tanganyika nk. nk.
Mimi hapa ndio sielewi kabisa utafiti uliofanywa na wataalam wa Harvard. Algeria ya mwaka 1963 ilikuwa haina uwezo wa kuchangia mapinduzi yeyote maana ndio kwanza ilitoka kwenye vita yao ya kudai uhuru kutoka kwa mfaransa. Israel ilikuwa macho yote nchi za kiarabu ambao tarehe 14 Januari 1964 walitangaza mapambano dhidi ya Israel. Algeria ikiwa moja ya mataifa ya kiarabu isingeweza kushirikiana na Israel kwa namna yeyote ile. Muingereza aliondoka na kuiacha nchi ikiwa chini ya utawala kamili wa Sultan ambae walifanya kila mbinu chama chake kishinde dhidi ya ASP na UMMA lakini hata mwezi haujapita wanatuma askari wake kushiriki kupindua nchi hiyo hiyo! Aidha, waingereza wasingeweza kushirikiana na UMMA kwa sababu waliwahesabu kuwa ni wakomunisti ambayp ilikuwa kweli. Tanganyika ndio pekee ambao angalau ungeweza kusema kuwa wangefurahia mapinduzi. Shida ni kuwa hao hao ndio walioruhusu meli ya Jamshed kutia nanga Dar kuepuka mapinduzi. Kama kweli walikuwa wana ubaya nae kwa nini hawakumkamata na kumkabidhi kwa wakina Karume na Babu? Tunaambiwa kulikuwa na jeshi la askari wa kukodi wa kimakonde bila kuambiwa walitokea wapi maana wamakonde wengi walitoka Msumbiji ambayo wakati ule ilikuwa chini ya wareno. Na kwa nini wamakonde peke yao? Walikuwa na special skills zipi? Au hawa ni wamakonde ambao walikuwa uzawa wa watumwa Zanzibar? Na kama alivyouliza Nguruvi3 , mtafiti alifanya jitihada gani kuthibitisha simulizi za yule babu? Haiwezekani jeshi ambalo limefadhiliwa na Tanganyika lipige kambi na bila shaka kufanya mazoezi bila wananchi wengine kuwaona. Aidha, haiwezekani wote wapotee bila trace baada ya Mapinduzi kufanikiwa na kubakia kama kumbukumbu za wazee wawili. Hawa kama walikuwa sehemu la jeshi lililopindua ni lazima wangejianika wazi kama alivyofanya Okello. Na kwa nini vijana wa ASP waseme wao ndio walioongoza mashambulizi ya kuiba silaha wakati wanajua uongo huo ulikuwa ni rahisi sana kugundulika?

Hii simulizi inazua maswali kuliko majibu.

Amandla...
 
Mimi shida yangu na wewe ni pale unapotaka kutuaminisha kuwa ni ndugu zako wa kiislamu peke yao ndio waliopigania uhuru. Unafanya kosa lile lile ambalo wapambe wa Nyerere walitaka kutuaminisha kuwa ni yeye peke yake ndie aliyepambana na mkoloni.
Hili tumelieleza sana kwa Mohamed, makosa ya Kivukoni yasijirudie kwake.
Wenye kufikiri tuliuliza sana kuhusu ujio wa Nyerere Dar na harakati

Nyerere
Mwaka 1929 alikuwa na miaka 7 wakati Mwl Matola anakuwa kiongozi
Mwaka 1948 alihudhuria mkutano mkuu akiwa katibu wa Tawi la Tabora
Mwaka 1952 anarudi akiwa na M.A
Mwaka 1954 TANU inaundwa
Mwaka 1955 anakwenda UN

''Chronologically' jinsi mwalimu ali- evolve na haiingii akilini alitoka Butiama na kuanzisha harakati. Hili linajulikana

Mohamed ana 'counter argument' kwa kosa lile lile la Kivukoni, kwamba, Syskes na Wazee wake ndio walioleta uhuru. Ukimuuliza aeleze sehemu moja tu nje ya Gerezani ambako Abdul alifanya mkutano wa siasa , Mo anaweka picha akinywa chai na maelezo mlolongo yasiyohusiana na mada
Ninachojua mimi ni kuwa wakina Sykes walipigania uhuru wetu kwa kushirikiana kikamilifu na wengine bila kujali dini, kabila au rangi zao. Watu kama nyinyi ndio mnataka ku distort mchango wao kwa kuingiza udini.

Amandla....
Na hili ndilo linaondoa nguvu ya hoja ya akina Sykes. Hawa watu walifanya mambo kwa kushirikiana, kinyume chake tusingewasikia akina Mwl Cecil Matola, Dr Kyaruzi, Rupia n.k. kwasababu hawakuwa katika 'dini'.

Mwisho, Fundi , Mohamed anapokueleza Vyuo, Library n.k. lengo lake ni kujenga ' legitimacy' kwamba anamiliki Historia ya Tanganyika.

Ukimsoma bandiko alilonijibu nilishtuka alipoandika '' ...ndipo nilipoijua historia ya Kweli ya Mapinduzi''. Yaani opion zake anaaminisha watu ndio ukweli

Angalia criteria za utafiti wake.
Hivi utamhoji Waziri wa Jamsheed utegemee atasema mapinduzi yalikuwa mazuri.

Ukiangalia anawahoji kuna 'prejudice' ya kuhoji waathirika wa Mapinduzi
Hutamsikia kama alihoji wana Mapinduzi katika ku balance story

Lile Fete la usiku wa Jan 12 liliandaaliwa na Wamakonde? Ni akina nani hao wanaoitwa wamakonde? Kama utakumbuka Abeid Karume anajulikana kama Mmalawi! sijui hao ndio wamakonde! na kwanini Wamakonde na si Wanajeshi! nini 'special skills gani walizonazo'
 
Angekuwa mzee wa gerezani Mohamed Said angemuandika hadi wake zake.
Inside 10.
Haya maneno nimeandika hapa mwaka wa 2014 kuhusu Chief Erasto Mang'enya:

Raia Fulani,
Umesema kweli kuwa mapambano hayakuwa yamebebwa na wazee
wetu wa Dar es Salaam peke yao.

Ikiwa umefuatilia mnakasha huu utagundua kuwa hiyo siyo hoja kuu
ambayo mimi, FaizaFoxy na wengine tulikuwa tunaisukuma.

Mimi binafsi nilichokuwa nakisema na hapa nitakufahamisha ni kuwa
mbona historia imefuta mchango wa Waislam ambao ndiyo walikuwa
mbele katika kuupigania uhuru wa Tanganyika?

