1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Ulitaka atajwe Saint Kama mlivyopendekeza?

Zawadi yako ya mwaka mpya hii

Mkizidiwa hoja ndio huwa mnakimbilia kupost clips ambazo hazina uhusiano wowote na mada.

Sina muda wa kuingia huko unapotaka na kuharibu mada.

Msaidie Mzee wako hapa kuweka picha ya Baba take akiwa TRAU.

Hilo tu ewe Bint Mwamedi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Wewe post video na pictures hata 100TB najua ni kuishiwa hoja

Msaidie Mzee wako au wote wazushi? [emoji23]
 
Makala...
Historia ina kawaida ya kujirudia.

Baada ya Kura Tatu na TANU kuingia LEGCO pakawa na mabadiliko makubwa sana katika siasa za TANU.

Huu mwaka wa 1958 baada ya Kura Tatu ndipo Sheikh Suleiman Takadir alipogombana na Nyerere.

Kisa kizito sana.

Wakati wa utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes hakuna aliyependa tumzungumze Sheikh Suleiman Takadir.

Ilikuwa Sheikh Haidar Mwinyimvu yeye alikubali na akanipa kisa chote.
Kipo kwa ukamilifu wake katika kitabu cha Abdul Sykes.

TANU ilipoanza ilikuwa inaanza mikutano yake kwa dua iwe New Street ofisini au Mnazi Mmoja.

Taratibu miaka ilipokuwa inasonga mbele mambo yakabadilika ikawa mikutano inaanza na kauli mbiu, ''Uhuru na Kazi.''

Uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961 pakawa na maneno kuwa Abdul Sykes hakuwa na chama cha siasa na TAA kilikuwa chama cha starehe.

Hii ilikuwa kebehi na kejeli.
Ndiyo hizi zinajirudia hapa.

Leo tunasikia kebehi akikebehiwa Abdul Sykes yuko kaburini.
Wanauliza wapi alihutubia mkutano.

Hawajui kuwa ziko shajara (diary) za Abdul Sykes zina hotuba za Nyerere za mwanzo Mnazi Mmoja.

Abdul Sykes akiyasikia haya maneno kuwa TAA kilikuwa chama cha starehe lakini alibakia kimya hakusema kitu.

Daisy Sykes katika kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha baba yake aliandika makala iliyochapwa na Raia Mwema.

Kaeleza haya na msimamo wa baba yake ya kustahamili na kuwa kimya.
Haya maneno yakiwachoma sana rafiki zake.

Yakiwachoma kwa sababu walikuwa wanajua nini Abdul kafanya.

Ahmed Rashad Ali akamwambia Abdul Sykes kuwa ikiwa yeye atafungua kinywa chake kueleza historia ya TANU hakuna atakaethubutu kumkabili kupingananae.

Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Idd Tulio lkavunjwa mwaka wa 1963 na ikawa sasa zile kanzu zilizozoeleka kuonekana ofisi ya TANU Lumumba zikawa zimetoweka.

Na zimetoweka hadi leo.

Abdul Sykes alikataa kusema chochote akawa kimya hadi umauti ulipomfika mwaka wa 1968.

Nimeweka hapa kisa cha ile fadhaa iliyotokea nyumbani kwa Abdul Sykes pale ilipohofiwa kuwa Nyerere kalishwa sumu anataka kuuliwa.

Nimekiweka kisa hiki baada ya kusoma kuwa mikutano ya TANU haikuwa ikifanyika nyumbani kwake wanasema mikutano inawezekana ikifanyika kwa Amir Jamal.

Pamekuwa na ukimya.
Kejeli, kebehi na matusi hayajibiwi bali yananyamaziwa.

Huu ndiyo uungwana tuliofunzwa na walimu wetu.

Sasa hata Abdul Sykes alipofutwa katika historia ya TANU kwa mtu kama Ahmed Rashad Ali haikuwa ajabu, ''He had seen it coming.''

Hizi kebehi ni kwa kuwa wameghadhibika kuwa wao walishamfuta Abdul Sykes na wenzake wote aliokuwanao mimi nimemrudisha.

Kitabu cha maisha yake kipo na sasa yale aliyofanya yanafahamika na nchi imemtunuku Medali ya Mwenge wa Uhuru.

Ngoja nihitimishe kwa kipande hiki.

Siku moja asubuhi nimepokea simu kutoka kwa Bi. Zainab katibu wa Ally Sykes, ''Mohamed mzee anataka kuzungumza na wewe.''

Siku zile Bwana Ally mgonjwa lakini mkaidi lazima aje ofisini.

Baada ya salamu akaniambia, ''Mohamed mimi na Bwana Abdul In Shaa Allah tutapewa nishani Ikulu kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.''

Watu wa Ikulu wamefika hapa ofisini wamenipa taarifa na wameniuliza, ''Kwani Bwana Ally wewe na kaka yako mmefanya nini kustahili hii heshima?''

Sote tukawa tunacheka katika simu.

Bwana Ally alihitimisha mazungumzo yetu kwa kuniambia kuwa aliwapa kitabu cha Abdul Sykes akawaambia, ''Someni hiki kitabu yote yameelezwa humo.''

View attachment 2064641

Ally Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwa Nyerere Magomeni 1958
Jibu maswali ya msingi Mzee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa hivyo kuondoka kwa Seaton nchini kama usemavyo kuna athari gani ya ushauri wake kupokelewa? Huu ubabaishaji wako unashangaza kwakweli hata marehemu ushauri wake unachukuliwa ikiwa ni mzuri sembuse mtu ambae yuko hai? , hiyo nafasi ya mjadala kwa television ni muhari kwako si yeye, yeye kaisha andika Kitabu miaka ishirini na zaidi na sasa yuko awamu ya tano

Je ni kweli una hakika hajatajwa popote mzee popo? Au wajaribu kuidhihirisha hasadi yako na choyo?
Makala...
Abdul Sykes hakutajwa popote hadi nilipoandika kitabu cha maisha yake na leo wako wanaomkejeli.

Hii ndiyo dunia.
Yako mengi ya kujifunza.

Babu yangu Salum Abdallah,

Ilikuwa mwaka wa 1965 babu yangu Salum Abdallah katoka jela ya Iyui Tabora alikowekwa kizuzini mwaka wa 1964 baada ya maasi ya Tanganyika Rifles tarehe 20 Januari 1964 hana kazi yuko nyumbani.

Zilipofika taarifa kuwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameanza kukamatwa Kassanga Tumbo alikimbilia Kenya.

Babu yangu na yeye akaenda ''underground.''
Babu alikuwa mtu wa mitala.

Alikwenda kujificha kwa mmoja wa wake zake katika moja ya mashamba yake mbali.
Hiki ni kisa kingine In Shaa Allah ikitokea fursa nitakieleza.

Mwaka wa 1953 akiwa na taarifa kutoka Dar es Salaam kuwa kuna harakati za kuunda chama cha siasa New Street yeye na wenzake Tabora wakawa wanafanya mikutano ya siri kila Jumapili Town School ambako Abubakar Mwilima alikuwa mwalimu na yeye Mwalimu Abuu kama walivyopenda kumwita ndiye aliyekuwa akiwafungulia darasa moja kukutana na kupeana habari kutoka New Street Dar es Salaam, Makao Makuu ya TAA.

Hii ilikuwa baada ya kumtuma Katibu wa TAA Western Province, Germano Pacha kwenda Makao Makuu ya TAA kuwapa taarifa kuwa Tabora inataka kuunda chama cha siasa.

Germano Pacha alipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes na akamwambia arudishe salamu Tabora kuwa wafanye subira.

Tufupishe kisa kwani kuna mengi.
TANU ikaundwa mwaka wa 1954 babu yangu akiwa mmoja wa wanachama wa mwanzo.

Babu yangu Salum Abdallah ana historia ya uzalendo ya kusisimua ambayo hutochoka kuisikiliza kila inapohadithiwa kwa kuwa mkasa una kuwa ndani ya mkasa mwingine visa vikiunganishwa kama ushanga katika uzi.

Mwaka wa 1965 baba akanifungia safari niende Tabora kumwangalia babu baada ya kutoka kifungoni.

