1995 Mbeya: Wakati ule OTTU ilipoachana na ujinga Wakamwalika Mwl.Nyerere badala ya Rais Mwinyi

1995 Mbeya: Wakati ule OTTU ilipoachana na ujinga Wakamwalika Mwl.Nyerere badala ya Rais Mwinyi

Ranger9

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2021
Posts
1,613
Reaction score
3,002
Wakati wa akina Bruno Mpangala, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lilipokuwa huru na lina viongozi wenye weledi na calibre ya kuongoza si tu Vyama vya Wafanyakazi, bali hata kuongoza nchi; siyo haya mapandikizi yaliyojaa kwenye vyama vya wafanyakazi kwa sasa.

Wakati ule serikali ilianza kuongozwa kisanii sanii kama ambavyo imeongozwa kwa miaka 7 sasa na kwanza John Magufuli na sasa Samia Suluhu.

Mwinyi nchi ilimshinda, wafanyakazi hawalipwi mishahara na migogoro na migomo ikatamalaki kila sekta..

Ndipo akina Bruno Mpangala wakati huo wakavunja mwiko badala ya kumwita Rais mwuza sura kwenye sherehe zao wakamwalika Mwl.Nyerere.

Mwalimu akafika pale akaupiga mwingi. Siyo hawa watu wafupi wa sasa. Akairarua serikali mbovu ya wakati ule na akajenga hamasa ya kwelikweli kwa Wafanyakazi, wakajawa imani japo hawakupata nyongeza ya mishahara.

Lkn matokeo yake ilikuwa ni kupiga kura kwa wingi kuweka serikali yenye uwezo wa kuongoza nchi ya Benjamin W. Mkapa; miaka yote ya Mkapa wafanyakazi wakaishi kwa neema, wakajenga majumba wakamiliki na magari.

Sasa ili tupone tumwage oil chafu ya maccm yaliyojazwa na Magufuli kwenye Vyama vya Wafanyakazi, then tuanze moja.

Royo Tua zii
 
Lkn matokeo yake ilikuwa ni kupiga kura kwa wingi kuweka serikali yenye uwezo wa kuongoza nchi ya Benjamin W. Mkapa; miaka yote ya Mkapa wafanyakazi wakaishi kwa neema, wakajenga majumba wakamiliki na magari.
Mavii!
 
Poleni sana wafanyakazi nchini.

Hivyo vyama vya wafanyakazi vipo kwa ajili ya viongozi wao kujinufaisha tu.
 
Ana lake jambo huyo, sema amelificha kwa mbaaali huko. Anatamani na huyo jpm hapo angemtoa sema ndo hivyo imeshindikana tu kwa vile haya ya kutoongezwa mishahara yameanzia kwake
 
Back
Top Bottom