Ndipo nilipoandika kitabu hiki: ''The Life and Times of Abdulwahid
Sykes
(1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against
British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press London 1998.

Nikimfahamu Mzee Man'genya kwa kuwa wanae nimekwendanao shule.

Katika ujana nilikuwa sikai mbali na mwanae mkubwa aliyekuwa jirani
yangu na katika siku za mwisho wa uhai wake Mzee Mange'nya
alikuwa akija pale kwa mwanae nami kila nikimuona kasimama nje ya
nyumba anapunga upepo nilkwenda kumuamkia na kuzungumzanae
machache.

Wakati huu kitabu hiki kilikuwa kimetoka mimi nilikuwa katika watu
wa mwanzo kukisoma na nilimpongeza Mzee Mang'enya kwa kazi
nzuri.

Kitabu hiki kipo katika ''bibliography'' ya kitabu changu hicho hapo
juu.

Raia Fulani,
Miaka mingi sana imepita toka nikisome kitabu cha Mzee Man'genyalakini hebu soma haya niliyoandika katika kitabu changu na katika
kushadihisha nimeweka ''footnote,'' kutoka kitabu hicho.

Nadhani utaona tofauti kubwa iliyokuwapo katika mchango wa
Chief Mang'enya na wengine kama yeye na mchango wa wazee
wangu katika kupigania uhuru wa nchi yetu:

''Associations purported to have been formed to safeguard workers’
interests had existed since early 1930s despite having introduced
the Trade Union Ordinance of 1932; the colonial government was
still very hostile to organised collective action of the working class. [1]
But this did not deter workers from fighting for their rights. None of
the unions or associations that were formed aroused the consciousness
of the working class in Tanzania as the dockworkers did in Dar es
Salaam. There was a very big difference between the Tanganyika
Territory Civil Servants’ Association (TTACA), founded in 1922
by Martin Kayamba, and the Dockworkers’ Union, both in leadership
and in direction. TTACA was a harmless genuine welfare association,
free from any conflict with the colonial administration. It was ‘a club
for clerks and teachers, with newspapers and a football team, encouraged
by the government’. [2] This association and others of similar nature
formed and led by the educated elite did not achieve much.''

[1] See Helge Kjeshus, Labour in Tanzania, (Dar es Salaam, 1977),
passim.
[2] Illife, ‘Tanzania Under British Rule’ in B.A. Ogot and J. Kieran (Eds)
Zamani: A Survey of East African History, East African Publishing House,
1968 p. 22 quoted in African Studies Working Paper No. 8, April, 1979, by
G.W. Reeves.
[3] See E.A. Mang'enya, Discipline and Tears, Dar es Salaam,
1984 p. 231.
Raia Fulani,
Huenda ukawa ufahamu yaliyofanywa na Dar es Salaam Dockworkers Union.
Chama hiki Katibu Mkuu wake kilipoanzishwa 1948 alikuwa Abdul Sykes.
Wakati ule alikuwa na umri wa miaka 24 na ni yale aliyofanya katika chama
hiki ndiyo yaliyompelekea achaguliwe kuwa secretary wa TAA mwaka wa
1950.
 
Mohamed, swali hili si mara ya kwanza kukuuliza. Ukinisoma nyuzi nilizokutaja nilieleza matarajio ya jibu lako, kwamba hutajibu bali utaleta maelezo mengi katika kuvuruga wasomaji.
Kati ya mapungufu yako ya kibinadamu ni kutokuwa ''concise'

Swali ni muhimu pale ambapo Mapinduzi yananasibishwa na Mwl Nyerere. Iwe Mwl alishiriki au la hilo si tatizo, Mwl ameshiriki mambo mengi sana kuanzia Biafra, Palestine, na SADC yote ambayo leo mmoja wa mashahidi wake Askofu D. Tutu ametutoka. Hivyo Mwl kushiriki si tatizi kabisa

Tatizo ni pale anapotuhumiwa kwa dhania tu na hisia za watu. Ikiwa Mwl alifanya ''Uvamizi' kama ulivyodai , mapinduzi yale hayana Uhalali na ni Haramu. Kwa uharamu wake ni haramu kwa Wazanzibar kushiriki kila mwaka Jan 12 kusherehekea Haramu ya Nyerere. Fair enough
Hii ni kwa mujibu wako Mohamed Said

Tuwaulize Wazanzibar , hivi huu 'wendwazimu wa kusherehekea Mapinduzi ya uvamizi wa Nyerere wameupata wapi? Ni lini wataacha uhayawani huo kama anavyobainisha Mwanahistoria Mohamed Said ambaye ameshirikiana na watu kama Harith Ghassany katika kuutafuta ''ukweli'' !

Someni hapa chini enyi Wazanzibar wa ''Mapinduzi Daima'' kisha mtafakari ikiwa mnayoyafanya kila Jan 12 yana maana yoyote.

Umewahi kukutana na viongozi walioongoza Mapinduzi kwa maongezi au video?

Umewahi kuwasikiliza 'Wana Mapinduzi' nao wanasemaje?

Umewahi kuzungumza na Mwanapinduzi yoyote katika serikali ya kwanza ya Mapinduzi?

Ya upande wa kwanza yako wapi?

Historia ya Kweli ya Mapinduzi? Mo , You're entitled to your own opinion...

Mohamed anatoa conclusion ya Ali Muhsin ili asionekane kasema yeye, lakini between the lines hicho ndicho anamaanisha

Mohamed, je, ulizungumza na akina Thabiti Kombo Jecha, Aboud Jumbe, Abdurahman Babu, Abdalla Natepe, Hassan Nassor Moyo, Ali Hassan Mwinyi kwa uchache ili kupata upande wa pili wa maongezi yao? Je, wao wanasemaje kuhusu Mapinduzi?
Nguruvi3,
Una mapenzi makubwa na mimi.
Alhamdulilah.

Unaniuliza suala hilo hilo mara kadhaa na unajua jibu langu lakini huachi kuniuliza na unajua kuwa mimi huwa sina kawaida ya kujibu swali kwa ufupi na wewe hupendi majibu marefu lakini huachi kuniita kwenye mnakasha.

Bila shaka uandishi wangu unakuvutia juu ya upungufu wangu.

Wazanzibari vipi wataacha kusheherekea mapinduzi wakati wamefanya chaguzi sita zote kura za wananchi haziheshimiwi?

Vipi wanataaishwa na sanduku la kura ilhali wao wamepeindua na wanadai wananchi wanawapenda?

Hao wanaochukua madaraka kwa nguvu si ndiyo waliopindua?
Vipi wataacha kuadhimisha mapinduzi?