Babu yangu jina lake alililopewa na baba yake Abdallah Mwekapopo (naweza kwenda vizazi saba hadi kwa waliokuwa Belgian Congo) ni Rashid lakini katika ujana wake akiwa mfanyakazi wa Tanganyika Railways katika miaka ya 1930 alimpiga Mzungu akafungwa na alipotoka jela akabadili jina lake akawa Salum Abdallah.

Kisa gani akampiga Mzungu?

Huyu Mzungu alikuwa mbaguzi, mnyanyasaji Waafrika kwa hiyo babu siku moja akaamua kumshughulikia.

Hili lilikuwa kosa kubwa sana wakati wa ukoloni.

Hukaa nikafikiri yule Mzungu alikuwa katika hali gani baada ya kuingia katika mikono ya babu kwani alikuwa kapanda juu futi sita ana kifua kipana ile mitambo ya Kimanyema.

Kwa ajili ya umbo hili akiwa kijana Waingereza walimfunza kazi ya kufua chuma, yaani ‘’foundry,’’ kazi ngumu katika moto na joto kali.

Hii ‘’foundry ’’ ilikuwa ndani ya karakana ya Tanganyika Railways.

Humo ndani ya karakana wanaume wako vifua wazi na nyundo nzito ni kelele za chuma kikigonga chuma cheche za moto zikiruka na miaka ile hakuna vifaa mfanyakazi atavaa kuzuia kelele.

Hii karakana ndiyo ilikuwa ikachonga spea za treni.
Wenyewe kwa wenyewe ndani ya karakana wakizungumza kwa sauti za juu.

Labda ndiyo sababu babu hata akizungumza hata katika mazungumzo ya kawaida sauti yake siku zote ilikuwa juu.

Hii karakana ilikuwa ndani ya eneo la Tanganyika Railway lakini jirani na Arab Street hivi sasa Mtaa wa Nkrumah na ndiko lilipokuwa lango kuu la wafanyazi wa Tanganyika Railways wakiingilia na kutokea katika miaka ile ya 1930.

Babu akiishi Mtaa wa Kipata.

Nyumba aliyokuwa akiishi ilikuwa inatazamana na nyumba ya Kleist Sykes ambae yeye alikuwa Accounts Clerk (Karani wa Mahesabu) Tanganyika Railways.

Nafasi kubwa sana wakati ule kwani hio kazi wakifanya Wahindi.

Lakini babu yangu juu ya ubabe wake na haya yote alikuwa mtu karimu sana mimi nimeshuhudia kwa macho yangu na labda huu ukarimu alimrithisha baba yangu kwani mara nyingi nikipisha wageni chumbani kwangu nami kwenda kulala ‘’sitting room,’’hadi waondoke.

Hii karakana ya Railway ikahamishwa Dar es Salaam mwaka wa 1947 kupelekwa Tabora na babu yangu akahamanayo kwenda huko.

Hakurudi tena Dar es Salaam.

Lakini mwaka huo huo alipofika Tabora akaongoza mgomo wa Railway ulioenea nchi nzima na akafanya hivyo mwaka wa 1947, 1949 na tena mwaka wa 1960 miezi michache kabla ya Tanganyika kupata madaraka.

Baada ya mgomo huu wa mwaka wa 1960 Nyerere ilimhidhihirikia kuwa mtu huyu atakuja kumpa shida katika Tanganyika huru akawa sasa anamtazama kwa macho mawili.

Kuna historia ya kusisimua hapo lakini na tuyaache hayo.

Nimetanguliza huu mkadama mrefu ili msomaji upate picha ya babu yangu uweze kuelewa haya ninayokusudia In Shaa Allah kukueleza.

Ramadhani ya mwaka wa 1965 nikiwa na umri wa miaka 13 ikanikuta Tabora nilipokwenda kumtembelea babu alipotoka jela.

Maghrib ikikaribia uwanja mbele ya nyumba yetu unafagiliwa na majamvi yanatandikwa adhana ikipigwa futari zinaanza kutolewa na kufunikwa na makawa makubwa.

Baada ya kushuka msikitini watu wanakaa kufuturu.
Watu wengi walikuwa wanakuja kufuturu pale nyumbani.

Sikumbuki katika miaka ile kuona watu wakila chapati, sambusa, na mapochopocho mengine kama futari katika miaka ile.

Siku zile futari ni mihogo, maharage, kunde, ndizi mzuzu na uji wa pilipili manga, chai ilikuwa si sana labda kama sikui ile kunakuja wageni kufuturu.

Tabora ndiko nilikojifunza kula mihogo iliyoungwa kwa karanga badala ya nazi vyakula vyote hivi vilikuwa vinatoka shambani kwetu.

Wala hapakuwa na unywaji wa juisi.
Hivi vitu vimekuja miaka hii ya hivi karibuni.

Sielewi kwa nini ilikuwa vile ni hali za watu au ndivyo ilivyotakiwa iwe?
Sasa nakuja kwa babu.

Baada ya sala ya tarweh watu hukaa wakazungumza kuvuta muda wa daku na pale nyumbani kwa babu ndipo ilikuwa barza kubwa ya mtaa watu wakikutana hapo.

Niliaaambiwa miaka ile ya kupigania uhuru miaka ya 1950 hapo ndipo taarifa zote za Nyerere zilipokuwa zikipatikana na watu kutiana moyo kuwa Muingereza siku zake zinahesabika uhuru unanukia.

Baada ya uhuru ghafla ndiyo balaa likamkumba babu yangu kwa kukamatwa na kuwekwa kuzuizini kwa tuhuma kuwa alikuwa katika njama za kupindua serikali ya Nyerere babu na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi akihusishwa na maasi yale.

Barza ile ya babu ilipooza alipokuwa kifungoni kwani marafiki zake wengi walikata mguu kufika pale na hata alipotoka ile ingia toka kama ya zamani haikuwapo.

Hakuna aliyetaka kunasibishwa na mtu haini.

Lakini juu ya haya kuna watu hawakumtupa mkono babu walikuja kila siku ya mwezi wa Ramadhani kumuimbia nyimbo ambayo ilikuwa haimbiwi yeyote mji mzima isipokuwa yeye babu yangu.

Nyimbo hii ilikuwa inaitwa ‘’Ndege Mwema.’’
Mashairi yake yalikuwa yakimsifia babu kwa ubinadamu na ukarimu wake.

Tabora kigoma cha daku ni tofauti na vigoma vya daku kwengineko ambako yanapigwa matari peke yake.

Tabora kigoma cha daku kina ngoma nyingi na goma kubwa na kigoma cha daku kinapigwa kwa staili ya mchanganyika wa ngoma za Kimanyema na Waswezi na nyimbo zake zina ‘’melody,’’ za kuvutia.

Kigoma cha daku wakishamuona huko wanakotoka babu kakaa nje sasa watakuwa wanakuja nyumba baada ya nyumba wanasimama na kupiga kwa dakika moja mbili wanazima wanaendelea hadi wanakaribia nyumba yetu.

Kabla ya kufika mapigo yanabadilika na lile goma kubwa utalisikia sasa likirindima na sauti za waimbaji utazisikia zikiimba kwa masikitiko.

Wanafika mbele ya babu hapo ndipo utazisikia ala zinazungumza.
Babu kakaa kajiinamia kama vile ngoma zile zinampeleka mbali sana.

Baada ya muda atanyanyuka atawafata huku anafungua pochi yake kuwatunza.

Watazima muziki kisha watapiga mwimbo mwingine kwa mdundo wa kuondoka na kwa mdundo huo watamuaga babu.

Babu hapo na yeye ataondoka kuingia ndani.
Maisha yake yote babu yangu aliishi na tuhuma ya kutaka kupindua serikali.

Alipofariki dunia mwaka wa 1974 TANU ilifika katika mazishi yake na walisoma risala nzuri sana ya kumsifia kwa mchango wake wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika akiwa mwanachama wa TANU na akiwa kiongozi wa TRAU wakamsifia kwa ukarimu wakasema kuwa mkono wake siku zote ulikuwa wazi akitoa kwa ajili ya nchi yake.

