1998 sitosahau vituo vya polisi vilivyojaza watu bila sababu mpaka FBI walipokuja na kumpata wanayemshuku

1998 sitosahau vituo vya polisi vilivyojaza watu bila sababu mpaka FBI walipokuja na kumpata wanayemshuku

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Mwaka 1998 nakumbuka nilikuwa nipo maeneo ya Kijitonyama mida ya saa 4 asubuhi hivi siku ya Ijumaa kama nitakuwa nakosea na ndio mara yangu ya kwanza kusikia bomu likilindima mpaka kutingisha ardhi.

Tuja kaa vizuri redio na tv zinaanza kutangazia umma kuwa kuna shambulio limetokea ubalozini mwa Marekani kabla kujapishana tunasikia tena Kenya nako hivyo hiyvo.

Tuje kwetu sasa kwa vile lile tukio lilikuwa kubwa na mambo kama haya yalikuwa mageni kwetu basi jeshi letu la polisi kuonesha wao wana weredi wa juu aisee yani watu waliopo Posta, Kinondoni, karibu na maeneo ya vituo vya polisi walibidi kukimbia ili wasije kukusanywa bila sababu.

Kuanzia Ijumaa mpaka FBI wanakuja vituo vyote vya polisi vilijaa kila aina ya watu ila wale jamaa walipokuja tu sijui walitumia mbinu gani kumpata chambo.

Mpaka leo sijui kama polisi wetu walishawai kuandika ili kuhusu walivyofanya
 
wanasema wale jamaa ni wachawi balaa! yani hatuwafikii hata punje! unaambiwa wanaweza kumjua adui hata kwa harufu tu!!..
 
kuanzia ijumaa mpaka FBI wanakuja vituo vyote vya polisi vilijaa kila aina ya watu .ila wale jamaa walipokuja tu sijui walitumia mbinu gani kumpata chambo.
ila mpaka leo sijui kama polisi wetu walishawai kuandika ili kuhusu walivyofanya
Ukizingatia kwamba hata ile 9/11 2001 ni njama za ndani kwa ndani za Marekani yenyewe, wala haihitaji akili nyingi kugundua kwa nini waliweza kumpata ^mtuhumiwa^ wao kirahisi hivyo.

Ni kama tu sakata la Lee Harvey Oswald na kuuawa kwa JFK.
 
Wengi wali chukuliwa mikitini maana ndo madharia ya magaidi yalipo
 
Polisi bongo weledi wao upo kwa kuhisi na kusikia zaidi (hear say)! Wao ni wazuri kwa kubashiri ili waonekane wanafanya kazi wanapotoa ripoti kwa wakubwa.
 
Back
Top Bottom