Tusubiri kwanza siku sanduku la kura litakapoheshimiwa tuone itakuwaje.
Sherehe za mapinduzi zitakuwapo au hazitakuwapo?

Unaniuliza kama nimepata kukutana na viongozi wa mapinduzi.
Niruhusu nilitengeneze swali lako na kutia nyongeza.

Kuna viongozi wa mapinduzi waliokuwa Zanzibar Kamati ya Watu 14 na wako waliokuwa Tanganyika ndani ya serkali na wengine nje ya serikali waliokuwa wanakwenda kuvua samaki Bahari ya Hindi na Myahudi mkubwa wa makachero Kimche wakati wanatayarisha mapinduzi.

Hawa marafiki wa Kimche siwezi kuwataja kwa kuwa ni wazee wangu na bado wako hai.
Ndipo siku zote nisemapo haya mambo kwangu mimi yalikuwa nyumbani kwetu.

Kuna viongozi wa mapinduzi waliokuwa Tanganyika ndani ya serikali mfano wa Oscar Kambona na kuwa viongozi wa mapinduzi waliokuwa Kipumbwi Mkuu wa Mkoa Jumanne Abdallah na Mkuu wa Wilaya Ali Mwinyi Tambwe.

Kisha kuna Mohamed Omari Mkwawa na Victor Mkello.

Kuna viongozi wa mapinduzi tarehe 12 Januari akina Seif Bakari na wengine wakaingia katika mapinduzi tarehe 13 Januari siku ya pili kuyaongoza kuzuia mauaji, vijana wa Umma Party, Badawiy Qulatein na wenzake akina Hashil Seif.

Umeniuliza historia ya mapinduzi ya upande wa kwanza.
Sikuona haja ya kueleza kwani ni historia maarufu kila mtu anaijua.

Hebu ingia hapo chini uone ni viongozi wangapi wa mapinduzi niliopata kuwajua tena kwa karibu sana:

''Mimi sikupatapo kumjua Badawi Qulatein wakati akiwa comrade.

Nilikuja kumjua wakati akiwa mmoja wa wanafunzi wa Sharif Abdulkadir Juneid msikiti wa Kitumbini Dar es Salaam.

Kaipa mgongo siasa na kamuelekea Allah.

Hatukujuana kwa karibu, kujuana kwetu ilikuwa kukutana hapo msikitini katika sala za jamaa tukapeana salaam na huo ndiyo ulikuwa mwisho wetu.

Lakini ikatokea siku moja Ahmed Rajab alikuja kutoka London na akataka mimi na Dr. Dau tumsindikize nyumbani kwa Ahmed Diria Upanga.

Ilikuwa katika pilkapilka hizi za kumpeleka Ahmed Rajab huku na kule ndipo tukakutana na Badawi Qulatein Mtaa wa Mkunguni na Ahmed Rajab akatutambulisha mimi na Dr. Dau kwake kama ndugu zake.

Kuanzia siku ile Badawi Qulatein akawa rafiki yangu na mzungumzaji wangu mkubwa.

Nilikuja kugundua kuwa tulikuwa tumeshahabiana kwa mengi sana.

Hata siku alipofariki Makka katika hija wakati ule ule hata saa moja haijamalizika Ahmed Rajab akaniletea taarifa za kifo chake. Kwangu nilikuwa nimepoteza rafiki na ndugu.

Hayo hapo chini ya kuchoma moto mji aliyoandika Salim Msoma, Badawi Qulatein alinieleza hivyo hivyo.

Nina mengi niliyopokea kutoka kwa Badawi Qulatein In Shaallah fursa ikijitokeza nitayaeleza.
Mohamed Said
 
Unathibitisha tena kuwa wewe ni authority wa historia ya wakina Sykes. Na kuhusu wakina Sykes, nilijua kuhusu mchango wao kabla ya wewe kuandika. Tofauti na wewe unavyotaka kutuaminisha mapambano ya uhuru hayakuwa ya watu wa Gerezani peke yao. Hao wakina Sykes na wengine uliowataja wasingekubalika kwa wanyakyusa bila wakina Mwakangale, Kanda ya ziwa bila wakina Bomani, Kilimanjaro bila wakina Mbowe, mission quarter bila wakina Phombeah na sehemu nyingine ni watu kama wakina Kasanga Tumbi, Rupia wazee wako wasingeona ndani. Bila wakina Robert Makange na gazeti lake kazi ingekuwa ngumu. Mimi sikatai mchango wa wakina Sykes, Mwapachu na wengine. Ninachopinga ni wewe kuwavisha joho la udini wakati wengi wao walikuwa Nationalists kuliko wadini ndio maana waliwakubali watu kama Dr. Kyaruzi, Julius Nyerere, Oscar Kambona na wagalatia wengine tu katika mpambano wa kudai uhuru. Hao wakina Sykes walikuwa wapiga muziki, watu wa Klabu, leo unataka kuwageuza wapigania ukombozi wa waislamu na sio watanzania wote?
Kupiga picha na kuhojiwa na watu kama Issa Shivji hakukufanyi authority wa historia ya Tanganyika, bali authority wa sehemu ya historia ya Tanganyika. Badala ya kutuwekea mapicha ukinywa chai nao weka mahali walipo ku cite kama source ya maandiko yao! Wewe unatoa anecdotal evidence ambazo unajipa authority ambayo sio yako. Kitabu kuwa Library of Congress sio ushahidi kuwa wewe ni authority maana ile ni maktaba na inakusanya maandiko karibu yote yanayofanyika Marekani.

Unasema uliwaona wakina Sykes katika party zao wakati Ally Sykes alikuwa active katika muziki katika miaka ya mwisho ya 1940s ( ulikuwa haujazaliwa). Ally Sykes na Peter Bernard walitoa nyimbo zao 1947, Ally Sykes na bendi yake the Merry Blackbirds nao walitamba katika miziki ya dansi ya early 1950s wakati ulikuwa haujazaliwa maana ulienda middle school 1960s. Wewe tambia nyimbo za wakina Salum Abdallah Yazide, sio za Ally Sykes.
Unasema Dennis Phombeah alikuja baadae lakini unakiri kuwa kadi ya 5 ya chama cha TANU alipewa yeye. Ni yale yale ya kutaka kuwazima wagalatia.

Wewe unaona tu kuwa Nyerere aliwanyima medali ndugu zako waislamu, niambie kama aliwapa medali wakina Kyaruzi, Phombeah, Kirilo n.k. na wagalatia wengi tu waliopigania uhuru wa nchi ya Tanganyika. Unajifanya hauoni yaliyompata Oscar Kambona na wakina Kassanga Tumbo.