Huyu ndiye babu yangu na kigoma cha daku na mwimbo wake, ‘’Ndege Mwema.’’

Makala...
Itapendeza na wenzetu kama watatuwekea historia za babu zao wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika na kama hawakuwa wapigania uhuru watueleze jinsi walivyoishi na jamii yao.

1641011186697.png

Salum Abdallah
 
Mkizidiwa hoja ndio huwa mnakimbilia kupost clips ambazo hazina uhusiano wowote na mada.

Sina muda wa kuingia huko unapotaka na kuharibu mada.

Msaidie Mzee wako hapa kuweka picha ya Baba take akiwa TRAU.

Hilo tu ewe Bint Mwamedi.

Ulisema Nyerere hakuandikwa kwenye kitabu chochote cha dini ya Catholic. ,Nilikuwekea ushahidi , dawa umeipata . Dawa imekupatia Side effects. Ndiyo hicho ulichokiandika
 
Makala...
Abdul Sykes hakutajwa popote hadi nilipoandika kitabu cha maisha yake na leo wako wanaomkejeli.

Hii ndiyo dunia.
Yako mengi ya kujifunza.

Babu yangu Salum Abdallah,

Ilikuwa mwaka wa 1965 babu yangu Salum Abdallah katoka jela ya Iyui Tabora alikowekwa kizuzini mwaka wa 1964 baada ya maasi ya Tanganyika Rifles tarehe 20 Januari 1964 hana kazi yuko nyumbani.

Zilipofika taarifa kuwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameanza kukamatwa Kassanga Tumbo alikimbilia Kenya.

Babu yangu na yeye akaenda ''underground.''
Babu alikuwa mtu wa mitala.

Alikwenda kujificha kwa mmoja wa wake zake katika moja ya mashamba yake mbali.
Hiki ni kisa kingine In Shaa Allah ikitokea fursa nitakieleza.

Mwaka wa 1953 akiwa na taarifa kutoka Dar es Salaam kuwa kuna harakati za kuunda chama cha siasa New Street yeye na wenzake Tabora wakawa wanafanya mikutano ya siri kila Jumapili Town School ambako Abubakar Mwilima alikuwa mwalimu na yeye Mwalimu Abuu kama walivyopenda kumwita ndiye aliyekuwa akiwafungulia darasa moja kukutana na kupeana habari kutoka New Street Dar es Salaam, Makao Makuu ya TAA.

Hii ilikuwa baada ya kumtuma Katibu wa TAA Western Province, Germano Pacha kwenda Makao Makuu ya TAA kuwapa taarifa kuwa Tabora inataka kuunda chama cha siasa.

Germano Pacha alipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes na akamwambia arudishe salamu Tabora kuwa wafanye subira.

Tufupishe kisa kwani kuna mengi.
TANU ikaundwa mwaka wa 1954 babu yangu akiwa mmoja wa wanachama wa mwanzo.

Babu yangu Salum Abdallah ana historia ya uzalendo ya kusisimua ambayo hutochoka kuisikiliza kila inapohadithiwa kwa kuwa mkasa una kuwa ndani ya mkasa mwingine visa vikiunganishwa kama ushanga katika uzi.

Mwaka wa 1965 baba akanifungia safari niende Tabora kumwangalia babu baada ya kutoka kifungoni.

Babu yangu jina lake alililopewa na baba yake Abdallah Mwekapopo (naweza kwenda vizazi saba hadi kwa waliokuwa Belgian Congo) ni Rashid lakini katika ujana wake akiwa mfanyakazi wa Tanganyika Railways katika miaka ya 1930 alimpiga Mzungu akafungwa na alipotoka jela akabadili jina lake akawa Salum Abdallah.

Kisa gani akampiga Mzungu?

Huyu Mzungu alikuwa mbaguzi, mnyanyasaji Waafrika kwa hiyo babu siku moja akaamua kumshughulikia.

Hili lilikuwa kosa kubwa sana wakati wa ukoloni.

Hukaa nikafikiri yule Mzungu alikuwa katika hali gani baada ya kuingia katika mikono ya babu kwani alikuwa kapanda juu futi sita ana kifua kipana ile mitambo ya Kimanyema.

Kwa ajili ya umbo hili akiwa kijana Waingereza walimfunza kazi ya kufua chuma, yaani ‘’foundry,’’ kazi ngumu katika moto na joto kali.

Hii ‘’foundry ’’ ilikuwa ndani ya karakana ya Tanganyika Railways.

Humo ndani ya karakana wanaume wako vifua wazi na nyundo nzito ni kelele za chuma kikigonga chuma cheche za moto zikiruka na miaka ile hakuna vifaa mfanyakazi atavaa kuzuia kelele.

Hii karakana ndiyo ilikuwa ikachonga spea za treni.
Wenyewe kwa wenyewe ndani ya karakana wakizungumza kwa sauti za juu.

Labda ndiyo sababu babu hata akizunngumza hata katika mazungumzo ya kawaida sauti yake siku zote ilikuwa juu.

Hii karakana ilikuwa ndani ya eneo la Tanganyika Railway lakini jirani na Arab Street hivi sasa Mtaa wa Nkrumah na ndiko lilipokuwa lango kuu la wafanyazi wa Tanganyika Railways wakiingilia na kutokea katika miaka ile ya 1930.

Babu akiishi Mtaa wa Kipata.

Nyumba aliyokuwa akiishi ilikuwa inatazamana na nyumba ya Kleist Sykes ambae yeye alikuwa Accounts Clerk (Karani wa Mahesabu) Tanganyika Railways.

Nafasi kubwa sana wakati ule kwani hio kazi wakifanya Wahindi.

Lakini babu yangu juu ya ubabe wake na haya yote alikuwa mtu karimu sana mimi nimeshuhudia kwa macho yangu na labda huu ukarimu alimrithisha baba yangu kwani mara nyingi nikipisha wageni chumbani kwangu nami kwenda kulala ‘’sitting room,’’hadi waondoke.

Hii karakana ya Railway ikahamishwa Dar es Salaam mwaka wa 1947 kupelekwa Tabora na babu yangu akahamanayo kwenda huko.

Hakurudi tena Dar es Salaam.

Lakini mwaka huo huo alipofika Tabora akaongoza mgomo wa Railway ulioenea nchi nzima na akafanya hivyo mwaka wa 1947, 1949 na tena mwaka wa 1960 miezi michache kabla ya Tanganyika kupata madaraka.

Baada ya mgomo huu wa mwaka wa 1960 Nyerere ilimhidhihirikia kuwa mtu huyu atakuja kumpa shida katika Tanganyika huru akawa sasa anamtazama kwa macho mawili.

Kuna historia ya kusisimua hapo lakini na tuyaache hayo.

Nimetanguliza huu mkadama mrefu ili msomaji upate picha ya babu yangu uweze kuelewa haya ninayokusudia In Shaa Allah kukueleza.

Ramadhani ya mwaka wa 1965 nikiwa na umri wa miaka 13 ikanikuta Tabora nilipokwenda kumtembelea babu alipotoka jela.

Maghrib ikikaribia uwanja mbele ya nyumba yetu unafagiliwa na majamvi yanatandikwa adhana ikipigwa futari zinaanza kutolewa na kufunikwa na makawa makubwa.

Baada ya kushuka msikitini watu wanakaa kufuturu.
Watu wengi walikuwa wanakuja kufuturu pale nyumbani.

Sikumbuki katika miaka ile kuona watu wakila chapati, sambusa, na mapochopocho mengine kama futari katika miaka ile.

Siku zile futari ni mihogo, maharage, kunde, ndizi mzuzu na uji wa pilipili manga, chai ilikuwa si sana labda kama sikui ile kunakuja wageni kufuturu.

Tabora ndiko nilikojifunza kula mihogo iliyoungwa kwa karanga badala ya nazi vyakula vyote hivi vilikuwa vinatoka shambani kwetu.

Wala hapakuwa na unywaji wa juisi.
Hivi vitu vimekuja miaka hii ya hivi karibuni.

Sielewi kwa nini ilikuwa vile ni hali za watu au ndivyo ilivyotakiwa iwe?
Sasa nakuja kwa babu.