Mimi shida yangu na wewe ni pale unapotaka kutuaminisha kuwa ni ndugu zako wa kiislamu peke yao ndio waliopigania uhuru. Unafanya kosa lile lile ambalo wapambe wa Nyerere walitaka kutuaminisha kuwa ni yeye peke yake ndie aliyepambana na mkoloni. Ninachojua mimi ni kuwa wakina Sykes walipigania uhuru wetu kwa kushirikiana kikamilifu na wengine bila kujali dini, kabila au rangi zao. Watu kama nyinyi ndio mnataka ku distort mchango wao kwa kuingiza udini.

Amandla....
Fundi...
Hapa tunaweza tukavutana hadi asubuhi.
Hakuna popote niliposema kuwa harakati za uhuru zilikuwa Gerezani.

Kitabu cha Abdul Sykes kina sura 11 na humu nimeandika harakati zote za TANU Tanganyika.

Wala hakuna udini katika kitabu hicho ila nimewarudisha Waislam ambao walifutwa katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nimeisahihisha historia potofu ya TANU iliyokuwa imetamalaki kwa miaka mingi.
Mimi nimezaliwa tarehe 25 Februari 1952.

Kunambia kuwa sikuwaona hawa baba zangu wakati tunaishi mtaa moja na wazee wakitembeleana ni kichekesho.

Peter Benard sijapata kumjua wala kumsikia nitashukuru kama utanipa historia yake.

Picha hiyo hapo chini kulia ni Kassanga Tumbo akifuatiwa na babu yangu Salum Abdallah rais muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) Tumbo akiwa katibu muasisi.

TRAU iliundwa 1955 na ilipigania uhuru bega kwa bega na TANU.

Hii ndiyo nafasi yangu katika historia ya Tanganyika sisomi kwa mtu historia hii walimu nilikuwanao ndani nyumbani kwetu.

Hii ndiyo tofauti yetu.

1640579698047.png
 
Nguruvi3,
Una mapenzi makubwa na mimi.
Alhamdulilah.

Unaniuliza suala hilo hilo mara kadhaa na unajua jibu langu lakini huachi kuniuliza na unajua kuwa mimi huwa sina kawaida ya kujibu swali kwa ufupi na wewe hupendi majibu marefu lakini huachi kuniita kwenye mnakasha.

Bila shaka uandishi wangu unakuvutia juu ya upungufu wangu.

Wazanzibari vipi wataacha kusheherekea mapinduzi wakati wamefanya chaguzi sita zote kura za wananchi haziheshimiwi?

Vipi wanataaishwa na sanduku la kura ilhali wao wamepeindua na wanadai wananchi wanawapenda?

Hao wanaochukua madaraka kwa nguvu si ndiyo waliopindua?
Vipi wataacha kuadhimisha mapinduzi?

Tusubiri kwanza siku sanduku la kura litakapoheshimiwa tuone itakuwaje.
Sherehe za mapinduzi zitakuwapo au hazitakuwapo?

Unaniuliza kama nimepata kukutana na viongozi wa mapinduzi.
Niruhusu nilitengeneze swali lako na kutia nyongeza.

Kuna viongozi wa mapinduzi waliokuwa Zanzibar Kamati ya Watu 14 na wako waliokuwa Tanganyika ndani ya serkali na wengine nje ya serikali waliokuwa wanakwenda kuvua samaki Bahari ya Hindi na Myahudi mkubwa wa makachero Kimche wakati wanatayarisha mapinduzi.

Hawa marafiki wa Kimche siwezi kuwataja kwa kuwa ni wazee wangu na bado wako hai.
Ndipo siku zote nisemapo haya mambo kwangu mimi yalikuwa nyumbani kwetu.

Kuna viongozi wa mapinduzi waliokuwa Tanganyika ndani ya serikali mfano wa Oscar Kambona na kuwa viongozi wa mapinduzi waliokuwa Kipumbwi Mkuu wa Mkoa Jumanne Abdallah na Mkuu wa Wilaya Ali Mwinyi Tambwe.

Kisha kuna Mohamed Omari Mkwawa na Victor Mkello.

Kuna viongozi wa mapinduzi tarehe 12 Januari akina Seif Bakari na wengine wakaingia katika mapinduzi tarehe 13 Januari siku ya pili kuyaongoza kuzuia mauaji, vijana wa Umma Party, Badawiy Qulatein na wenzake akina Hashil Seif.

Umeniuliza historia ya mapinduzi ya upande wa kwanza.
Sikuona haja ya kueleza kwani ni historia maarufu kila mtu anaijua.

Hebu ingia hapo chini uone ni viongozi wangapi wa mapinduzi niliopata kuwajua tena kwa karibu sana:

''Mimi sikupatapo kumjua Badawi Qulatein wakati akiwa comrade.

Nilikuja kumjua wakati akiwa mmoja wa wanafunzi wa Sharif Abdulkadir Juneid msikiti wa Kitumbini Dar es Salaam.

Kaipa mgongo siasa na kamuelekea Allah.

Hatukujuana kwa karibu, kujuana kwetu ilikuwa kukutana hapo msikitini katika sala za jamaa tukapeana salaam na huo ndiyo ulikuwa mwisho wetu.

Lakini ikatokea siku moja Ahmed Rajab alikuja kutoka London na akataka mimi na Dr. Dau tumsindikize nyumbani kwa Ahmed Diria Upanga.

Ilikuwa katika pilkapilka hizi za kumpeleka Ahmed Rajab huku na kule ndipo tukakutana na Badawi Qulatein Mtaa wa Mkunguni na Ahmed Rajab akatutambulisha mimi na Dr. Dau kwake kama ndugu zake.

Kuanzia siku ile Badawi Qulatein akawa rafiki yangu na mzungumzaji wangu mkubwa.

Nilikuja kugundua kuwa tulikuwa tumeshahabiana kwa mengi sana.

Hata siku alipofariki Makka katika hija wakati ule ule hata saa moja haijamalizika Ahmed Rajab akaniletea taarifa za kifo chake. Kwangu nilikuwa nimepoteza rafiki na ndugu.

Hayo hapo chini ya kuchoma moto mji aliyoandika Salim Msoma, Badawi Qulatein alinieleza hivyo hivyo.