Baada ya sala ya tarweh watu hukaa wakazungumza kuvuta muda wa daku na pale nyumbani kwa babu ndipo ilikuwa barza kubwa ya mtaa watu wakikutana hapo.

Niliaaambiwa miaka ile ya kupigania uhuru miaka ya 1950 hapo ndipo taarifa zote za Nyerere zilipokuwa zikipatikana na watu kutiana moyo kuwa Muingereza siku zake zinahesabika uhuru unanukia.

Baada ya uhuru ghafla ndiyo balaa likamkumba babu yangu kwa kukamatwa na kuwekwa kuzuizini kwa tuhuma kuwa alikuwa katika njama za kupindua serikali ya Nyerere babu na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi akihusishwa na maasi yale.

Barza ile ya babu ilipooza alipokuwa kifungoni kwani marafiki zake wengi walikata mguu kufika pale na hata alipotoka ile ingia toka kama ya zamani haikuwapo.

Hakuna aliyetaka kunasibishwa na mtu haini.

Lakini juu ya haya kuna watu hawakumtupa mkono babu walikuja kila siku ya mwezi wa Ramadhani kumuimbia nyimbo ambayo ilikuwa haimbiwi yeyote mji mzima isipokuwa yeye babu yangu.

Nyimbo hii ilikuwa inaitwa ‘’Ndege Mwema.’’
Mashairi yake yalikuwa yakimsifia babu kwa ubinadamu na ukarimu wake.

Tabora kigoma cha daku ni tofauti na vigoma vya daku kwengineko ambako yanapigwa matari peke yake.

Tabora kigoma cha daku kina ngoma nyingi na goma kubwa na kigoma cha daku kinapigwa kwa staili ya mchanganyika wa ngoma za Kimanyema na Waswezi na nyimbo zake zina ‘’melody,’’ za kuvutia.

Kigoma cha daku wakishamuona huko wanakotoka babu kakaa nje sasa watakuwa wanakuja nyumba baada ya nyumba wanasimama na kupiga kwa dakika moja mbili wanazima wanaendelea hadi wanakaribia nyumba yetu.

Kabla ya kufika mapigo yanabadilika na lile goma kubwa utalisikia sasa likirindima na sauti za waimbaji utazisikia zikiimba kwa masikitiko.

Wanafika mbele ya babu hapo ndipo utazisikia ala zinazungumza.
Babu kakaa kajiinamia kama vile ngoma zile zinampeleka mbali sana.

Baada ya muda atanyanyuka atawafata huku anafungua pochi yake kuwatunza.

Watazima muziki kisha watapiga mwimbo mwingine kwa mdundo wa kuondoka na kwa mdundo huo watamuaga babu.

Babu hapo na yeye ataondoka kuingia ndani.
Maisha yake yote babu yangu aliishi na tuhuma ya kutaka kupindua serikali.

Alipofariki dunia mwaka wa 1974 TANU ilifika katika mazishi yake na walisoma risala nzuri sana ya kumsifia kwa mchango wake wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika akiwa mwanachama wa TANU na akiwa kiongozi wa TRAU wakamsifia kwa ukarimu wakasema kuwa mkono wake siku zote ulikuwa wazi akitoa kwa ajili ya nchi yake.

Huyu ndiye babu yangu na kigoma cha daku na mwimbo wake, ‘’Ndege Mwema.’’

Makala...
Itapendeza na wenzetu kama watatuwekea historia za babu zao wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika na kama hawakuwa wapigania uhuru watueleze jinsi walivyoishi na jamii yao.

View attachment 2064669
Salum Abdallah
Mohamed Mwenyezi kakukirimu, unafunza, unastarehesha, unaelimisha bali unaadabisha, hii stori ya babu yako inasisimua sana, hapa kwetu si ajabu kuwakuta watu waonao ajabu ya wewe kueleza historia ya watu wako, kwingine duniani ni jambo la kawaida

Umewanasihi vyema kwamba nao waandike historia za jamaa zao ambao huenda walishiriki katika harakati za uhuru huenda ikawaponguzia choyo nafsini mwao, kuna mmoja alishangaa ulipoeleza vikao kufanyika majumbani kipindi hicho eti akistaajabu kana kwamba ni udhariri, hali ya kuwa Leo ukitazama au ukisoma habari za wacomonisti kina Mao wa China utakuta vikao vingi ndani ya majumba yao na wao wakiwa na zile alama za kuwasiliana "codes" mfano morse kupitia magazeti, matangazo n. K

Kaka Mohamed Said natumai hutatuangusha wasomaji wako, hebu kamilisha tawasifu yako ambayo naimani itasheheni mengi, kadhalika hata haya yapatikanayo kutoka kwa wanafunzi wako(ambao wengi wamejivika koti la ukosoaji) yaeleza japo hutamaliza kiu yao
 
Bila Google Mohammed Said angetudanganya sana. Na kwa vile Google iko wazi kwa kila mtu basi na wewe itumie ili uthibitishe kuwa hatumtendei haki.

Amandla....

Bwana Mdogo Fundi Mchundo

Cc Nguruvi3
Unahitaji Google ikufasirie maana ya ukoloni? Ili ujue kama kweli Muingereza alikuwa Mkoloni au laa?
 
Kuna uzi mwembamba sana kati ya kuwa koloni na kuwa chini ya udhamini wa UNO.

Ukitazama hali ya jinsi Waingereza walivyokuwa wakitawala Kenya na Tanganyika hakuna tofauti yeyote.

Kama Waingereza walivyopora ardhi wa ya Wakikuyu Kenya ndivyo walivyopora ardhi ya Wameru Tangayika.

Katika kitabu cha Abdul Sykes nimejadili hali hii:

Tanganyika Kama Nchi Chini ya Udhamini wa Umoja wa Mataifa

Uingereza ilikuwa ikitawala Tanganyika chini ya kifungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Kama mamlaka tawala Uingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala.

Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo.

Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe ya kikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafrika waliokuwa wengi na wenye nchi.

Labda kwa kuanua ngoma juani, Gavana Twining alikaribisha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyama vya ustawi wa jamii na Native Authorities, kutaka mapendekezo ya jinsi Tanganyika itakavyotawaliwa.

Kamati ya Siasa ya TAA ( TAA Political Subcommitee) ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ile: Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo.

Katika taarifa yake ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika:

''Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria.

Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi.

Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba.''

(Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951. Sykes' Papers).

Abdul Sykes alitambua kuwa matatizo mengi kuhusu haki za Waafrika yalikuwa masuala ya kisheria ambayo yalihitaji ushauri wa wanasheria.

Kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Seaton, TAA kilitoa hoja zake zilozotiwa nguvu na ukweli takwimu zilizoonyesha udhalimu ndani ya mfumo wa kikoloni ambao ulikuwa kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Memorandum ya TAA kwa Constitutional Development Committee ambayo Pratt amesema iliandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu na uongozi wa makao makuu ya Tanganyika African Association ilipendekeza kuwa ndani ya baraza la kutunga sheria.

Waafrika watashika nusu ya viti kwa miaka 12 na baada ya hapo ipigwe kura kuwachagua wajumbe kwa kura moj mtu mmoja.

Gavana Twining iliyapuuza mapendekezo ya kamati ya TAA.

Serikali iliendelea na mipango yake ya muda mrefu ya kuwaimarisha Wazungu na Waasia waliokuwa wachache na kuwasukuma kando Waafrika kinyume kabisa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi zilizokuwa chini ya udhamini.

Waafrika wengi wenye elimu walionelea kuwa mapendekezo ya TAA ndiyo yangekuwa msingi wa katiba ya baadae ya Tanganyika kama jamii ya watu wa rangi zote.

Lakini moyo wa mapendekezo yale ya TAA haukufa.

Mapendekezo yale yaliletwa tena katika mkutano wa kuanzishwa kwa TANU tarehe 7 Julai, 1954.

Mapendekezo hayo ndiyo baadaye yalitiwa katika hotuba ya Julius Nyerere aliyoisoma mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, mwezi wa Machi, 1955.

Tarehe 7 Januari, 1951 mkutano muhimu sana ulifanyika katika Ukumbi wa Arnatouglo Dar es Salaam.