Nina mengi niliyopokea kutoka kwa Badawi Qulatein In Shaallah fursa ikijitokeza nitayaeleza.
Mohamed Said

Mzee wangu Mzee Muhammed haya alituandikia Mzee wangu Fulani na yuko hai

Ushiriki wa Waingereza na jeshi la Watanganyika

Tukiwa siku 3 baada ya mavamizi katika meli ya MV Salama nje kidogo ya gati ya Zanzibar

Asubuhi ya siku ya nne haikua nzuri kwani jamaa (askari) walikwisha anza UCHURU, tena walikua SERIOUS, MELI ISENDE POPOTE ISIPOKUA PEMBA Kuangalia mbalibaharini UNION JACK inapepea kwenye BOATS TATU ambazo zilkua zinakuja tuliko kwa speed kali sana Niliwajulisha jamaa sasa Kumekucha mbona hali ya hewa haiko vizuri?Mbona leo Boats ni tatu?

Sikumaliza kusema Ahmed Guliva ( HUYU GULIVA NI KIJANA WA KIKUMBARO WALE WA SOKO MUHOGO TULIMWITA JINA HILO KWA LILE UMBO LAKE ALIKUA ANATISHA NAE NIMARKSMAN GUU LAKE NI GUU KWELI KAMA GULIVA) Sigara zake ni zile sigara BIRI; wengi munazikumbuka; halafu yeye anatumia sigra kubwa .

Guliva nilimsikia anasukuma Rounds 20 kwenye mtutu aliokua nao na mara kaelekeza vitu vyote kwenye zile BOATS; HAMMADII KUFA KWAJA Kwani nilijua atafanya maajabu, na sisi tunge malizwa wote;

Hapo nilikumbuka yale mafunzo tuliokua tukipata kule Chukwani na MR. CARROLE.

Nilimvamia Guliva bilayeye kutegemea huku mtutu wake , nimesha utupa hukooo; Abdullah Salim ( NDUGUYE HAMAD SALIM -PEMBA)wengi munamjua ,amesha muwekea MK 3,juu yaKichwa.

Nilirudisha Bastola yangu pahala pake . nae akaungama na yakesha hapo hapo. kila mmoja aka TAKEPOSITION.

Kusudio la Guliva ni OPEN FIRE, HAYA NAMBIE TUNGE PONA?

Boats tatu zote zilikua zimejaa ROYA MARINES pamoja na baadhi ya wakuu wa Jeshi Jipya la Wachafuzi na wavamizi.

MA OFISA wa ROYAL MARINES WALITWAMBIA"HIVI SASA MUKO KWENYE ULINZI WA JESHI JIPYA LA MAPINDUZI, NA NYINYI NYOTE MUTAKUA KATIKA JESHI HILO;

SERIKALI YA MAPINDUZI INAFAHAMU KUA MULIKUA MUNAFANYA KAZI YENU NA WAJIBU WEN WAKATI WA SERKALI ILIOPITA HIVI SASA MUNATAKIWA KURUDISHA SIALHA ZENU ZOTTE KWA WAKUU WA SERIKALIYA MAPINDUZI TUMEKUBALIANA NA SERIKALI YA MAPINDIZI HAKUNA MATATIZO YEYOTE WALA HASAMA YEYOTE JUU YENU ;

ZANZIBAR NI NCHI YENU LAZIMA KUSHIRIKANA NA JESHI JIPYA LA MAPINDUZI KWA USALAMA WA NCHI YENU NA USALAMA W ENU.(HUYO ALIKUA MTAWALA---KOSA HILOO0)Kila mmoja wetu alipewa barua ya uthibitisho wa usalama wetu.

Wakati tunahutubiwa kama vile hotuba ya sala ya IJUMAA huko baharini tume shazungukwa na kikosi cha jeshi la TANGANYIKA;

Tulipewa barua za kuhakikisha usalama wetu kwamba sio ruhusa mtu yeyote kutukamata wala kutusimanga , na turudishwe katika kazi zetu na tupewe vyeo vyetu haraka kama iwezekanvyo baada ya kupewa mapumziko ya mwezi mmoja kila mmoja wetu.

Yaliyotokea baadaye ni kinyume kabisa na hayo tuliyoambiwa
 
Mohamed, swali hili si mara ya kwanza kukuuliza. Ukinisoma nyuzi nilizokutaja nilieleza matarajio ya jibu lako, kwamba hutajibu bali utaleta maelezo mengi katika kuvuruga wasomaji.
Kati ya mapungufu yako ya kibinadamu ni kutokuwa ''concise'

Swali ni muhimu pale ambapo Mapinduzi yananasibishwa na Mwl Nyerere. Iwe Mwl alishiriki au la hilo si tatizo, Mwl ameshiriki mambo mengi sana kuanzia Biafra, Palestine, na SADC yote ambayo leo mmoja wa mashahidi wake Askofu D. Tutu ametutoka. Hivyo Mwl kushiriki si tatizi kabisa

Tatizo ni pale anapotuhumiwa kwa dhania tu na hisia za watu. Ikiwa Mwl alifanya ''Uvamizi' kama ulivyodai , mapinduzi yale hayana Uhalali na ni Haramu. Kwa uharamu wake ni haramu kwa Wazanzibar kushiriki kila mwaka Jan 12 kusherehekea Haramu ya Nyerere. Fair enough
Hii ni kwa mujibu wako Mohamed Said

Tuwaulize Wazanzibar , hivi huu 'wendwazimu wa kusherehekea Mapinduzi ya uvamizi wa Nyerere wameupata wapi? Ni lini wataacha uhayawani huo kama anavyobainisha Mwanahistoria Mohamed Said ambaye ameshirikiana na watu kama Harith Ghassany katika kuutafuta ''ukweli'' !

Someni hapa chini enyi Wazanzibar wa ''Mapinduzi Daima'' kisha mtafakari ikiwa mnayoyafanya kila Jan 12 yana maana yoyote.

Umewahi kukutana na viongozi walioongoza Mapinduzi kwa maongezi au video?

Umewahi kuwasikiliza 'Wana Mapinduzi' nao wanasemaje?

Umewahi kuzungumza na Mwanapinduzi yoyote katika serikali ya kwanza ya Mapinduzi?

Ya upande wa kwanza yako wapi?

Historia ya Kweli ya Mapinduzi? Mo , You're entitled to your own opinion...

Mohamed anatoa conclusion ya Ali Muhsin ili asionekane kasema yeye, lakini between the lines hicho ndicho anamaanisha

Mohamed, je, ulizungumza na akina Thabiti Kombo Jecha, Aboud Jumbe, Abdurahman Babu, Abdalla Natepe, Hassan Nassor Moyo, Ali Hassan Mwinyi kwa uchache ili kupata upande wa pili wa maongezi yao? Je, wao wanasemaje kuhusu Mapinduzi?
Wagalatia kuna mahala mnakwama, iweje vikitajwa vichwa kama Askofu Tutu hamshangazwi waislam wakivipa tick ila zinapokuja sifa za Shaykh Hassan bin Ameir mnachachawa eti "ni udini", hivi kweli hamjui kilochomfikisha katika utetezi Askofu Tutu kwamba ni Imani yake ya ukristo?