Abdul Sykes aliwasilisha taarifa yake kwa mkutano mkuu akieleza kuwa mwaka huo ulikuwa mgumu kwa TAA.

Wanachama walijulishwa kuhusu mwanasheria kutoka Bermuda, Earle Seaton kama mshauri wa TAA wa sheria na mchango wake katika kutayarisha mapendekezo iliyowasilishwa kwa Gavana Twining.

Wanachama walijulishwa kuhusu kufufuliwa kwa matawi ya TAA, mawasiliano yake na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa na uhusiano ulioanzishwa na TAA na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria.

Abdulwahid aliwaeleza wanachama juu ya ziara yake ya Nairobi aliyofanya mwezi Oktoba, 1950, na kukutana kwake na Balozi wa India katika Afrika ya Mashariki.

Vilevile aliwaeleza wanachama kuhusu mshikamano ulioanzishwa kati ya TAA na KAU; na kutolewa nafasi za kusoma katika vyuo vikuu vya India na serikali ya nchi hiyo kwa Waafrika wa Tanganyika.''

Sasa ikiwa mtu anataka kupata picha kamili ya hali ya ukoloni Tanganyika na Kenya asome kitabu cha Bildad Kaggia, ''Roots of Freedom,'' ataona kuwa mstari unaotenganisha ''koloni'' na ''udhamini'' ni mwembamba sana.
 
Kile Kitabu cha padre sivalon hakubahatika kukisoma?

Kanisa Katoliki na siasa ya Tanzania bara, 1953 hadi 1985 (Swahili Edition) Amazon product ASIN 9976633173
View attachment 2064918
Makala...
Kitabu hiki ilipokuja kudhihirika kuwa kina taarifa zisizojenga umoja nchini kilitolewa sokoni na kikawa hakichapwi.

Kanisa linasema maadui zake ni Uislam na Ukomunisti.
Hili lilipojulikana kuwa ni kauli mbaya vitabu vikazuiwa kuchapwa.

Wachapaji wa mitaani wakaona wamepata njia nyepesi ya kutengeneza fedha.
Hivi vitabu vikawa sasa vinachapwa kwa staili ya "pirate publication.''

Hii nakala hapo chini ni kati ya hizo:

IMG_20220101_141453_764~2.jpg
 
Unahitaji Google ikufasirie maana ya ukoloni? Ili ujue kama kweli Muingereza alikuwa Mkoloni au laa?
Wewe si ndio hujui? Google haitakupa maana ya "ukoloni" bali itakuwezesha kujua tafsiri zilizopo za "ukoloni". Wewe utachagua unayoona inakufaa.

Amandla...
 
Amandla.

Makala...
Kuna uzi mwembamba sana kati ya kuwa koloni na kuwa chini ya udhamini wa UNO.

Ukitazama hali ya jinsi Waingereza walivyokuwa wakitawala Kenya na Tanganyika hakuna tofauti yeyote.

Kama Waingereza walivyopora ardhi wa ya Wakikuyu Kenya ndivyo walivyopora ardhi ya Wameru Tangayika.

Katika kitabu cha Abdul Sykes nimejadili hali hii:

Tanganyika Kama Nchi Chini ya Udhamini wa Umoja wa Mataifa

Uingereza ilikuwa ikitawala Tanganyika chini ya kifungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Kama mamlaka tawala Uingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala.

Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo.

Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe ya kikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafrika waliokuwa wengi na wenye nchi.

Labda kwa kuanua ngoma juani, Gavana Twining alikaribisha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyama vya ustawi wa jamii na Native Authorities, kutaka mapendekezo ya jinsi Tanganyika itakavyotawaliwa.

Kamati ya Siasa ya TAA ( TAA Political Subcommitee) ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ile: Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo.

Katika taarifa yake ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika:

''Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria.

Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi.

Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba.''

(Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951. Sykes' Papers).

Abdul Sykes alitambua kuwa matatizo mengi kuhusu haki za Waafrika yalikuwa masuala ya kisheria ambayo yalihitaji ushauri wa wanasheria.

Kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Seaton, TAA kilitoa hoja zake zilozotiwa nguvu na ukweli takwimu zilizoonyesha udhalimu ndani ya mfumo wa kikoloni ambao ulikuwa kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Memorandum ya TAA kwa Constitutional Development Committee ambayo Pratt amesema iliandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu na uongozi wa makao makuu ya Tanganyika African Association ilipendekeza kuwa ndani ya baraza la kutunga sheria.

Waafrika watashika nusu ya viti kwa miaka 12 na baada ya hapo ipigwe kura kuwachagua wajumbe kwa kura moj mtu mmoja.

Gavana Twining iliyapuuza mapendekezo ya kamati ya TAA.

Serikali iliendelea na mipango yake ya muda mrefu ya kuwaimarisha Wazungu na Waasia waliokuwa wachache na kuwasukuma kando Waafrika kinyume kabisa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi zilizokuwa chini ya udhamini.

Waafrika wengi wenye elimu walionelea kuwa mapendekezo ya TAA ndiyo yangekuwa msingi wa katiba ya baadae ya Tanganyika kama jamii ya watu wa rangi zote.

Lakini moyo wa mapendekezo yale ya TAA haukufa.

Mapendekezo yale yaliletwa tena katika mkutano wa kuanzishwa kwa TANU tarehe 7 Julai, 1954.

Mapendekezo hayo ndiyo baadaye yalitiwa katika hotuba ya Julius Nyerere aliyoisoma mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, mwezi wa Machi, 1955.

Tarehe 7 Januari, 1951 mkutano muhimu sana ulifanyika katika Ukumbi wa Arnatouglo Dar es Salaam.

Abdul Sykes aliwasilisha taarifa yake kwa mkutano mkuu akieleza kuwa mwaka huo ulikuwa mgumu kwa TAA.

Wanachama walijulishwa kuhusu mwanasheria kutoka Bermuda, Earle Seaton kama mshauri wa TAA wa sheria na mchango wake katika kutayarisha mapendekezo iliyowasilishwa kwa Gavana Twining.

Wanachama walijulishwa kuhusu kufufuliwa kwa matawi ya TAA, mawasiliano yake na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa na uhusiano ulioanzishwa na TAA na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria.

Abdulwahid aliwaeleza wanachama juu ya ziara yake ya Nairobi aliyofanya mwezi Oktoba, 1950, na kukutana kwake na Balozi wa India katika Afrika ya Mashariki.

Vilevile aliwaeleza wanachama kuhusu mshikamano ulioanzishwa kati ya TAA na KAU; na kutolewa nafasi za kusoma katika vyuo vikuu vya India na serikali ya nchi hiyo kwa Waafrika wa Tanganyika.''

Sasa ikiwa mtu anataka kupata picha kamili ya hali ya ukoloni Tanganyika na Kenya asome kitabu cha Bildad Kaggia, ''Roots of Freedom,'' ataona kuwa mstari unaotenganisha ''koloni'' na ''udhamini'' ni mwembamba sana.
Moh waonaje ukikiweka hapa Kitabu cha Bildad
 
Makala,
Naamini umekusudia picha ya kitabu.

Huyu Bildad Kaggia ni katika wale viongozi wa KAU ambao Abdul Sykes alikutananao Nairobi katika ule mkutano wa siri.

Ukisoma taarifa ya Abdul Sykes ya 1950 ametaja safari yake ya Nairobi lakini hakueleza alikutana na nani huko.

Lakini bure Special Branch walikuwa wana taarifa zake zote.
Nataka nikupe kitu kidogo kuhusu Bildad Kaggia.

Katika jambo ambalo linanisikitisha ni kule kutopewa shajara (diary) za Abdul Sykes kuzisoma.

Naamini zina mengi.

Kuwa wakati ndani ya shajara zile akiandika kwa hati za kawaida na kuna wakati akiandika kwa ''short hand.''

Kaka usisikie Abdul Sykes alikuwa na vibweka hapana mchezo si ajabu aliandamwa na hasad.

Aliwatangulia mbele kwa mbali sana wenzake wa wakati wake.

Katika miaka ya nyuma nilikuwa nikienda sana Nairobi na nilijitahidi sana kutaka kukutana na Kaggia lakini sikufanikiwa.