Hii dhambi ya wivu, choyo, Husda na ubaguzi itakutafuneni hadi mwisho wa pumzi zenu' ukweli huwa haupingiki badala yake hupokewa
 
Endeleeni kuliogopa kanisa hivyo hivyo
Kanisa lililokuja kuvunja misikiti zaidi ya 50 kilwa? Au ni lile kanisa lililochinja wazee wetu walioongozwa na jemedari kinjekitile ngwale? Au unazungumzia kanisa lililomtukuza mmisheni livingstone aliewahadaa wahenga? Au lile lililosema lazima uwepo muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Ajabu kanisa kukataa muungano wa Tanganyika na Congo
 
Chagua wewe mfilisti[emoji16]
 
Fundi...
Hapa tunaweza tukavutana hadi asubuhi.
Hakuna popote niliposema kuwa harakati za uhuru zilikuwa Gerezani.

Kitabu cha Abdul Sykes kina sura 11 na humu nimeandika harakati zote za TANU Tanganyika.

Wala hakuna udini katika kitabu hicho ila nimewarudisha Waislam ambao walifutwa katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nimeisahihisha historia potofu ya TANU iliyokuwa imetamalaki kwa miaka mingi.
Mimi nimezaliwa tarehe 25 Februari 1952.

Kunambia kuwa sikuwaona hawa baba zangu wakati tunaishi mtaa moja na wazee wakitembeleana ni kichekesho.

Peter Benard sijapata kumjua wala kumsikia nitashukuru kama utanipa historia yake.

Picha hiyo hapo chini kulia ni Kassanga Tumbo akifuatiwa na babu yangu Salum Abdallah rais muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) Tumbo akiwa katibu muasisi.

TRAU iliundwa 1955 na ilipigania uhuru bega kwa bega na TANU.

Hii ndiyo nafasi yangu katika historia ya Tanganyika sisomi kwa mtu historia hii walimu nilikuwanao ndani nyumbani kwetu.

Hii ndiyo tofauti yetu.

View attachment 2058990
Mohammed,
Usisogeze goli. Hatujaanza kusoma mabandiko yako leo. Hakuna mtu anapinga wewe kuandika kuhusu ndugu na jamaa zako. Ni haki yako ya msingi. Shida yetu ni pale unapofanya simulizi zao ndio historia nzima ya Tanganyika. Aidha, unaposema kuwa hawakutendewa haki kwa sababu ya uislamu wao ndio unaharibu kabisa. Nyerere hakusita kuwashughulikia watu aliotofautiana nao kwa sababu za kisiasa bila kujali dini zao. Alipotaifisha shule, wagalatia ndio waliopoteza shule zao nyingi kuliko waislamu, hasa wakatoliki. Alipotaifisha nyumba, wakina Rupia nao walipoteza nyumba zao nyingi tu, sio wakina Sykes peke yao. Lakini katika yote hayo alifanya upendeleo kwa watu wake kama wakina Sykes. Ilikuwa ukitaka vaccination certificate unaenda Sykes Travel Agency, sio STS. Wakina Sykes, Munanka na kadhalika walichuma sana kama commission agents. Watoto wa Mwapachu nao hakuwasahau katika ajira. Wakati sisi tunakua wakina hatukuwajua wakina Cecil Matola, Dr. Kyaruzi, Dennis Phombeah na wengine wengi tu. Tuliimba nyimbo za kumtukana Kambona wakati tunakimbia mchakamchaka. Lakini tuliwajua wakina Sykes.
Maandiko na mahubiri yako yanachangia sana kujenga chuki kati ya wagalatia na waislamu, chuki ambayo inaota mizizi kwa kasi. Kwenye hilo nitakupinga kwa kadri ya uwezo wangu.
Sijawahi kusema kuwa hukuwajua wakina Sykes. Ninachokataa ni kusema kuwa wewe ulihudhuria dansi za bendi zao. Kuwa na santuri za Elvis Presley haina maana kuwa wewe ni mtu mzima. Mimi nilicheza twist za Chubby Checker Lakini siwezi kudai kuwa nilikuwa namfahamu!
Nakuomba tu uwe muangalifu katika maandiko na mahubiri yako maana vijana wa siku hizi ni wavivu kujisomea na kufanya utafiti na hivyo ni rahisi sana kupotea njia.

Amandla...
 
Kanisa lililokuja kuvunja misikiti zaidi ya 50 kilwa? Au ni lile kanisa lililochinja wazee wetu walioongozwa na jemedari kinjekitile ngwale? Au unazungumzia kanisa lililomtukuza mmisheni livingstone aliewahadaa wahenga? Au lile lililosema lazima uwepo muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Ajabu kanisa kukataa muungano wa Tanganyika na Congo
Humjui Askofu Desmond Tutu. Tutu alisimama kidete kutetea haki za wapalestina mpaka Israel kumuona sio rafiki wao. Wapalestina ni wakristu? Hakusita kumsema Mandela na Mugabe pale walipokosea. Hao nao ni waislamu. Alipingana na ANC kiasi cha ANC kutaka asihusike kwenye mazishi ya Mandela.
Livingstone alitukuzwa na wakoloni wenzake. Lakini tunachomshukuru ni kuwa alitangaza pia kuhusu ubaya wa biashara ya watumwa iliyokuwa ikifanywa na waarabu. Kwetu sisi wamatumbi, kwenye hilo tunamheshimu. Nyinyi waarabu na/au puppets wao ni lazima hamtampenda kwa sababu aliwaharibia dili yenu ya kuwabebesha babu zetu meno ya tembo na kuwaswaga kama ng'ombe.
Tofauti yangu na wewe ni kuwa mimi sikatai maovu ambayo yalifanywa na kanisa, kuanzia walipokuja wakina Vasco da Gama na hadi inquisition ulaya na marekani. Sikatai uhusika wa kanisa katika biashara ya utumwa Afrika Magharibi na hivi karibuni uhusika wa baadhi ya mapadri katika matendo maovu. Yote hayo nayakemea kwa nguvu zangu zote na wala siwatafutii visingizio.
Ila ujinga wa kusema kuwa Kanisa ndio lililazimisha Muungano haustahili kujibiwa maana utapata mileage ya bure.
Sisi tunawakosoa Nyerere na Magufulu bila kujali kuwa ni wagalatia wenzetu na tuliwskosoa Mwinyi na Kikwete kwa vitendo vyao na sio dini zao. Kwetu tunampima mtu bila kujali imani yake, concept ambayo kwa watu kama wewe ni ngumu mno kuielewa.