Yeye alikataa kabisa kujiunga na wenzake waliokuwa wanajitajirisha kupitia kupora nk.

Nikasikia kuwa kuna wakati alikuwa na kiosk mjini Nairobi anauza maziwa lakini juhudi zangu za kumpata zilishindwa hadi anafariki.

1641043960674.png
 
Mohamed Mwenyezi kakukirimu, unafunza, unastarehesha, unaelimisha bali unaadabisha, hii stori ya babu yako inasisimua sana, hapa kwetu si ajabu kuwakuta watu waonao ajabu ya wewe kueleza historia ya watu wako, kwingine duniani ni jambo la kawaida

Umewanasihi vyema kwamba nao waandike historia za jamaa zao ambao huenda walishiriki katika harakati za uhuru huenda ikawaponguzia choyo nafsini mwao, kuna mmoja alishangaa ulipoeleza vikao kufanyika majumbani kipindi hicho eti akistaajabu kana kwamba ni udhariri, hali ya kuwa Leo ukitazama au ukisoma habari za wacomonisti kina Mao wa China utakuta vikao vingi ndani ya majumba yao na wao wakiwa na zile alama za kuwasiliana "codes" mfano morse kupitia magazeti, matangazo n. K

Kaka Mohamed Said natumai hutatuangusha wasomaji wako, hebu kamilisha tawasifu yako ambayo naimani itasheheni mengi, kadhalika hata haya yapatikanayo kutoka kwa wanafunzi wako(ambao wengi wamejivika koti la ukosoaji) yaeleza japo hutamaliza kiu yao
Makala...
In Shaa Allah nitaandika.

Hawa ndugu zetu wanahangaishwa na kule kuwa wao hawana historia ambayo wanaweza wakatafakhar nayo.

Sisi kwa nini tunatafakhar na historia ya wazee wetu?
Tunatafakhar kwa kuwa ni historia ya kupigania uhuru wa nchi yetu.

Nyerere ni kiongozi mkubwa sana Afrika na sifa zake zimetapakaa kwingi.
Sasa imetokea kuwa historia hii ya kupigania uhuru na yeye yumo pamoja na wazee wetu.

Hatuwezi kuandika historia ya wazee wetu tukaacha kumtaja itakuwa historia haijakamilika.

Tatizo linakuja wao wanataka Nyerere atajwe bila wazee wetu.

Wao wanaona vibaya kutafakhar na wazee wetu ubongo wao umejazwa fikra kuwa, ''hawa ni Waswahili,'' tu wanaweza nini.

Bahati mbaya wakaamini.
Sasa nilipowadondoshea historia ya kweli mstuko uliowapata hausemeki.

Haiwezekani kumfuta Abdul Sykes kwenye historia ya uhuru kwani historia itakuwa haijakamilika.

Hapa ndipo lilipokuja tatizo na kutufikisha hapa kuwa leo tunasoma upya historia ya TANU na historia ya Nyerere.

Kama walivyofanya waliowatangulia na wao wanajaribu kupita mle mle kujaribu kufuta historia ya wazee wetu.

Wanauliza wapi Abdul Sykes alihutubia mkutano.

Abdul hakuwa mtu wa majukwaa kama vile Nyerere alivyokuwa mtu wa majukwaa lakini hakuwa na fedha za ku-bankroll harakati za uhuru.

Abdul Sykes angepewa jukwaa ahutubie asingejua hata aseme nini halikadhalika ungemwambia Nyerere atoe fedha kwa ajili ya hiki au kile angeshindwa.

Abdul alikuwa mtu wa mipango na mmoja kati ya wafadhili wakubwa wa TAA na TANU.
Baba yake Kleist Sykes mimi nimempa jina, ''Man of Ideas'' katika kitabu cha mwanae.

Kaasisi African Assocaition, kajenga shule kwa ajili ya Waislam wa Dar es Salaam na akaasisi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Na kama Abdul asingefanya yale aliyofanya baba yake ya kuweka mkono wake wazi angekuwa amemuangusha baba yake na ''legacy'' ya jina lao.

Uhuru ulikuja na changamoto kubwa sana ambazo hakuna yeyote katika wazee wetu alitegemea.
 
Hakuna mahala umembana, hebu taja hata sehemu tano ambazo umembana na kama unavyojiaminisha zinaashiria haijui historia, wewe bwana mdogo shida yako nyingine nadhani ni "ulipyoto" kwasababu nukta zako zinajificha sana kisha zinakuwa na Uongo ama kukosa umakini, lakini pia hebu jikiteni katika hoja moja moja na ikitamatika ndio iende nyingine, huu mtindo wa kuzungumza kwa ujumla kwamba tumembana, hajui historia, hawataji wasukuma n. k kisha akiwabainisha mnarukia hoja nyingine si mzuri nadhani hata nafsi zenu zawasuta
Makala...
Sasa tuje kwenye mgomo wenyewe wa 1960.
Vipi waliweza kugoma kwa siku 82 hawana mshahara?

Kabla ya ule mgomo TRAU ilipata msaada wa fedha kutoka Ujerumani ya Mashariki na Chama Cha Wafanyakazi wa Reli wa Uingereza na sehemu nyingine.

TRAU ikachagua maduka maalum ya vyakula na wakatoa kadi kwa wanachama wao wote ambayo kadi hii iliwawezesha kupata mahitaji yao ya kila siku kuanzia mchele, unga, maharage, mafuta ya kupikia mafuta ya taa hadi viberiti.

Treni zilisimama, meli na mabasi yote ya Railway.

Nyumbani kwa babu yangu ikawa ndiyo Command Post wafanyakazi waliokuwa katika mgomo wanakutana hapo kupashana taarifa.

Hiki kilikuwa kipindi kigumu lakini wagomaji walijua kuwa huo mgomo ni moja ya njia ya kuwadhoofisha wakoloni na hatimaye kuwaondoa kabisa katika ardhi ya Tanganyika.

Kwa bahati mbaya sana mume wa shangazi yangu jina lake Msafiri Ali Mgawe hakugoma.
Hili lilikuwa pigo kubwa sana kwa babu yangu.

Mzee Ali Mgawe na babu yangu Salum Abdallah walikuwa majirani wakati wa ujana wao babu yangu akiishi Kipata na Ali Mgawe Kirk Street (sasa Mtaa wa Lindi) nyumba yake ikitazamana na nyumba ya Kleist iliyokuwa mtaa huo.

Mzee Ali Mgawe alikuwa mtu wa kujiweza kwa majumba.

Alikuwa na nyumba nzuri sana Mtaa wa Kitchwele kona na Congo ambayo kwa miaka mingi ilipangishwa na Muhindi kama duka la viatu.

Huu ujirani na urafiki ndiyo ulisababisha watoto wao kuoana.

Ajabu ya Allah ni kuwa Tabora Mzee Ali Mgawe alikuwa na nyumba nyingine nyuma ya nyumba ya babu yangu na wakikaa ndugu zake.

Msafiri Mgawe hakugoma akawa kibaraka.

Rafiki zake wakawa wanamtania wanamwambia, ''Baba Popo una kibaraka nyumbani kwako.''

Haya maneno yalikuwa yakimchoma sana babu.

Babu yangu kuanzia mwaka wa 1960 hakusema na mkwewe na Bwana Msafiri hakukanyaga nyumba ya babu yangu mpaka babu yangu anaingia kaburini.

Babu akija sana Dar es Salaam na atakwenda nyumba zote ila nyumbani kwa shangazi yangu mke wa Msafiri Mgawe.

Huu pia ndiyo ukawa mwisho wa urafiki wa babu yangu na Mzee Ali Mgawe.

Nakuelezeni haya mpate kujua hisia zilizokuwapo wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ngoja nikupeni mkasa uliotokea siku ya harusii ya shangazi yangu na Msafiri Mgawe.

Sherehe ilikuwa kubwa nyumbani kwa babu Kipata vyakula na magoma kupigwa kusheherekea harusi.

Baba yangu ananihadithia anasema Abdul Sykes alikuwa na bastola ametokanayo vitani basi akaingia ndani kwao akaichuku akajaza risasi akatoka nje akawa anapiga risasi juu moja baada ya nyingine kusheherekea harusi.