Sielewagi kwanini waislamu;
1. Wanajionaga wanyonge
2. Wanajiona wanaonewa
3. Wanapenda kulialia hasa Waislam wa Tanzania.
Huku ni kutojiamini na kujaa ujinga ujinga tu.
 
Sielewagi kwanini waislamu;
1. Wanajionaga wanyonge
2. Wansjiona wanaonewa
3. Wanapenda kulialia hasa Waislam wa Tanzania.
Huku ni kutojiamini na kujaa ujinga ujinga tu.
Hawa kina Muhammad said? Labda humfahamu, moh yeye hujishusha si kwamba ni mnyonge laa, bali humpati kwa ilmu wala mali si yeye wala mkewe wala wanawe
 
Hawa wakristo wengi wa huku kwetu wamekuwa ni Kama ile hadithi ya Yesu ,imekuwa jambo lililofanyika miaka 2000 iliyopita imekuwa wayahudi wote wa Leo wamefanya. Utumwa wa zaidi ya miaka 200 iliyopita imekuwa waarabu wa leo ndio walifanya, wamesahau makanisa Yao Na biblia zao zilivyoshadidia utumwa
Huu ni msiba mkubwa
Na wanasahau hawa CCM wanavyowatesa raia waafrika wenzao hii Leo.
Ndiyo maana Hao wanaosema wamewakomboa, leo wanawakata korodani Kule South Africa
 
Mohammed,
Usisogeze goli. Hatujaanza kusoma mabandiko yako leo. Hakuna mtu anapinga wewe kuandika kuhusu ndugu na jamaa zako. Ni haki yako ya msingi. Shida yetu ni pale unapofanya simulizi zao ndio historia nzima ya Tanganyika. Aidha, unaposema kuwa hawakutendewa haki kwa sababu ya uislamu wao ndio unaharibu kabisa. Nyerere hakusita kuwashughulikia watu aliotofautiana nao kwa sababu za kisiasa bila kujali dini zao. Alipotaifisha shule, wagalatia ndio waliopoteza shule zao nyingi kuliko waislamu, hasa wakatoliki. Alipotaifisha nyumba, wakina Rupia nao walipoteza nyumba zao nyingi tu, sio wakina Sykes peke yao. Lakini katika yote hayo alifanya upendeleo kwa watu wake kama wakina Sykes. Ilikuwa ukitaka vaccination certificate unaenda Sykes Travel Agency, sio STS. Wakina Sykes, Munanka na kadhalika walichuma sana kama commission agents. Watoto wa Mwapachu nao hakuwasahau katika ajira. Wakati sisi tunakua wakina hatukuwajua wakina Cecil Matola, Dr. Kyaruzi, Dennis Phombeah na wengine wengi tu. Tuliimba nyimbo za kumtukana Kambona wakati tunakimbia mchakamchaka. Lakini tuliwajua wakina Sykes.
Maandiko na mahubiri yako yanachangia sana kujenga chuki kati ya wagalatia na waislamu, chuki ambayo inaota mizizi kwa kasi. Kwenye hilo nitakupinga kwa kadri ya uwezo wangu.
Sijawahi kusema kuwa hukuwajua wakina Sykes. Ninachokataa ni kusema kuwa wewe ulihudhuria dansi za bendi zao. Kuwa na santuri za Elvis Presley haina maana kuwa wewe ni mtu mzima. Mimi nilicheza twist za Chubby Checker Lakini siwezi kudai kuwa nilikuwa namfahamu!
Nakuomba tu uwe muangalifu katika maandiko na mahubiri yako maana vijana wa siku hizi ni wavivu kujisomea na kufanya utafiti na hivyo ni rahisi sana kupotea njia.

Amandla...
Fundi...
Kuna baadhi ya uliyoandika nitakaa kimya.

Nataka niandike yale ambayo wasomaji wataweza kufuatilia wakipenda waingie katika ''links,'' au wafanya ''search na kujifunza.

Kitabu ndiyo hicho kipo kishachapwa mara nne.

Kitabu cha historia ya TANU cha Chuo Cha CCM Kivukoni toka kilipotoka 1981 ndiyo mwanzo na mwisho wake.

Nadhani ushaona au kusikiliza vipindi nilivyofanya na FM na TV stations tofauti vingine wakinialika studio na vipindi vingine wakija nyumbani kwangu.

Nimefanya vipindi na Azam TV, Hamza Kassongo, Mohamed Ghassani, Channel Ten, Masudi Kipanya, DW TV Online, Time FM, Clouds Plus wengine hata siwakumbuki.

Kila anaenihoji ataniuliza, ''Ilikuwaje watu hawa wote wakawa hawapo katika historia ya Tanganyika?''

Jibu langu huwaambia, ''CCM ndiyo warithi wa TANU swali hilo bora muwaulize wao.''

Wakati mwingine huongeza nikasema, ''Itapendeza kama pale CCM Ofisi Ndogo Lumumba Avenue wakaweka katika kuta zao picha ya Bi. Chiku bint Said Kisusa, Tatu bint Mzee na Bi. Titi Mohamed wako Uwanja wa Ndege wanamsindikiza Nyerere safari ya kwanza UNO Februari, 1955.''

Unajua nini kinawavutia hawa wote kwangu?

Ni historia kama hizi ninazowaeleza na hizi picha ninazowaonyesha kusadikisha niyasemayo.

Hii ni historia ambayo haikupata kufundishwa popote toka tupate uhuru.
Kama nisingeandika kitabu cha Abdul Sykes TANU ingekuwa na historia gani?

Hivi sasa watu wanasoma na kusikiliza historia mpya ya TANU, Nyerere na uhuru wa Tanganyika.

1640603164654.png

Mzee wangu Mzee Muhammed haya alituandikia Mzee wangu Fulani na yuko hai

Ushiriki wa Waingereza na jeshi la Watanganyika

Tukiwa siku 3 baada ya mavamizi katika meli ya MV Salama nje kidogo ya gati ya Zanzibar

Asubuhi ya siku ya nne haikua nzuri kwani jamaa (askari) walikwisha anza UCHURU, tena walikua SERIOUS, MELI ISENDE POPOTE ISIPOKUA PEMBA Kuangalia mbalibaharini UNION JACK inapepea kwenye BOATS TATU ambazo zilkua zinakuja tuliko kwa speed kali sana Niliwajulisha jamaa sasa Kumekucha mbona hali ya hewa haiko vizuri?Mbona leo Boats ni tatu?

Sikumaliza kusema Ahmed Guliva ( HUYU GULIVA NI KIJANA WA KIKUMBARO WALE WA SOKO MUHOGO TULIMWITA JINA HILO KWA LILE UMBO LAKE ALIKUA ANATISHA NAE NIMARKSMAN GUU LAKE NI GUU KWELI KAMA GULIVA) Sigara zake ni zile sigara BIRI; wengi munazikumbuka; halafu yeye anatumia sigra kubwa .

Guliva nilimsikia anasukuma Rounds 20 kwenye mtutu aliokua nao na mara kaelekeza vitu vyote kwenye zile BOATS; HAMMADII KUFA KWAJA Kwani nilijua atafanya maajabu, na sisi tunge malizwa wote;

Hapo nilikumbuka yale mafunzo tuliokua tukipata kule Chukwani na MR. CARROLE.

Nilimvamia Guliva bilayeye kutegemea huku mtutu wake , nimesha utupa hukooo; Abdullah Salim ( NDUGUYE HAMAD SALIM -PEMBA)wengi munamjua ,amesha muwekea MK 3,juu yaKichwa.

Nilirudisha Bastola yangu pahala pake . nae akaungama na yakesha hapo hapo. kila mmoja aka TAKEPOSITION.

Kusudio la Guliva ni OPEN FIRE, HAYA NAMBIE TUNGE PONA?

Boats tatu zote zilikua zimejaa ROYA MARINES pamoja na baadhi ya wakuu wa Jeshi Jipya la Wachafuzi na wavamizi.

MA OFISA wa ROYAL MARINES WALITWAMBIA"HIVI SASA MUKO KWENYE ULINZI WA JESHI JIPYA LA MAPINDUZI, NA NYINYI NYOTE MUTAKUA KATIKA JESHI HILO;

SERIKALI YA MAPINDUZI INAFAHAMU KUA MULIKUA MUNAFANYA KAZI YENU NA WAJIBU WEN WAKATI WA SERKALI ILIOPITA HIVI SASA MUNATAKIWA KURUDISHA SIALHA ZENU ZOTTE KWA WAKUU WA SERIKALIYA MAPINDUZI TUMEKUBALIANA NA SERIKALI YA MAPINDIZI HAKUNA MATATIZO YEYOTE WALA HASAMA YEYOTE JUU YENU ;

ZANZIBAR NI NCHI YENU LAZIMA KUSHIRIKANA NA JESHI JIPYA LA MAPINDUZI KWA USALAMA WA NCHI YENU NA USALAMA W ENU.(HUYO ALIKUA MTAWALA---KOSA HILOO0)Kila mmoja wetu alipewa barua ya uthibitisho wa usalama wetu.

Wakati tunahutubiwa kama vile hotuba ya sala ya IJUMAA huko baharini tume shazungukwa na kikosi cha jeshi la TANGANYIKA;

Tulipewa barua za kuhakikisha usalama wetu kwamba sio ruhusa mtu yeyote kutukamata wala kutusimanga , na turudishwe katika kazi zetu na tupewe vyeo vyetu haraka kama iwezekanvyo baada ya kupewa mapumziko ya mwezi mmoja kila mmoja wetu.

Yaliyotokea baadaye ni kinyume kabisa na hayo tuliyoambiwa
Kamwe...
Hakika laiti angewashambulia Waingereza huo ndiyo ungekuwa ndiyo mwisho wao.
Wangezamishwa wote.

Ningefurahi kama hiistoria hii ingeendelea tufaidike zaidi.
 
Fundi...
Kuna baadhi ya uliyoandika nitakaa kimya.

Nataka niandike yale ambayo wasomaji wataweza kufuatilia wakipenda waingie katika ''links,'' au wafanya ''search na kujifunza.

Kitabu ndiyo hicho kipo kishachapwa mara nne.

Kitabu cha historia ya TANU cha Chuo Cha CCM Kivukoni toka kilipotoka 1981 ndiyo mwanzo na mwisho wake.

Nadhani ushaona au kusikiliza vipindi nilivyofanya na FM na TV stations tofauti vingine wakinialika studio na vipindi vingine wakija nyumbani kwangu.

Nimefanya vipindi na Azam TV, Hamza Kassongo, Mohamed Ghassani, Channel Ten, Masudi Kipanya, DW TV Online, Time FM, Clouds Plus wengine hata siwakumbuki.

Kila anaenihoji ataniuliza, ''Ilikuwaje watu hawa wote wakawa hawapo katika historia ya Tanganyika?''

Jibu langu huwaambia, ''CCM ndiyo warithi wa TANU swali hilo bora muwaulize wao.''

Wakati mwingine huongeza nikasema, ''Itapendeza kama pale CCM Ofisi Ndogo Lumumba Avenue wakaweka katika kuta zao picha ya Bi. Chiku bint Said Kisusa, Tatu bint Mzee na Bi. Titi Mohamed wako Uwanja wa Ndege wanamsindikiza Nyerere safari ya kwanza UNO Februari, 1955.''

Unajua nini kinawavutia hawa wote kwangu?

Ni historia kama hizi ninazowaeleza na hizi picha ninazowaonyesha kusadikisha niyasemayo.

Hii ni historia ambayo haikupata kufundishwa popote toka tupate uhuru.
Kama nisingeandika kitabu cha Abdul Sykes TANU ingekuwa na historia gani?

Hivi sasa watu wanasoma na kusikiliza historia mpya ya TANU, Nyerere na uhuru wa Tanganyika.

View attachment 2059412

Hamna anaepinga kuwa kuna wengi waliochangia historia ya TANU lakini hawatajwi katika historia. Shida yangu na wewe ni pale unapojenga conspiracy theory kwenye kutengwa huko. Kwa mfano, kwenye picha hiyo kuna wanawake watano, wanne wamevaa baibui na mmoja hajavaa lakini wewe umewaona waliovaa baibui peke yake. Na kuweko picha yao pamoja na Nyerere hakuna maana kuwa wao walikuwa wanawake pekee waliomsindikiza Nyerere airport. Hauwezi kutumia picha kama hii kujenga hoja kuwa ni wanawake wakiislamu peke yao ndio waliomuunga mkono Nyerere. Na kutokuwepo picha hii Lumumba hakumaanishi kuwa ni ushahidi wa nia mbaya dhidi yao. Nyerere alipiga picha nyingi na watu tofauti na itakuwa vigumu kuwatendea wote haki sawa. Unapofanya kuwa absence ya picha kama hizi ni ushahidi wa hujma za Nyerere na TANU dhidi ya uislamu ni distortion ya makusudi ya historia.

Amandla...
 
Back
Top Bottom