Pale Kipata nyumba ya babu yangu na ya Kleist zilikuwa zinaangaliana.

Kitendo hiki kilimkera sana mama yake Bi. Mruguru kwani aliona lile ni jambo la hatari ingawa risasi ikipigwa juu hewani haina madhara yoyote.

Mama Abdul akawa kuanzia siku ile anaivizia ile bastola.
Siku alipoipata na kuitia mkononi aliitumbukiza chooni na ndiyo ukawa mwisho wa bastola ile.

Ile bastola Abdul alipewa na ofisa Mwingereza wakiwa vitani ambae siku yake ya kuzaliwa na siku ya Abdul zilikuwa sawa.

Hii picha amevaa mgolole nimeambiwa alivishwa na wafanyakazi wa Railway kama ishara ya yeye kuwa jemadari akiongoza mapambano nadhani ilipigwa wakati wa huu mgomo wa 1960.

Kulia ni Kassanga Tumbo.

1641073302645.png
 
Hawa ndugu zetu wanahangaishwa na kule kuwa wao hawana historia ambayo wanaweza wakatafakhar nayo.
Kama yupo aliyeandika historia ya Wazee wangu, kuna haja ya kuandika tena!
Sasa nilipowadondoshea historia ya kweli mstuko uliowapata hausemeki.
Kweli kwa mujibu wako! Wasomaji wataamua si wajibu wako kuwaambia ni kweli
Your entitled to your opinion but not your own facts
Haiwezekani kumfuta Abdul Sykes kwenye historia ya uhuru kwani historia itakuwa haijakamilika.
Na Abdul Sykes si Historia ni sehemu tu ya watu walioshiriki. Nitakuonyesha kwanini hapo chini
Kama walivyofanya waliowatangulia na wao wanajaribu kupita mle mle kujaribu kufuta historia ya wazee wetu.
Nani anafuta historia ya wazee wako?Mbona unakuwa na hisia tu. Umeandika Historia ya Babu yako nani kahoji. Tunachohoji ni pale unapoingiza Babu Salum Abdallah kama kiongozi wa TRAU! Ukweli ni kuwa hawakufanya kazi na Kasanga Tumbo(Rejea somo jadidi la Fundi Mchundo )

Ndio maana tukasema tusihukumu haraka, tueambie ile picha ya Mzee Salum Abdallaha na Kasanga tumbo ilichukuliwa lini? Kama huna jibu tutakwambia 'stop' fabrications. Hilo ni kosa?
Wanauliza wapi Abdul Sykes alihutubia mkutano.
Abdul hakuwa mtu wa majukwaa kama vile Nyerere alivyokuwa mtu wa majukwaa lakini hakuwa na fedha za ku-bankroll harakati za uhuru.
Kubali ukweli kuwa AbdulWahid Sykes hakuwahi kuhutubia Mkutano nje ya Gerezani.
Hata Mdaula Morogoro au Segera hakuwahi.
Huyu ndiye unataka kutuaminisha ''alibeba uhuru wa Tanganyika'.

Nyerere hakuwa na fedha na hilo si siri lakini usijaribu kulinganisha mapungufu yao.

Kwamba Nyerere hakuwa na fedha basi ni sawa Abdul hakuwahi kutubia mkutano ni ridiculous!
kichekesho sana.

Hoja inajibiwa na hoja haijibiwi kwa ulinganifu Mohamed!!. Hapa utachekwa

Swali lilihusu Abdul Sykes ikiwa alifanya siasa nje ya Gerezani, Nyerere hawezi kuziba mapungufu ya Abdul. Abdul hakufanya Mkutano nje ya Gerezani, sasa kwanini unahangaika mara Kapenguria mara roll bank mara kule!

Tunaelewa, kwa jinsi unavyomhusudu Abdul kupindukia hoja nyingine ni embarassing lakini ni sehemu ya mnakasha, so sorry for that

Jaribu japo kidogo kuelewa na kukubali mapungufu.

Kwani ukisema Abdul hakuwahi kuhutubia kuna kosa gani. Kumleta Nyerere ni jitihada za kumlinganisha Abdul na Nyerere . Sikia Mohamed, Nyerere alikuwa next level. Period.
Abdul Sykes angepewa jukwaa ahutubie asingejua hata aseme nini halikadhalika ungemwambia Nyerere atoe fedha kwa ajili ya hiki au kile angeshindwa.
Kwanini unalinganisha hawa watu? Hizi ni jitihada za kumu-elevate Abdul alingane na Nyerere.

Hawa ni watu wawili tofauti na wanasifa tofauti katika nyakati tofauti na background tofauti na ningehusia mtu anayefikiri vema asiwalinganishehata kidogo.

Ukimlinganisha Nyerere na Abdul mwisho wa siku utamdhalilisha Abdul.
''Please be careful what you wish for'
 
Kama yupo aliyeandika historia ya Wazee wangu, kuna haja ya kuandika tena!

Kweli kwa mujibu wako! Wasomaji wataamua si wajibu wako kuwaambia ni kweli
Your entitled to your opinion but not your own facts

Na Abdul Sykes si Historia ni sehemu tu ya watu walioshiriki. Nitakuonyesha kwanini hapo chini

Nani anafuta historia ya wazee wako?Mbona unakuwa na hisia tu. Umeandika Historia ya Babu yako nani kahoji. Tunachohoji ni pale unapoingiza Babu Salum Abdallah kama kiongozi wa TRAU! Ukweli ni kuwa hawakufanya kazi na Kasanga Tumbo(Rejea somo jadidi la Fundi Mchundo )

Ndio maana tukasema tusihukumu haraka, tueambie ile picha ya Mzee Salum Abdallaha na Kasanga tumbo ilichukuliwa lini? Kama huna jibu tutakwambia 'stop' fabrications. Hilo ni kosa?

Kubali ukweli kuwa AbdulWahid Sykes hakuwahi kuhutubia Mkutano nje ya Gerezani.
Hata Mdaula Morogoro au Segera hakuwahi.
Huyu ndiye unataka kutuaminisha ''alibeba uhuru wa Tanganyika'.

Nyerere hakuwa na fedha na hilo si siri lakini usijaribu kulinganisha mapungufu yao.

Kwamba Nyerere hakuwa na fedha basi ni sawa Abdul hakuwahi kutubia mkutano ni ridiculous!
kichekesho sana.

Hoja inajibiwa na hoja haijibiwi kwa ulinganifu Mohamed!!. Hapa utachekwa

Swali lilihusu Abdul Sykes ikiwa alifanya siasa nje ya Gerezani, Nyerere hawezi kuziba mapungufu ya Abdul. Abdul hakufanya Mkutano nje ya Gerezani, sasa kwanini unahangaika mara Kapenguria mara roll bank mara kule!

Tunaelewa, kwa jinsi unavyomhusudu Abdul kupindukia hoja nyingine ni embarassing lakini ni sehemu ya mnakasha, so sorry for that

Jaribu japo kidogo kuelewa na kukubali mapungufu.

Kwani ukisema Abdul hakuwahi kuhutubia kuna kosa gani. Kumleta Nyerere ni jitihada za kumlinganisha Abdul na Nyerere . Sikia Mohamed, Nyerere alikuwa next level. Period.

Kwanini unalinganisha hawa watu? Hizi ni jitihada za kumu-elevate Abdul alingane na Nyerere.

Hawa ni watu wawili tofauti na wanasifa tofauti katika nyakati tofauti na background tofauti na ningehusia mtu anayefikiri vema asiwalinganishehata kidogo.

Ukimlinganisha Nyerere na Abdul mwisho wa siku utamdhalilisha Abdul.
''Please be careful what you wish for'

Ni kweli huwezi kumlinganisha Nyerere Na Abdul ,
Nyerere alikuwa kibaraka wa Waingereza Na kanisa Katoliki Hakuna siri hapo
 
Nitaanza na kuzungumzia kitabu cha Dr. John Sivalon kilichoitwa "Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara kuanzia 1953 hadi 1985". Kitabu hiki kilichapishwa na Benedictine Publications Ndanda, Peramiho. Kilitokana na Doctoral dissertation ya Dr. Rev. John Sivalon iliyoitwa " Roman Catholicism and the Defining of Tanzanian Socialism 1955-1985" aliyoitetea mwaka 1990 katika Chuo Kikuu cha St. Michael's College, Toronto School of Theology. Dr. Rev. John Sivalon alikuwa Mkurugenzi wa Maryknoll Fathers and Brothers Africa. Ameandika sana kuhusu masuala ya Ukatoliki katika nyanja tofauti na ni Professor wa Theology. Kitabu chake kimekuwa cherry picked kuonyesha kuwa Kanisa Katoliki lilikuwa na ajenda ovu ya kutawala Tanzania na kuwanyima fursa waislamu.

Mimi ningependa kujua kwa wale waislamu ambao wanakubaliana na hii theory ya ubaguzi na nia ovu ya wakatoliki watuambie ni shule gani ya kikatoliki ilikuwa haipokei waislamu au watu wa madhehebu mengine. Ninavyojua mimi ni kuwa kuna wazazi wa kiislamu ambao hawakutaka watoto wao wasome katika shule hizo kwa hofu ya kuwa watarubuniwa ili waingie kwenye ukristu au watalishwa vyakula ambavyo ni haramu kwao. Hii haishangazi maana naamini hata sasa kuna wagalatia ambao hawako tayari kuwapeleka watoto wao Al Muntazir au Feza kwa hofu ya kubadili dini au kuvishwa hijab, vazi ambalo wanaliona ni ishara ya uislamu.

Watutajie vile vile vituo vya afya na hospitali ambazo zilikuwa zinakataa kuwahudumia waislamu. Ninavyojua mimi ni kuwa katika sehemu nyingi hospitali zinazothaminiwa kuliko za serikali kutokana na huduma bora na gharama nafuu ni zile zinazoendeshwa na makanisa. Mimi naamini ni haya matumizi mabaya ya maandiko ya Rev. Sivalon ndio yamewafanya publishers waache kukichapisha. Au mauzo madogo ya chapisho za awali.

Amandla...
Kijana Fundi Mchundo
Cc. Nguruvi3
 
Suala lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni suala la kesi ya ardhi ya Meru ambayo Moham ameielezea kwa kirefu akisistiza ukaribu na uhusika mkubwa wa Abdul Sykes kama Katibu wa TAA na Abbas Sykes katika kuzunguka na Kirilo Tanganyika nzima kuwaelimisha watanganyika kuhusu kesi hiyo. Amesema Abdul Sykes, kama rafiki wa Easton ndie aliyezungumza nae ili kuwasaidia wameru kuandika petition kwenda UNO. Katika bandiko lote la tarehe 28 Aprili 2021, hamna alipomtaja Nyerere isipokuwa alipotoa utambuzi wa picha aliyosema ni ya waasisi wa TANU ambayo imeandikwa Dodoma 1954. Vile vile kuna picha yake na Abdulwahid Ally Sykes ambayo anasema ilipigwa nje ya nyumba ya Kirilo mwaka 1989. Nahisi huyu Abdulwahid ni mtoto wa Ally Sykes kwa sababu Abdulwahid Sykes alizaliwa 1924 na alifariki 1968.

Mimi simulizi yangu ya mgogoro wa ardhi ya wameru nita i "base" zaidi kwenye kitabu cha John IIiffe cha mwaka 1976 ambacho Mohamed amekitumia sana katika maandiko yake.

John IIiffe anasema petition kuhusu kesi hii ilitayarishwa na wameru wenyewe na kiongozi wao aliyekuwa anaitwa Raphael Mbise aliituma kwa Chief Koinange wa wakikuyu ili aipeleke Umoja wa Mataifa. Katika petition hiyo ya tarehe 9 Juni 1952, viongozi wa wameru waliomba kuwa wapewe nafasi ya kuwepo wakati inajadiliwa na Trusteeship Council. Ombi lao lilikubaliwa na wakaambiwa kikao kitakuwa tarehe 30 Juni 1952. Uliitwa mkutano wa hadhara ambao uliwachagua mwanasheria Seaton na Katibu wa Meru Citizens Union na TAA tawi la Arusha kwenda New York. Seaton aliweza kuondoka mapema lakini waingereza walimchelewesha Kirilo kuondoka. Seaton aliweza kutetea petition hiyo katika tarehe iliyopangwa lakini Kirilo alipata nafasi ya kufanya hivyo tarehe 21 July. Seaton alirudi Tanganyika moja kwa moja lakini Kirilo alipitia kwanza London, Uingereza ambako alikutana na Lord Fenner Brockway wa chama cha labour kujaribu kushawishi serikali ya Uingereza. Alikutana pia na Julius Nyerere ambae alikuwa yuko likizo kutoka Edinburg. Alikutana pia na Peter Koinange, Fred Kubai na Dr. Munyua Waiyaki na Semakula Mulumba wa Uganda kuhusu shauri lake. Wote hawa walimpa moyo na ushauri wa namna ya kuendelea

Mwezi Septemba aliandika barua ya pili TAA kuwauliza kama kuna kitu ambacho wangependa kiongezwe kwenye petition yake. Abdulwahid Sykes akamjibu na kumuambia kuwa hilo suala ni muhimu kwa waafrika wa Tanganyika lakini TAA hawana pesa yeyote ya kumsaidia. Iliffe anasema " In terms of political action TAA was a broken reed" ( ukurasa 502). Ikumbukwe hii ni TAA ya Abdul Sykes kabla Nyerere hajachaguliwa kuwa rais wake. Kirilo akajirudia nyumbani.

Kirilo na Seaton walirudi tena New York mwezi Novemba mwaka huo lakini hawakupata mafanikio waliyotegemea. UNO ilikubali kuwa kweli Muingereza alikuwa mkosaji lakini hamna haja ya wao kuwarudishia ardhi wameru. Kirilo alirudi Tanganyika mwaka 1953 ambako alikutana na Nyerere. Kirilo amesema kuwa ni Julius Nyerere na Kandoro ndio waliomshauri kuzunguka Tanganyika nzima kuwaelezea watanganyika kuhusu ukatili wa waingereza. Nadhani wakati huo Nyerere alikuwa tayari Rais wa TAA. Watu wengi wanaamini kuwa ni safari hii ya wakina Kirilo ndio ilibadilisha muelekeo wa siasa Tanganyika kuelekea kwenye kudai uhuru badala ya masuala ya mishahara na uwakilishi katika Legislative Assembly. Wakina Kirilo walijenga hoja kuwa njia pekee ya kuepukana na dhulma kama walizofanyiwa ni kupata uhuru. Tume kutoka UNO zilizotembelea Tanganyika kabla ya hii kesi zilishangazwa jinsi watanganyika walivyokuwa hawana habari na masuala ya uhuru. Migomo iliyokuwa inaendelea mara nyingi ilitokana na dhana ya kuwa mwenzao ametukanwa/amenyanyaswa kwa sababu ya rangi yake na /au kudai nyongeza za mshahara, au kulipwa mshahara sawa na wahindi.

Ikumbukwe pia kuwa Japhet alikuwa mgalatia na wameru wengi walikuwa waluteri. Hii inathibitisha kuwa ile dhana ya kuwa wagalatia walikuwa ni vibaraka wa waingereza kuwa ni ya uongo. Inathibitisha kuwa moto wa kudai uhuru ulishika kasi baada ya kuwashwa na wagalatia wa Meru. Moto huu usingekuwa na mafanikio kama ungebakia Gerezani peke yake.

Ukisoma maelezo ya waandishi wengine wa historia utatambua kuwa ingawa wakina Sykes walichangia sana juhudi za ukombozi wa nchi hii lakini sio kwa kiasi ambacho Mohammed anataka kutuaminisha. Aidha, juhudi hizi hazikufanywa na watu wa dini fulani au kabila fulani peke yao. Hawa mashujaa walijitambua zaidi kama sehemu ya ukombozi wa mwafrika na mtanganyika kuliko kujiona sehemu ya jeshi la dini yao dhidi ya wale wenye dini tofauti.

Amandla...

Cc: Nguruvi3
 
Back
Top Bottom